ADDS

ADDS

Tuesday, 22 August 2017

DK.KIKWETE SIJAANZA KILIMO/UFUGAJI BAADA YA KUSTAAFU WATAKAOSUBIRI KUANZA UZEENI WAMECHELEWA

 Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete,akionyesha Kilimo cha mahindi ya njano kwa ajili ya kuongeza rutuba kwa ng'ombe .
 Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete,akionyesha eneo analohifadhi majani ya malisho ng'ombe .Rais mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete,akionyesha baadhi ya mifugo yake na kueleza umuhimu wa Ufugaji wa kisasa ili kupata maziwa ya kutosha na ng'ombe kuwa na afya.(Picha na Mwamvua Mwinyi )

Na Mwamvua Mwinyi,Msoga

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne ,Dk.Jakaya Kikwete ,amesema ameanza kufanya kilimo na ufugaji tangu mwaka 1988/1989 hivyo anaetegemea kufanya shughuli hizo baada ya ustaafu amechelea .

Aidha ameeleza matarajio yake kwa sasa ni kuongeza mifugo ya ng'ombe majike wa maziwa 500 watakaoweza kutoa maziwa lita 2,000 hadi 4,000 kwa siku .

Katika hatua nyingine dk.Kikwete amesema endapo wafugaji watazingati ufugaji wa kisasa kwa kuwa na maji ya kutosha ,malisho ,kinga ya chanjo na kuogeshwa ni lazima watanufaika kwa kupata soko la uhakika hasa maziwa 

Akizungumza baada ya kutembelewa na baadhi ya waandishi wa habari mkoani Pwani ,shambani kwake Msoga ,Kikwete alisema anaetarajia kufuga na kulima akifika miaka 67 atapata changamoto kwani sio kazi rahisi .

"Ukishazeeka ndio uanze kufuga ama kulima ,ahaahha haahah (alicheka) itakuwa ngumu sana ,kwani pia hata miaka ya kuishi hatujui " alisema dk.Kikwete .

Alifafanua ,endapo atafikia malengo aliyojiwekea ataweza kuanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza siagi .

Alisema kwasasa anang'ombe zaidi ya 400 mchanganyiko ambapo 46 ndio wanakamuliwa maziwa na kutoa lita 400 kwa siku na hununuliwa yote .

Alieleza maziwa yana soko kama utamtunza ng'ombe hivyo kutokana na ufugaji anaoufanya anauhakika atafikia adhma yake .

Alielezea kuwa,kwa kufuata ufugaji wa kitaalamu amelima hekari 30 za mahindi ya njano kati ya hekari 800 alizonazo ambayo husaidia virutubisho kwa ng'ombe ambapo wameshavuna hekari nne na wanaendelea kuvuna .

Dk.Kikwete alisema ,anatarajia pia kulima majani ya malisho zaidi hekari 200 zaidi ili zitosheleze mahitaji.

"Nilianza kufuga ng'ombe 20 kule Bagamoyo wakati nikiwa waziri baadae nikawahamishia Msoga na wameendelea kuongezeka " alisema dk.Kikwete .

Alibainisha ,miaka miwili iliyopita wafugaji hususan wa Msoga walipata hasara ya mifugo yao kufa kwa wingi kutokana na ukame .

Dk.Kikwete ,alisema yeye alibahatika ,hakuna hata mfugo wake uliokufa kutokana na akiba aliyojiwekea ya malisho na maji .

Kuhusu kilimo cha mananasi alisema alianza mwaka 1989 .

"Mananasi huvunwa baada ya  miezi 18 tangu kupandwa "

Dk.Kikwete alisema ,shamba lake lina ukubwa wa hekari 200 ambapo hekar 64 ndizo zimelimwa .

Alisema wakulima wa mananasi wana changamoto ya maji ya umwagiliaji ,wakipata maji wataweza kuvuna wakati wowote .

Mstaafu huyo alisema ,wanahitaji dola mil.15 katika mradi wa maji ya umwagiliaji kwani maji yapo mbali WAMI.

Alisema ametumia umaarufu wake na kuweka mitego yote lakini bado hajafanikiwa ila ipo siku watafanikiwa kupata mradi huo .

Baadhi ya wakazi waliopata kibarua cha kuvuna mahindi ya njano kwenye shamba la dk.Kikwete wamemshukuru kwa kuwapatia ajira .

Walisema ,wameweza kujiendesha na maisha yao ya nyumbani ikiwemo watafutia watoto wao mahitaji ya kielimu .


Monday, 21 August 2017

MJENGONI CLASSIC BAND WANG'ARA KWENYE MASHINDANO YA NYAMA CHOMA FESTIVAL MERERANI

Mjengoni classic Band wakiwa wanawantumbuiza katika mashindano ya nyamachioma festival yaliyoandaliwa na Kampuni ya Geen Plan iliyopo mji mdogo wa Mererani ambapo mashindano hayo  yamefanyika katika hotel ya Mazubu Grand Hotel.Picha na Vero Ignatus Blog.Ktibu tawala wa wilaya ya Simanjiro Zuena Omary akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa WA Wilaya hiyo Jenald Lama .wakati huo picha inayofiata anaonekana mkurugenzi wa Mazubu Grand Hotel akibadilishana mawazo na Katibu Tawala.
Muandaaji wa mashindano ya nyamachoma Festival bi.Grace Mmari akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria pamoja na washiriki wa mashindano hating. picha na Vero Ignatus Blog.
Mkurugenzi waWilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi akizungumza na Wageni waalikwa katika mashindano ya Nyamachoma Festival yaliyofanyika mji mdogo wa Mererani katika  mkiwanja cha Nasibu Grand Hotel. 

Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro Zuena Omary ambae alimuwakilisha mkuu wa wilaya Hiyo akizungumza katika usiku wa mashindano y'a kumtafuta mchoma nyama Nora. picha name Vero Ignatus Blog. 
Mkurugenzi wa Mazubu Grand Hotel ndugu Elias Kipuni akiwa anafuatilia shughuli zinvyoondelea.Picha na  Vero Ignatus Blog. 
Mmiliki wa mjengoni club ambae  pia ni mkurugenzi wa Mjengoni Classic Band ndugu John Mdenye. Picha na Vero Ignatus Blog 
Wageni mbalimbali wakiwa katika shughuli hiyo ya mashindano ya Nyamachoma Festival iliyofanyoka katika Mazubu Grand Hotel. picha na Vero Ignatus Blog. 
 
Zoezi la ukaguzi wa jiko la uchomaji nyama Pamoja na uonjaji wa nyama likiendelea kwa kuongozwa na mgeni rasmi Zuena Omary pamoja na Mkurugenzi  Yefred Myenzi. Picha na Vero Ignatus Blog
 Mkurugenzi wa wilaya ya Simanjiro akizungumza kabla ya kutangazwa kwa washindi. picha na Vero Ignatus Blog.

Mshindi wa Kwanza katika shindano la Nyamachoma Festival pichani ni Meneja wa Mazubu Grand Hotel James Mongella akipokea Cheti kutoka kwa mgeni rasmi Zuena Omary. Picha na Vero Ignatus Blog.

Mshindi wa pili wa shindano la Nyamachoma Festival Given Mlay akipokea Cheti kutoka kwa mgeni rasmi Zuena Omary. picks na Vero Ignatus Blog. 
Mjengoni Classic Band wakiendelea kutoa burudani baada ya washidi kukabidhiwa zawadi zao. picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus .Manyara.

Mashindano za nyama choma yamefanyika kwa mara za kwanza mji mdogo wa Mererani wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara katika hoteli ya Mazubu Grand Hotel ambapo iliwashirikisha wachoma nyama wa mji huo kwa lengo la kukuza na kuimarisha biashara  hiyo mjini hapo

Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa mkuu wa wilaya za simanjiro ambapo aliwakilishwa na katibu tawala wa wilaya hiyo  wakiwepo viongozi mbalimbali wa serikali na wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya mkoa huo.

Akizungumza kuhusiana na mashindano hayo katibu tawala wilaya ya Manyara   Zuena Omary ambae alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Manyara amesema kuwa washiriki wote wamefanya vizuri kila mmoja amejifunza kwa mwenzake ,Pamoja na yote mshindi lazima apatikane

Kwa upande wa kunogesha shughuli hiyo burudani ilitolewa mwanzo mwisho na Bendi  kutoka Jijini Arusha  ijukikanayo Kama Mjengoni Classic Band 


Aliyeibuka kidedea katika mashindano hayo ni Mazubu Grand Hotel.ambae alikuwa mshindi wa kwanza alipatiwa sh. 500,000 pamoja na cheti  namba mbili ni Given Mlay cheti na creti 6 za bia (aka mzee wa mbuzi ) na mshindi wa tatu ni Songambele bar walipewa cheti na kreti 2 za bia.

Serikali Yakanusha Kumpa Siku 7 Tundu Lissu Kuomba MsamahaSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba imempa siku 7 Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Mh. Tundu Lissu kuomba radhi kwa kupotosha umma

Kwenye ukurasa wa twitter wa msemaji wa serikali ametoa taarifa akisema kuwa taarifa hizo si za kweli, kwani hata mtu aliyetumika kuandika hiyo taarifa yupo msibani.

"Umma unaarifiwa kuwa baada ya tamko la jana Serikali haijatoa tamko lolote tena.Uzushi unaosambazwa mitandaoni  Jumapili hii  ni wa kupuuzwa, taarifa inayosambazwa ni ya uongo kwa kuwa hata Dkt. Abbas anayetajwa kusaini bado yuko likizo ya kufiwa. Hatua kali zitachukuliwa", aliandika twitter ya Msemaji wa serikali.

Hapo awali kulikuwa na taarifa iliyosambaa ikionyesha imetoka serikalini, ikimtaka Mh. Tundu Lissu kuomba radhi huku ikimpa siku 7 tu za kufanya hivyo

Mali za Lugumi Kupigwa Mnada


Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd iliyotajwa katika sakata la zabuni ya Sh34 bilioni ya kuweka mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole ya Jeshi la Polisi, iko hatarini kupoteza mali zake kutokana na kudaiwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mnada wa maghorofa hayo utafanywa na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, kwa niaba ya TRA Mkoa wa Ilala. Maghorofa hayo yapo maeneo tofauti jijini Dar es Salaam; moja Mtaa wa Mazengo, Upanga na mawili yako Mbweni JKT wilayani Kinondoni.

Kuuzwa kwa maghorofa hayo kumetangazwa jana katika gazeti la Serikali la Sunday News, tangazo hilo likieleza kwamba ghorofa la Upanga linafaa kwa ofisi wakati yale ya Mbweni JKT yanafaa kwa makazi.

Mkurugenzi mtendaji wa Yono, Scolastica Kevela alisema mnada huo utafanyika Septemba 9, kuanzia saa 4:30 asubuhi kwenye maeneo yalipo maghorofa hayo.

Kevela alisema Lugumi Enterprises imeshindwa kulipa kodi ya TRA kwa wakati ndiyo maana wakapewa kazi ya kuuza majengo hayo.

Mkurugenzi huyo alikataa kutaja kiasi ambacho Lugumi anadaiwa na TRA pamoja na thamani ya maghorofa hayo.

Kevela alitoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, masharti ya mnada ni kulipa asilimia 25 ya thamani ya bei kwa atakayefanikiwa kuyanunua maghorofa hayo.

Kiasi kilichobaki kitatakiwa kulipwa ndani ya siku 14, tangu siku ya mnada na kwamba atakayeshindwa kulipa katika kipindi hicho hatarudishiwa fedha alizotoa na mnada utafanyika kwa mara nyingine.

Ukaguzi wa nyumba hizo unatakiwa kufanywa siku 10 kabla ya siku ya mnada.

Akizungumzia hilo, mkurugenzi wa huduma na elimu ya mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema Lugumi inadaiwa kodi za aina mbalimbali zinazotokana na mapato yake.

Lugumi ilikuwa gumzo mwaka jana baada ya taarifa ya CAG kuonyesha kuwa ililipwa zaidi ya asilimia 90 ya fedha za zabuni kwa ajili ya kuweka vifaa hivyo katika vituo 138, lakini hadi wakati wa ukaguzi ilikuwa imeweka katika vituo 14 tu.

Taarifa hiyo ilifika bungeni na kuundwa kamati ndogo ambayo ilichunguza na kuwasilisha taarifa. 

Sunday, 20 August 2017

Manispaa ya Sumbawanga watakiwa kujenga vituo vya afya zaidi

Waziri wa Afya Ummy Mealimu akiongea na mmoja wa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye kituo cha afya cha Mazwi kilichopo Manispaa ya Sumbawanga

Waziri Ummy mwalimu akimuuliza mmoja wa mama aliyefika kupata matibabu ya nje kwenye kituo cha afya cha Mazwi kama amefika muda mrefu na hajapata matibabu,waziri huyo yupo mkoani Rukwa kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kukagua huduma za afya zinazotolewa kwenye vituo vya huduma nchini
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na mama mjamzito aliyelazwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa.Waziri Ummy alisisitiza watoa huduma kuhakikisha awatoa huduma wa afya wanajitahidi kuepusha vifo vianavyoweka kuepukika kutokana na uzazi

Waziri wa Afya akiongea na akina mama wajawazito waliolazwa kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Rukwa
Waziri akimjulia hali mama mjamzito aliyelezwa kwenye kituo cha afya katika manispaa ya SumbawangaMoja ya kipaumbele cha wizara ya afya katika kuokoa vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua ni Damu Salama,Waziri wa Afya akiangalia akikagua bank ya damu salama iliyopo kwenye hospitali ya rufaa ya MkoaBaadhi ya watumishi wa sekta ya afya wa manispaa na mkoa wa Rukwa wakimsikiliza waziri wa afya(hayupo pichani) wakati wa kuongea na watumishi hao ambao walitoa changamoto zao zinazowakabili katika utendaji kazi zao za kila siku 
Mmoja wa watumishi wa kada ya afya akiulizwa swali wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara ya waziri huyo.Waziri wa afya yupo mkoani Rukwa kikazi ambapo aliweza kutembelea vituo vya afya na hospitali zilizopo wilaya za Nkasi,Kalambo ,Manispaa ya Sumbawanga na hospitali ya Mkoa ya Rukwa(picha zote na Wizara ya afya)


Rukwa 


Manispaa ya Sumbawanga imeelekezwa kuongeza kujenga vituo vya afya kulingana na jiografia ilivyo ili hospitali ya Rufaa ya mkoa ibaki kutoa huduma za kibingwa mkoani hapa.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na watumishi wa sekta ya afya wa Mkoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wakati wa majumuisho ya ziara ya siku mbili ya kikazi

Alisema Serikali inaboresha hospitali za Rufaa za Mkoa kwa ajili ya huduma za kibingwa hivyo hospitali hizo ziweze hutoa huduma za kimatibabu ya kibingwa hasa kwa watu wenye huitaji huo,”lakini wananchi wanapaswa kufuata utaratibu wa sera unavyosema kwenda kupata matibabu katika hospitali za Rufaa ni lazima mgonjwa aandikiwe rufaa na sio kila mtu anaenda moja kwa moja kwenye hospitali hizo”

Waziri Ummy alisema kulingana na kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini ni vyema na mkoa kwa ujumla ni vyema kujenga vituo hivyo vitakavyoweza kutoa huduma kwa wananchi waliopo maeneo husika kuliko kujenga hospitali ya Wilaya ambayo wananchi waliopo maeneo ya mbali wapate huduma za afya huko huko karibu na huduma hizo ziwe bora.

“Fanyeni maamuzi yenye manufaa kwa wananchi wa wilaya yenu ili muwasogezee huduma watu wenu,alisema kwa Wilaya ya Nkasi wao wanatakiwa kujenga hospitali ya wilaya ya serikali ambapo Wizara yake itasaidia kutoa milioni 350 kati ya 650 ambayo itajenga wodi ya wazazi,maabara pamoja na nyumba moja ya mtumishi

Aidha,kwa Wilaya ya Kalambo alisema wanatakiwa kuboresha kituo cha afya Bimbwi kwa kujenga chumba cha dharura cha upasuaji ambacho kitasaidia kumtoa mtoto salama.

Hata hivyo waziri Ummy alizitaka hospitali za DDH na CDH ambazo zinamilikiwa na mashirika ya dini kufanya kazi kwa kuzingatia sera na miongozo ya afya na kufanya kazi kwa pamoja na Serikali kwani hospitali hizo zimeingia ubia na serikali hivyo watoe huduma kama inavyoelekezwa na serikali ikiwemo huduma bure kwa akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano pamoja na wzee wasio na uwezo

Kwa upande wa watumishi Waziri huyo alikiri Rukwa kuwa na idadi ndogo ya watumishi wa kada ya afya hivyo ameahidi katika kibali kijacho cha ajira atawapa kipaumbele “ila nawataka mtoe mahitaji sahihi ili tuweze kuondoa changamoto hizo, ila kwa sasa mnaweza kuwatawanya baadhi ya watumishi kwenye uhaba zaidi ili muweze kuongeza nguvu kwenye vituo vya kutolea huduma ili kuokoa maisha ya watanzania”

Waziri wa Afya aliwasihi watumishi wa sekta yake kuacha kufanya kazi kwa mazoea,wanatakiwa kujituma na kuwa waadilifu kwani mambo yamebadilika hivyo kuweka mifumo rahisi nay a kirafiki kwa wananchi ya kutoa malalamiko

“Wakuu wa Wilaya kama kuna Daktari ama Muuguzi amekosa tuleteeni watumishi hao tuwapeleke kwenye mabaraza ya kitaaluma ,na hivi sasa tumeanza kuwafutia leseni baadhui ya watumishi wa kada ya afya ambao hawatotimiza wajibu wao katika sehemu ya kazi

Wanafunzi 22 Milambo Wafikishwa Mahakamani


Wanafunzi  22 wa Shule ya Sekondari ya Milambo ya mkoani Tabora wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashitaka 12 matano yakiwa ya kujeruhi na saba ya kuharibu mali, ambapo mmoja amesomewa tuhuma zake akiwa amelazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.

Upande wa serikali ukiongozwa na wakili Iddy Mgeni ulidai mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Tabora, Emanuel Ngingwana kuwa washitakiwa walitenda makosa hayo 12 Agosti 14 mwaka huu majira ya usiku.

Wakili Mgeni alidai katika mashitaka ya kwanza hadi ya tano kuwa siku hiyo, watuhumiwa kwa pamoja waliwashambulia na kuwajeruhi wakazi watano wa kata ya Chemchem kinyume na kifungu namba 241 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Aliwataja walioshambuliwa na kujeruhiwa kuwa ni Juma Farahani, Iman Elias, Salehe Ally na Ahmed Haruna wakazi wa mtaa wa Uhuru na Hamza Jafary mkazi wa mtaa wa Dawa.

Katika mashitaka ya sita na saba, walidaiwa siku hiyo watuhumiwa kwa pamoja waliharibu mali ya Shaban Farahani chini ya kifungu namba 326 (1) cha sheria ya makosa ya jinai huku wakijua kwamba ni kosa.

Upande wa mashitaka ulidai katika mashitaka ya nane kuwa watuhumiwa waliharibu vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 440,000 zikiwemo spika mbili, dirisha moja na simu mbili mali ya Hemed Rajab.

Wanafunzi wa sekondari ya Milambo wanatuhumiwa kuvamia nyumba ya kulala wageni iitwayo Nyakitonto na kuharibu taa tano na bango vyote vikiwa na thamani ya Sh 750,000 mali ya Asia Maulid wakati katika shitaka la 10 ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao waliharibu turubai mbili, milango miwili, sahani na vikombe, dirisha mbili, juzuu boksi tatu zinazotumiwa na waumini wa dini ya kiislam mali ya Ally Juma, yote ikiwa na thamani ya Sh 4,278,000.

Watuhumiwa wote walikana na mahakama ilisema dhamana ipo wazi na walitakiwa wadhamini wawili kwa kila mtuhumiwa mmoja ambao watasaini mkataba wa ahadi ya Sh milioni mbili kila mmoja na shauri hilo limeahirishwa hadi Agosti 31, 2017.

ZIARA YA RAIS DK.SHEIN WILAYA YA MAGHARIBI A


DSC_9755
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika viwanja vya Skuli ya msingi Kihinani Jimbo la Mfenesini kuweka jiwe la msingi Jengo jipya la Skuli hiyo leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
DSC_9852
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akifungua pazia kama ishara ya   kuweka jiwe la Msingi Jengo jipya la Skuli ya msingi Kihinani leo akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
DSC_9886
Baadhi ya wananchi na Wazee wa Wanafunzi wa Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa Jengo jipya la Skuli hiyo leo iliyowekwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani )akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,
DSC_9918
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Kihinani walipokuwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) alipokuwa akizungumza na Wanafunzi hao pamoja na Wazee wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli hiyo leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo
DSC_9919
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Wananchi,Wazee na Wanafunzi   wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud
DSC_9933
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Wananchi,Wazee na Wanafunzi   wakati wa Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,
DSC_9964
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipofika kutembelea Ofisi ya Walimu mara baada ya kuweka  Jiwe la Msingi Jengo jipya katika Skuli ya msingi Kihinani jimbo la Mfenesini  leo,akiwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma na (kushoto) Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo  Bi.Mafunda Juma Khamis,
DSC_0022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” Nd,Mwinyiussi (katikati) wakati alipofika kutembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,(kulia) Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud Talib,
DSC_0036
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipofuatana na Viongozi mbali mbali  wakati alipofika kutembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo,
DSC_0073
Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe.Salama Aboud Talib alipokuwa akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) wakati alipotembelea Mradi wa Visima vya Maji Safi na salama katika Shehia ya Bumbwisudi leo alipofanya ziara yake katika  Wilaya ya Magharibi”A” kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo.Picha na Ikulu.20/08/2017

WAKINA BABA WATAKIWA KUTOA TAARIFA ZA MAENDELEO YA WATOTO KWA WENZA WAO

Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu akitoa elimu juu ya wajibu wa wazazi wa kiume katika malezi ya mtoto katika kikao cha wazazi kilichofanyika jana kwenye shule ya Saint Monica iliyopo jijini Arusha (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 Mwalimu Mkuu wa shule ya Saint Monica Sister Pauline Etyang Nasike akitoa shukrani zake kwa Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mara baada ya Mkuu wa kitengo hicho kutoa elimu kwa wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo juu ya malezi ya watoto wao. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Wazazi wa wanafunzi wa shule ya Saint Monica waliohudhuria kikao hicho wakionekana wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu alipokuwa akitoa elimu juu ya umuhimu wa wazazi wa kiume kuwa karibu na watoto wao. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Kumekuwa na tabia iliyojengeka kwa baadhi ya jamii zetu kwamba taarifa za maendeleo ya masomo au ukatili na unyanyasaji wa watoto lazima zitoke kwa mzazi wa kike kwenda kwa mzazi wa kiume.

kufuatia hali hiyo Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto mkoani hapa kimetoa ushauri kwa wazazi wa kiume kurudi nyumbani mapema pia kuwa na muda wa kuongea au kukaa na watoto wao na kuwa wa kwanza kutoa taarifa za maendeleo ya watoto kwa wake zao badala ya hali hiyo kufanywa na wenza wao pekee kama ilivyo sasa.

Akizungumza jana Jumamosi katika kikao cha wazazi wa wanafunzi ya Saint Monica iliyopo maeneo ya Moshono jijini hapa, Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Happyness Temu alisema kwamba, imekuwa kawaida kwa baadhi ya wazazi wa kiume kutokuwa na muda wa kukaa na watoto kwa kile tunachokiita uwajibikaji katika utafutaji na kushindwa kujua matatizo ya watoto wao.

Alisema mara nyingi wazazi wengi wa kiume wamekuwa wakijiweka pembeni katika kuwasikiliza  watoto wao  kwa masuala madogo madogo na kudhani kwamba wenzi wao pekee ndio wanapaswa kujua masuala hayo na kufikiri wao huwa wanatatua shida kubwa kama vile chakula, mavazi na ulipaji wa ada.

Alisema vitendo vya ukatili na unyanyasaji hasa ubakaji na ulawiti vinavyowakumba watoto vinatokana na wazazi kutokuwa na muda wa kuongea na watoto wao na hivyo kusababisha watoto hao kushindwa kutoa duku duku lao kwa watu wao wa karibu katika wakati sahihi.

Alisema wakati umefika sasa kwa baadhi ya wazazi wa kiume pamoja na kutimiza mahitaji mbalimbali ya nyumbani lakini wanatakiwa kutenga muda wa kukaa na watoto, kuwadadisi mambo mbalimbali, kuwasikiliza lakini pia kufuatilia nyendo zao badala ya kuwaachia wazazi wa kike pekee.

Alisema kama wazazi wote watasaidiana katika malezi ya watoto hasa kuwa nao karibu na kuwasikiliza itasaidia kwa kiasi kikubwa kugundua maendeleo yao lakini pia matatizo yao ambayo pengine walishindwa kuyaeleza kwa watu wengine.

Wakichangia katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na wazazi 580 miongoni mwa wazazi waliohudhuria kikao hicho Bw. Felix Mwetha alisema amevutiwa na elimu hiyo iliyotolewa na kitengo hicho lakini pia aliwataka wazazi wenzake wawe wanafanya maombi ili watoto wao wasikumbwe na vitendo hivyo.

Huku Bw. Mhando Bamara alisema kutokana na umuhimu wa elimu hiyo alilishauri jeshi la Polisi kuandaa programu maalum ambayo itatengeneza vipindi vya uelimishaji kupitia kitengo hicho ili watu wengi wafahamu badala ya kuishia kwenye vikao pekee.

Naye Sister Pauline Etyang Nasike ambaye ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambayo inamilikiwa na Augustinian Missionary Sisters alilishukuru Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto kwa kutoa elimu kwa wazazi pamoja na walezi lakini pia aliahidi kuandaa kikao kingine kitakachotoa fursa kwa kitengo hicho kutoa elimu kwa wanafunzi.

Imekuwa kawaida wanafunzi hasa wa shule za msingi kujitokeza kwa wingi na kuelezea matatizo yao mara baada ya Kitengo hicho cha Dawati la Jinsia na Watoto kutembelea shule hizo na kutoa elimu juu ya masuala ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji, hali inayojidhihirisha baadhi ya wazazi hawatoi nafasi ya kuwasikiliza watoto wao mara kwa mara. 

VILIO NA SIMANZI ZATAWALA KATIKA UZINDUZI WA MNARA WA KUMBUKUMBU YA MAJINA YA WANAFUNZI WA LUCKY VICENT32,WALIMU2,NA DEREVA 1 WALIOFARIKI KATIKA AJALI


Wanafunzi wa Shule ya Lucky Visent wakiwa katika simanzi  Katina uzinduzi WA mnara wa kumbukumbu ya wenzao 32 waliofariki kwa ajali waalimu 2 Pamoja na dereva1.picha na Vero Ignatus Blog.
Mbunge wa Singinda Kaskazini Lazaro Nyalandu, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mnara wa kumbukumbu ya wanafunzi shule ya Lucky Vicente waliofariki kwa ajali mei 6 2017 eneo la Rotia wilaya ya Karatu mkoani Arusha. picha na Vero Ignatus Blog. 
Wanafunzi Doreen, Sharia, Pamoja na  Wilson wakiweka shada katika mnara kuwakumbuka wenzao waliopata nao ajali, wao 3 walinusurika .Picha na Vero Ignatus Blog. 
Wanafunzi wa Lucky Vicent wakiwa wamemzingira mwanafunzi mwenzao Doreen Mara baada ya kuweka shada la maua,akiwa chini ya uangalizi wa Dr. Steve Mayer.  Picha na Vero Ignatus Blog. 
Wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya Lucky Vicent wakiweka Masada pamoja na kuwasha mishumaa kumbukumbu kwa wenzao waliopoteza Marsha. Picha na Vero Ignatus blog. 
Waalimu akiweka mashada