ADDS

ADDS

Thursday, 19 October 2017

Uzinduz wa kampen ya kutokomeza gugu karoti iliyofanyika leo Jijini Arusha katika chuo chq Utafiti cha TPRI Ngaramtoni

NAIBU WAZIRI KAKUNDA AFANYA ZIARA KILWA


 Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo kulia akitoamaelezo ya mradi mkubwa wa uoteshaji wa miche ya korosho kwa Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George  Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai 


Afisa kilimo na ushirika wilaya ya Kilwa John Mkinga kushoto akitoa taarifa ya mradi wa uoteshaji wa miche ya korosho mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George  Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo


Picha ikionyesha viriba vya kuoteshea miche ya korosho

Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George  Kakunda akiingia katika eneo la uoteshaji wa miche ya korosho,kushoto ni Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai 

KILWA

Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI George  Kakunda amewataka viongozi wa serikali wilayani Kilwa Mkoani Lindi kuhakikisha wanasimamia vyema upandaji wa miche mipya yazao la korosho hali ambayo itaongeza uzalishaji wa zao hilo kwa wananchi na kuinua uchumi wa Taifa

Hayo aliyasema jana wilayani Kilwa wakati wa ziara yake baada ya kuelezwa kuwa mkakati wa wilaya uliopo ni kuhakikisha wanazalisha na kupanda miche milioni moja kila mwaka hali ambayo itaongeza mashina ya zao hilo kutoka laki sita yaliyopo na zaidi kutokana na mpango huo kuwa wakudumu

Kufuatia hali hiyo Kakunda alisema ili miche hiyo iote vizuri na kustawi lazima uwepo usimamizi mkubwa kwa viongozi wote wa serikali wilayani humo kuliko kuacha usimamizi kwa wakulima peke yao ambao wanaweza kusababisha kukauka na kushindwa kufikia malengo

Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo alisema tayari hatua za awali za kuotesha miche milioni moja kila mwaka zinaendelea ambazo miche hizo itagawiwa bure kwa wakulima hali ambayo itainua uchumi wao

Bugingo alisema mpango huo ni wakudumu ambapo kila mwaka wilaya itazalisha miche hiyo milioni moja na kuigawa kwa wakulima bure hali ambayo itakuwa zaidi ya mara mbili ya uzalishaji wa miche iliyopo ambayo kwa sasa ni laki sita tu iliyowaingizia shilingi Bilioni 13 na halmashauri kujipatia zaidi ya shilingi milioni220

Aliongeza kuwa mbali na kujipatia fedha kwa wakulima pia halmashauri itajiongezea mapato ya ushuru baada ya serikali kufuta baadhai ya vyanzo ikiwemo ya mabango iliyorudishwa serikali kuu hivyo zao hilo la korosho linaweza kuingizia halmashauri zaidi ya shilingi bilioni 40 kutokana na mpango huo kuwa zaidi ya mara mbili zaidi

Mbali na hali hiyo Waziri Kakunda ameupongeza mpango huo wa upandaji wa miche hiyo milioni moja kila mwaka kutokana na kuvuka malengo ya serikali ya kupanda miche elfu 50 kwa kila wilaya inayolima zao la korosho ingawa Afisa kilimo na ushirika wa halmashauri hiyo ya Kilwa John 

Mkinga amesema changamoto iliyopo ni ucheleweshwaji wa mbegu hali inayosababisha zoezi la uoteshaji miche hiyo kwenda taratibu ingawa Kakunda amesema atawasiliana na wizara ya kilimo kumaliza tatizo hilo

SERIKALI YAZIONYA TAASISI ZA UMMA ZISIZOTUMIA WAKALA WA UNUNUZI NA UGAVI SERIKALINI (GPSA)


 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na Viongozi na watumishi wengine wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera (hawapo pichani) alipotembelea ofisi hizo kuhusu kuhakikisha Taasisi zote za Serikali zinapata huduma kutoka Wakala huo, alipofanya ziara katika Mkoa huo.

 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maagizo kwa Kaimu Meneja  wa Wakala Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi, kuhusu kuwahudumia Taasisi zote za Serikali kwa kuwa ndio wajibu wa Wakala huo, alipofanya Ziara katika Ofisi hizo za Mkoani Kagera.


 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro akielezea namna atakavyoshirikiana na Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini katika Mkoa huo ili kuhakikisha kunakuwa na matumizi adili ya fedha za Serikali, Naibu Waziri wa  Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea Ofisi za Wakala huo Mkoani Kagera.

 Kaimu Meneja wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) namna tetemeko la ardhi lilivyo haribu miundombinu ya Ofisi hizo, alipotembelewa na Naibu Waziri huyo katika Ofisi za GPSA Mkoani humo.

 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba  Bw. Deodatus Kinawiro (kulia) akizungumza jambo wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) alipotembelea Ghala la Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) Mkoani Kagera.


 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) akitembelea maeneo ya Ofisi za Wakala wa Ununuzi na Ugavi Serikalini (GPSA) ambapo aliweza kupata maelezo namna  Wakala huo unavyofanya kazi.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa nne kushoto), Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw. Deodatus Kinawiro (wa tano kulia), Kaimu Meneja wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi  Serikalini (GPSA) Mkoa wa Kagera, Bi. Dorothea Bugenyi (wa tatu kushoto) na watumishi wengine wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa ziara ya Naibu Waziri huyo katika Ofisi hizo Mkoani Kagera.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

Benny Mwaipaja, Kagera


NAIBU waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameziagiza Mamlaka na Taasisi zote za Umma kufanya ununuzi wa vifaa na mafuta kupitia Wakala wa Serikali wa ununuzi na ugavi (GPSA) kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge na kuwaonya wahusika wote watakaoendelea kukaidi maagizo hayo kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Dkt. Kijaji ametoa maagizo hayo mkoani Kagera baada ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Wakala wa Ununuzi na Ugavi GPSA mkoani humo na kubaini kuwa taasii na idara nyingi za umma zinafanya manunuzi nje ya mfumo wa GPSA jambo ambalo amesema ni ukiukwaji mkubwa wa sheria.

Alisema kuwa lengo la Serikali la kuanzishwa kwa wakala huo pamoja na mambo mengine ilikuwa kudhibiti matumizi ya Serikali na kuonya kuwa Serikali haitakubali kuona sheria zinakiukwa kwa makusudi na kwa malengo yanayoonesha kuna nia isiyo njema katika matumizi ya fedha za umma.

“Hili si ombi ni maelekezo na ni agizo, taasisi zote zipate huduma kutoka kwa wakala wetu (GPSA) kwani Serikali ilikuwa na dhamira ya uwepo wa matumizi sahihi ya fedha za matumizi wanazopelekewa na ndiyo maana ukaanzishwa Wakala huu” Alisema Dkt. Kijaji

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawiro, akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, aliiagiza Wakala wa Ununuzi na Ugavi (GPSA) mkoani humo kumpelekea orodha ya taasisi ambazo hazitumii huduma za wakala huo ili aweze kuchukua hatua.

Alisema kuwa ni jambo lisilofaa kwa Taasisi za Umma kukiuka sheria na kwamba watatekeleza maelezo yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango haraka ili kuokoa fedha za Serikali na kuweka uwajibikaji.

Awali, Kaimu Mkuu wa Wakala wa Ununuzi na Ugavi GPSA mkoa wa Kagera Bi. Dorothea Bugenyi alieleza kuwa katika kipindi cha miaka 3 iliyopita Wakala huo umeongeza makusanyo yatokanayo na mauzo ya vifaa na mafuta kutoka Shilingi bilioni 1.9 hadi kufikia Shilingi bilioni 2.34.

Alisema kuwa mapato hayo yangekuwa makubwa zaidi endapo taasisi zote za umma zingetii sheria na kufanya manunuzi yao ya vifaa na mafuta kutoka kwa Wakala huo na kuiomba Serikali kuusaidia Wakala huo kuziagiza taasisi zake za umma kutekeleza sheria hiyo kwa vitendo


Wednesday, 18 October 2017

Jeshi la Polisi ,Wadau wa Usalama barabarani wafanya ukaguzi wa Magari Kilimanjaro


Kaimu RTO mkoa wa Kilimanjaro ASP Willy Mwamasika. akiwa katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mkoani Kilimanjaro alipokuwa akitekeleza moja ya majukumu kabla magari hayajaondoka kulelekea mikoani .Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya Mabalozi wa usalama barabarani (RSA) wakiwa katika stendi kuu ya mabasi Mkoani Kilimanjaro wakiwa wanatoa elimu kwa abiria kabla ya mabasi kuondoka kuelekea mikoani.Picha na Vero Ignatus Blog.

Wakaguzi wa magari na wasaili wa Madereva wakiendesha ukaguzi wa magari stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Moshi Kilimanjaro leo.Picha na Vero Ignatus Bog.
Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa barabara Sumatra SACP Johansen Kahatano ASP Willy Mwamasika .Mkurugenzi wa Habari Elimu na Mawasiliano kutoka Taasisi ya  Mabalozi wa Usalama kaimu meneja Salum Pazzy Afisa mawasiliano mwandamizi sumatra

Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa barabara Sumatra SACP Johansen Kahatano ASP Willy Mwamasika,Mkurugenzi wa Habari Elimu na Mawasiliano kutoka Taasis ya Mabalozi wa Usalama Barabarani Augustus Fungo
 Koplo Peter akiwa na mabalozi wa usalama barabarani stendi kuu ya mabasi Moshi mkoani Kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mabalozi wa Usalama barabarani (RSA)wakizungumza na Ibrahim Shayo (aliyevaa kofia) ambae ni mmiliki wa mabasi ya Ibra Line.Picha na Vero Ignatus Blog.

Mabalozi wa Usalama barabarani ,Afisa mfawidhi sumatra mkoa wa kilimanjaro Johns Makwale aliyevaa kizibao cha njano wakiendelea kutoa Elimu katika Stendi kuu ya mabasi mkoani Kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mkurugenzi Uthibiti usafiri wa barabara Sumatra SACP Johansen Kahatano,ASP Willy Mwamasika ,Afisa Pazzy kutoka Sumatra wakiendelea kukagua magari katika Stendi kuu ya Mabasi Moshi Kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus Blog.

Mmoja wa Abiria akiwa amebeba mzigositi ya mbele akiwa amepakata mzigo mkubwa ambao ni hatari kwake na dereva pia kama alivyokutwa leo na Blog hii.
Mabalozi wa usalama barabarani wakiwa katika stendi kuu ya mabasi Moshi mkoani Kilimanjaro wakiendelea kutoa elimu kwa abiria pamoja na makondakta/abiria kuhusiana na Usalama barabarani.Picha na Vero Ignatis Blog.
Balozi Elizabeth Maembe akitoa elimu kwenye moja ya mabasi yaendayo mikoani katika stendi kuu ya mabasi Moshi mkoani Kilimanjaro .Picha na Vero Ignatus Blog.


Na.Vero Ignatus Blog

Jeshi la polisi Kitengo cha Usalama barabarani kwa kusirikiana na wadau wa usalama barabarani wamefanya zoezi la  ukaguzi wa magari stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na kugundua makosa mbalimbali yanayofanyawa na madereva pamoja na makondakta.

Akizungumzia zoezi hilo Kaimu RTO mkoa wa Kilimanjaro ASP Willy Mwamasika amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu na wameliendesha kwa muda mrefu sasa ambapo amesema magari ambayo yamekutwa na makosa yanatozwa faini na mengine Kupelekwa kituoni au kufunguliwa mashtaka .

Amewataka wamiliki wa mabasi yanayosafirisha abiria wanapobadili ratiba zao wakumbuke na kufuta kwenye magari yao ili wasiwachanganye abiria wanaposafirikauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Zuia Ajali Tii Sheria Okoa Maisha".

Mkurugenzi wa Elimu Habari na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Usalama barabarani (RSA)Augustus Fungo amesema kuwa zoezi hilo limekuwa zuri kwani limefanyika sambamba na mihimili  mikuu ya usalama barabarani ikiwemo  Polisi,Sumatra na Jeshi la zima moto pamoja na wadau mbalimbali wa usalama barabarani .

Kwa sasa zoezi hili ni msisitizo katika wiki ya nenda kwa usalama barabarani lengo kupeana elimu ya usalama na usafirishaji ,kukumbushana wajibu wetu barabarani kqa abiria na dereva ,kuwachukulia hatua wale amabao anavunja sheria za uaalama barabarani

Huku akisema kauli mbiu yao Mabalozi wa Usalama barabarani n#Safiri Salama Ajali sasa basi#"Tuesday, 17 October 2017

Imamu aigomea Tanroads kubomoa mskiti Kimara

Imamu wa Msikiti wa Al Masjid Kirumbi Islamic Center uliopo Kimara amewazuia waumini wake kutoshiriki katika kuvunja au kutoa kitu chochote katika msikiti huo ambao unatakiwa kuvunjwa na Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS.

Imamu wa Msikiti huo Ramadhan Juma  amesema hayo jana  wakati akifanyiwa mahojiano na MCL na kudai kutokana na imani yao ni kosa kubwa mtu yoyote kuvunja nyumba ya ibada kwa kuwa hiyo ni nyumba ya Mungu na kusema wao hawajatoa kitu chochote zaidi ya vitu vidogo ambavyo vinatumika kusaidia jamii kama jeneza.

"TANROADS wametupa barua ya kuvunja msikiti ndani ya wiki moja kwa kile wanachodai umevamia eneo la barabara hivyo walitaka tutoe vifaa ndani ya wiki moja kupisha zoezi la barabara lakini kutokana na imani yetu na Uislam unavyotufundisha ni kosa kubwa kuvunja nyumba ya 'Allah Subhanahu Wa Ta'ala' 

"Hii ni nyumba ya ibada hivyo hatutainua mikono yetu kwa kujihukumu sisi wenyewe kwa amri ya dini yetu ya Kiislam kwetu sisi ni kosa mtu kutoa mkono wake kutoa sijui bati au chochote kile kinachohusu msikiti kwa hiyo ndiyo maana tumeshindwa kuvunja msikiti huu" alisisitiza Imamu Ramadhan

Hata hivyo Imamu alisisitiza kuwa wao wameiachia serikali na hao TANROADS waweze kubomoa wenyewe na kusema yeye amewakataza waumini wake wasishiriki cha chochote katika kubomoa nyumba hiyo ya ibada

"Nimewaambia waumini wangu wasitoe chochote katika kuvunja kwa msikiti huu, tutatoa vitu vidogo vidogo ambavyo vinasaidia jamii kama vile jeneza na vinginevyo tumevitoa lakini katika majengo kwa chochote kile tunawaachia wenyewe, hii ni nyumba ya Allah hivyo wavunje wao halafu Mungu mwenyewe ndiye atajua kwa kuwa hiyo ni nyumba yake atakavyohukumu yeye ndiye anajua kwa kuwa hiyo ni nyumba yake" alisema Imamu Ramadhan Juma

NAIBU WAZIRI MGALU AITAKA TANESCO KUWAJIBIKA IPASAVYO KWA WATEJA

Na Veronica Simba - Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linawajibika ipasavyo kwa wateja wake ili kukuza imani yao kwa shirika hilo.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa shirika hilo wa Mkoa wa Dodoma, leo Oktoba 17, 2017, Naibu Waziri amebainisha kuwa mojawapo ya njia muhimu ya uwajibikaji kwa jamii ni kupitia utoaji taarifa kwa wateja kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu.

“Mathalani, kunapokuwa na katizo la umeme, wateja walioko eneo husika wanapaswa kutaarifiwa kabla ya katizo hilo ili wajipange,” alisisitiza.

Ameeleza njia nyingine ya shirika hilo kuwajibika kwa jamii, kuwa ni kushughulikia matatizo mbalimbali ya wateja wao kwa wakati na kuachana na utaratibu wa kufanya kazi kwa mazoea.

Kwa upande wake, akiwasilisha taarifa ya kazi ya ofisi yake kwa Naibu Waziri, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu, ametaja baadhi ya mafanikio ambayo Ofisi hiyo imepata kuwa ni pamoja na kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia 100 pamoja na kubadilisha mita ndogo zote, zilizokuwa zikitumika zamani na kufunga LUKU.

Naibu Waziri Mgalu, ametembelea Ofisi za TANESCO Dodoma kwa lengo la kuzungumza na wafanyakazi na kujitambulisha kwao.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma (hawapo pichani), alipowatembelea kwa lengo la kujitambulisha kwao na kueleza vipaumbele vyake vya kazi.


Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (kushoto), akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi yake kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), wakati Naibu Waziri alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na viongozi.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyesimama) akizungumza na viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, alipotembelea Ofisi hizo leo Oktoba 17, 2017.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dodoma, alipotembelea Ofisi hizo na kuzungumza na viongozi wake (hawapo pichani). Kushoto ni Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.Baadhi ya viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakimpokea Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye nguo nyeusi) alipowasili katika Ofisi hizo kuzungumza na viongozi wake


NAIBU WAZIRI MGALU AITAKA TANESCO KUWAJIBIKA IPASAVYO KWA WATEJA

Na Veronica Simba - Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhakikisha linawajibika ipasavyo kwa wateja wake ili kukuza imani yao kwa shirika hilo.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa shirika hilo wa Mkoa wa Dodoma, leo Oktoba 17, 2017, Naibu Waziri amebainisha kuwa mojawapo ya njia muhimu ya uwajibikaji kwa jamii ni kupitia utoaji taarifa kwa wateja kuhusu masuala mbalimbali yanayowahusu.

“Mathalani, kunapokuwa na katizo la umeme, wateja walioko eneo husika wanapaswa kutaarifiwa kabla ya katizo hilo ili wajipange,” alisisitiza.

Ameeleza njia nyingine ya shirika hilo kuwajibika kwa jamii, kuwa ni kushughulikia matatizo mbalimbali ya wateja wao kwa wakati na kuachana na utaratibu wa kufanya kazi kwa mazoea.

Kwa upande wake, akiwasilisha taarifa ya kazi ya ofisi yake kwa Naibu Waziri, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu, ametaja baadhi ya mafanikio ambayo Ofisi hiyo imepata kuwa ni pamoja na kukusanya mapato kwa zaidi ya asilimia 100 pamoja na kubadilisha mita ndogo zote, zilizokuwa zikitumika zamani na kufunga LUKU.

Naibu Waziri Mgalu, ametembelea Ofisi za TANESCO Dodoma kwa lengo la kuzungumza na wafanyakazi na kujitambulisha kwao.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma (hawapo pichani), alipowatembelea kwa lengo la kujitambulisha kwao na kueleza vipaumbele vyake vya kazi.


Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu (kushoto), akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi yake kwa Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), wakati Naibu Waziri alipotembelea Ofisi hiyo na kuzungumza na viongozi.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyesimama) akizungumza na viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, alipotembelea Ofisi hizo leo Oktoba 17, 2017.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dodoma, alipotembelea Ofisi hizo na kuzungumza na viongozi wake (hawapo pichani). Kushoto ni Meneja wa Shirika hilo Mkoa wa Dodoma, Zakayo Temu.Baadhi ya viongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakimpokea Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye nguo nyeusi) alipowasili katika Ofisi hizo kuzungumza na viongozi wake


Mahakama Kuu Kenya yaondoa zuio la maandamano

Mahakama Kuu nchini Kenya imeondoa kwa muda zuio la maandamano ya muungano wa vyama vya upinzani nchini humo (NASA) katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu lililowekwa na Serikali.

Zuio hilo la kufanya maandamano katika miji hiyo ya kibiashara ilitolewa wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Kenya, Fredi Matiangi ili kuweza kuondokana na uharibifu ambao ungeweza kujitokeza, lakini zuio hilo limeondolewa baada ofisa mtendaji mkuu wa Nasa, Norman Magaya kufungua kesi mahakamani.

Aidha, Jaji John Mativo ametoa zuio la kukamatwa kwa Magaya kutokana na maandamano ya Nasa hadi kesi yake itakaposikilizwa na kutolewa hukumu.

Hata hivyo, Katika kesi hiyo, Magaya amemfungulia kesi Inspekta Jenerali wa Polisi, Joseph Boinnet, Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, Keriako Tobiko na Kaimu  Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i kwa kuzuia maandamano dhidi ya tume huru ya uchaguzi IEBC

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemaliza ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama uliofanyika Kitaifa mkoani Kilimanjaro na kurejea Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kufungua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo Kitaifa yamefanyika mkoani Kilimanjaro.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Mambo Ndani Mh Mwigulu Nchemba katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kufungua maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo Kitaifa yamefanyika mkoani Kilimanjaro.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais


Waziri Mkuu awaonya mawaziriWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya mawaziri na kuwataka watumie madaraka yao kwa manufaa ya Taifa na kamwe wasiyatumie kama fursa ya kujitajirisha wao binafsi.

Kassim Majaliwa amesema hayo leo Oktoba 16, 2017 alipozungumza na baadhi ya Mawaziri, Manaibu na Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

Aidha Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza kwamba amewateua ili wafanye kazi na kamwe wasitumie madaraka waliyopewa kwa maslahi yao binafsi.

“Madaraka haya ya Uwaziri si fursa ya kujipatia utajiri, tunatakiwa tufanye kazi kwa weledi, uadilifu, bidii na uaminifu mkubwa ili kuondoa kero za wananchi kwa wakati.”

Waziri Mkuu amesema Mawaziri hao wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021. Pia utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri hao wakapunguze urasimu katika utekelezaji wa malengo ya Serikali kwa sababu wananchi wanahitaji kuhudumiwa kwa wakati 

Mawaziri waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Bw. Suileiman Jaffo pamoja na Manaibu wake Bw. Joseph Kandege na Bw. George Kakunda, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile.

Wengine ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu wake Bw. Jumaa Aweso, Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijabe na Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Bw. Josephat Hasunga, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Naibu wake Bw. William Ole Nasha, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw. Abdallah Ulega pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo