Top Menu

Saturday April 30,2016.KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHAFUNGUA MAFUNZO YA AJALI,VIFO NA MAJERUHI BARABARANI

4/30/2016 08:35:00 am

Saturday, 30 April 2016
Kaimu kamanda kikosi cha
usalama barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Polisi
Fortunatus Musilimu akifungua mafunzo kwa mawakili,waendesha
mashitaka na askari wapelelezi wa kesi za ajali barabarani
iliyoandaliwa na wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na
watoto kwa kushirikiana na shirika la afya Duniani kupitia mpango
wa Bloomberg Initiative Global Road Safety,jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya mawakili,waendesha mashitaka na askari wapelelezi wa kesi za ajali
barabarani wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani)wakati wa
ufunguzi huo.Mradi wa Bloomberg una nia ya kupunguza ajali,vifo
na majeruhi barabarani pamoja na kuweka vipaumbele kuzuia
vyanzo hatarishi vya ajali kama mwendokasi,kutovaa kofia
ngumu,kutofunga mikanda,vifaa maalum vya kuwakinga watoto
kwenye magari na ulevi.

Mwenyekiti wa kamati ya
Bloomberg Initiative Global Road Safety Tanzania,Mrakibu Msaidizi
wa Polisi Mathew Msuyale akimkaribisha mgeni rasmi(hayupo
pichani)pamoja na wadau wa mafunzo hayo.

Baadhi ya wadau na askari wapelelezi wa kesi za a halo za barabarani wakifuatilia
mada wakati wa mafunzo hayo.Nchini takwimu zinaonesha ukubwa wa
tatizo la ajali ni kubwa ambapo mwaka 2014 zilitokea ajali 14,360,vifo
3,760 na majeruhi 14,530 ukilinganisha na mwaka 2015 zilitokea ajali
8,337,vifo 3,468 na majeruhi 9,383 Wazazi nchini wametakiwa kuwakinga watoto wao wakati waendeshapo magari kwa kuhakikisha wanawafunga mikanda ili
kuwaepusha na ajali za barabarani na kudhibiti madhara yatokanayo na ajali.

Rai hiyo imetolewa leo jijini hapa na kaimu kamanda kikosi cha
usalama barabarani Tanzania,Kamishna Msaidizi wa Polisi
Fortunatus Musilimu wakati akifungua mafunzo kwa
Mawakili,Mahakimu ,Waendesha Mashitaka na Askari wapelelezi wa
kesi za ajali za barabarani,iliyoandaliwa na wizara ya afya kwa
kushirikiana na shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia mpango wa
Bloomberg Initiative Global Road Safety.

Alisema wazazi wengi wanapokuwa wanaendesha magari
hawawafungi mikanda watoto wao na hivyo ajali inapotokea watoto
wanakuwa ni wahanga wakubwa kwa kupoteza maisha au kupata
ulemavu wa kudumu
?Wazazi mnawalindaje watoto,baba anaendesha gari,mtoto yupo
kwenye usukani anaendesha nae gari,hiyo siyo sahihi ,tuwalinde
watoto wawe salama kwa kuvaa mikanda?

Aidha, Kamanda Musilimu alisema tatizo la ajali barabarani nchini
imekua ikiongezeka kila mwaka na hii ni kutokana na wananchi
kutokuona kama ajali ni tatizo kubwa na la haraka ambalo linafanya
kuongezeka kwa vifo nchini kulinganisha na magonjwa mengine na
hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa kiuchumi
?Watu bado hawaoni kama ajali ni tatizo ,vifo inatokea hapohapo na
watoto wanabaki kuwa tegemezi,hizi ni changamoto hivyo
mshirikiane kubadilishana uzoefu ili muweze kutatua kesi zote
zinazowafikia na kupunguza malalamiko pamoja na kutenda
haki,alisema

Takwimu za hapa nchini kwa miaka miwili zinaonesha mwaka 2014
zilitokea ajali 14,360,vifo 3,760 na majeruhi 14,530 na mwaka 2015
zilitokea ajali 8,337,vifo 3,468 na majeruhi 9,383, hata hivyo Ripoti ya
Shirika la Afya Duniani ya mwaka 2015 zinaonesha ajali huua watu
1.25 milioni Duniani kila mwaka, watu kati ya 20 na 50 milioni
hujeruhuwa kila mwaka na hivyo asilimia 90 ya ajali hizi na vifo
hutokea katika nchi zenye uchumi wa kati na wa chini kama
Tanzania.

Kamanda Musilimu alisema kasi hii ya ajali ikiendelea hadi ifikapo
mwaka 2030,ajali itashika nafasi ya 5 kwa kusababisha vifo Duniani.
Mradi wa Bloomberg Initiatives ni mradi wa miaka mitano hapa
nchini umeanzishwa mwaka 2015 ukiwa na nia ya kuweka vipaumbele
vya kuzuia vyanzo vya ajali hatarishi kama vile mwendo
kasi,kutokuvaa kofia ngumu,kutokufunga mikanda,vifaa maalumu
vya kuwakinga watoto kwenye magari pamoja na ulevi.

BASATA KUADHIMISHA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ

4/30/2016 08:20:00 am

Saturday, 30 April 2016

National Arts Council BASATA
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la
Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Elimu na Sayansi
(UNESCO) litaungana na wasanii mbalimbali nchini na wadau wa
Sanaa kuazimisha siku ya muziki wa Jazz duniani ambayo kwa
mara ya kwanza itaazimishwa nchini Mei 2, 2016.
Maazimisho hayo ambayo yatapambwa na burudani mbalimbali
kutoka kwa Wasanii wa muziki wa jazz hususan Band maarufu ya
Das Jazz yanatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Baraza hilo
ulioko Ofisi za BASATA Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.
Sambamba na burudani hizo, kutakuwa na mada mbalimbali
zitakazowasilishwa na wadau wa muziki huu wa jazz ambazo
zitalenga kuamsha ari, thamani na ufahamu wa muziki huu
maarufu duniani miongoni mwa wasanii nchini.
Wawasilishaji wa mada hizo pamoja na mada zao kwenye mabano
ni pamoja na John Kitime (Matumizi ya neno Jazz), Carola Kinasha
(Uhusiano kati ya Elimu ya Muziki na Jazz) na Kurwigira Mareges
(Historia ya Muziki wa Jazz) na Masoud Masoud (Ujue Muziki wa
Jazz)
Mbali na burudani na mada hizo kuhusu muziki huo wa Jazz
kutakuwa na wageni waalikwa kutoka kwenye balozi na vituo vya
Utamaduni vya nchi mbalimbali zilizopo hapa Tanzania
BASATA linatoa wito kwa wasanii na wadau wa muziki huu wa
jazz kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya ambayo
yatakuwa yakifanyika kila mwaka sambamba na mataifa mengine
duniani.
Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Godfrey Mngereza
Katibu Mtendaji – BASATA

Friday, April 29,2016 Spika Apangua tena Kamati za Bunge, Wabunge Wapinga

4/29/2016 11:57:00 pm

Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko mengine ya kamati za Bunge
kwa kuwaongeza wabunge wapya na kuwahamisha wengine kwenda kwenye
kamati nyingine, jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wabunge wakidai
linapunguza ufanisi.
Juzi, Spika Ndugai (pichani) aliwaongeza wabunge wanne wapya walioapishwa
bungeni Aprili 19, kwenye kamati za Miundombinu; Ardhi, Maliasili na Utalii;
Kilimo, Mifugo na Maji; na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Hayo ni mabadiliko ya pili tangu Bunge la 11 lianze rasmi vikao vyake katikati
ya Novemba mwaka jana, ikiwa ni kipindi kifupi cha mabadiliko ikilinganishwa
na Bunge la Tisa na 10.
Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Bunge,
mabadiliko hayo yamefanyika kwa mujibu wa kanuni ya 116 (3) na (5) ya
Kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2016, ili kuhakikisha kila mbunge
anakuwa mjumbe wa kamati mojawapo ya Bunge.
“Aidha, mabadiliko haya ni kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kadri
itakavyowezekana, Muundo wa Kamati za Kudumu za Bunge unazingatia aina
za wabunge kwa jinsia, pande za Muungano na Vyama vya Siasa vyenye
uwakilishi bungeni, ujuzi maalumu, idadi ya wajumbe kwa kila kamati na
matakwa ya wabunge wenyewe,” inasema taarifa hiyo.
Baadhi ya wabunge jana walipinga mabadiliko ya mara kwa mara ya wajumbe
wa kamati, wakieleza kuwa hayaleti tija na uamuzi huo haufanywi kwa umakini.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT Wazalendo), alisema mabadiliko
hayo yanaonyesha namna ambavyo Spika Ndugai “anavyokosa umakini katika
uundaji wa kamati hizo”.
“Spika hakuwa makini wakati anaziunda kamati hizo na sina jingine zaidi ya
kusema, maana hilo liko wazi,” alisema Zitto.
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Mariam Msabaha alisema uundaji wa
kamati kila mara, unatokana na kiongozi huyo kutokuwa na umakini na mara
nyingi anafanya kazi kwa shinikizo la vikao vya chama.
Msabaha alisema utaratibu wa kuvunja kamati na kuziunda unatokana na vikao
vya wabunge wa CCM, ambavyo humshauri Spika juu ya nini kifanyike ili
waweze kuubana upinzani, ushauri ambao anadai wakati mwingine unakosa
tija.
Mbunge wa Sengerema William Ngeleja (CCM) alisema mabadiliko
yanayofanywa hayana madhara yoyote, kwa kuwa ni jambo la kawaida kufanya
maboresho na kuwataka wabunge kujifunza kupitia mchezo wa mpira ambao
kila mtu anakuwa na namba yake, lakini uwanjani anacheza namba zote.
“Waangalie mfano wa Profesa Makame Mbarawa ambaye alipewa Wizara ya
Maji, lakini akaondolewa baada ya wiki tatu na kupelekwa kusimamia barabara
ambako ameonyesha uwezo mkubwa, iweje kwa wabunge?” alihoji Ngeleja.
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola alisema mabadiliko yanayofanywa
hayawezi kuleta tija katika bunge hilo, kwani watu wanashindwa kujipanga
vyema kwa kuwa hawajui kesho itakuwaje.
Lugola alihoji juu ya mafunzo waliyopata kila kamati, lakini wanabadilishwa bila
utaratibu huku akisema hata kamati ya uongozi inaathirika zaidi, kwani
wanapobadilishwa na kuondolewa wenyeviti lazima kamati ya uongozi ibadilike.
Spika Ndugai hakupatikana jana kueleza kwa kina mabadiliko hayo. Naibu
Spika, Dk Tulia Ackson alisema siyo msemaji na Ndugai na ndiye angepaswa
kuulizwa jambo hilo.
Katika taarifa hiyo ya Bunge, Spika Ndugai aliwataka wajumbe wa kamati sita
ambazo hazina viongozi kuwachagua mapema iwezekanavyo kama kanuni za
Bunge zinavyohitaji.
Kamati hizo ni Hesabu za Serikali (PAC) Mwenyekiti; Kamati ya Nishati na
Madini, (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti); Kamati ya Ardhi, Maliasili na
Utalii (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti); Kamati ya Hesabu za Serikali za
Mitaa (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti); Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya
Umma (Mwenyekiti) na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Makamu
Mwenyekiti.

Friday, April 29, 2016 UVCCM Wamtaka Fredrick Sumaye Amwache Rais Magufuli Afanye Kazi Yake

4/29/2016 09:34:00 pm


Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi umesema Waziri Mkuu mstaafu
Frederick Sumaye hana vigezo wala sifa zozote zinazoweza kumfanya awe na
uwezo wa kumkosoa Rais Dk John Magufuli katika uendeshaji wa serikali na
masuala ya utawala.
Sumaye ametakiwa amuache Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk
Magufuli ili atimize majukumu yake kwa sababu alipewa dhamana ya kuwa
Waziri mkuu lakini hakufikia hata theluthi ya utendaji unaofanyika sasa.
Msimamo huo umetolewa jana na Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu
shaka alipokuwa akizungumza na wanachama wa ccm wa kata mbili za
kwandele na mbichi jimbo la Rombo mkoani kilimanjaro.
Shaka alisema anachokifanya Sumaye na baadhi ya wanasiasa muflis
wanaojaribu kukosoa utendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya tano ni
kutaka nao wasikike wakidhani yale walioyafanya wakati wakiwa madarakani
wananchi wameyasahau.
Alisema kama yupo waziri mkuu ambaye ameonyesha udhaifu katika utendaji na
usimamizi wa serikaki huku akishindwa kumsaidia Rais hakuna atakayempita
Sumaye.
Aidha Kaimu huyo alimuonya Sumaye kuacha kumfuatafuata Dk Magufuli katika
mikakati yake ya kutumikia nchi na juhudi anazozichukua dhidi ya mafisadi na
wabadhirifu wa mali za umma nchini.
Alisema wakati Rais Magufuli akiwa katika dhamira njema na nia ya wazi
kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, uaminifu na heshima kina sumaye na
wenzake wafumbe midomo yao na waache mara moja kumbughudhi Rais kwa
ajili ya kusaka umaarufu wa kisiasa.
Pia shaka aliwataka wananchi wa jimbo la Rombo kujitayarisha ili kumpiga
chini mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya chadema Joseph Selasini kwa sabahu
ni dhaifu na hatoshi kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
"Siku zake za kuitwa mbunge wa Rombo sasa zinahesabika, Selasimi hajui
anachokifanya wala hajali shida na matatizo yaliopo katika jimbo lake,lazima
adui huyo apigiwe mwaka 2020 "alisisitiza shaka
Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa uvccm mkoa wa kilimanjaro
Juma Raib Juma aliwakanya wananchi wa kanda ya Kaskazini kuacha mara
moja tabia ya kushiriki na kuchagua vyama na wagombea wa nafasi mbali
mbali kwa ukabila, ujimbo au nasaba.
Raibu alisema ikiwa wananchi wa kaskazini sasa wanaishi katika Mikao yote ya
Tanania, si jambo la maana wao wakahesabiwa kama ni wabaguzi kwa misingi
ya asili au ujamaa.
"Tunachotaka kukisafanya baadhi ya wananchi wa Mikao ya Kaskazini ni
kumuasi baba wa Taifa marehemu Mwalimu julius Nyerere, hakutuacha tukiwa
tumegawanyika , tumeishi miaka yote hatukuongozwa kwa ukabila au udini,
chadema acheni kwasabahu hilo ni balaa au janga katika jamii "alisema Raib.
Jumla ya wanachama wapya 103 walijiunga na chama cha mapinduzi pia
shaka alipata nafasi ya kuangalia mechi ya soka kati ya timu za kata za
makiidi na mahare wilaya ya Rombo.

Friday, April 29, 2016 Bosi wa Zamani wa TRA na Wenzake Wawili Warudishwa Tena Rumande Hadi Tarehe 3 Mwezi Ujao

4/29/2016 09:28:00 pm


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imesita kutoa
uamuzi wa kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni kwa
madai, jalada lake limeitishwa Mahakama Kuu.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA);
Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na
Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, hana mamlaka ya
kutolea uamuzi wa kesi hiyo kutokana na jarada lake kuitishwa Mahakama Kuu
leo asubuhi.

Kutokana na hali hiyo Hakimu Mchaura amesema kwamba, kesi itatajwa tena
tarehe 12 Mei mwaka huu na watuhumiwa watarudishwa rumande.
Muda mfupi baada ya hakimu Mchaura kusema hivyo, Kitilya na wenzake
walirudishwa tena mbele ya Hakimu huyo baada ya hakimu kupata amri
kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
akimtaka kesi hiyo itajwe Mei 3, mwaka huu badala ya tarehe 12 Mei mwaka
huu aliyoipanga awali.

Hakimu Mchauru amesema, sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi
itatajwa tena tarehe 3 Mei mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi
yatabaki kama ilivyo.

Friday, April 29, 2016. Serikali Yashauriwa Kuwa na Hisa Kwenye Kampuni za Madini ili Kujua Mapato halide Yanayoingizwa na Wawekezaji wa Kigeni

4/29/2016 11:59:00 am


Serikali imeshauriwa kuwa na sehemu ya umiliki katika kampuni zinazochimba
madini na gesi ili kujua mapato halisi yanayoingizwa na wawekezaji wa kigeni.
Aidha, imeshauriwa kuzilazimisha kampuni hizo kurejesha nchini asilimia 60 ya
mauzo yake, ili kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, pamoja na
kuimarisha Shilingi ya Tanzania.
Ushauri huo ulitolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
aliyestaafu, Ludovick Utouh pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji
wa Uwazi katika mapato ya Madini, Gesi na Mafuta (EITI), Jaji mstaafu Mark
Bomani, wakati wa uzinduzi wa ripoti za kamati za mwaka 2013 na 2014
uliofanyika jana Dar es Salaam.
Akizindua ripoti hizo, Utouh alisema, Tanzania haijafaidika na rasilimali za
madini, jambo lililosababishwa na kujiondoa kufanya biashara, hivyo kuzipa
mwanya kampuni za kigeni kuendesha biashara bila uwazi kuhusu mapato
zinazoyapata kutokana na mauzo ya madini.
“ Serikali iliangalie jambo hili na kulirekebisha, Serikali ya Botswana ina hisa
kwenye migodi hiyo, hivyo wanakuwa na mwakilishi kwenye bodi jambo ambalo
linakuwa rahisi kufuatilia mapato yanayopatikana, lakini sisi hapa tulijiondoa
kwa madai kuwa Serikali haifanyi tena biashara,” alisema Utouh.
Alisema, Serikali ikifanya hivyo itaweza kupata mapato mengi zaidi kuliko ilivyo
sasa, ambapo imejiondoa kabisa katika umiliki wa migodi ilhali rasilimali hizo ni
za Watanzania.
“Wawekezaji wanakuja na fedha na utaalamu, lakini sisi cha kwetu ni rasilimali,
ni lazima tugawane nao na tuwe na mwakilishi kwenye bodi, badala ya kusubiri
mrabaha unaotokana na faida anayopata mwekezaji. Huu utaratibu wa
kuwaachia kila kitu sio mzuri,” alisema Utouh.
Naye Jaji Bomani alisema, Serikali inatakiwa kuzilazimisha kampuni
zinazochimba madini nchini kurejesha asilimia 60 ya mauzo yake ili kuimarisha
akiba ya fedha za kigeni. Alisema, kwa kufanya hivyo, Shilingi ya Tanzania
itaimarika.
Alisema, hatua hiyo ikichukuliwa, sekta ya madini itakuwa imetoa mchango
wake kwa pato la Serikali, licha ya kuwepo changamoto mbalimbali zinazoikabili
sekta hiyo.
Alitaja moja ya changamoto hizo kuwa ni kupanua wigo wa wachimba madini
kama vile wachimbaji wa kati na ambao pato lao linazidi Sh milioni 200, kwa
mwaka ambao, alisema wanastahili kutoa mchango kwa pato la Serikali.
Alisema mpaka sasa ni kampuni kubwa tu zinahusika, lakini akasema umefika
wakati wachimbaji wa kati nao waingizwe kwenye utaratibu huo.
Alipendekeza kuwa umefika wakati sekta ya madini ipanuliwe hadi kwenye
uchimbaji wa makaa kuiwezesha nchi kufaidika zaidi na shughuli za rasilimali
hiyo, ambayo inaweza kuwa na manufaa makubwa kwa nchi.
EITI ni shirika la kimataifa ambalo liliundwa mwaka 2002 na nchi mbalimbali
zenye sekta ya madini. Linafanya ufuatiliaji juu ya sekta ya madini na gesi na
kuona kama kuna uwazi katika biashara yake.
Tanzania ilijiunga na shirika hilo mwaka 2009. Kazi kubwa ya kamati
iliyoundwa kushughulikia shughuli hizo hapa nchini ilikuwa ni kukusanya taarifa
juu ya malipo ambayo kampuni za madini zilikuwa zinalipa serikali ya Tanzania
na kuzilinganisha na mapato ambayo yalikuwa yamepokelewa serikalini na
kutoa taarifa kila mwaka.

Friday, April 29, 2016 .Kuachiwa Huru Abdallah Zombe na Wenzake kusikilizwa Leo

4/29/2016 11:53:00 am

Friday, April 29, 2016

Mahakama ya Rufaa leo inatarajiwa kusikiliza rufaa ya kupinga kuachiwa huru
kwa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na askari wenzake wanane waliokuwa
wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.
Rufaa hiyo inatarajiwa kusikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa
na Jaji Bernard Luanda, wengine ni Jaji Sauda Mjasiri na Jaji Semistocles
Kaijage.
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), alikata rufaa mwaka 2013, akipinga hukumu
ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliyowaachia huru Zombe na
wenzake, baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi ya mauaji ya watu
wanne iliyokuwa inawakabili.
Katika rufaa hiyo, DPP anadai kuwa Jaji Salum Massati alikosea kuwaachia
huru washitakiwa hao kwa sababu kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia
hatiani wote.
Mbali na Zombe, wajibu rufaa wengine ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed
Makelle, Konstebo Jane Andrew, Konstebo Emanuel Mabula, Konstebo Michael
Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rajabu Bakari na Koplo Festus Gwabisabi.
Katika kesi ya msingi inadaiwa Januari 14, 2006, katika msitu wa Pande uliopo
Mbezi Luis, Dar es Salaam Zombe na wenzake waliwaua kwa makusudi
wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Morogoro, Mathias Lunkombe,
Sabinus Chigumbi na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, pamoja na dereva teksi
Juma Ndugu.
Baada ya kusikiliza kesi hiyo, Agosti 17, 2009, Jaji Massati aliwaachia huru
washitakiwa kwa kuwa upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha mashitaka
dhidi yao bila kuacha shaka na Mahakama ikiwaona hawana hatia kwa makosa
yaliyokuwa yanawakabili.
Oktoba 6, 2009, DPP alikata rufaa Mahakama ya Rufani, akipinga hukumu hiyo
kwa madai kuwa Jaji Massati alikosea kuwaachia huru washtakiwa hao, pia
kulikuwa na ushahidi wa dhahiri na wa kimazingira unaotosha kuwatia hatiani
washtakiwa wote.
Hata hivyo Mei 8, 2013 Mahakama ya Rufaa ilitupilia mbali rufaa hiyo kutokana
na dosari za kisheria zilizobainika kwenye rufaa, lakini DPP alipeleka maombi
Mahakama Kuu ili aruhusiwe kukata tena rufaa nje ya muda.
Mahamaka Kuu ilikubali maombi yake, akakata tena rufaa inayotarajiwa
kusikilizwa leo.

Friday, April 29, 2016 Naibu Spika Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumwita Mbunge BWEGE

4/29/2016 11:45:00 am


Naibu Spika Tulia Ackson, ambaye katika vikao vya Bunge anatakiwa
kusimamia mijadala kwenye chombo hicho cha kutunga sheria, jana alizua
kizaazaa baada ya kumuelezea mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Said
Bungara kuwa ni bwege, akimtaka aache kuonyesha hali hiyo.
Kwa mujibu wa toleo la pili la Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford) la mwaka
2004, neno bwege linamaanisha “mtu mjinga, mpumbavu, bozi, fala gulagula”.
Kitendo cha kutumia neno bwege kumuelezea mbunge huyo kilisababisha
wapinzani wacharuke, na kuibua bungeni kesi ya mtu aliyefunguliwa mashtaka
mkoani Arusha kwa kosa la kumuelezea Rais John Magufuli kuwa ni bwege.
Bila ya kuruhusiwa, mmoja alifungua kipaza sauti na kusema: “Hatimaye
msamiati wa bwege watua bungeni sasa kutumika rasmi. Futa lugha ya kuudhi;
bwege bwege.”
Hata hivyo, wabunge hao wa upinzani hawakushinikiza Dk Tulia kufuta kauliz
yake, lakini baadaye wakiwa nje ya ukumbi waliponda kitendo hicho cha
kiongozi huyo wa Bunge ambaye aligombea uspika kwa tiketi ya CCM kabla ya
kujitoa na muda mfupi baadaye kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa mbunge na
hivyo kupata sifa ya kugombea nafasi hiyo ya naibu spika.
Dk Ackson aliamsha tafrani hiyo saa 5:48 asubuhi baada ya Bungara, ambaye
ni maarufu kwa jina la Bwege, kusimama bila kufuata kanuni za Bunge, kupinga
maelezo ya Waziri wa Habari, Nape Nnauye juu ya uamuzi wa Serikali kusitisha
shughuli za Bunge kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini.
“Na wewe Mheshimiwa Bwege, hebu kaa chini. Usionyeshe ubwege wako hapa,”
alisema Dk Ackson kumzuia mbunge huyo asiendelee kuzungumza wakati
mjadala ukianza kuwa mkali.
Mjadala huo uliendelea bila ya wapinzani kuhamaki, lakini baada ya Nape kutoa
taarifa akieleza kuwa uamuzi wa kuanzisha studio za Bunge ulifanywa na
Bunge la Kumi ambalo yeye hakuwamo, ndipo wapinzani walipokumbusha kauli
hiyo ya naibu spika.
“Bunge linaonyeshwa asubuhi na kurudiwa kuonyeshwa usiku na kuna
wanahabari hapa Dodoma wana kamera zao na wanaripoti bunge hili. Tusitumie
bunge hili kupotosha,” alisema Nape kabla ya mbunge wa Iringa Mjini
(Chadema), Mchungaji Peter Msigwa kuingilia kati.
Msigwa: Hii ni taarifa au hotuba?
Spika: Msigwa jifunze kusikiliza kwanza, unaipokea taarifa yake ama vipi?
Msigwa: Taarifa yake naikataa kwa sababu anasema uongo. Leo na wewe
umemuita mtu bwege. Kuna mtu kule Arusha alimuita Rais Magufuli bwege na
akapelekwa mahakamani. Na wewe tutakupeleka mahakamani.
Mkazi huyo wa Arusha, Isaack Habakuk Emily alipandishwa kizimbani takribani
wiki mbili zilizopita akikabiliwa na shtaka la kumuita Rais kuwa ni bwege.
Msigwa alisema Bunge “nalo ni jipu” kwa kuwa haliwezi kuishauri Serikali
kutokana na kufanya maamuzi bila ya kushirikisha makamishna wake, akitoa
mfano wa chombo hicho kurejesha Sh6 bilioni serikalini ambazo zilibanwa
kwenye matumizi yaliyoelezewa kuwa hayakuwa muhimu.
Baada ya Msigwa kumaliza kuchangia, alifuatia mbunge wa viti maalumu
(Chadema), Tunza Malapo ambaye aliungana kauli na Msigwa na kumponda
Nape na uamuzi wa Serikali.
Wakati Malapo akiendelea kuchangia, alisimama Khatibu kutoa taarifa.
“Kwa taarifa yako wewe Malapo aliyelishauri Bunge kutorushwa live ni Nape
vuvuzela,” alisema.
“Kwani kuanzisha studio za Bunge maana yake ni Bunge kutorushwa moja kwa
moja?”
Wakizungumzia tukio hilo la asubuhi, mbunge wa Kalenga (CCM), Godfrey
Mgimwa alisema Dk Tulia alighafilika wakati akitoa kauli hiyo baada ya
kurushiwa maneno mara kwa mara na wabunge wa upinzani, tena bila kufuata
kanuni na taratibu za kibunge.
“Kwanza mtu mwenyewe (Bungara) huwa anapenda kuitwa bwege sasa kama
ukiamua kumuita bwege utakuwa umekosea?” alihoji.
Alisema mara nyingi huibuka mvutano bungeni kwa sababu baadhi ya wabunge
hawataki kuzingatia kanuni za chombo hicho cha kutun ga sheria.
Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Antony Komu alisema: “Kauli iliyotolewa
na Naibu Spika inaonyesha wazi kuwa ni kiongozi anayekiuka misingi, taratibu
na kanuni za Bunge. Tazama anatukana watu tu bila kujali jambo lolote, hii si
sawa kabisa.”
Alisema Bunge linapaswa kuongozwa kwa haki na si kama ilivyo sasa ambayo
inawafanya wabunge wa CCM waonekane kuwa na haki zaidi ya upinzani.
“Mfano (mbunge wa Tarime Vijijini-Chadema, John) Heche aliomba mwongozo
akanyimwa ila Dk Kigwangalla akapewa,” alisema.
Kwa takribani wiki moja Bunge lilikuwa limepoa kutokana na wabunge wa
vyama vya upinzani kususia kuchangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya
Waziri Mkuu, lakini jana walishiriki kwenye mjadala wa wizara ya Ofisi ya Rais
na kurejesha uhai kwenye chombo hicho.
Katika hoja zao jana, wabunge hao walijikita zaidi kuponda Serikali ya Awamu
ya Tano kuwa inakiuka kanuni za utawala bora na kupinga uamuzi wake wa
kusitisha matangazo ya Bunge, jambo lililomlazimu Nape kusimama mara kwa
mara kutetea uamuzi wa Serikali, huku Dk Ackson akitoa ufafanuzi wa kanuni
za Bunge.
Mara zote ambazo Nape na Dk Ackson walikuwa wakitoa ufafanuzi wao,
walizomewa na wabunge hao wa upinzani huku mbunge wa Konde (CUF),
Khatibu Said Haji akimfananisha Nape na “vuvuzela” kwa maelezo kuwa ndiye
aliyeishauri Serikali kusitisha matangazo hayo.
Akichangia mjadala huo, Mchungaji Msigwa alisema utawala bora na
unaozingatia sheria hauanzi na bajeti, bali huanza na utawala bora.
“Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, dhana nzima ya utawala
bora haionekani. Utawala bora ni kuongoza nchi kwa ufanisi, tija na kwa uwazi,
uadilifu, uwajibikaji na ushirikishwaji wa watu kwa kufuata utawala wa sheria,”
alisema.
Alisema ni ajabu Ofisi ya Rais-Utawara Bora kuomba bajeti ya Sh800 bilioni
wakati nchi haina utawala bora. Alirejea kauli ya kiongozi wa upinzani bungeni,
Freeman Mbowe kuwa Serikali inaongozwa bila ya maamuzi yake kuwekwa
kwenye Gazeti la Serikali.
“Walikuwa wanafanya kazi kama sisi tu mawaziri vivuli wa upinzani.Wanatoa
maagizo wakati hawapo kisheria. Huu si utawala bora,” alisema Mchungaji
Msigwa.
Alisema licha ya jambo hilo kubainika wazi Bunge lilikaa kimya huku akidai
kuwa hata baadhi ya mawaziri walikuwa wanajua jambo hilo, na kwamba
wanapokuwa nao katika mgahawa wa Bunge, wamekuwa wakiponda na
kuukosoa utendaji kazi wa Serikali ya Rais Magufuli.
“Mawaziri mnakuwa kama vinyonga. Kwenye chai mnasema ukweli, mkija
bungeni mnakaa kimya.Huwa tunawarekodi na mkibisha tutataja mmoja mmoja
humu ndani,“ alisema Msigwa huku akimtaja Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi
Kigwangalla kuwa ni mmoja wa mawaziri hao baada ya waziri huyo kusimama
kuomba mwongozo, kupinga kauli ya mbunge huyo.
Dk Kigwangalla alitumia kanuni 68 (7) na 63 (1) kuomba mwongozo, akimtaka
Mchungaji Msigwa athibitishe kauli yake kwa kuwataja kwa majina mawaziri
wanaopingana na uongozi wa Serikali.
Dk Ackson naye alitoa ufafanuzi akinukuu kifungu cha 63 (1) (2), kinachomtaka
mbunge kuthibitisha jambo analolisema hapohapo ama apewe muda na
kwamba atatoa maelezo ya kuwataka Dk Kigwangalla na Mchungaji Msigwa
kuwasilisha ushahidi wao.
Msigwa: Mbona Kigwangalla unajihisi mwenye hatia?
Dk Ackson: Msigwa unaongea na kiti usibishane na mbunge.
Msigwa: Mheshimiwa Spika wakati wa kuchangia tunakuwa na taarifa sio
mwongozo ila nashangaa huyu (Dk Kigwangalla) kaomba mwongozo kapewa.
Ila tunaendelea tu ila kiti bado kinayumba.
Dk Ackson: Mbunge anaweza kukosea na wengi tu hukosea. Ametaja kanuni
zinazohusu utaratibu naomba tusiendelee kujibizana.
Akiendelea na mjadala huo Mchungaji Msigwa alisema Bunge la Tisa na la Kumi
yaliendeshwa kwa uwazi mkubwa tofauti na Bunge la Kumi na Moja, kwamba
hata utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne ulikuwa haubani demokrasia na
kuzuia matangazo ya Bunge kurushwa moja kwa moja.
“Bunge ni mkutano wa wazi wa wananchi wote, lakini Serikali hii inaanza
kuminya na kuweka siri. Huu si mkutano wa unyago, tunaongelea matumizi ya
fedha za Watanzania,” alisema.
“Serikali inayokandamiza uwazi ni Serikali iliyojaa uoga na inayoficha madudu.
Mnasimama na kusema mnakusanya fedha za kuvunja rekodi sasa mnaficha
nini kuwaonyesha Watanzania hiki mnachokifanya?”
Huku akiipongeza Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Rais mstaafu Jakaya
Kikwete, Mchungaji Msigwa alisema pamoja na udhaifu wake, ilikuwa haizuii
watu kuzungumza na kusema ukweli.
“Nyinyi mmekuja na ‘hapa kazi tu’, lakini hamtaki kukosolewa. Wakati
tunamkosoa Kikwete wabunge wa CCM mlikaa kimya na kutuzomea, leo
mnaufyata na inaonekana hata Dk Magufuli akidondosha kijiko, mtasimama na
kupiga makofi kwa sababu ya uoga wenu,” alisema Mchungaji Msigwa na
kuwataka wabunge kuhoji mambo kwa maslahi ya wananchi.

Friday, April 29, 2016 Mfanyabiashara Auawa gesti Kwa Kuchomwa Kisu

4/29/2016 11:39:00 am

Mfanyabiashara wa mazao, Eliusta Peter(40), amefariki dunia baada ya
kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni akiwa katika nyumba ya kulala
wageni wilayani Kilombero.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema tukio hilo
lilitokea Aprili 22 baada ya wahudumu wa nyumba ya wageni ya Sayari
kubaini maiti katika chumba namba mbili.
Inadawa Aprili 20 mwanamke huyo akiwa na kijana mmoja ambaye jina lake
limehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi, walifika kwenye nyumba hiyo na kuchukua
chumba kimoja wakisema wao ni wafanyabiashara wa mazao.
“Mwili wa marehemu uligundulika ukiwa kwenye nyumba ya kulala wageni
iitwayo Sayari chumba namba mbili saa 11 jioni na ulipochunguzwa
ikagundulika kuwa kifo kilisababishwa maumivu ya jereha,” alisema Matei.
Mwanamke huyo alikuwa na jeraha kushoto mwa bega lake lililotokana na
kuchomwa na kitu chenye ncha kali
Matei alisema kwa taarifa walizozipata bila shaka kijana aliyekuwa naye
anahusika na mauaji hayo.
Wakati huo huo, jeshi la polisi wilayani Kilosa limemkamata Rogasian Jeremia
kwa tuhuma za kumshambulia mkewe, Faustina Sizayi(25) kwa kumkatataka
kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Mtuhumiwa alikamatwa akiwa anajihusisha na kazi ya ulinzi wa maduka baada
ya polisi kumsaka kwa muda mrefu na ndipo Aprili 24 alikamatwa baada ya
polisi kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Watu Watatu Wanaosadikiwa Kuwa Majambazi Wauawa Katika Jaribio La Uhalifu Wilayani Chunya Mkoani Mbeya

4/28/2016 10:25:00 pm


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA.
Mnamo tarehe 27.04.2016 majira ya saa 20:00 usiku huko katika Kijiji na
Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa
Mbeya, watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliuawa katika
majibizano ya risasi na askari polisi wakiwa katika harakati za kufanya
uhalifu kwenye duka bia la jumla mali ya bwana HAMIS mkazi wa
Matundasi.
Inadaiwa kuwa majambazi hao wapatao watano walikuwa wakitumia
pikipiki mbili huku pikipiki moja ikibeba majambazi watatu na nyingine
majambazi wawili huku wakiwa na silaha aina ya SMG yenye namba
1996 AFU 1120 na risasi 26 kwenye magazine walitaka kufanya uhalifu
kwenye duka la jumla la kuuza bia mali ya HAMISI.
Kutokana na taarifa za siri/intelejensia, Jeshi la Polisi lilijipanga
kukabiliana na majambazi hao na katika majibizano ya risasi, jambazi
mmoja ambaye alikuwa na silaha aina ya SMG yenye namba 1996 AFU
1120, risasi 26 kwenye magazine aliuawa baada ya kujeruhiwa kwa
kupigwa risasi tumboni na mguuni na aliweza kufahamika kwa jina moja
BARAKA, anayekadiliwa kuwa na umri kati ya 35 hadi 38, fundi ujenzi
mkazi wa Makongolosi.
Aidha majambazi wengine wanne walifanikiwa kukimbia kuelekea kijiji
cha Matondo na ndipo askari polisi waliendesha msako mkali kuelekea
kijiji hicho na majambazi hao baada ya kuwaona Polisi waliwasha pikipiki
zao kwa nia ya kukimbia huku wakirusha risasi ovyo ndipo Polisi walijibu
mapigo na kufanikiwa kuwaua majambazi wengine wawili na kukamata
Pikipiki moja yenye namba ya usajili MC 761 AFS aina ya Sanlg
iliyokuwa ikitumiwa na majambazi hao.
Majambazi wengine wawili walikimbia na msako mkali unaendelea ili
kuwakamata. Miili ya marehemu imehifadhi katika Hospitali ya Wilaya
Chunya.
Wito:
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi Butusyo A. Mwambelo anatoa wito kwa wananchi kuendelea
kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za siri ili kuzuia vitendo
vya kihalifu mapema kabla ya kutokea.
Imesainiwa na:
[BUTUSYO A. MWAMBELO – SSP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Thursday, April 28, 2016 Vipaza Sauti Vya Bunge Vyaharibika, Bunge Lasimama kwa Dakika 30

4/28/2016 04:31:00 pm

Shughuli za Bunge la Muungano leo zilisimama kwa dakika 30 kabla ya
kuendelea tena, baada ya vipasa sauti vya ukumbini kushindwa kufanya
kazi

Spika wa Bunge, Job Ndugai amelazimika kuahirisha shughuli mara
baada ya kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu
ambacho hata hivyo wabunge walichukua muda mrefu kuuliza maswali
kutokana na kuhama hama wakitafuta mahali pa kusikika.

Awali, wabunge waliokuwa na nafasi ya kuuliza maswali walilazimka
kuhama maeneo yao na kuzua minong’ono ndani ya ukumbi, huku
Mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega na Mbunge wa Manonga
(CCM), Seif Gulamali wakilazimika kuuliza maswali yao wakiwa uso kwa
uso na Waziri Mkuu mbele ya ukumbi.

Hata hivyo, kuna hali ya sintofahamu, kwani vipaza sauti vimeharibika
ikiwa ukumbi huo umefanya kazi kwa siku sita tu tangu ulipokabidhiwa
baada ya ukarabati mkubwa.

April 18, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alikabidhiwa ukumbi
huo ikielezwa kuwa ulikuwa umefanyiwa matengenezo makubwa katika
maeneo mbalimbali kwa lengo la kuuboresha.

Thursday, 28 April 2016 Mwili wa Papa Wemba wawasili DRC

4/28/2016 03:06:00 pm

Mamia ya watu wamekongamana nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa
kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka
Abidjan

Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki
wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya
mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za
mwisho.

Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka
mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo mwanamuziki
huyo alianguka alipokuwa akiimba.Mwanahabari wa BBC Tamasin Ford
anasema kuwa mashabiki wengi walivalia nguo nyeusi na kubeba mishumaa ili
kutoa heshima kwa nguli huyo wa muziki.
Mkewe Papa Wemba na wasaidizi wake pia walikuwepo.

Thursday, April 28, 2016 Madiwani wa Chadema Wilayani Hai Wasusa Kuhudhuria Kikao cha Mkuu wa Mkoa Said Meck Sadiki

4/28/2016 03:00:00 pm


Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wakiongozwa na Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo, Helga Mchomvu, wamesusa kuhudhuria kikao cha Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki wakati akizungumza na viongozi wa
vitongoji, vijiji, kata, viongozi wa taasisi za serikali na dini.
Sadiki alifika wilayani Hai jana, ikiwa ni moja ya ziara zake katika wilaya zote
za Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kuzungumza na
viongozi mbalimbali wanaowakilisha wananchi, pamoja na kusikiliza kero
zinazozikabili wilaya hizo.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri,
Usharika wa Hai Mjini, madiwani hao ambao wote ni wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hawakuonekana hata mmoja huku eneo
walilokuwa wameandaliwa likibaki na viti vilivyo wazi.
Awali, Mkuu wa Mkoa alipowasili ofisini kwa Mkuu wa Wilaya kwa lengo la
kupokea taarifa ya wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mchomvu aliwasili kwa
kuchelewa na muda ulipofika wa kuelekea ukumbini, alitokomea kusikojulikana.
Hali hiyo ilimshangaza Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ambaye
alisema siasa ziliisha baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana,
lakini inashangaza kwenye masuala ya maendeleo ya wananchi bado viongozi
wanaendelea kuziendekeza.
Byakanwa alisema, licha ya madiwani wote 17 wanaounda Baraza la Madiwani
Wilaya ya Hai kuwa ni wa Chadema, bado wanasimamia na kutekeleza Ilani ya
Chama Cha Mapinduzi ambacho ndicho chama kilichopewa ridhaa na
Watanzania kuongoza kwa awamu nyingine ya tano.
“Ni jambo la kushangaza kuona viongozi waliochaguliwa na wananchi
wanashindwa kuwakilisha wananchi wao katika kupeleka na kuzisemea kero zao
mbalimbali zinazowakabili, na badala yake wamekuwa wakisusa vikao vya
kupanga maendeleo. Kwa siasa hizi wananchi hawawezi kupata maendeleo,”
alisema Byakanwa.
Akiwasilisha taarifa za kutofika kwa madiwani hao, Katibu wa Mbunge wa
Jimbo la Hai, Rosemary Kuringe alisema, amewasiliana na madiwani wake na
kuelezwa kuwa hawakupata taarifa za ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa.
Akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na viongozi mbalimbali, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Saidi Mderu alikiri kutoa taarifa
kwa madiwani wote katika kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani
kilichofanyika Aprili 22, mwaka huu.
“Kwa suala hili la viongozi hawa kususa, namwachia Mungu, niliwapa taarifa
madiwani wote tena nilisisitiza, cha kushangaza wakati Mkuu wa Mkoa
amewasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri alifika
akiwa amechelewa lakini wakati tumekuja kwenye ukumbi hatukumuona,”
alisema Mderu.

Thursday, April 28, 2016 Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC

4/28/2016 02:17:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),
Bi. Juliet Kairuki kuanzia tarehe 24 Aprili mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa Biashara na
Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, imesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya rais
Dkt. Magufuli kupata taarifa kuwa Mkurugenzi huyo alikua hachukui mshahara
wa serikali tangu alipoajiriwa mwaka 2013 jambo ambalo linazua maswali
mengi.
Aidha, taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu huyo imeongeza kuwa endapo
Bi. Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanyakazi na Serikali ya Awamu ya Tano
atapangiwa kazi nyingine. Mchakato wa kumpata Mkuregenzi mpya umeanza
mara moja.
Kwa mujibu wa Prof. Mkenda kwenye taarifa yake hiyo amesema Bw. Clifford
Katondo Tandali, atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho cha
Uwekezaji nchini TIC.

Thursday, April 28, 2016 Wabunge Mabubu kubanwa Bungeni ,Ni wale wanaoshiriki Vikao vya Bunge Lakini Hawachangii Chochote

4/28/2016 10:37:00 am


Kiti cha Spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Sheria
pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi aliyofanya
bungeni, badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio pekee.
Aidha, kimewataka wabunge kubadilika na kuacha tabia ya kuchukua posho za
vikao vya Bunge bila kuzitolea jasho.
Kauli hiyo imekuja kutokana na Mwongozo ulioombwa Aprili 25, mwaka huu na
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ambaye alikitaka kiti cha Spika
kutoa Mwongozo kuhusu usahihi wa wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni kulipwa posho na mishahara wakati hawashiriki na kutimiza wajibu
wao wa kuchangia kwenye mjadala wa Bunge la Bajeti linaloendelea katika
Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11.
Bashe alisema mbunge huyo alitumia Kanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu za
Bunge akiomba Mwongozo wa Spika kutokana na Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, kuamua kutoshiriki mjadala unaoendelea bungeni, lakini wabunge hao
wanasaini na kulipwa mishahara na posho.
Hivyo akaomba Mwongozo endapo ni haki kwa wabunge hao kupokea posho
wakati hawashiriki wala kutimiza wajibu wao wa kisheria.
Katika kujenga hoja hiyo, Bashe alitumia Ibara ya 63(3) ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania isemayo, “Kwa madhumuni ya utekelezaji wa
madaraka yake Bunge laweza kujadili utekelezaji wa kila Wizara wakati wa
Mkutano wa Bunge wa kila mwaka wa bajeti.”
Aidha, Bashe alitumia Ibara ya 73 ya Katiba ya Tanzania kufafanua kuhusu
malipo ya mshahara, posho na malipo mengine kwa wabunge.
Akitoa Mwongozo wa Spika, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alisema
kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Ibara ya 73 imeainisha masharti ya kazi ya
wabunge.
Alisema mbunge anastahili kulipwa mshahara kwa kila mwezi, na kufafanua
kuwa mbunge anapohudhuria vikao bungeni na kamati atalipwa posho ya vikao
kwa kiwango kitakachowekwa na Serikali na Kanuni za Bunge.
Alisema malipo ya mshahara ni suala la Kikatiba na Sheria hulipwa kwa mbunge
kutokana na kazi yake ya ubunge.
Hivyo malipo ya posho kwa wabunge yanatokana na mahudhurio yao bungeni
na siyo kwa kuchangia kama ambavyo wengi wao wanapenda iwe hivyo.
“Kimsingi kuhudhuria bungeni pekee siyo njia inayopendeza kwa kuwa mbunge
anapofika bungeni anatarajiwa atekeleze majukumu yake yalivyoainishwa katika
Ibara ya 63.
“…Tabia hii ya kutochangia mijadala na kuzunguka zunguka bungeni haikubaliki
na haitakiwi kuendelea, kila mbunge atekeleze wajibu wake na sio anahudhuria
ili alipwe posho,” alisema Dk Ackson.
Wakati huo huo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko katika
Kamati mbalimbali za Bunge, kwa kubadilisha wabunge 16 wa Kamati za Awali
kwenda nyingine.
Aidha, Spika amewapangia Kamati wabunge wapya wanne, walioapishwa
mwanzoni mwa Mkutano huu wa Bunge, ambao ni Shamsi Vuai Nahodha, Rita
Kabati, Oliver Semuguruka na Lucy Owenya.

Thursday, April 28, 2016 Serikali Kuwasilisha Mswada wa wa sheria wa Ndoa.

4/28/2016 10:06:00 am

Serikali imejiandaa kuleta Muswada wa Sheria bungeni kutoa haki ya kusoma
kwa watoto wote wa kike na kiume wa shule za msingi, sekondari na
kutoruhusiwa kuoa au kuolewa.

Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali
inaendelea kukamilisha utaratibu wa kupata maoni ya wananchi kuhusu
marekebisho ya Sheria ya Ndoa na kutungwa kwa Sheria mpya ya Mirathi na
Urithi kuondokana na mkanganyiko uliopo kuhusu sheria hiyo.

Bunge lilielezwa hayo jana mjini Dodoma wakati waziri huyo akijibu swali la
nyongeza la Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene (CCM) aliyehoji ni lini serikali
itaanza maandalizi ya kuchukua maoni juu ya kufanya marekebisho sheria ya
ndoa ya mwaka 1971.

Akijibu swali hilo, Dk Mwakyembe alisema hatua za awali zimeshaanza
kuchukuliwa na wizara hiyo ili kupata maoni ya wananchi juu ya marekebisho
ya sheria hiyo ya ndoa ya mwaka 1971 na kutungwa kwa sheria mpya ya
mirathi na urithi.

Alisema serikali ina nia ya dhati ya kufanyia marekebisho sheria ya ndoa na
kwamba mchakato huo ulisitishwa kwa kuwa Tume ya mabadiliko ya Katiba
ilikuwa ikikusanya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba , hivyo walidhani
wananchi wangetoa pia maoni juu ya sheria hiyo.


Waziri wa Katiba na Sheria  Dkt.Harrison Mwakyembe.

Wednesday, April 27, 2016 Rais Magufuli Awaapisha Makatibu Tawala Wapya Wa Mikoa

4/27/2016 10:50:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewaapisha Makatibu Tawala wapya kumi aliowateua tarehe 25 Aprili, 2016
na kuwapangia vituo vyao vya kazi.
Makatibu Tawala hao wameapishwa leo tarehe 27 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar es
salaam na kisha wametia saini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa
umma, zoezi lililoendeshwa na Kamishna wa maadili Sekreatieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, Mheshimiwa Jaji Salome Kaganda na kushuhudiwa na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Makatibu Tawala walioapishwa ni;
1. Arusha - Richard Kwitega
2. Geita - Selestine Muhochi Gesimba
3. Kagera - Armatus C. Msole
4. Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
5. Pwani - Zuberi Mhina Samataba
6. Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
7. Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
8. Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
9. Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
10. Tanga - Eng. Zena Said
Makatibu Tawala wengine wa Mikoa ambao hawakuapishwa leo, ni wale
waliohamishwa vituo vya kazi na wale waliobaki katika vituo vya kazi
walivyokuwep,o ambao tayari walishakula kiapo cha kuwa Katibu Tawala wa
Mkoa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaa
27 Aprili, 2016

Wednesday, April 27, 2016 Picha za jinsi katibu mpya wa EAC alivyokaribishwa

4/27/2016 09:41:00 pm

ARUSHA

Jumuiya ya Afrika Mashariki  imeendelea na hatua yakubadilishana uongozi ambapo sasa hivi Katibu Mkuu Dr Richard Sezibera  kutoka Rwanda amemaliza muda wake nakumkaribisha Katibu mpya kutoka Burundi Liberat  Mfumukeko kuendelea na nafasi hiyo   nimezinasa picha za kwanza wakati wa makabidhiano

Dr.Richard  Sezibera amabaye amemalizamuda wake akimkaribisha Katibu mpya wa EAC kutoka nchini Burundi Liberat Mfumukeko.


Dr.Richard Sezibera akisalimiana na Katibu mpya wa EAC Liberat Mfukeko kutoka nchini Uganda


Picha ya pamoja
m

Wednesday, April 27, 2016 Polisi Temeke Wakamata 'Panya Road 18

4/27/2016 09:34:00 pm


Jeshi la Polisi linawashikilia vijana zaidi ya 18 wenye umri kati ya miaka 14 na
20 kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo ya Wilaya
ya Temeke.

Kamanda wa polisi wa Temeke, Gilles Muroto amesema leo kuwa vijana hao,
wanaohusishwa na kundi la Panya Road linalofanya unyang'anyi maeneo ya jiji
la Dar es Salaam, walikamatwa jana nyakati tofauti baada ya polisi kuendesha
msako wa kuzuia na kupambana na wahalifu.

Alisema vijana hao wanatoka maeneo ya Buza Kanisani, Chanika, Yombo
Kirakala, Buza Changulu, Yombo Makangawe na moja anayeishi maeneo ya
Mwananyamala lakini alikamatwa Temeke.

"Kama Kamanda Simon Sirro alivyosema kuwa ni lazima wahalifu wadhibitiwe
katika mko huu. Temeke hatuwez kumwangusha, tunatekeleza agizo lake,"
alisema Kamanda Muroto.

Alisema vijana hao wanajihusisha na vitendo vya uporaji wa mali mbalimbali
kuanzia mitaani, pia kujeruhi watu hali inayosababisha wakazi wa eneo husika
kuishi kwa hofu.

Alisema upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa
hatua za kisheria.

Wakati huohuo, Kamanda Muroto amesema polisi inashikilia mwanamke mmoja
mwenye umri wa miaka 38, mkazi wa Buza baada ya kumkuta na puli 120 za
dawa za kulevya aina ya bangi.

Wednesday 27April,2016. Ripoti ya CAG Yawaweka Kikaangoni Vigogo wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD)

4/27/2016 12:15:00 pm

Ripoti iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Profesa Musa Juma Assad imezichanganya Hospitali ya Taifa Muhimbili na
Bohari ya Dawa (MSD), huku Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu akihitaji maelezo ya kina kuhusu mkanganyiko huo.
Ummy ameitaka MSD kuandika maelezo ya kina kwa maandishi, kuhusu vifaa
vya Sh2 bilioni ambavyo viko njiani kwenda Muhimbili kwa miaka minne sasa,
kabla wizara yake haijatoa tamko rasmi.
Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu jana alisema bohari haina mzigo
wowote ulio njiani kuelekea Muhimbili bali imekuwa ikisambaza dawa zake nchi
nzima.
Bwanakunu alisema tatizo lililojitokeza ni mfumo wa kompyuta ambao
unaonyesha mzigo upo njiani, hivyo muamala katika kompyuta unavyoshindwa
kukamilika, mzigo lazima uonekane upo njiani.
“Mwaka 2012 tulibadilisha mfumo wa kompyuta kutoka wa awali mpaka
tunaotumia sasa, hivyo kuna miamala ilihitaji kubadilishwa, mwaka huu
tulifanya zoezi la kukamilisha baadhi na si kwa Muhimbili pekee kwa mfano
kuna mzigo unatoka MSD Ubungo kwenda Muleba ukifika kule mtu anashindwa
kuingiza kwenye mfumo kwamba umepokelewa,” alisema Bwanakunu.
Alifafanua kwamba majibu ya MSD kwa CAG yalieleza kuwa walitengeneza timu
ya uchunguzi na baadhi ya watu walichukuliwa hatua, “nimeshachukua hatua
za haraka baada ya kupata hiyo ripoti, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wale
ambao hawakujaza hiyo miamala tulishawachukulia hatua, hakuna mali
iliyopotea MSD.”
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba kuna ripoti ya Muhimbili ambayo inaonyesha
katika vitabu kwamba kuna mzigo ambao Muhimbili iliununua kutoka MSD,
lakini haujafika, lakini Bwanakunu alipoulizwa alisema hakuna vitabu
vinavyoonyesha kuwa Muhimbili inadai vifaa tiba na dawa MSD.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru
alisema kwa taarifa alizonazo mpaka sasa CAG alifanya ukaguzi katika vitabu
vya MSD na si wao na alipouliza vifaa viko wapi alijibiwa kuwa vinakwenda
MNH.
Alisema kuwa Watanzania wawe na subira na kwamba watapewa majibu kesho
(leo), baada ya Muhimbili kupekua kwa kina vitabu vya mwaka 2012, ili
kujiridhisha iwapo vifaa vilipokelewa au havikuwahi kununuliwa Muhimbili.
“Hiyo ripoti tumeiona leo Jumanne. Hayo mambo yametokea mwaka 2012
huwezi kuwa na jibu la kila kitu, kesho tunataka tukapitie hiyo ripoti kwa
sababu ni ukaguzi wa MSD, tukaangalie vitabu hivyo vifaa vilifika?” Alisema
Museru.
Naye Waziri Ummy Mwalimu alisema katika ripoti hiyo kuna hoja mbili ambazo
ni MSD na TFDA, huku akifafanua kwamba amezungumza na Mkurugenzi wa
MSD lakini hajaridhika na majibu na kumtaka aandike maelezo ya kina.
“Nimetaka maelezo ya maandishi kutoka kwa MSD na TFDA kuhusu ripoti ya
CAG tumekubaliana na Katibu Mkuu walete maandishi ndiyo tutatoa msimamo
rasmi wa wizara, kwa upande wa MSD ndiyo maana tuliweka pembeni wale
wakurugenzi wanne sababu ya changamoto hii ambayo CAG amekutana nayo,”
alisema Ummy.

Rais John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 3,551, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Muungano wa Tanzania

4/27/2016 08:58:00 am


Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja
Jenerali Projest Rwegasira ilisema wafungwa 580 wataachiwa huru, huku
wengine 2,971 watapunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao.

Alisema rais ametoa msamaha huo kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya
ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliwataja watakaonufaika na msamaha huo kuwa ni wafungwa wenye ugonjwa
wa ukimwi, kifua kikuu na saratani ambao wapo kwenye hatua za mwisho.
Wengine ni wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, wajawazito na wale
waliongia na watoto gerezani.

Wafungwa wengine watakaonufaika na msamaha huo ni wenye ulemavu wa akili
ambao wamethibishwa na jopo la waganga kuwa wana tatizo hilo.
Katibu mkuu wa wizara hiyo alisema msamaha huo hautawagusa wafungwa
waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa au kifungo cha maisha jela.

Pia, wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya usafirishaji na matumizi
ya dawa za kulevya, upokeaji na utoaji rushwa, matumizi mabaya ya madaraka,
unyang’anyi kwa kutumia silaha na kubaka ni miongoni mwa waliokosa
msamaha huo.

Wengine ambao hawataguswa na msamaha huo ni wale wanaotumikia vifungo
kwa makosa ya kupatikana na silaha, wizi wa magari na pikipiki, kuwapa
mimba wanafunzi na ubadhirifu wa fedha za Serikali.

Wafungwa wengine watakaoendelea kubaki magerezani ni wale waliohukumiwa
kutokana na usafirishaji wa nyara za Serikali na ujangili, utekaji wa watoto,
biashara ya binadamu, kukutwa na viungo vya binadamu na waliojaribu
kutoroka wakiwa chini ya ulinzi.

Katika maadhimisho ya Uhuru yaliyofanyika Desemba 9, 2015, Rais Magufuli
aliwasamehe wafungwa 2,336, kati ya hao 117 waliachiwa huru huku 2,219
wakipunguziwa moja ya sita ya vifungo vyao.

Kwa idadi hiyo mpaka sasa wafungwa 5,887 wamenufaika na msamaha wa
Rais Magufuli tangu aingie madarakani baada ya kushinda katika Uchaguzi
Mkuu Oktoba 25, 2015.

Wednesday, April 27, 2016 Mwenyekiti Aweka Majina HEWA Mradi wa Kuokoa kaya Masikini (TASAF

4/27/2016 07:05:00 am


Wananchi wamemkataa mwenyekiti wa kitongoji cha Mwanogi kijiji cha Bulima,
Kata ya Nyashimo wilayani Busega katika Mkoa wa Simiyu, wakimtuhumu
kuweka majina hewa katika mradi wa kuokoa kaya masikini unaosimamiwa na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf).

Mwenyekiti huyo wa kitongoji, Ester Ng’ombe anatuhumiwa pia kufanya kazi
kwa ubaguzi wa vyama vya siasa.

Akizungumza katika kikao, mwenyekiti wa kamati ya mipango na fedha ya kijiji
cha Bulima, Zablon Ntinika alisema wamefikia uamuzi wa kumsimamisha kazi
mwenyekiti huyo baada ya uchunguzi walioufanya kubaini majina matano
ambayo ni hewa yakipatiwa fedha.

Alisema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa mwenyekiti huyo
katika utendaji wake wa kazi katika kitongoji hicho lakini wamebaini mengi.
Mwenyekiti huyo anayetuhumiwa, alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema kuwa
yeye hayatambui bali ni siasa za chuki dhidi yake.

Ng’ombe alisema chanzo si majina feki bali ni siasa zinazochochewa na
wanasiasa wa kata hiyo ambao wanataka kuichafua sifa yake ili aweze
kuondolewa na wananchi waliomchagua.

Wednesday, April 27, 2016 Mwanafunzi Amkaanga kortini polisi anayedaiwa kumbaka katika kibanda cha ulinzi cha benki.

4/27/2016 07:00:00 am

Mwanafunzi wa kidato cha tatu, juzi alimkaanga askari polisi anayedaiwa
kumbaka kwa kuieleza Mahakama jinsi alivyotendewa kitendo hicho katika
kibanda cha ulinzi cha benki.

Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Misungwi, Ruth
Mkisi, shahidi huyo alidai siku ya tukio askari huyo, Raphael Sixstus (30),
alimuita alipokuwa akipita karibu na Benki ya CRDB Tawi la Misungwi,
alipoitikia wito ghafla alivutiwa ndani ya kibanda hicho na kumbaka.

“Wakati akinitendea kitendo hicho, alikuwa akinitishia kisu huku akiniambia
nikipiga kelele ataniua, niliogopa nikaa kimya ingawa niliumia na kutokwa damu
nyingi sana,” alidai shahidi huyo.

Akiongozwa na Mwendasha Mashtaka wa Polisi, Doreth Mgenyi, mwanafunzi
huyo mwenye umri wa miaka 16 alidai kabla ya kumbaka, mshtakiwa huyo
alimvua nguo zote za ndani.

Awali, Mwendesha mashtaka alipokuwa akimsomea makosa mshtakiwa huyo
alidai kuwa Novemba 20, mwaka jana, akiwa eneo la lindo katika Benki ya CRBD
Tawi la Misungwi, alimbaka mwanafunzi huyo saa 1.00 usiku wakati akitoka
mashine kusaga unga katika maeneo ya Bomani.

Hakimu Mkisi aliahirisha kesi hiyo hadi leo itakapoendelea kusikilizwa kwa
upande wa mashtaka kuita mashahidi wengine. Mshtakiwa yuko nje kwa
dhamana.

Aliyevumbua “Please Call Me” ashinda kesi 26 Aprili 2016

4/26/2016 02:46:00 pm


Mahakama ya Kikatiba nchini Afrika Kusini imeiamuru kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom kumlipa mwanamume aliyebuni wazo la kutuma
ujumbe wa kumuomba apigiwe simu.

Gazeti la Sowetan la Afrika Kusini linasema mwajiri wa zamani wa Vodacom
Nkosana Makate aliambia mahakama kwamba huduma ya "please call me"
ilitokana na wazo lake.

Huduma hiyo humuwezesha anayetumia simu kutuma ujumbe bila malipo kwa
wateja wengine akiwaomba wampigie simu.
Tovuti ya Tech Central ya Afrika Kusini inasema uamuzi wa kesi hiyo, ambayo
imesikizwa tangu 10, itakuwa na athari kubwa.

Haijabainika Bw Makate atalipwa pesa ngapi na Vodacom.
Lakini awali amewahi kuambia Moneyweb kwamba uvumbuzi huo wake
ulizalishia kampuni hiyo karibu randi 70 bilioni za Afrika Kusini ($5bn; £3bn) na
alitaka alipwe 15% ya pesa hizo.

Tuesday, April 26, 2016 Breaking Newa: Rais Magufuli Aivunja Bodi ya TCRA na Kumsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hiyo Dr Ally Yahaya Simba

4/26/2016 02:27:00 pm


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ameivunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na
kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya
Simba kutokana na kutosimamia ipasavyo Mkataba wa utekelezaji wa mfumo
wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), na kusababisha nchi kupoteza
mapato ya takriban shilingi bilioni 400 kwa mwaka.

Rais Magufuli amechukua hatua hiyo leo tarehe 26 Aprili, 2016 Ikulu Jijini Dar
es salaam baada ya kufanya kikao cha kazi kati yake na viongozi na wataalamu
kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Wizara ya fedha na
Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Tarehe 22 Machi, 2013 Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) iliingia mkataba
na kampuni ya SGS juu ya uwekaji, uendeshaji na uhamishaji wa mapato ya
simu ambapo kampuni hiyo ilipaswa kutekeleza vipengele vitano lakini mpaka
sasa kampuni ya SGS haijaanza kutekeleza kipengele kidogo kinachohusiana na
uthibiti wa mapato ya simu za ndani (Offnet), hali ambayo imesababisha

serikali kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi bilioni 400 kwa mwaka.
Pamoja na kuivunja bodi ya TCRA inayoongozwa na Profesa Haji Semboja na
Kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba, Rais
Magufuli pia amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Profesa
Makame Mbarawa Mnyaa kumteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo
mara moja.

Aidha, Rais Magufuli amewataka Waziri Prof. Mbarawa, Katibu Mkuu na Naibu
Katibu katika wizara hiyo kuchukua hatua mara moja ili mfumo wa ukusanyaji
wa mapato ya simu kwa simu za ndani (Offnet) uanze kufanya kazi, na nchi
ipate mapato yanayostahili kukusanywa.

“Waziri hakikisha unachukua hatua mara moja, nataka tukusanye mapato yote
ya serikali yanayostahili na sitasita kuchukua hatua dhidi ya yoyote
atakayekwamisha jambo hili” Amesisitiza Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
26 Aprili, 2016

Tuesday 26 Aprili 2016 Aliyekuwa mke wa Rais wa zamani Nchini Kenya Lucy Kibaki amefariki.

4/26/2016 01:48:00 pm

Lucy alifariki katika hospitali ya Bupa Cromwell mjini London. Alisafrishwa hadi
mjini Landon wiki moja iliopita kwa matibabu.

Akithibitisha kifo chake rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa kenya
imesikitishwa na kifo cha mama Lucy mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai
Kibaki.

Katika taarifa iliotumwa katika vyombo vya habari Uhuru amesema bi Lucy
amekuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Amesema kuwa Kenya imempoteza mwanamke aliyechangia mengi katika
maendeleo ya taifa la Kenya hususan katika vita dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.
Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mtangulizi wake Mwai Kibaki pamoja
na familia yake.


Aliyekuwa mke wa zamani wa Nchi ya Kenya Mama Lucy Kibaki amefariki dunia.

Tuesday, April 26,2016 .Ripoti ya CAG Yaanika 'Madudu' Kibao Serikalin

4/26/2016 10:58:00 am

iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha ana
kazi kubwa zaidi kupata ushindi kwenye vita hiyo.
Ripoti hiyo ya mwaka 2014/ 2015 iliyowasilishwa bungeni jana na CAG Mussa
Juma Assad imeibua uozo zaidi kwenye halmashauri, taasisi za Serikali na
mashirika ya umma, ikibainisha kuwa nchi ina tatizo kubwa zaidi ya watu
ambao wamekuwa wakishughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Ripoti hiyo ya pili ya Professa Assad tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo mwaka
juzi, imegusa taasisi zilizowahi kuwa chini ya Rais John Magufuli na Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi Asha Rose
Migiro, ambaye alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba.
Ripoti hiyo pia inaonyesha ufisadi katika ununuzi na uingiaji mikataba
uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), matumizi yasiyo ya lazima
kwenye Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Jeshi la Wananchi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi na mkoa
wa Tabora.

Pia ripoti hiyo imebainisha kuwa mapendekezo mengi ambayo CAG amekuwa
akiyatoa kwa takribani miaka saba sasa, hayatekelezwi.
Katika ripoti hiyo, CAG anaonyesha dosari kwenye utendaji wa Wakala wa
Huduma za Ufundi na Umeme (Temesa), na Wakala wa Barabara (Tanroads),
taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi ambayo wakati huo ilikuwa ikioongozwa
na Dk Magufuli.

Profesa Ndalichako alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania
(Necta), wakati NEC imeguswa na ripoti hiyo katika suala la mchakato wa
kuandika Katiba upya ulioongozwa na Wizara ya Katiba na Sheria.
Ripoti hiyo ya Profesa Assad pia imebainisha kuwa Deni la Taifa, ambalo
hutokana na fedha zinazopowa kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya
kugharimia matumizi ya Serikali, limekuwa kwa tofauti ya Sh7 trilioni.
Tangu aingie madarakani Novemba 5 mwaka jana, Dk Magufuli amekuwa
akitumia ripoti zilizopita za CAG kusimamisha kazi au kutengua uteuzi wa
watumishi wa umma wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi, lakini amekuwa
akikosolewa kuwa hajaweka mfumo wa kukabiliana na hali hiyo.

Katika ripoti hiyo, CAG anasema Temesa ilinunua kivuko chenye kasi ndogo
kuliko ilivyotarajiwa na hadi ulipokuwa unafanyika ukaguzi Agosti 2015, chombo
hicho kilikuwa hakifanyi kazi kwa zaidi ya mwaka.
“Kuhusu dosari katika ununuzi wa kivuko chenye thamani ya Sh7,916,955,000,
Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Umeme, mitambo na ufundi (Temesa)
iliingia mkatabana M/s Johs.Gram-Hanssen Bergensgade 10, DK 2100
Copenhagen Oe Denmark wa ununuzi wa kivuko cha Dar es Salaam –Bagamoyo
chenye thamani ya Dola za Marekani 4,980,000 bila Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT),” anasema CAG.

“Dosari zifuatazo zilibainika katika manunuzi hayo. Kasi ya kivuko haikuzingatia
matakwa ya mnunuzi. Ripoti ya mtaalamu wa ukaguzi ilibainisha kwamba
kiwango cha juu na chini cha kasi ya kivuko wakati wa majaribio kilikuwa na
kiwango kati ya knots 19.45 na knots 17.25 kinyume na makubaliano
yaliyoainishwa kwenye mkataba wa kasi ya kiwango cha 20,” anafafanua.
“Pili kivuko kilikabidhiwa bila hati ya makabidhiano Novemba 17, 2014 baada ya
ucheleweshwaji wa siku 16; Pia nilibaini kwamba mpaka wakati wa ukaguzi,
Agosti 2015, hati ya makabidhiano ilikuwa haijatolewa na mzabuni.”

Ununuzi wa feri hiyo uliwahi kuzua sakata bungeni huku wabunge wa upinzani
wakilalamika kwamba kilikuwa bomu kwani kinatumia zaidi ya saa tatu kati ya
Dar es Salaam na Bagamoyo badala ya dakika 45 za gari.
Eneo jingine lililoguswa na CAG ni la malipo yaliyofanywa na Tanroads kwa
makandarasi waliomaliza kazi zao. Kwamba moja ya matatizo makubwa ya
taasisi hiyo ni udhaifu katika menejimenti.
“Wakala wa Barabara (Tanroads) iliingia mikataba mbalimbali ya ujenzi wa
barabara na madaraja.

"Wakati wa ukaguzi nilibaini kwamba baadhi ya mikataba haikukamilika kwa
muda uliopangwa kutokana na kuchelewa kwa ulipaji wa fedha.
"Pia, nilibaini kwamba ucheleweshwajiwa malipo ya kati ya mikataba 16
ulisababisha ulipaji wa riba kiasi cha Sh 5,616,652,022 na Dola za Marekani
686,174.86, ” alisisitiza CAG.
Profesa Assad amezungumzia pia ukaguzi maalumu alioufanya kuhakiki fedha
zilizowahi kutolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa taasisi
mbalimbali zilizoko chini yake.

Ukaguzi huo ulifanywa kutokana na ombi lililowasilishwa na katibu wa Bunge
kwa barua yenye Kumb. NaCBC.155/188/01/26 ya Desemba 19, 2013.
Bunge lilitaka kujua kama fedha zilizotolewa na wizara hiyo kwenda idara na
taasisi zilizo chini yake zilipokewa na kutumiwa na wahusika kama
ilivyopangwa.

Katika ukaguzi huo, CAG alibaini kasoro katika vitabu vya akaunti za fedha vya
Necta mwaka 2010, Sekretarieti ya Elimu ya Jumuiya ya Madola, Chuo Kikuu
Huria (OUT), na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (Adem).
“Udanganyifu wa malipo ya Sh185,350,000 yaliyolipwa Necta. Aprili 2010 kiasi
cha 185,350,000 kilitumwa Necta kama matumizi ya kawaida. Wakati wa
ukaguzi ilibainika kuwa kiasi hiki cha fedha hakikuandikwa kwenye vitabu vya
uhasibu vya Necta. Hata hivyo, ilibainika kuwa stakabadhi ya mapokezi ya
fedha hizo iliyotolewa na watumishi wasio waaminifu wa Necta ilikuwa ya
kugushi,” anasema.

“Kuhusu fedha zilizopelekwa OUT ni kwamba kati ya mwaka 2009/2010 Wizara
ilihamisha Sh90,000,000 kwenda Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, ni kiasi
cha Sh40,734,000 ambacho kilipokewa huku Sh49,266,000 hakijulikani.
“Pia katika mwaka wa fedha 2010/2011 Wizara ilipeleka OUT Sh10,486,252,913
lakini ni Sh10,427,109,020 tu zinazoonekana kwenye vitabu huku Sh59,143,893
zikiwa hazimo kwenye vitabu.”

Vilevile, CAG amesema katika ukaguzi huo Sh188, 838,528 zilizopelekwa Adem
mwaka 2009/2010 zimeyeyuka. Mwaka huo Wizara ilipeleka Sh712,798,788 kwa
taasisi hiyo, lakini vitabu vinaonyesha Sh523,960,260 zilipokewa na kurekodiwa,
huku Sh188, 838,528 zikikosekana kwenye vitabu.
Mbali ya CAG kuonyesha madudu katika matumizi ya fedha, pia ameonyesha
matumizi mabaya ya Sh7,080 milioni katika mchakato wa uchapaji Katiba
Inayopendekezwa.

“Katika ukaguzi wangu nilibaini kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ilipokea fedha
kiasi cha Sh7,125 milioni kwa ajili ya kulipia gharama za kuchapisha vitabu vya
Katiba Inayopendekezwa.
"Kutokana na ufinyu wa muda, Wizara iliomba na kupewa kibali na Wakala wa
Huduma za Manunuzi Serikalini kufanya manunuzi kwa njia ya dharura kupitia
barua yenye kumbukumbu Na CAD.124/318/01/25 ya Desemba 11, 2014,”
anasema CAG.

“Katika ukaguzi wangu nilibaini vitabu vya katiba vilipokelewa kabla ya kuingia
mkataba. Nilibaini kuwa mkataba ulisainiwa Februari 2, 2015, lakini vitabu vya
katiba vilipokelewa Januari 26, 2015.”
Ukaguzi uliofanywa Oktoba Mosi, 2015 umebaini kuwa nakala 158,003 za Katiba
Inayopendekezwa zenye thamani ya Sh559,330,620 bado viko stoo au
havijatumwa kwa wananchi ili vitumike kwa uhamasishaji

“Kwa hiyo, haikuwa rahisi kujua kama thamani halisi ya fedha ilipatikana na lini
vitabu hivi vitasambazwa kwa walengwa. Pia, ilibainika kuwa vitabu hivyo
havikujumuishwa kwenye Taarifa za Fedha za Mwaka husika,” anasema.
Katika ripoti hiyo ya mwaka 2015/16, CAG Assad anasema ukaguzi wake
umebaini matumizi ya mabilioni ya fedha katika ununuzi wa vitu visivyokuwa
vya lazima au bila kuonyesha ushahidi wa malipo husika.

Alibainisha matumizi ya zaidi ya Sh53 bilioni zilizotumiwa na taasisi sita
pamoja na Sekretarieti mbili za mikoa katika mambo ambayo hayakuwa ya
lazima, kama faini za kuchelewa kulipa kodi ya pango.
Taasisi hizo ni Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Makazi na Mkoa wa Tabora.

CAG Assad amebainisha matumizi ya ziada ya Sh109,722, 539 kwa ajili ya
ununuzi wa gari aina ya Toyota Land Cruiser VX V8 kwa Sh297.5 milioni kutoka
kampuni ya Toyota (T) badala ya kutumia mfumo wa ununuzi wa pamoja
ambao ungefanya gari hilo lipatikane kwa Sh187.8 milioni.
Alisema katika kipindi hicho, wizara 17, balozi mbili na sekretarieti za mikoa 11
zilitumia zaidi ya Sh11.3 bilioni bila kuwapo vielelezo vyovyote, hivyo
kusababisha ashindwe kujua uhalali wa malipo hayo.

==> Kwa taarifa zaidi, pitia ripoti hizi za CAG
1. Ripoti ya Jumla ya Serikali Kuu 2014/2015
2. Ripoti ya Jumla ya ufanisi na Uchunguzi 2014/2015
3. Ripoti ya Jumla ya Mashirika ya Umma 2014/2015
4. Ripoti ya Jumla ya Miradi ya Maendeleo 2014/2015
5. Ripoti ya Jumla ya Serikali za Mitaa 2014/2015

Jumatatu, 25 Aprili 2016 17:53 Matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika mkutano na Rais wa Afrika Kusini

4/25/2016 11:53:00 pm


Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambaye Jumapili aliwasili Tehran akiongoza
ujumbe wa ngazi za juu alikutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi
Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika
mkutano na Rais Zuma alisisitiza kuhusu udharura wa kuimarishwa ushirikiano
miongoni mwa nchi huru na zinazojitegemea duniani.

Katika kikao hicho aliashiria nukta muhimu katika uhusiano wa Iran na Afrika
Kusini. Awali ni hatua ya Iran kukata uhusiano wake mara moja na utawala wa
ubaguzi wa rangi wa Makaburu wa Afrika Kusini mara baada ya kupata ushindi
Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran ilikata uhusiano wake na utawala wa Kizayuni wa Israel na utawala wa
ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini takriban kwa wakati mmoja.
Kiongozi

Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbushia nafasi muhimu ya hayati
Nelson Mandela wa Afrika Kusini katika kuanguka utawala wa ubaguzi wa rangi
nchini humo na historia yake nzuri, ya kiudugu na kimapenzi na Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran. Nukta ya pili ambayo Kiongozi Muadhamu aliitaja ni kuwa,
mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu Afrika Kusini ni mtazamo
mzuri na kubainisha kuwa, uhusiano wa Iran na Afrika Kusini ni mzuri sana.
Ameongeza kuwa, ushirikiano wa nchi hizo mbili katika jamii za kimataifa pia
unasaidia sana. Pamoja na hayo amesema, bado uwezo wa nchi hizi mbili
haujatumiwa ipasavyo kwa ajili ya kukuza mabadilishano ya kiuchumi na
kibiashara baina ya pande mbili.

Kwa upande wake Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameishukuru Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake kwa wananchi wa nchi yake wakati
wa mapambano na ubaguzi wa rangi na kusema kuwa, wananchi wa Afrika
Kusini kamwe hawawezi kusahau uungaji mkono huo wa taifa la Iran kwao.
Katika hali ya sasa ya mfumo wa kimataifa, nchi huru na zinazojitegemea
zinaweza kukidhi maslahi yao na hilo litategemea kiwango cha ushirikiano baina
yao katika nyuga mbali mbali. Lakini pamoja na hayo, hakuna shaka kuwa kuna
vizingiti katika njia ya ushirikiano huu. Hii ni kwa sababu madola makubwa ya
kibeberu na kiistikbari kamwe hayataafiki ushirikiano kama huo ambao ni kwa
madhara ya maslahi yao haramu.
Ni kwa sababu hii ndio baadhi ya madola makubwa kwa visingizio
visivyokubalika, yanajaribu kuweka vizingiti katika uhusiano wa nchi huru na
zinazojitegemea.
Iran na Afrika Kusini ni kati ya nchi zinazolengwa na njama hizo za madola ya
kibeberu.

Uzoefu umeonyesha kuwa, ushirikiano ni kwa maslahi ya nchi zinazojitegemea.
Moja ya misdaki za ushirikiano huo ni maingiliano mema ya Iran na Afrika
Kusini katika Harakati ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote.
Afrika Kusini kwa mtazamo wa kisiasa na kiuchumi ni moja kati ya nchi muhimu
na zenye taathira barani Afrika na inahesabiwa kuwa kati ya nchi zinazoibuka
kiuchumi. Iran kwa upande wake pia ni nchi yenye uwezo mkubwa na hadhi ya
kipekee katika uga wa kieneo na kimataifa na hivyo kushirikiana na Afrika Kusini
kunaweza kuwa fursa nzuri kwa nchi hizo mbili.
Kwa hakika tunaweza kusema matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
ya Kiislamu na Rais wa Afrika Kusini ni ramani ya njia ya kufikiwa malengo ya
pamoja ya Tehran na Pretoria.

Monday 25 April 2016 Matukio Ya Ubakaji Yaongezeka Nchini Na Kufikia 1765.

4/25/2016 11:39:00 pm


Matukio ya ubakaji hasa kwa watoto wadogo yamekuwa yakiongezeka kwa
kiwango kikubwa, ongezeko hili limebainika kutokana na ufuatiliaji tulioufanya
kupitia matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi ambapo katika kipindi cha
mwezi Januari hadi Machi 2016 kumeripotiwa matukio 1765 ukilinganisha na
matukio 1585 katika kipindi kama hicho mwaka 2015 ikiwa ni ongezeko la
matukio 180.

Katika matukio ya Januari hadi machi 2016, jumla ya watuhumiwa 823
wamekamatwa na kufikishwa mahakamani ingawa bado kumekuwa na tabia ya
wazazi na walezi kuficha watuhumiwa wa ubakaji na kumaliza kesi hizo kirafiki
au kifamilia jambo ambalo ni kinyume cha sheria bila kuzingatia madhara
aliyoyapata mtoto.

Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linakemea vikali wale wote
wanaojihusisha na vitendo hivyo viovu vya ubakaji na wazazi ama walezi
wanaofumbia macho vitendo hivyo na kuingia makubalino na watuhumiwa kwa
kupeana fedha kama fidia ili wamalize kesi kiundugu au kifamilia.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Wazazi, walezi, Viongozi wa dini, Asasi za
kiraia, walimu na Wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa ushirikiano katika
kushughulikia vitendo hivyo ikiwemo kuwafichua wazazi au walezi wanaofanya
makubaliano ya kumaliza kesi za ubakaji kirafiki au kifamilia ili kukomesha
vitendo hivyo.

Imetolewa na:
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

Monday 25 April 2016 Rais Magufuli Ateua Makatibu Tawala wa Mikoa 26

4/25/2016 11:24:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 25 Aprili, 2016 amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya
Tanzania Bara.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza
kuwa kati ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya
kazi na 13 wamebakisha katika vituo vyao vya sasa.
Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;

1.Arusha - Richard Kwitega
2.Geita - Selestine Muhochi Gesimba
3.Kagera - Armatus C. Msole
4.Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
5.Pwani - Zuberi Mhina Samataba
6.Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
7.Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
8.Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
9.Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
10.Tanga - Eng. Zena Said

Makatibu Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;

1.Kigoma - Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
2.Morogoro - Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)
Makatibu Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama
ifuatavyo;

1.Dar es salaam - Theresia Louis Mbando
2.Dodoma - Rehema Hussein Madenge
3. Iringa - Wamoja Ayubu Dickolagwa
4.Katavi - CP Paul Chagonja
5.Lindi - Ramadhan Habibu Kaswa
6.Mara - Benedict Richard Ole Kuyan
7.Manyara - Eliakimu Chacha Maswi
8.Mbeya- Mariam Amri Mjunguja
9.Mtwara - Alfred Cosmas Luanda
10.Mwanza - CP. Clodwing Mathew Mtweve
11.Njombe - Jackson Lesika Saitabau
12.Rukwa - Symthies Emmanuel Pangisa
13.Ruvuma - Hassan Mpali Bendeyeko

Makatibu Tawala wa Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza,
wataapishwa siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu
Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Aprili, 2016

Monday,April 25 , 2016 Serikali.imeunda Kamati ya Kuanzisha Tume ya Tehama.

4/25/2016 12:08:00 pm

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, ameunda Kamati ya mpito ya kusimamia uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  (TEHAMA) ambapo ameipa miezi sita kufanya kazi kuanzia mwezi Aprili, 2016 ya kuhakikisha kuwa Tume ya TEHAMA inaanza kazi rasmi.

Katika kuhakikisha kuwa Tume ya TEHAMA inaanza kazi mara moja, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano, Prof. Faustin Kamuzora, amewakabidhi wajumbe wa Kamati hiyo Amri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na.532 iliyotolewa kupitia gazeti la Serikali Na. 47 la tarehe 20 Novemba, mwaka 2015 iliyoanzisha Tume na Hadidu za Rejea zinazoainisha majukumu yao.

Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia uanzishwaji wa Tume, kuandaa sheria ya kuanzisha Tume, na kutengeneza Mpango Mkakati wa Tume. 

Prof. Kamuzora amewataka wajumbe wa Tume hiyo  kuepuka kuweka mitazamo au maslahi binafsi ya wao wenyewe au ya taasisi zao katika kipindi cha kuanzisha Tume, bali waishauri Serikali namna nzuri ya kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaanza kazi ya kusimamia na kuratibu masuala ya TEHAMA nchini.

Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao na Katibu wa Kamati ya Kuanzisha Tume ya TEHAMA nchini ni kama ifuatavyo:
James Kilaba (Mwenyekiti), Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
Samson Mwela (Katibu), Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Idris Rai (Mjumbe), Makamu Mkuu wa Chuo, SUZA,
Joan Mbuya (Mjumbe), Mkurugenzi wa Sera na Mipango-Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali,
George Mulamula (Mjumbe), Mkurugenzi Mtendaji-DTBi,
Juma Rajabu, (Mjumbe), Mkurugenzi Mtendaji-Maxcom Africa,
Maharage Chande, (Mjumbe), Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi, Ofisi ya Rais-President’s Delivery Bureau, na
Nicolaus Mhonyiwa (Mjumbe), Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA-Ofisi ya Msajili wa HAZINA.
Aidha, Tume ya TEHAMA inatarajiwa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na yafuatayo: Kushiriki katika kushauri juu ya uwekezaji wa TEHAMA nchini kwa ubia na sekta binafsi; kuwatambua, kujenga uwezo na kuwaendeleza wataalam wa TEHAMA; kushauri na kushiriki pamoja na wadau katika tafiti za TEHAMA, uwekaji viwango na ubunifu katika sekta ya TEHAMA; na kushiriki katika kusimamia miundombinu na programu za kitaifa za TEHAMA.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Dkt. Eng. Maria Sasabo, alisisitiza kuwa Kamati ina kazi kubwa ya kuona namna bora zaidi ya kuhakikisha kuwa Tume itatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni pamoja na masuala ya uwekezaji; na kusimamia vema  viwango vya wataalamu wa Sekta. Naye Mwenyekiti, Inj. James Kilaba, kwa niaba ya Kamati alishukuru kwa kuaminiwa na Serikali na pia aliahidi kuwa watatekeleza majukumu yao kikamilifu. Pia alimalizia kwa kusema, “hatutawaangusha”.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali


Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,Profesa Makame Mbarawa.

Sijawahi kuwa na mahusiano na msanii Lady JayDee

4/25/2016 10:40:00 am

Mwanadada anayetamba kwa ngoma yake ya NdiNdiNdi Lady JayDee amesema kwa kipindi chote ambacho anafanya muziki wa Bongo Flava hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii yeyote.

JayDee ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa papo wakati akizindua video ya NdiNdiNdi kwenye kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV.

Katika uzinduzi huo msanii huyo aliweka bayana kwamba ameandaa albam nzima ambapo ameanza kutoa single ya NdiNdiNdi na nyingine zitaendelea kutoka.

Aidha amewashukuru watu wote ambao wanaendelea kumuunga mkono katika kazi zake kwa muda mrefu sasa na kuahidi kwamba hatawaangusha

Lady JayDee


Mwanamuziki wa Bongo Flava Judith Wambura aka.Lady JayDee ( pichani)

THURSDAY 30 MARCH 2016MWANAMKE MTANZANIA ANG'ARA KATIKA MASHINDANO YA KARATE KATIKA NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI

4/25/2016 10:17:00 am


Mwanadada Getrude Macha ameshika nafasi ya kwanza katika mchezo wa karate ambapo mashindano hayo  yanajulikana kwa jina la  (GOJUKAI) karate ya Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Uganda ambapo yamejumuisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

Rais wa chama cha GOJUKAI Karate Tanzania ambae pia ni Mkufuzi wa Gojukai Geofrey Cleodo Kalonga amesema kuwa,mchezo wa huu unamjenga mshiriki kiafya katika maisha yake yote, ambapo ameongeza kuwa mchezo huo hauna ukomo ukilinganisha na michezo mingine,kwani kadri umri unavyaozidi kuwa mkubwa ndipo mchezo unakuwa mkubwa zaidi.

Geofrey Kalonga amesema wao kwa ujumla wao kama chama cha Gojukai Karate Tanzania wanaiomba serikali wauruhusu mchezo huu uruhusiwe kuingia kwenye taasisi za elimu kuanzia shule za awali,shule za msingi, sekondari na vyuoni kwani ni taaluma inayofundisha nidhamu katika kiwango cha hali ya juu,pia inafundisha mbinu za kujihami.

Naye Rais wa shirikisho la West Coast Shotokan Karate Tanzania lililopo Jijini Arusha ,Bwana Dady Kassim Ramadhani, ameelekeza ombi lao kwa waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo ,Mhe Nape Moses Nauye kutupia macho katika mchezo huo kwani ni karate inafundishwa katika majeshi mengu ,wameomba mchezo huo uthaminiwe kama inavyathaminiwa michezo mingine.

Amesema kuwa mchezo wa katate unatambulika Kimataifa ,ila wanasikitika kuwa.mchezo.huo hapa ndani yanchi hautambuliki hivyo wamemuomba Waziri mwenye dhamana kulitazama jambo hili kwa umakini kwani itakuwa faraja kubwa kwao.

Mwanadada Getrude Macha akiwa na mshindi wa pili kwa upande wa wanaume kutoka Tanzania katikati ni  Sesei Geofrey Kalonga ambaye ni Rais wa chama cha Gojukai Karate Tanzani, pia ni Mkufunzi wa Gojukai.
Getrudi Macha akiwa katika pozi baada ya Mazowezi.

Monday 25 April 2016 UDUMAVU KWA WATOTO HALMASHAURI YA KISHAPU UPO JUU SABABU LISHE DUNI NA UKOSEFU WA ELIMU TANGAZO

4/25/2016 08:12:00 am


TATIZO la udumavu kwa watoto chini ya
miaka mitano halmashauri ya wilaya
ya Kishapu mkoani Shinyanga limefikia
asilimia 43 ukilinganisha na kiwango cha
mkoa kuwa na asilimia hiyo, ambapo
imeelezwa kusababishwa na lishe duni
kwenye baadhi ya kaya na ukosefu wa
elimu ya lishe.

Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana mganga mkuu wa
wilaya hiyo dkt. Josephat Shani ,
alisema mwamko mdogo kwa jamii
jinsi ya kuwalisha watoto pamoja na
vyakula vinavyotakiwa bado ni
changamoto ambayo wanaendelea
kuifanyika kazi kwa kutoa elimu.
Alisema baadhi ya wazazi hawajui
vyakula ambayo mtoto mdogo anatakiwa
kupewa ili kuijenga afya yake na
kumkinga na magonjwa , matokeo yake
anakuwa na udumavu ambalo ni tatizo
kubwa kwa wilaya hiyo na mkoa kwa
ujumla na elimu inaendelea kutolewa na
wataalamu .

“Watoto wanaobainika kuwa
wameathirika zaidi na udumavu
wanapatiwa tiba ya vyakula dawa ili
kurudisha afya yao, pia jamii
inatakiwa kubadilika sasa waanze
kulima viazi lishe kukabiliana na tatizo
la lishe duni ambalo linasumbua
kwenye wilaya yetu”alisema Dkt. Shani.
Mganga mkuu alisema katika
kuhakikisha tatizo la udumavu
linakwisha au kupungua kwani asilimia
hiyo inalingana naya mkoa mzima,
wametenga sh 29 milion katika bajeti
ijayo fedha zitakazotumia kupambana na
tatizo hilo kwa kutoa elimu kwa jamii
ili ifahamu athari zake.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga
dkt Ntuli Kapologwe hivi karibuni
alisema kiwango cha tatizo la utapiamlo
na udumavu katika mkoa wa Shinyanga
ni kikubwa, ambapo ni asilimia 43
huku akibainisha kuwa sababu kubwa
ya kudumaa kwa watoto ni ukosefu wa
uhakika wa chakula na umaskini katika
ngazi ya kaya.

Takwimu za kitaifa zinaonyesha kuwa
asilimia 42 ya watoto wenye umri chini
ya miaka mitano nchini Tanzania ,
wanaukuaji wa kudumaa kutokana na
lishe duni wakati wa ujauzito na
miaka miwili ya mwanzo ya uhai wao.
Alisema hali hiyo inasababisha watoto
kudumaa kimaumbile na akili na
kufanya kutomudu masomo shuleni na
hata kupunguza ufanisi wa kazi
wanapokuwa watu wazima.

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel