Top Menu

BASI LAPARAMIA KITUO CHA MABASI YAENDAYO KASI ENEO LA KIMARA JIJINI DAR USIKU HUU

3/26/2016 07:12:00 am

Saturday, 26 March 2016

BASI LAPARAMIA KITUO CHA MABASI YAENDAYO KASI ENEO LA KIMARA JIJINI DAR USIKU HUU

Basi la kampuni la pricess Muro limeparamia kibanda chamabasi yaaendayo kasi kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo wakati likiingia mjini kutoka mkoani .Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM ATANGAZA DAU.

3/18/2016 11:47:00 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Atangaza Zawadi ya Milioni 1 Kwa Askari Polisi Atakayepambana na Jambazi na Kulishinda

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi kanda maalum Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea mwenendo wa jeshi hilo ambapo wamekubaliana kutoa zawadi ya milioni moja kila baada ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na majambazi.

"Askari wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa. Nmeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha.
 
"Kuna watu wengi wana silaha halali na  wengine wanamiliki isivyo halali, kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za uhalali wa silaha zao.

"Tunataka kujihakikishia tunazo silaha ngapi katika mkoa wetu maana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu.

"Sasa olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye mabenki wala kuwapora watu kwa silaha." Amesema RC Paul Makonda

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel