Top Menu

HABARI MPYA

1/20/2019 06:18:00 pm
12/04/2018 09:06:00 am

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA KONGAMANO LA MWAKA LA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NCHINI

11/27/2018 04:25:00 pm
 Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Sera, Bunge, kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu Mhe Jenista Joachim Mhagama, akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alipoenda kwajili ya uzinduzi wa Uzinduzi wa Jengo jipya la kisasa la Maktaba ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii 

Na. VERO IGNATUS, ARUMERU

Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Sera, Bunge, kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu Mhe Jenista Joachim Mhagama leo Tarehe 27/11/2018 amewaongoza wananchi wa Wilaya ya Arumeru katika Uzinduzi wa Jengo jipya la kisasa la Maktaba ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru

Mara baada ya kuzindua jengo hilo mhe Mhagama baadae alishiriki Uzinduzi wa Kongamano na mkutano mkuu wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii ambao kitaifa umefanyika katika Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arumeru na kuhudhuria na zaidi ya maafisa Maendeleo ya Jamii mia tatu kutoka sehemu mbalimbali nchini

 Pamoja na hayo Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii iliwasilishwa na katibu mkuu anaeshughulikia masuala ya ustawi wa Jamii Dkt. Jingu, uku Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akiwamwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo

Awali akizundua Maktaba katika Taasisi ya Maendeleo ya Tengeru Mhe Mhagama ameutaka Uongozi wa Taasisi pamoja na wafanyakazi na wanafunzi kuitumia vizuri Maktaba hiyo katika kuongeza Kiwango Cha taaluma Kwa wanafunzi ambao Serikali inawahitaji katika kuunganisha jamii na uchumi wa kati unaochochewa na Kasi ya uanzishwa wa viwanda nchi Tanzania

Akiwa katika Kongamano la wataalamu wa Maendeleo ya Jamii Mhe Mhagama amesema maafisa Maendeleo ya Jamii nchi wana nafasi Kubwa ya kuisadia serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata Maendeleo ya kweli yanayotokana na viwanda, Kilimo na ufugaji 

Amesisitiza kuwa  amesema haiwezekani wananchi waendelee kuwa maskini wakati nchi imeweka mifumo madhubuti ya kuhakikisha Jamii inaondokana na umasikini kupitia miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Tasaf 

Mhe. Mhagama ametoa maelekezo ya kuzitaka kila halmashauri nchini ziwe zinatenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani katika kuwawezesha vijana,wanawake pamoja na watu wenye ulemavu katika kuwaletea Maendeleo.

Kabla ya kufungua kongamano hilo Mhe Mhagama alipata fursa ya kutembelea Mabanda ya maonyesho ya kazi mbalimbali za wajasirimali ambao wamewezeshwa na serikali kupitia halmashauri na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii ambapo amewapongeza wajasirimali hao na kuwasisitiza kurejesha Kwa wakati fedha wanazokopeshwa ili ziweze kuwasiadia wengine. 
Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Sera, Bunge, kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu Mhe Jenista Joachim Mhagama, akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakiwa katika Uzinduzi wa Kongamano na mkutano mkuu wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii ambao kitaifa umefanyika katika Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arumeru. 
 Baadhi ya Maofisa wa maendeleo ya jamii waliohudhuria Uzinduzi wa Kongamano na mkutano mkuu wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii ambao kitaifa umefanyika katika Mkoa wa Arusha Wilaya ya Arumeru na kuhudhuria na zaidi ya maafisa Maendeleo ya Jamii mia tatu kutoka sehemu mbalimbali nchini


WATATU WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

11/26/2018 01:52:00 pm
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga 

Na. VERO IGNATUS, MANYARA

Jeshi la polisi Mkoani Manyara, linawashikilia watu watatu kwa kudaiwa kukutwa na nyara za serikali ikiwemo vipande vitatu vya jino la Tembo. 

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga akizungumza jana alisema watu hao walikamatwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Top In One iliyopo mtaa wa Oysterbay mjini Babati. 

Kamanda Senga aliwataja watu hao kuwa ni Anthony Paschal (28) na Juma Ingi wote wakazi wa Endasak wilayani Hanang' na Tluway Gosi mkazi wa Simbay wilayani Hanang'. 

Alisema mbinu waliyotumia ni kuficha vipande hivyo ndani ya mfuko wa sulphate kisha kuweka chini ya uvungu wa kitanda ili wakaiuze. 

Alisema baada ya timu ya makachero kwa kushirikiana na maofisa wanyamapori wa shirika la hifadhi ya Taifa ya Tarangire kupata taarifa walifika eneo hilo na kuwakamata watu hao. 

"Watuhumiwa hao wote wanashikiliwa na polisi na tunaendelea na upelelezi kabla ya kuwafikisha mahakama kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabili," alisema kamanda Senga. 

Katika tukio lingine, kamanda Senga alisema watu watatu wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na lita 40 za pombe haramu ya moshi maarufu kama gongo. 

Alisema watu walikamatwa juzi kwenye kijiji cha Kazamoyo kata ya Kisangaji wilayani Babati wakiwa wamebeba kwenye pikipiki aina ya Skygo yenye namba za usajili MC 970. 

Aliwataja watu hao kuwa ni Daniel Hewasi (47) mkazi wa Magugu, Hussein Athuman (50) mkazi wa kijiji cha Kazaroho na Idd Hamis (35) mkazi wa kijiji cha Magugu. 

Alisema watu hao walikuwa wamebeba pombe hiyo haramu kwenye pikipiki hiyo wakiwa wamehifadhi kwenye madumu mawili ya lita 20 kila moja.

Alisema pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba pombe hiyo haramu ni mali ya Idd Hamis na lengo lao ilikuwa ni kwenda kuuza ili kujipatia kipato. 

Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha mahakamani wakajibu mashtaka yanaoyowakabili.

MWISHO

ZAIDI YA MADEREVA 1600 WAPATIWA MAFUNZO ARUSHA

11/26/2018 10:00:00 am

Mrakibu wa polisi Joseph   Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  mkoani Arusha 

Na. Vero Ignatus, Arusha


Madereva wa mabai ya kubebea abiria katika mkoa wa Arusha wamepatiwa mafunzo ilihali wengine waki3ndelea na mafunzo


Akizungumza  Mrakibu wa polisi Joseph   Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani  mkoani Arusha amesema lengo kuu ni kuhakikisha kuwa madereva wote wanapata elimu na wanatoa huduma inayoendana na elimu waliyoipata


Tangia kuanzishwa kwa mafunzo ya madereva miezi minne iliyopita madereva 1600 wamehitimu mafunzo wa magari ya kubeba abiria  (PSV)kupitia chuo cha Veta pamoja na chuo rafiki wa NIT cha Moden driving vyote vya mkoa wa Arusha.


 "Pamoja na mapambano hayo ya ajali za barabarani ni  lazima kuhakikisha kuwa wapo madereva wenye weledi" alisema Bukombe. 


Aidha amesema mafunzo haya yamesaidia sana kwani mkoa hapo pamekuwa salama bila Ajali  


"Tangia tumeanzisha mafunzo takribani miezi minne iliyopita kwa mkoa wa Arusha tupo salama, na ukikuta ajali imesababishwa na bodaboda na siyo magari ya abiria" alisema Bukombe


Mara baada ya kuona ajali zimeongezeka jeshi la polisi liliendesha ukaguzi wa leseni na kugundua kuwa madereva wengi wana leseni lakini hawana vyeti, kwahiyo yamkini wanazipata leseni kwa njia wanazozijua wao


"Sisi tukasema hawawezi kuendelea na leseni walizonazo badala yake warudi darasani kwenda kusoma ili waweze kupata vyeti"alisema


Akizungumza wimbi  la Magari ya viongozi wa serikali kupata ajali Bukombe amesema hakuna aliye juu ya sheria kwani hata madereva  hao wameshaanza kushughulikiwa

"Mara ya kwanza ulipita tu kama upepo wa kuwasaha ulakini sasa unapoaona kitu kinazidi kuleta shida ule upepo tumeshafutilia mbali na wao wanachukuliwa hatua "alisema


Amesema Jeshi la polisi linafikiria ninamna gani wanaweza kushirikiana na wizara kuhakikisha madereva wao wanawapeleka mafunzoni


Aidha Bukombe ametoa wito kwa madereva wakaidi ambao hawaoni umuhimu wa kuingia darasani, wale ambao wanasubiri waone ninini hatima ya jambo hilo amewashauri kuw ni  vyema wakarudi darasani kujisomea wasisibirie matokeo kwani jeshi la poisi hatitawafumbia macho.


Bikombe amesema maelekezo hayo yalipoyolewa na serikali yalikuwa ni kwa minubu wa miezi mitatu ambapo zoezi hilo likikuwa limalizike tarehe 1 novemba 2018, ikaonekana vyuo vilelemewa na maderevya hivyo serikali ikaongeza hadi miezi miwili hivyo litamalizika januari mosi 2019

Ukaguzi wa leseni na vyeti utaendeshwa rasmi januari mosi 2019 hivyo madereva ambao watakutwa hawana leseni na vyeti sheria itafuata mkondo wake. 


WIZARA YA MALIASIALI NA UTALII YAWATOA HOFU WATALII

11/22/2018 05:25:00 pm
.
 Naibu Waziri Wizara ya Mali asili na Utalii  Constatine  Kanyasu

Na. Vero Ignatus Arusha


Siku chache baada ya Benki kuu ya Tanzania kutoa ufafanuzi  Juu  ya Oparesheni ya Ukaguzi wa Maduka ya kubadilishia Fedha za Kigeni Jijini Arusha ,Wizara ya Mali asili na Utalii imejitokeza na kusema Zoezi hilo halijaathiri shughuli za Kitalii


Naibu waziri wa maliasili na Utalii Constatine Kanyasu ameyasema hayo wakati lipotembelea  taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwenye mkutano wake na wafanyakazi wa shirika la hifadhi
za taifa(TANAPA) jijini Arusha na kusema watalii wanaendelea kupata huduma kwani zoezi hilo ni la kawaida na limelenga maslahi ya nchi.


Mara baada ya Mazungumzo hayo Naibu Waziri akiwa nje ya Ukumbi wa Mamlaka hiyo , amezungumza na Wanahabari kisha kugusia suala la oparesheni iliyofanywa na Benki Kuu hivi karibu Jijini hapa.


Ameeleza kuwa zoezi hilo lililovishirikisha vyombo vya dola na
halijaathiri uchumi katika sekta ya fedha za kigeni hasa kwa upande wa
utalii kwa kuwa ni zoezi hilo  la mara moja kuwahusisha  wanajeshi
ambao wanawajibu wa kulinda rasilimali za nchi yao.

'' Wanajeshi hawawezi kuathiri uchumi wa nchi hasa sekta ya utalii kwakuwa wanawajibu wa kulinda rasilimali zetu‘’alisema Kanyasu

Akiongelea suala la migogoro ya Ardhi na mipaka kwa baadhi ya mipaka amesema wizara yake imejipanga kukomesha changamoto hiyo ambayo imekuwa ikitumia fedha nyingi bila kupatiwa ufumbuzi.

Aidha amesema migogoro baina ya Hifadhi na Wananchi,Naibu waziri anasema hakuna mtu ama taasisi inayonufaidika na Migogro hiyo na imekuwa ikichochewa na makundi machache na tayari serikali imekwisha anza kuchukua hatua.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Jumla ya Vijiji mia tatu tisini na mbili vitanufaika na zoezi la upimaji wa matumizi bora ya ardhi lenye lengo la Kupunguza 

Migogoro ambapo tumepanga billion 2.5 kwa miradi midogo midogo kuweza kuweka nguvu kwa wananchi kuondoa misuguano isiyo na lazima ambayo inaathiri kiasi kikubwa shughuli za uhifadhi.Mwisho.

BOT YAFANYA OPARESHENI MAALUMU YA UKAGUZI NA UDHIBITI WA MADUKA YA KUBADILISHIA FEDHA SAMBAMBA NA KUSITISHA UTOAJI LESENI

11/20/2018 06:51:00 pm
Gavana wa Benki Kuu Nchini Tanzania Profesa Florence Luoga akitoa ufafanuzi kuhusiana na ukaguzi na udhibiti wa biashara haramu ya fedha za kigeni na ukiukwaji wa sheria katika kuendesha biashara ya ubadilishaji fedha yaani (Bureau de Change)Picha na Vero Ignatus

Gavana wa Benki Kuu Nchini Tanzania Profesa Florence Luoga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha katika Hotel ya Mount meru .Pcha na Vero Ignatus


Na. Vero Ignatus, Arusha

Benki Kuu ya Tanzania imeendesha operesheni ya kushtukiza ya kukagua maduka ya ubadilishaji fedha(Bureau de Change) na kubaini  baadhi ya maduka bubu yasiyokuwa na  leseni ambayo yalikuwa yakiendesha biashara hiyo kinyume na sheria

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha  Gavana wa Benki kuu nchini profesa Florence Luoga amesema kuwa zoezi hilo liliratibiwa na kitengo cha ukaguzi cha Benki Kuu katika kutekeleza majukumu yake kisheria

Aidha amesema kuwa Operesheni hiyo ni ya tatu kufanyika ambapo uchunguzi wa kina wa miezi sita umebaini kuongezeka kwa biashara za kubadilisha fedha kinyume cha sheria na kukua kwa biashara haramu ya fedha za kigeni, utakatishaji fedha, hususani kupitia maduka ya kubadilisha fedha

Aidha Luoga amesema kuwa BOT imechukua hatua kusitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha kwa takribani miezi mitatu, na wale wote watakaokutwa na makosa ya uvunjaji sheria,leseni zao zitafutwa na hawataruhususiwa kufanya biashara hiyo tena

'' Katika kipindi hikiwakati wa kesi zao zinashughulikiwa kisheria na ili kuzuia kuendesha biashara haramu leseni zao zinasitishwa na wanatakiwa kuzirudisha Benki kuu mpaka kesi zao zitakapokamiika baada ya hapo taratibu mpya zitatumika''

Amesema wale wote ambao wana tuhuma za kukiuka sheria katika oporesheni mbili zilizopita na kufikishwa polisi, wanatakiwa kurejesha leseni zao BOT mara moja ambapo leseni hizo zitasitishwa hadi pale kesi zao zitakapokamilika

Uchunguzi uliofanywa na BOT umebaini waendeshaji wengi wa maduka ya kubadilisha fedha hawajakidhi vigezo vyote japokuwa leseni zilitolewa kwao baada ya taarifa kupitoshwa

'' Hao wote watapewa notisi ya kusitisha leseni na maduka yao kufungwa, yeyote anayejua kuwa upatikanaji wa leseni yake unadosari anashauriwa kurejesha kwa hiari''alisema Gavana

Pia amewataka wale wote   wanaoendesha maduka ya kubadilisha fedha bila leseni au kwa kutumia leseni zisizo za kwao kufunga maduka hayo mara moja kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria

Aidha Gavana Luhoga amesema kuwa BOT haitazungumza chochote kwa sasa, mahojiano na wahusika yanaendelea na wale watakaokutwa na tuhuma za ukiukwaji wa sheria watashughulikiwa kufuatana na taratibu za kisheria

Gavana amesema kuwa juhudi za kitengo cha ukaguzi  kuwapata wahusika hazikuzaa matunda katika operesheni mbili zilizopita kwani imegundulika kuwa kuna mtandao mpana na madhubutu wa shughuli hizo na ambao ulilenga kuhakikisha shughuli za udhibiti hazifanikiwi.

Ameeleza kuwa ukaguzi huo wa kushtukiza ulifanyika jana Jijini Arusha mara  baada ya mashauriano na wataalam kwa kushirikisha vyombo vya upelelezi, na usimamizi ilionekana ili kufanikisha zoezi hilo wahusika wote wadhibitiwe kwa wakati mmoja na kufanyiwa ukaguzi ,ambapo ilihusisha maofisa wengi kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi

"Baadhi ya washiriki katika zoezi hilo ni askari wa jeshi la wananchi Tanzania wakiwa katika sare zao bila silaha, tulilazimika kutumia Jeshi la wananchi kwenye  operesheni kwani askari wengi wa jeshi la polisi walikuwa kwenye kusimamia usalama katika vituo vya mitihani ya kidato cha pili iliyokuwa ikiendelea''alisema Luhoga

Gavana Profesa Florence Luoga amesema BOT inayo hifadhi ya pesa za kigeni ambazo zinaweza kuendesha nchi ndani ya miezi mitano na siyo kwamba kuendesha kwao ukaguzi ni kutokana kupungukiwa na  fedha kama inavyodhaniwa lahasha,bali Tanzania ina hifadhi ya fedha  Afrika.

TCRA :WAUZAJI WA VIFAA VYA MAWASILIANO ,MAFUNDI WATENGENEZAJI SIMU ZA MKONONI WOTE WANATAKIWA KUWA NA LESENI KUTOKA MAMLAKA HUSIKA

11/18/2018 07:03:00 pm
Na. Vero Ignatus, Arusha

Mamlaka ya mawasiliano Nchini kanda ya kaskazini imeendesha semina ya siku moja kuhusu huduma za utangazaji kwa chanel zinazotazamwa bila kulipia 

Akizungumza  katika semina hiyo Mkuu wa Kanda ya Kaskazini Francis Msungu amesema leo ngo kuu la serikalini kuwataka watoa huduma kujenga miundo mbinu ya Minara hapa nchini na hii itapelekea watanzania wengi watapata ajira. 

 Katika semina hiyo iliyojumuisha viongozi mbalimbali wa serikali ngazi ya mkoa washiriki kuweza kuuliza maswali nje ya mada yanayohudu vifaa vya mawasiliano, simu, tekevisheni pamoja na radio.

 Mamlaka hiyo ya Mawasiliano  iliweza kutoa ufafanuzi kwamba maduka yanayouza vifaa vya mawasiliano vya eletroniki wauzaji wake wanatakiwa  kuwa na leseni  kutoka mamlaka ya mawasiliano sambamba na ile ya biashara

Msungu amesema kuwa  mafundi wanaotengeneza simu za mkononi wanapaswa pia kwa mujibu wa sheria wawe na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini.

Ndiyo maana tumeshauri wananchi kupotia viongozi kwamba unapopeleka kutengeneza simu yako kabla hujampa mtu kuitengeneza hakikisha je anacho kibali kinachomruhusu kufanya hiyo shughuli hiyo?

Unapokwenda dukani kununua kifaa chako cha mawasiliano radio, televisheni ni haki yako kujua je huyu anayeniuzia ametasimishwa kufanya hiyo kazi?
Amesema lengo kubwa la  Mamlaka kuwataka watu hawa kuwa na leseni ni kumlinda mtumiaji wa hizo huduma(mlaji).

Unapoenda kununua kifaa chako hakikisha umepewa risiti na sasa risiti hiyo imeongezewa kazima iwe na Efd ya TRA, lazima uwe na garantiii kama kunatokea lolote uweza kufidiwa kile kifaa na kupatiwa kingine hiyo ndiyo nia njema ya serikali kuweka huo utaratibu. Alisema

Amesema baadhi ya mafundi wanapotengeneza vifaa vya wateja wao asilimia kubwa wanabadilisha namba tambulishi na kupewa namba ya mtu mwingine ambapo amesema hilo ni tatizo

Kwa usalama wa nchi hili swala la msingi sana najua namba ya simu kitamvulishi ni kitambulisho muhimu kwa watumiaji wa simu hivy kuweni makini, hata vocha mnapozitumia msizitumie hovyo. Alisema


Msungu amewashauri wananchi kunua Madishi ya setilite badala ya kununua antena za kawaida hii itasaidia kuto kununua vingamuzi vingi. 

Katika semina hiyo muwezeshaji injinia Jan Kaaya amefundisha kuhusu masharti ya urushaji wa Maudhui. 

Amesema Masharti ya Leseni yananawataka watoa  huduma kuhakikisha maudhui yao yanatazamwa bila Malipo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arusha Dc akifungua semina hiyo Gabriel Daqqaro amesema viongozi walio hudhulia Mafunzo  haya ni vema zaidi kutumia Mafunzo hayo kuwafundisha wananchi. 

Moja ya washiriki  katika semina hiyo Mwalimu mkuu Salei Bi. Miminini Payema ameiomba mamlaka ya Mawasiliano ifanye mawasiliano kufanya Mazungumzo na Wamiliki wa DSTV  ili kupata chanel za ndani Bure. 
Wapili kutoka kulia ni Katibu Tawala David Mwakiposa wa wilaya ya Arusha akibadilishana mawazo na Kaimu mkurugeni wa jiji la Arusha Valentine Makuka pamoja  na Mkuu wa wilaya Arusha Gabriel Daqqaro

Washirili wa warsha hiyo wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea 
Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TCRA Francis Msungu
Muwezeshaji wa Warsha hiyo Injinia Jan Kaay (TCRA) akiendekea kutoa elimu kwa washiriki.
Wakwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro ndiye akiyefungua warsha hiyo ya siku moja ya watumishi na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani Arusha katika ukumbi wa Goldenrose.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakiendelea kufuatilia kwa makini


UMOJA WA ULAYA(EU) WAKABIDHI VIFAA KWAAJILI YA MAABARA YA KISASA TAEC

11/16/2018 05:29:00 pm
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini Profesa Lazaro Busagala   akizungumza na Meneja Mredi kutoka Jumuiya ya nchi za Ulaya Genevieve Liz pamoja na wageni wengine alioonhozana nao. 
Denis Mwalongo Mkuu wa Idara ya Mionzi, mashine za kuhakiki vifaa vya mionzi katika mwili wa binadamu akiwaonuesha wageni hao kutoka Umoja wa Ulaya jambo 
Dkt Wilbroad Muhogora mwenye (shati la draft) Mtafiti wa Tume akifafanua jambo kwa wageni kutoka Umoja wa Ulaya pamoja na, waandishi wa habari

Na, Vero Ignatus Arusha 

Umoja wa Ulaya (EU) umerithishwa na ujenzi wa maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) ikiwemo uwekaji wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya sh, bilioni 2.3. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea maabara hiyo, Meneja Mradi na Usalama wa Masuala ya Mionzi, kutoka EU, Genevieve Lizin alisema umoja huo umerithishwa na kazi nzuri ya uwekaji vifaa uliofanywa na serikali. 

Alisema Umoja huo umeamua kutoa vifaa hivyo kwaajili ya kudhibiti masuala ya mionzi ndio maana wametoa ili kudhibiti masuala ya mionzi katika nchi za Afrika. 

"Maabara hii ni ya kisasa na hakuna mfano wake katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla hivyo tumeridhika na kazi waliyofanya Taec katika zoezi la uwekaji vifaa ambavyo sisi tumevitoa "

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Profesa Lazaro Busagala  alisema serikali imetoa Sh, bilioni 2.3 kwaajili ya ujenzi wa maabara ya kisasa ya Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kwa lengo la kuhakikisha maabara hiyo inatoa huduma bora za kisasa za masuala ya mionzi kwa nchi za Afrika. 

Aidha alishukuru Umoja wa Ulaya kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya Sh, bilioni 11.5 vilkvyofungwa kwenye maabara za Tume hiyo ambavyo vimetolewa na Umoja wa Ulaya (EU)

Alisema  serikali kwa awamu ya kwanza imetoa Sh, bilioni 1  huku fedha nyingine Sh, bilioni 1.3 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara hiyo ya kisasa ambayo itaweza kutumiwa na watu mbalimbali nchini na nchi za Afrika 

"Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa kuwezesha maendeleo ya nchi yanasonga haswa katika kuhakikisha tume hii inapata maendeleo na kuchangia fedha katika mfuko huu serikali "

Katika maabara hiyo kutakuwa na uhakiki wa vifaa vya kupimia mionzi, chumba cha mionzi mikali kwaajili ya kupikia vyuma kwa njia ya kupiga picha kwa kutumia mionzi pamoja na chumba cha kutumia mionzi kwaajili ya shughuli nyingine ambamo kitasimikwa kifaa cha kupima viasili vya mionzi vilivyopo mwilini mwa binadamu. 

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mashine ya kupima mionzi iliyoko ndani ya Mwili wa binadamu (whole body counter), mashine ya kuhakiki vifaa vya mionzi , Secondary standard dosimetry laboratory ( SSDL)

Mashine ya kupima viasili vya mionzi kwenye mazingira , maji na hewa TXRF, mashine ya kupima mionzi kwenye vyakula aina ya Hyper pure Germanium detector. 

Sambamba na mashine ya kupima mionzi kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye mazingira ya vyanzo vya mionzi inayoitwa Harshaw 6600

Mwisho

TANZANIA YAPIGA HATUA KATIKA SEKTA YA BARABARA

11/15/2018 06:51:00 pm

Na. Vero Ignatus, Arusha

Serikali ya Tanzania  imefanikiwa  kuboresha   ujenzi  wa  barabara  kwa kutumia Teknolojia ya kuchanganya  lami  Kulingana  na  Mazingira  husika  katika  kanda  mbalimbali  Nchini na ipo teyari kwa ajili ya uwekezaji kwa maendeleo ya uchumi wa taifa . 

Akizungumza na waandishi  wa habari  mkoani  Arusha Waziri  wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele katika  mkutano wa  kimataifa  Mhandisi  amesema  wakala  wa  barabara  nchini   Tanroads   wameanzisha  miongozo  ya  kuchanganya  lami  Kulingana  na Mazingira  ya     hali  ya hewa  ya  mikoa  mbalimbali  ili  kuweza  kujenga  barabara  imara zitakazoendana  na  mazingira husika. 

Ameleza kuwa Tanzania  kutokana  na  mikutano hiyo wameweza kufanikiwa kutengeneza  Teknolojia  mpya ya kuchanganya  lami  kutokana na mazingira na jiografia ya maeneo  ambapo mfano  lami inayojengwa  Katavi  itaendana  na  hali  ya  hewa  ya Mazingira  yake  ili  barabara  zisiharibike na kudumu kwa muda mrefu hivyo kusaidia kukuza uchumi. 

Amewata  wataalamu  wa  TANROADS kutofanya  kazi  Kwa  mazoea  na  pia  kuhakikisha  wanatatua matatizo  ya  sehemu  zao  za  kazi wasisubiri hadi  mamlaka  za  juu  kuwapangia  majukumu  yanayowahusu. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TPA Deusdedit Kakoko akiongea kama mshiriki wa mkutano huo amesema kuwa mkutano huo umekuwa ni sehemu muhimu kwao kama mamlaka ya bandari wamejipanga kutumia mkutano huo kuboresha utendaji wao wa kazi

Kuangalia mabadiliko ya teknolojia ya usafirishaji na matumizi ya Tehama yatasaidia kuboresha na kubadilika kwa kwenda kwenye kizazi cha nne cha mapinduzi ya usafirisha duniani ambapo jambo hilo litaharakisha utoaji wa bidhaa katika bandari .

Kauli  mbiu  ya  mkutano  huo  ni  'Mapinduzi  ya  nne  ya  sekta  ya  usafirishaji  yanayohusiana  na mabadiliko  ya  kiuchumi  katika  nchi  zinazoendelea.

Mwisho.

MAKAMU WA RAIS, AZINDUA MAJENGO YA CHUO CHA MISITU OLMOTONY

11/08/2018 07:45:00 pm

Na. Vero Ignatus, Arusha

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungani wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameipongeza serikali ya Norway kupitia Tanzania kwa kufadhili ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Olmotonyi, halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru.

Makamu wa Rais, ametoa pongezi hizo, mapema leo,  wakati akizindua jengo la mihadhara na bweni la wanafunzi, katika Chuo cha Misitu Olmotony, na kuipongeza Serika kifalme ya Norway kwa kwa juhudi zake za kufadhili Taasisi za Elimu ya Uhifadhi wa Misitu na Mazingira.

Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amezindua jengo la mihadhara lenye uwezo wa uwezo wa kusomesha wanafunzi takribani  240, pamoja na Bweni la wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 100, majengo yaliyogharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 1.8, ujenzi uliofadhiliwa na Serikali ya Kifalme ya Norway kupitia Mradi wa Kujenga uwezo wa Jamii kwa njia ya mafunzo katika Usimamizi Shirikishi wa Misitu, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi maarufu kama ECOPRC.

Makamu huyo wa Rais, amesema kuwa, majengo ni muhimu sana kwa chuo hicho, kwa kuwa yatasaidia kupunguza uhaba wa madarasa uliokuwepo, pamoja na kuimarisha ustawi wa wanafunzi wa kike licha ya waondolea adha ya kupanga nyumba za watu binafsi nje ya chuo.

Aidha Mhe, Samia ameendelea kuushukuru Ubalozi huo  kwa  kutoa ufadhili kwa wanafunzi 128 kimasomo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada, chuonini hapo huku wanafunzi 56 kati yao wakiwa ni wanawake.

Zaidi Mhe Samia ameushukurumambo mengi yaliyofanywa na  Ubalozi huo  ikiwa ni pamoja na kukiunganisha chuo hicho kwenye Mkongo wa Taifa, kuboresha maktaba  pamoja na kukiwezesha kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya  kufundishia.

Ameongeza kuwa, juhudi zote hizo zitasaidia kuimarisha mazingira ya kujifunzia, pamoja na kutoa taaluma bora, itakayowezesha kuzalisha watalaam wenye ujuzi wa kiwango cha hali ya  juu.

Awali, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga, alieleza kuwa kutokana na uhaba wa mabweni na kumbi za mihadhara, Chuo kilikuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wachache kulingana na mahitaji, kwa kudahili wanafunzi 600 tu badala ya kudahili wanafunzi zaidi ya 1,000.

Mhe, Hasunga amesema kuwa licha ya ujenzi wa miundombinu hiyo kusaidia kuboresha utoaji wa mafunzi ya kiwango cha juu lakini pia utawezesha chuo hicho kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa.

Aidha, Naibu Waziri Hasunga, ameuomba  Ufalme wa Norway kuendelea kushirikiana na Chuo hicho, ikiwemo kuendelea kuongeza mabweni ya wavulana, madarasa pamoja na kuboresha vifaa vya mafunzo ili chuo kiweze kufikia lengo lake la kuongeza udahili wa wanafunzi chuonj hapo.

Naye Balozi wa Norway nchini, Elizabeth Jacobsen amesema kuwa, lengo la nchi yake kufadhili  mradi huo, ni kuimarisha ustawi wa miti na kuhakikisha, miti iliyopo haikatwi ovyo badala yake jamii ijikite zaidi katika kupanda miti, ili kuepuka majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.

Chuo cha Misitu-Olmotonyi  kilianzishwa mwaka 1937, kwa madhumuni ya kufundisha elimu ya uhifadhi wa misitu kwa ngazi ya ufundi-sanifu na  kimekuwa tegemeo kubwa ndani na nje ya Tanzania, hasa katika ukanda wa Kusini mwa Afrika.

JUKWAA LA WAKULIMA ARUMERU LAPATA NEEMA

11/07/2018 06:59:00 am
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa mmoja wa mkulima katika maonyesho ya wakulima wilayani hapo. 
 DC Muro akizungumza na wakulima katika maonyesho hayo ya kilimo yaliyoanza tarehe 1-3 Novemba 2018 wilayani humo. 
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na wakulima na wananchi wa wilaya hiyo katika maonyesho hayo ya wakulima
 Mmoja kati ya mkulima. Wilayani humo akimpatia maeleza ya mbegu ya mahindi kama inavyoonekana katika picha Mkuu wa wilaya Jerry Muro katika maonyesho hayo
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiwa katika picha ya pamoja na wakulima katika maonyesho hayo ya wakulima Meru. 

Na. Vero Ignatus, Arumeru. 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amejitolea  kuwasadia kuandika Maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara ili waweze kukopesheka na Ta asisi za kifedha 

Amesema hatua hiyo imefikia baada ya kubaini kuwepo kwa vikwazo katika maandiko katika hatua za awali kwani Taasisi hizo kabla ya kutoa msaada au mkopo huitaji mchanganuo, andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.

 Wanapoanza safari ya kutimiza ndoto zao za kuwekeza katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa vikwazo hivyo aliamua kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia wananchi  kuondoa Vikwazo hivyo.

Mhe Muro amesema tayari kampuni Binafsi ya Wawezeshaji wa wakulima (PASS)Private Agricultural Sector Support imekubali kuwaandalia na kugharamia Mpango kazi wa kibiashara zitakazowasaidia Wakulima na Wafugaji katika kupata Mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia katika uendelezaji wa Kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara. 

Akifungua maonyesho ya jukwaa la wakulima Meru ambayo yamefanyika Kwa siku tatu na kuwaleta pamoja wakulima, wafugaji na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo kwa pamoja  wamekukubali kutoa msaada katika kuandaa, kuandika maandiko ya mchanganuo wa kibiashara 

Muro amewapatia chumba Cha ofisi ya kuratibu na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji Jukwaa hilo la Wakulima Meru  ili kuwawezesha kufanya kazi zao Kwa haraka zaidi, na kuhaidi kuwatafutia kompyuta Kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za taarifa za wakulima na wafugaji.

Kwa upande Meneja wa Tawi la kampuni ya ( PASS)amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkuu huyo wa wilaya kwa kuonyesha kuwajali wakulima na wafugaji ambapo amewataka wananchi hao Kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika kupitia na Taasisi hiyo. 

Mwisho. 

WAFANYABIASHARA TUMIENI MAKAMPUNI YALIYOSAJILIWA KUAGIZA BIDHAA

11/05/2018 04:59:00 pm
Na. Vero Ignatus, Manyara

Kamishna  wa Bima Tanzania Dkt.Abdallah Saqware Baghayo amewata wafanyabiashara  hapa nchini wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kwa kutumia njia  ya magari,ndege,meli ikatiwe Bima kutoka katika makampuni yaliyosajiliwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Madarasa Mawili Ofisi Pamoja na Vyoo  katika shule ya msingi Gedamar iliyopo Wilayani  Babati  Mkoani Manyara,Baghayo amesema ni kosa kwa mfanyabiashara kisheria kwa mfanyabiashara kunua bidhaa ambayo haijasajiliwa na mamlaka hiyo.

Amesema ni tegemeo la serikali kuwa makampuni yaliyopewa leseni yatapata biashara ya uagizaji wa bidhaa huku akiwataka wananchi kutambua  umuhimu wa bima na kufuata sheria.

Dkt.Baghayo amesema mabadiliko ya sheria hiyo yalisainiwa na raisi Dkt.John Pombe Magufuli ili kuweza kutekelezwa na kuzuia wafanyabiashara kutumia bima kupitia makampuni yasiyo sajiliwa.

Kwa Upande wake Mkuu wa Kitengo cha fedha kutoka  Jubilee Life Insuarence Helena Mzena alisema kuwa kampuni hiyo inatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake, hivyo kuamua kurudisha faida kwa jamii kwa kuangalia changamoto mbali mbali zilizopo katika shule ya msingi hapa nchini.

Aidha alisema kuwa mradi huo walipanga kutumia kiasi cha shilingi Milioni 200 kwa Ajili ya kukarabati Vyumba vya Madarasa,Ujenzi wa Vyoo,Ujenzi wa Nyumba mbili za walimu na Ujenzi wa Ofisi ya Walimu kulingana na mahitaji ya shule husika.

Mzena alisema kuwa Kampuni hiyo mpaka sasa imetumia kiasi cha shilingi milioni 152 katika Shule saba katika Mikoa ya Morogoro,Manyara,Bukoba,Mbeya,Dar es Saalam,Dodoma na Zanzibar.

Naye  Meneja wa Kanda ya Kaskazini Sweetbert Lasway alisema kuwa kampuni hiyo imeweza kukarabati madarasa mawili,Kumalizia Ofisi ya walimu na Ujenzi wa Vyoo katika shule ya msingi Gedamar kwa gharama ya shilingi milioni 25.
 Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Dkt. Abdallah Saqware Baghayo akizungumza na waalimu, viongozi wa kijiji cha Gedamar 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya Jubilee. Dipankar Acharya 
 Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza
Mkuu wa Kitengo cha fedha kutoka  Jubilee Life Insuarence Helena Mzena akizungumza katika hafla hiyo

 Meneja wa Kampuni ya Bima Jubilee Kanda ya Kaskazini Sweetbert Lasway akizungunza na wazazi na wanafunzi katika shule ya msingi Gedamar
 Kamishana wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini  Dkt.Abdallah Saqware
akibadilishana mawazo na viongozi wa kijiji cha Gendemar pamoja na waalimu wa shule ya msingi Gendermar
Picha ya pamoja. Picha zote na Vero Ignatus

ARUSHA KUJA NA VITUO 4 MAALUMU VYA POLISI VILIVYOGHARIMU ZAIDI YA MIL. 80

11/03/2018 10:36:00 am

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Kutoka kushoto ni mhifadhi mkuu wa mamlaka ya  Ngorongoro Dkt. Fredy Manongi akifuatiwa na Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Alan Kijazi
 Wamiliki wa makampuni ya Utalii wakifuatilia mjadala wa kuweka vituo maalumu vya polisi mkoani Arusha.
Mdau wa Sekta ya Utalii wakitoa maoni yao juu ya zoezi la uwekaji wa vituo maalum vya polisi.

Na Vero Ignatus, Arusha. 

Kikao cha Sekta ya wadau wa Utalii kimefanyika Mkoani Arusha kikiwa na lengo la kuona namna wanatekeleza azimio la kusimika vituo vinne Maalum vya Polisi kwa ajili ya Ukaguzi wa magari yanayosafirisha watalii.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii ambapo Mkuu wa mkoa Mrisho Gambo amesisitiza azma yake katika kuhakikisha utalii unatengenezewa mazingira mazuri ya ukuaji.


Hakuna kitu kinatupa sifa mbaya kwa wageni kama kusimamishwa na askari kila baada ya kilomita moja''alisema Gambo


Amesema Vituo hivyo maalum vya ukaguzi  vitasaidia kuondokana na changamoto hiyo kwakuwa sekta ya utalii inategemewa sana katika kuliingizia taifa pato 


"Magari yote yatakua na vituo maalum vya ukaguzi, tunafanya yote haya kwakua sekta ya utalii tunaitegemea sana kama taifa kwa kutuingizia pato la taifa.” Alisema Gambo.


Vituo hivyo vinne vinavyogharimu zaidi ya shilingi Milioni 80 vimetengenezwa kwa michango ya wafanyabiashara ya Utalii TATO na vinatarajiwa kuwekwa katika maeneo ya Kikatiti, Ngaramtoni, Makuyuni na Karatu.


Kwa upande wa serikali kupitia mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na TANAPA, Mkurugenzi mkuu wa hifadhi za Taifa Dr. Kijazi amesema wao kama wadau wa mkubwa wa sekta hii wanaunga mkono wazo hili na wako tayari kuhakikisha taasisi zao zinajenga vyoo katika vituo hivi.


Sisi kama hifadhi za Taifa ni wanufaika namba moja endapo sekta hii inaboreshewa mazingira, na kwa kuunga mkono jitihada hizi mimi na wenzangu wa mamlaka ya Ngorongoro tunaahidi kujenga vyoo katika vituo vyote vinne kwa kushirikiana na ofisi za wakuu wa wilaya” alisema Kijazi.


Kwa niaba ya wafanyabiashara ya utalii Bwana Sirili Nko ambaye ni Katibu wa TATO, ametoa pongezi kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kuonyesha juhudi za kUkuzaji na kUboresha sekta ya Utalii Mkoani Arusha.


Toka kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Gambo amefanya jitihada nyingi za kuboresha sekta ya utalii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
.

Mwisho

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel