Top Menu

MWANO: SERIKALI ITUPIA MACHO WAWEKEZAJI WA NDANI

5/31/2016 06:17:00 pm
Mkurugenzi wa Old East International co.Ltd. Moses Edward Mwano

NA VERO IGNATUS ARUSHA.

Wito umetolewa kwa serikali kuwatipia macho zaidi wawekezaji wa ndani ya nchi,kuwapa ushirikiano wa karibu katika uendeshaji wa viwanda vidogo vidogo,ili waweze kukua zaidi na kufika mbali .

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Old East International co.Ltd iliyopo jijini Dar es salaam, ndugu Moses Edward Mwano, kuwa wanaiomba serikali kuwapa kipaumbele wawekezaji wa ndani ya nchi zaidi  kuliko wawekezaji wageni.

Moses ameiomba serikali na TBS kiweka mikakati wa kuhakikisha bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe na viwango vinavyokidhi, kwani kwenye soko kuna bidhaaa feki zinaingia na bei zake ni za chini .

Pia amewataka wananchi wathamini bidhaa zinazozalishwa na wazawa kuliko kushabikia bidhaa za nje ambazo kwa asilimia kadhaa hazina ubora na viwango vilivyo thabiti na mara nyingine zimekuwa zikileta madhara kwa jamii kutokana na kutokuwa na ubora.


Kampuni ya Old East International ambayo ipo chini ya Shirika la uwekezaji Tanzania, Makao yake makuu yapo Jijini Dar es salaam wanajishughulisha nakutengeneza wino wa Crown Catridges ,pia wanauza mashine za uchapishaji pamoja na kuzifanyia matengenezo,wino huo unatumika katika mashine mabalimbali za uchapaji pamoja na vinakilishi mbalimbali ,hivyo amewataka watanzania wasikimbilie kuagiza bidhaa hizo nje ya nchi kwani kwa sasa unapatikana hapa nchini kwa bei nzuri nanafuu.

Pia ni kampuni ya kwanza ya Kitanzania ambayo inatengeneza wino huo wa Crowin Catridge, ambapo wameweza pia kuwapatia vijana ajira,amesema changamoto kubwa waliyonayo kwa sasa ni Watanzania wengi wamezowea kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi hivyo wanadhani ya kwamba bidhaa za ndani ya nchi hazina ubora.

Mwano amewataka watanzania kuondoa dhana potofu kuwa bidhaa za ndani ya nchi hazina ubora kama za nje,bali wathamini bidhaa za ndani ya nchi na wawaunge mkono wazawa wenye makampuni ya ndani ambayo yanafanya uzalishaji tena wenye ubora sahihi.

Wino wa Crown Catridge katika muonekano ukiwa kwenye maboksi tayari kwa kumfikia mteja.
Baadhi ya Mashine za Uchapishaji za Kampuni ya Old East International co.Ltd.


Aidha Moses amesema tayari katika Jiji la Arusha yupo msambazaji wa bidhaa za kampuni yao ambapo ni BNZ Technologgy Jengo la Uchumi ghorofa ya kwanza chumba no 107.

RITA:KUANDIKA WOSIA SIYO UCHURO.

5/31/2016 08:19:00 am

Afisa Usajili kutoka Rita Makao makuu Jijini Dar es salaam, Augustin Thomas Mbuya ,ambaye ndiye mtaribu wa zowezi la Kampeni ya kitoa huduma Rita,Akizungumza na wananchi Jijini Arusha ambapo kampeni hiyo imezinguliwa rasmi.


Mkuu wa  Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu,ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kampeni ya Rita , ambapo imeanza rasmi katika Wilaya ya Arusha Mjini na itaendelea kwa siku nne.
Muwakilishi wa Rita Mkoa wa Arusha Bi Janeth Mandawa.


Afisa Usajili kutoka Rita makao makuu Jijini Dar es salaam Joseph Mwakatobe akizungumza na wananchi ,akitoa maelekezo namna ya kuandika wosia na umuhimu wa kuhifadhi wosia.
Afisa Usajili kutoka Rita Makao Makuu Bi Grace Shao.


Afisa habari kutoka Rita Makao makuu Jijini Dar es salaam Bi Grace Kyasi.


Wananchi kutoka katika Wilaya ya Arusha Mjini wakfuatilia mafunzo 

NA VERO IGNATUS  ARUSHA

Wito umetolewa kwa wananchi kuepuka dhana potofu kuwa kuandika wosia ni Uchuro,jambo ambalo siyo kweli bali kuandika wosia ni kuepusha usumbufu na migogoro kwa ndugu watakaokuwa wamebaki aidha watoto au mjane.

Hayo yamesemwa na Afisa Usajili kutoka Rita ndugu Joseph Mwakatobe katika ufunguzi wa zowezi la kampeni ya kutoa huduma za Rita kwa wananchi ,kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuandika wosia, namna ya kuhifadhi wosia.

Joseph amesema kuwa mara nyingi wosia ni muhimu sana kuandikwa kwasababu inawarahisishia wale wanaobaki kuepusha kunyimwa haki zao ,kudhulumiwa ,Rita inawashauri wananchi kuandika wosia,kwani watu wengi hawana elimu ya kutosha juu ya wosia.

Naya mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu amewahasa Rita wawaelimishe wananchi sheria ya mirathi pamoja mwongozo,pia wawasaidie wananchi kufahamu na kuelewa maeneo sahihi ya kuhifadhi wosia

Nkulu amesisitiza  kuwa mtu akiandika wosia ni vizuri zaidi maana ndiye anayejua mali zake, na pia anamfahamu mtu sahihi wa kumpatia urithi huo,na hii itaepusha migogoro na migongano ambayo ingeliweza kujitokeza.

Naye Mratibu wa zowezi la kampeni hiyo Augustin Mboya amesema kuwa lengo kuu la kampeni hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi waifahamu umuhimu wa.kuandika wosia nakuhifadhi, watambue kuwa ile dhana ya kuwa kuandika wosia ni Uchuro na kujitabiria kifo ni potofu na haina mashiko yeyote ,Pia watambue kuwa mtu anayeandika wosia lazima awe na akili timamu ,bila kusahau kuwa wosia huandikwa kwa hiari na siyo kulazimishwa

Mke wa Trafiki Kinyogori Adaiwa Kukiri Kumuua Mumewe

5/31/2016 08:06:00 am

MKE wa askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani
(trafiki), Sajenti Ally Salum (Kinyogori) aliyeuawa hivi
karibuni, inadaiwa amekiri kuhusika kwenye mauaji hayo,
akidai ilitokana na mumewe kumuacha na kuoa mke
mwingine.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon
Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwanamke
huyo anashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo yaliyofanyika
nyumbani kwa Kinyogori, Mkuranga mkoani Pwani.
Wakati huo huo, Kamanda Sirro amezungumzia pia mauaji ya
Anathe Msuya yaliyofanyika hivi karibuni Kigamboni na
kusema polisi inaendelea kumtafuta msichana wa kazi za
nyumbani aliyetoroka siku moja kabla ya kifo cha
mwanamke huyo.
Anayetuhumiwa kuua mumewe
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu matukio
mbalimbali ya uhalifu yaliyojitokeza jijini Dar es
Salaam, Sirro alisema katika mahojiano ya awali mke wa
Kinyogori amekiri kuhusika.
Kwa mujibu wa kamanda, mwanamke huyo ambaye hata hivyo
hakutaja jina lake kwa sababu za kipelelezi, aliamua
kumtuma mtu kutekeleza mauaji hayo baada ya mumewe
kumwacha na kuoa mke mwingine.
“Ni jambo la kusikitisha kuona mtu anatoa uhai wa mtu
sababu ya kuachwa. Tunawasihi wananchi kuepuka
kujihusisha na matukio kama haya, eti sababu tu ya
kuachwa wanawake wapo wengi na wanaume wapo wengi
unaweza kuachwa na ukaolewa na ukaoa kuliko kuondoa uhai
wa mtu,” alisisitiza Sirro.
Hata hivyo, Sirro alisema wanaendelea kuwahoji
watuhumiwa hao ili waweze kuwataja watu wengine
walioshirikiana nao kutekeleza tukio hilo baada ya
kuonekana kuwepo kwa wahusika wengine.
‘Hausigeli’ asakwa
Kuhusu mauaji ya Anathe aliyechinjwa nyumbani kwake
Kibada, Kigamboni, Kamanda Sirro alisema wanaendelea na
jitihada za kumtafuta msichana huyo ahojiwe kuhusu tukio
hilo.
Aidha alisema mtu mmoja anashikiliwa akituhumiwa
kuhusika na tukio hilo huku polisi ikiwa imeandaa timu
ya upelelezi itakayoshughulikia tukio hilo kufanikisha
kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.
Sirro alisema msichana huyo aliondoka siku moja kabla ya
tukio hilo la mauaji hivyo kupatikana kwake, kunaweza
kusaidia polisi kujua kama kuondoka kwake kulikuwa salama
au kuna kitu kimejificha.
“Msichana huyu tunaendelea kumsaka tujue kama aliondoka
salama na kumhoji zaidi juu ya kuondoka kwake siku moja
tu, tukio linatokea nina imani tutafanikiwa kumpata na
wote waliohusika na kukomesha matukio haya,” alisema
Sirro.
Mamia wajitokeza msibani
Vilio na simanzi jana vilitawala wakati mamia ya wakazi
wa Kibada Kigamboni na Salasala walipokuwa wakiuaga mwili
wa marehemu Anathe Msuya (30), aliyeuawa Mei 25 nyumbani
kwake kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.
Mwili ulichukuliwa jana asubuhi kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Kibada, kwa
ajili ya kuagwa na majirani zake kabla ya kusafirishwa
kwenda kuzikwa mkoani Arusha leo.
Akizungumza baada ya mamia kumuaga nyumbani kwa
marehemu, mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyakwale
Kibada, Said Pazi alisema kuwa wao kama majirani
waliomba familia wapate fursa ya kumuaga jirani yao
ambaye tangu ahamie ana muda wa miezi sita.
“Baada ya kuambiwa msiba upo Salasala tuliomba kama
majirani na sisi tupatiwe fursa ya kuuaga mwili wa ndugu
yetu ambaye alihamia mwaka jana… kwa kweli msiba wake
umetusikitisha sana” alisema.
Akizungumzia tukio hilo alisema kuwa mtoto wa marehemu
huyo, Allan Kimario (4) aliwataarifu majirani kuwa mama
yake haamki na ndipo walipofika wakakuta ameuawa.
Mwenyekiti huyo alitoa pole na kusema atahakikisha
wanaimarisha ulinzi na kuhimiza wenye viwanja ambavyo
havijajengwa, wavifanyie usafi ili kuondoa vichaka ambavyo ni hatari kwa usalama.14 Mbaroni kwa Tuhuma za Ujambazi

5/31/2016 07:46:00 am
KAMANDA WA POLISI MKOA WA KILIMANJARO  WILBROAD MTAFUNGWA.

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 14 wakiwamo wanawake
wawili na mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwika
wilayani Moshi, kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha.

Miongoni mwa watuhumiwa hao wapo wanaodaiwa kuwa majambazi sugu 10,
waganga wa kienyeji wawili ambao walikuwa wakitumika kwa ajili ya kuwapa
dawa watuhumiwa hao ili wasikamatwe na polisi na kuzindika silaha zilizokuwa
zikitumika katika ujambazi na wanawake wapishi wa watuhumiwa hao wakiwa
mafichoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mtafungwa alisema jana
kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Tanga
na Kilimanjaro kufuatia msako mkali wa askari uliotokana na taarifa za siri.

Mtafungwa alisema mwanafunzi wa sekondari ya Mwika, Kelvin Shayo (17)
miongoni mwa matukio anayotuhumiwa kushiriki ni pamoja na la kumpora
bastola yenye namba YP0466 Tz Car aina ya brown, askari mstaafu wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Elibariki Urio (67).

Kamanda alisema silaha hiyo iliporwa Februari 25 mwaka huu baada ya
majambazi kumvamia nyumbani kwake na kupora mali pamoja na silaha hiyo
kisha kwenda kuificha nyumbani kwa Eleutery Nguma (62) mkazi wa Makami
Chini, Tarafa ya Vunjo ikiwa imefukiwa ardhini kwenye mfuko wa plastiki.

Aidha, Mtafungwa alisema kwa mujibu wa kumbukumbu za polisi mtuhumiwa
huyo (Nguma) ilidhaniwa kuwa ameacha vitendo vya ujambazi lakini
amebainika kuwa ni mpangaji wa njama za ujambazi, kuficha mali za wizi
pamoja na kuficha silaha zinazotumika katika uhalifu.hw

WAZIRI MKUU KASIMU MAJALIWA KESHO ANATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA KULINDA URITHI WA DUNIA NA AFRIKA JIJINI ARUSHA .

5/30/2016 06:22:00 pm

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi mara baada ya kuwasili katika Kiwanja cha Ndege Kia tayari kwa ufunguzi wa Mkutano huo hapo kesho.


Na  Vero Ignatus Arusha.

Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu
Majaliwa kesho anatarajiwa kufungua mkutano wa kulinda urithi wa
dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu utakao fanyika
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha
unaotarajiwa kufanyika kwa siku nne .

Akiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa wizara ya maliasili
na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi wakati akiongea na
waandishi wa habari jijini hapa juu ya maandalizi ya mkutano huo
ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa serekali ya Jamuhuri ya
muungano wa Tanzania pamoja na shirika la UNESCO nakituo chake
cha urithi wa dunia.

Alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto
na mambo ambayo yanatishia na kuadhiri uhifadhi bora wa maeneo
ya urithi wa dunia katika afrika .
Aidha mkutano huo utapendekeza suluisho kwa kupitia upya shughuli
zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango
wa miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi
ijayo.

Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa
kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi
inayoendana na uhifadhi wa urithi na maendeleo endelevu pamoja
kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea kwenye maeneo urithi wa
dunia kutokana na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni
na uridhi asilia.

Aliongeza kuwa pia mkutano hu o umejikita kwenye sera ya UNESCO
ya mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye
mkataba wa uridhi wa dunia.

“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia uatakuwa
na manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa
bali pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya
wageniwatakao uthudhuria mkutano huu pamoja na kuanzisha
mitandao wa kitaaluma na kujenga mataji wa kijamii”alisema Malinzi
Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote
kutakuwa na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa
yakifanyika siku zote za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa
katika hifadhi ya taifa ya Ngorongorohsvsghwhwwbsgs
ABC : WANATOA MIKOPO KWA RIBA NAFUU.

5/30/2016 09:23:00 am

Meneja wa ABC Benki Tawi la Arusha akiwa kwenye banda lao katika maonyeho yaliyofanyika katika Kiwanja cha Magereza Jijini Arusha.


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kati na Kibiashara katika Kibenki Bi Joyce Malai akizungumza na wateja waliotembelea Banda la ABC Bank katika Kiwanja cha Magereza Jijini Arusha.

Bi Emma Saria  ambaye ni Treasury Dearler kutoka ABC Banki akionyesha aina za Visa kadi ambazo mteja anaweza kutoa pesa kwenye ATM yeyote Duniani bila usumbufu wowote na inawemuwezesha mteja kufanya manunuzi  kwa njia ya Mtandao.


NA   VERO IGNATUS ARUSHA

Banki ya abac Tawi la Arusha imewataka wananchi kutokuogopa kufungua
akaunti kwani sheria ya kufungua ni rahisi ukilinganisha na benki nyingine .

Hayo yamesemwa na meneja wa Tawi la ABC Jijini Arusha  Bi  Mbuche Zamdi Magawa katika
maonyesho ya Utalii ya Karibu fair yaliyofanyika  katika kiwanja cha Magereza
Jijini Arusha

Bi Mbuche amesema ABC Banki huwa wanamjali mteja hivyo mara zote wamekuwa
akiandaa na kufanya kile mteja anahitaji, pia kiwango cha chini cha kufungua
akaunti ni shilingi 5000 ikimlenga pia mwananchi mwenye maisha ya hali ya
chini anaweza kufungua.

Aidha ameongeza kuwa kwa upande wa wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi kwani Benki inatoa mikopo
yenye riba nafuu ambayo haitamsumbua mteja, pia kwa wateja wanaotaka
kubadilisha fedha za kigeni au wanataka kuuza fedha ,ABC Banki wanatoa
huduma hiyo kwa bei nzuri.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kati na Kibiashara za Kibenki,  Bi Joyce Malai amesema kuwa
Banki  inatoa  Visa kadi zenye ubora wa hali ya juu inayomuwezesha mteja
kutoa pesa kwenye ATM zote duniani, na pia inaweza kumsaidia mteja kufanya
manunuzi kwa njia ya mtandao bila usumbufu wowote.Olemeiseiyeki:Tozo kubwa ni Kero kwa Utalii Tanzania.

5/29/2016 07:34:00 amMbunge wa Arumeru Magharibi Gibson Olemeiyeseki.

Na Vero Ignatus Arusha.

Serikali  imetakiwa kufungua ofisi za utalii katika kila nchi  ambazo zinaleta watalii hapa nchini pamoja na kupunguza viingilio vya wageni wanaotembelea hifadhi zetu za taifa ili kuweza kuongeza idadi ya watalii wanaoingia hapa nchini  .

Hayo yamesemwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru magharibi  Gibson Olemeiseyeki wakati  akiongea na waandishi wa habari alipotembelea katika maonyesho ya utalii ya Karibu fair yanayofanyika ndani ya viwanja ya magereza nje vilivyopo ndani ya jiji la Arusha .

Amesema kuwa  serekali inapaswa kufungua ofisi katika kila  nchi ambazo zinaleta wageni hapa nchini ili kuweza kutangaza utalii wetu vizuri,na ili kuweza kupata wageni wengi zaidi  ambapo wakiingia kwa wingi watasaidia kuongeza pato la taifa na kupunguza tatizo la ajira kwani vijana.

Mbunge huyo amesema  kuwa ni jambo la ajabu nchi kama Tanzania ambayo inavivutio vingi vya utalii , hukubikishika nafasi ya  kumi bora ambazo zinaongoza kwa kuwa na vivutio vya utalii lakini ni nchi ambayo inaongiza watalii wachache sana ukilinganisha na vivutio vilivyopo,kwa mwaka mzima inapata watalii milioni moja ambapo huliingizia Taifa pato la asilimia kumi na saba kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha navivutio vilivyopo nchini Tanzania.

  Kwapitia utalii serekali inaweza kuingiza fedha nyingi sana  pia inaweza kuwaajiri vijana wengi sana  ,iwapo ikijipanga  vizuri  na kutumia fursa vizuri kama nchi zingine  serekali yetu itaweza iwapo  itaajiri wafanyakazi ambao wanauchungu na Nchi pamoja na hifadhi zetu,pamoja na kuwa na wanataaluma wa  kutosha kuhusiana na utalii na sio kuajiri watu ambao hawana taaluma ,na siyo kuwaajiri watu kiundugu undugu na kiubinamu.

“unajua ukiona bidhaa aina soko unatakiwa uishushe bei na uangalie nini cha kuboresha ili uweze kuuza bidhaa yako sasa hapa kwetu viongozi wanapandisha bei kila siku hawaangalii chakufanya ili utalii na watalii waje kwa wingi  hapa nchini ,badala yake wanapandishi kila kitu sasa kibaya zaidi hata bei za ndege ambazo zinaleta wageni  zikitaka kutua hapa kuleta watalii wanapangiwa garama kubwa mno kiasi kwamba wanashindwa kuja, inabidi waende katika nchi jirani ya Kenya wakatue maana wenzetu wanatambua umuhimu wa kushusha bei ,na ukilinganisha Tanzania tuna vivutio vingi tofauti na nchi ya Kenya inajulikana zaidi kuliko Tanzania. “alisema Olemeiseyeki

Kwa upande afisa usiano wa chama cha waajiri  (ATE) Patricia Chao alisema kuwa maonyesho ni mazuri  na  kwani mwamko upo kwani watu wameuthuria tofauti na kipindi kingine  kwani amewaona washiriki wengi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya ,Uganda ,Rwanda ,Burundi na hata Afrika ya Kusini tofauti na kipindi kingine.
Mazito Yaibuka Mauaji ya Dada yake Bilionea Msuya .........Yadaiwa Binti wa Kazi Alitoweka Mchana, Usiku Dada Akachinjwa

5/28/2016 08:05:00 pm


Siku moja baada ya kifo cha dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth imebainika kuwa msaidizi wa ndani aliondoka saa sita mchana kwa kuacha funguo nyumba ya jirani.

Akizungumza nyumbani.

dada wa marehemu, Mbezi Juu, mama mdogo wa marehemu Lilian Benjamin alisema msaidizi huyo alimpigia simu bosi wake mchana na kumwambia anaondoka na hataendelea na kazi.

Alisema marehemu alilazimika kuomba ruhusa mapema kazini ili arudi nyumbani kwake Kibada lakini ilimlazimu kukaa nje ya nyumba kwa saa mbili baada ya kufika saa tisa alasiri na kukuta mlango umefungwa.

Mama huyo alisema baada ya kusubiri kwa muda aliwauliza majirani wakamweleza kuwa walipelekewa funguo na mwanafunzi wasiyemfahamu akadai kuwa alipewa na dada mmoja aliyemuelekeza aipeleke nyumba hiyo.

Haifahamiki mpaka sasa mahali alipo mfanyakazi huyo anayedaiwa kuwa mwenyeji wa Arusha.

Dada mkubwa wa marehemu, Happy Msuya alisema marehemu aliwaeleza mambo hayo baada ya kupigiwa simu na msichana huyo wa kazi.

Dada mwingine wa marehemu ambaye ni wa nne kuzaliwa kati ya watoto saba wa Elisaria Msuya, Ester, alisema wauaji hao hawakuwa na nia ya kuiba, bali ni kuua kwa sababu hawakuchukua kitu chochote zaidi ya televisheni ambayo nayo waliitupa mbali na nyumbani.

Ester alisema mara ya mwisho kuonana na marehemu ilikuwa Mei saba walipokutana benki na mazungumzo yao yalihusu hali ngumu ya maisha. Alisema hakuwahi kumwambia kama ana ugomvi na mtu kwa sababu alikuwa mpole na msiri.

Akielezea tukio hilo alisema inaonekana kulikuwa na purukushani kubwa chumbani kwa sababu besela la kitanda lilikuwa limevunjika na neti ilikuwa imetoka, huku nyaraka zikiwa zimepekuliwa na kusambazwa karibu kila kona ya chumba.

“Walikuja kuua, kuna kitu walikuwa wanatafuta katika nyaraka pia, ooh... Aneth umekufa kinyama, umechinjwa kama mnyama,” Ester alishindwa kuendelea na kuanza kulia na baadaye kidogo alisema wauaji walimkata marehemu koromeo lakini hawakutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Simulizi ya mtoto 
Mtoto wa marehemu mwenye umri wa miaka minne ambaye alikuwa akiishi na mama yake alisema: “Walikuja watu watano weusi usoni, wakanifanya na kitu shii usoni, nikalala kwenye kiti mbu wameniuma hadi niliposikia gari la shule likiita pipii, nikaamka na nikamuamsha mama anivalishe nguo za shule lakini akakataa kuamka, ”alisema mtoto huyo na kuongeza.

“Nikavaa mwenyewe nguo za shule na nikamwambia mama nitaendaje shule huku sijafanya “Home work” lakini mama hakujibu, mbu walining’ata pale kwenye kochi nilipolala, nikatoka nje nikakuta gari limeshaondoka, nikaenda kwa mama Salum,” alisema.

Alisema alienda huko akale kwa sababu njaa ilikuwa inamuuma hakula jana yake baada ya ‘wageni’ hao kuja na yeye kulala.

Alieleza kuwa alipowaambia mama yake hamjibu amelala tu alirudi na dada ambaye amemsahau jina kutoka hapo kwa mama Salum ambaye alipofika nyumbani kwao na alipomuona mama yake alianza kupiga kelele.

Ester alisema mwili wa marehemu utasafirishwa Jumatatu ijayo kuelekea kijijini kwao Kairo, Simanjiro mkoani Manyara.

Mtu wa karibu na familia ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema mbali ya kaka yao Erasto kuuawa kwa risasi, dada yao Ester akiwa na mumewe katika Baa ya Hongera, Dar es Salaam alipigwa risasi na kunusurika kufa.


Mbaroni Kwa Kukutwa Wakitoa Mamilioni Kwa ATM Za Watu 19

5/28/2016 08:45:00 am
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za
kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha
shilingi 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti pamoja na
namba za siri za kadi hizo. .

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi Damasi Nyanda amesema
watuhumiwa hao watatu walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku katika
Tawi la NMB Mpanda .
Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado
unaendelea, wamekamatwa na askari wa jeshi la polisi waliokuwa wakilinda
Benki hiyo.

Nyanda ameeleza kuwa watumiwa walikamatwa baada ya askari polisi
kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa wamekaa muda mrefu kwenye
chumba cha mashine ya kutolea fedha .

Amesema baada ya kuwatilia mashaka polisi waliingia ndani ya chumba hicho
na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa wanaendelea kutoa fedha katika mashine
tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea fedha.

Kaimu Kamanda alieleza ndipo askari polisi walipoamua kuwapekua
watuhumiwa na waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19 mali za watu tofauti
pamoja na namba za siri za kadi h izo na walikuwa tayari wameishatoa kiasi
cha fedha taslimu shilingi 3,680,000.

Amezitaja Namba za Kadi za ATM walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni
AC 61908000058,AC 61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC
61902240100,AC 61908000237, AC 61902400518 AC 61910000645, AC
61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168

Kaimu kamanda Nyanda amezitaja kadi za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni
zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653, AC 61910000250, Ac
61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na AC
70408100131.

Amesema watuhumiwa wanatarajia kufikishwa mahakamani baada ya
uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na bado watuhumiwa wote watatu
wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi .

Kaimu kamanda ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa
watu za namba zao za siri za kadi wanazozitumia kwenye ATM za benki .

Kijana Anusurika Kifo Baada Ya Kupanda na Kujirusha Kutoka Kwenye Mnara Wa Simu Jijini Mwanza

5/28/2016 08:29:00 am

KIJANA ALIYENUSURIKA KUJIUA AKIWA AMEBEBWA.

Kijana Mmoja (pichani aliyeshikiliwa ) ambaye jina lake halikupatikana kwa
haraka, mkazi wa Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka
katikati moja ya minara wa simu iliopo jijini humo, 

Tukio hilo limetokea jana na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana
huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia
mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo,
wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa
maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na
kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa
akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Uokoaji na Zima Moto mkoani
Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, ametoa rai kwa
makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili
kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha
kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa,
ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea
morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.

Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza
fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour
Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.


KESI YA UCHAGUZI LONGIDO SHAHIDI WA 19 NA 20 WATOA USHAHIDI

5/27/2016 10:09:00 pm


NA VERO IGNATUS LONGIDO

Shahidi wa 19 katika kesi ya uchaguzi Jimbo la Longido Mkoani Arusha,Lomayani Mollel{62] aliieleza mahakama jana kuwa alitoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi kata ya Kamwanga kuwepo kwa majina ya wakenya kuwepoa katika daftari la wapiga kura katika kata hiyo.

Mollel alisema hayo mbele Jaji Mfawidhi kanda ya Bukoba,Silvangirwa Mwangesi anayesikiliza kesi hiyo wakati akihojiwa na wakili wa serikali Fortunatus Mhalila na wenzake Neema Mwanga na David Akway.

Amesema mbali ya kuwaona wakenya katika daftari hilo pia aliwashuhudia wakipiga kura katika kutuo cha madukani na wengine maeneo mengine kwani walikuwa na wino katika kidole ulionyesha kuwa walipiga kura siku ya uchaguzi octoba 25 mwaka jana.

Shahidi huyo aliulizwa na mwanasheria wa serikali Mhalila kuwa aliwajuwaje kama walikuwa wakenya alisema kuwa anawajuwa kwa kuwa ni majirani zake kwa upande wa Kenya na wao wanaishi upande wa Tanzania hivyo wanafahamiana vizuri.

Mollel alisema kutoka na utata huo wa wakenya kupiga kura nchini kinyume na uratatibu alitoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi kata lakini hakuchukuwa hatua yoyote na pia alitoa taarifa kwa mgombea wa CCM,Dkt Stephen Kiruswa kuwepo kwa wakenya katika daftari la wapiga kura.

Shahidi huyo alisema kuwa yeye anajuwa kusoma na kuandika Kiswahili na kiapo alichokiwasiliha mahakamani  aliandika mwenye na kutafsiliwa kiingereza na wakili wake Edmund Ngemela na Daud Haraka.

Akihojiwa na wakili,John Materu aliulizwa ni watu gani wanapaswa kupiga kura,Mollel alisema ni watanzania wazalendo ndio wastahili kupiga kura na hajui kama wakenya hao walimpigia Dkt Kiruswa au la ila kitendo cha wao kupiga kilikiukwa.

Shahidi huyo aliulizwa ni kwa nini hakutoa taarifa kituo cha polisi Kamwanga wakati ni kosa la jinai,shahidi alisema jukumu lake lilikuwa kutoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi wa kata tu na sio vbinginevyo.

Shahidi wa 20 katika kesi hiyo Isaya Mollel {43} mkazi wa kijiji cha Lalilangwa kata ya Olmoloko wilayani Longido yeye alisema mgombea wa Chadema Onesmo Ole Nangole alitumia lugha za kashfa katika mikutano ya kampeni iliyofanyika katika kata hiyo.

Alisema kashfa zilizotolewa na Nangole alizisikia mwenye katika mikutano mbalimbali ya kampeni na hajui kama mlalamikaji hajawasilisha katika malalamiko yake bali anajuwa alichoandika katika kiapo chake kilichosomwa mahakamani hapo.

Shahidi alikiri mahakamani hapo kuwa alimpigia kura ya ubunge Dkt Kiruswa lakini alisema alitaka mshindi ashinde kwa kufuata taratibu za uchaguzi.

Kesi hiyo inaendelea tena jumatatu mei 30 mwaka huu ambapo  mashahidi wa upande wa mlalamikaji wanatarajiwa kutoa ushahidi wao.

Dada wa Bilionea Msuya Auawa Kinyama Dar.

5/27/2016 08:22:00 am
Aneth Msuya enzi za Uhai wake.


Mtumishi wa Wizara ya Fedha, Aneth Msuya (30) ambaye ni mdogo wa Bilionea
Erasto Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi 22 KIA, ameuawa kwa kuchinjwa
nyumbani kwake eneo la Kigamboni jijini Dar Es Salaam.

Mmoja wa ndugu wa familia hiyo, Shujaa Khamis, jana alithibitisha kuuawa
kwa Aneth, lakini alikataa kuingia kwa undani.
“Ni kweli wamemchinja usiku wa kuamkia leo (jana) na hapa nipo kwenye
msiba hapa nyumbani (Mererani) kwa baba. Tumeambiwa wamechukua Tv tu,”
alisema.

Hata hivyo, Khamis alikataa kueleza lolote kama wana mashaka na mauaji hayo
zaidi ya kuliomba Jeshi la Polisi nchini, kuchunguza kiini cha mauaji hayo na
kuwasaka waliohusika.

Habari nyingine kutoka Wizara ya Fedha, ziliwakariri baadhi ya watumishi
wakisema wamepata taarifa za msiba huo, lakini hawajapewa taarifa rasmi.
“Tuna taarifa tunazisikia sikia kuwa ameauawa, lakini jana (juzi) tulikuwa naye
kazini ila leo (jana) ndiyo tunasikia amechinjwa na watu wasiojulikana.
Imetusikitisha sana,” alisema mmoja wa watumishi hao ambaye hakutaja jina
kwa kuwa si msemaji.

Kamanda wa mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Andrew Satta alipofutwa jana
kuthibitisha taarifa za mauaji hayo alisema yuko kwenye kikao.Wabunge EAC  watangaza kumuunga mkono Rais Magufuli,waomba kukutana nae

5/25/2016 11:03:00 pm
.

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Shy-Rose
Bhanji.PICHA|MAKTABA.

NA  VERO  IGNATUS ARUSHA

Mbunge Shyrose Bhanji wa Tanzania, alisema kasi ya Rais Magufuli, imekuwa na manufaa makubwa sio kwa watanzania bali kwa wananchi wote wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

"vita dhidi ya rushwa na ufisadi ambayo imeanzishwa na Rais Magufuli, ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, inapaswa kuungwa mkono na bunge hilo"alisema

Mbunge Martin Ngoga wa Rwanda, alisema kasi ya Rais Magufuli ambaye ni mwenyekitiwa jumuiya hiyo,inapaswa kuungwa mkono na sio vibaya jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuonesha kwa dhati inapambana na rushwa.

"Rais Magufuli anafanyakazi nzuri sana na sisi kama wabunge tunamuuunga mkono ili kuwa na manufaa katika jumuiya ya Afrika ya Mashariki mataifa yote yanapaswa kushirikiana kuondoa rushwa"alisema


TPRI YATOA ONYO KWA WANANCHI

5/25/2016 11:02:00 pmNA VERO IGNATUS ARUSHA.

TAASISI YA UKAGUZI NA UTHIBITI WA VIWATILIFU TPRI IMETOA ONYO KWA WANANCHI, KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA VYANDARUA VILIVYO INGIA NCHINI KUTOKA NJE YA NCHI,  HUKU VIKIWA NA ALAMA YA UWEPO WA DAWA YA KUUA MBU LAKINI HAVINA MAELEZO YA KULINDA AFYA ZA WATUMIAJI  NA HAVIMO KWENYE ORODHA YA MSAJILI WA VIUATILIFU.

MSAJILI WA VIUATILIFU  DK ELIKANA LEKEI AMETOA KAULI HIYO ALIPOKUWA ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUFUATILIA SHEHENA YA VYANDARUA HIVYO KUINGIZWA NCHINI, HUKU VIKIWA HAVINA MAELEZO YA TPRI HUKU AKIONESHA BAADHI YA VYANDARUA  HIVYO.

KWA UPANDE WAO WAZALISHAJI WA VYANDARUA WAMESEMA HALI HIYO INATOKANA NA VYANDARUA VYA NJE KUINGIZWA NCHINI BILA USHURU NA KWAMBA IMEATHIRI VIWANDA VYA NDANI NA KULAZIMIKA KUPUNGUZA ZAIDI YA WAFANYAKAZI ELFU MBILI.WATU WA JAMII YA WAHAZABE WALALAMIKA KUTENGWA.

5/25/2016 05:32:00 pm

NA VERO IGNATUS  KARATU.

WATU WA JAMII YA WAWINDAJI WAOKOTA MATUNDA NA WALINA ASALI KUTOKA KABILA LA WAHAZABE KATIKA KIJI CHA ENDAMAGH WILAYA YA KARATU ,WAMELALAMIKA KITENDO CHA KUTENGWA KUINGIZWA KWENYE MPANGO WA RUZUKU KWA KAYA MASIKINI ,UNAOENDESHA NA TASAF WAKATI WAO NI JAMII MASIKINI ZAIDI, KWANI KATI  YAO NI KAYA SABA TU NDIZO ZILIZO INGIZWA KWENYE MPANGO ,HIVYO WANALAZIMIKA KUGAWANA KIASI KIDOGO WANACHO  KIPATA.WATU HAO WA KABILA LA WAHAZABE WAMETOA KAULI HIYO  KATIKA KIJIJI CHA ENDAMASH,WALIPOTEMBELEWA NA MAAFISA WA TASAF KUTOKA MAKAO MAKUU, PAMOJA NA WAWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA, AMBAPO WAMEDAI SASA WANALAZIMIKA KUGAWANA FEDHA ZINAZO TOLEWA KWA KAYA SABA KWAKUWA WOTE HAWANA UWEZO NA MATUNDA NA WANYAMAPORI WAMEADIMIKA KUTOKANA NA UKAME .

KWA UPANDE WAKE MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA DUNIA  BI BILLAR BIRD AMESEMA AMESIKITISHWA NA HALI WALIYO NAYO WATU HAO, LAKINI AMECHUKUA MAOMBI YAO NA ATAYAFIKISHA KWENYE KIKAO CHA NCHI WAFADHILI WANAOTARAJIA KUKUTANA MWEZI UJAO.

 

MKURUGENZI MTENDAJI WA TASAF LADISLAUS MWAMANGA AMESEMA KASORO HIZO ZIMETOKANA NA TABIA YA JAMII HIYO YA KUHAMAHAMA NDIYO MAANA WALIKOSA FURSA HIYO LAKINI  TASAF ITAANGALIA NAMNA YA KUWASAIDIA.

MFUMO WA USIMAMIZI WA NYARAKA KIDIGITI KUONGEZA KASI YA UTENDAJI SERIKALINI .

5/25/2016 08:00:00 am


Mfumo wa usimamizi wa nyaraka kidigiti
utaongeza kasi serikalini na hivyo kuchochea
maendeleo chanya katika kila nyanja.

Hayo yamesemwa leo na Katibu mkuu Wizara
ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Prof.Elisante Ole Gabriel wakati wa mafunzo
yanayotolewa na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano kwa Menejimenti ya wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakati
walipotembelea mfumo wa usimamizi wa nyaraka wa kidijiti.

Alisema pia kuwa mfumo huu una faida nyingi na ndio ambazo zimeifanya
wizara hii kutaka kujifunza ni pamoja na suala la gharama na kwa kuwa
serikali ya awamu ya tano iko katika jitihada kubwa za kupunguza matumizi
na kwa kuwa bajeti ya shajala ni kubwa katika taasisi nyingi za serikali hivyo
mfumo huu wa kidijiti utasaidia kupunguza garama kwani hapatakuwa na haja
ya kutumia karatasi na hivyo kupunguza gharama kubwa.

Prof Elisante pia aliongeza kuwa mfumo huu utaongeza usiri wa nyaraka hizi
na kwa sasa zitakuwa zinasomwa na yule tu aliyekusudiwa na kutoa pongezi
kwa ofisi ya rais manejimenti ya umma kwa kuhamasisha matumizi ya mfumo
huu kwani ukitumiwa vyema utakuwa na manufaa sana.

Kwa upande wake Katibu mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
Prof.Faustin Kamuzora alisema kuwa mfumo huo ulijengwa miaka mitatu
iliyopita na unaweza kutumika katika wizara yeyote kwani una ufanisi mkubwa
sana kwani kwa sasa utaweza kuangalia mafaili gani yameingia kwa mfumo
wa kidijitali na kwa namna hii itapunguza garama na muda kwani hatutakuwa
tunatumia karatasi tena.

Prof.Kamuzora alizitaka Taasisi na Wizara mbalimbali kuwapa elimu ya
kutosha watunza kumbukumbu kwani wao ndio wahusika wakuu wa kwanza
wa mfumo huu na hivyo kuwataka wahusika kuwapa mafunzo ya kompyuta na
kuboresha vifaa kama scanner maofisini mwao.

Nae mmoja wa watunza kumbukumbu kutoka wizara Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Bi.Felomena Swai alisema amenufaika na mafunzo hayo na
yatawasaidia katika utunzaji wa kumbukumbu kwani sasa watapeleka barua
kwa wakati na kurahisisha utunzaji wa mafaili.

MWAMKO MDOGO WA WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA WAATHIRI UTALII WA NDANI .

5/24/2016 10:12:00 pm

Mwamko mdogo wa Watanzania
kutembelea hifadhi za Taifa zilizo katika
maeneo mbalimbali nchini umeathiri
kiwango cha idadi ya watu wanaotembelea
hifadhi hizo kwa mwaka hivyo kuzorotesha
mapato yanayotokana na watalii wa ndani
ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Maliasili na Utalii
Prof. Jumanne Maghembe wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Amesema kuwa licha ya Serikali kuweka gharama ndogo za viingilio katika
hifadhi za Taifa kwa watanzania na raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
bado mwamko ni mdogo hasa idadi ya watanzania wanaokwenda kutembele
hifadhi hizo jambo linalopunguza mapato yanayotokana na utalii wa ndani wa
watanzania.

Ameeleza kuwa kwa sasa watanzania kwa maana ya watu wazima
wanaotembelea hifadhi za ndani zilizoko eneo la Kaskazini hutakiwa kulipa
kiingilio cha shilingi elfu kumu (10,000) na shilingi elfu 5000 hadi 15,000
kwa hifadhi zote zilizoko kusini mwa Tanzania huku watoto wakilipia shilingi
2000 kutembelea hifadhi yoyote nchini.

Prof. Maghembe ameeleza kuwa kufuatia hali hiyo Wizara yake inaendelea na
kampeni mbalimbali ili kuwahamasisha Watanzania Wengi zaidi kushiriki
katika shughuli za utalii ndani ya nchi hivyo kuongeza patoa la Taifa.
Amesema katika kulinda na kutunza hifadhi za Taifa ili kuhakikisha zinakuwa
endelevu na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, Serikali ya
awamu ya tano imejipanga kikamilifu ujangili wa wanyama pori kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa uhifadhi.

Amefafanua kuwa katika kupambana na ujangili nchini Wizara kwa
kushirikiana na wadau wa uhifadhi imeshawabaini na kuwashughulikia baadhi
ya wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayopakana na hifadhi
wanaoshirikiana na watumishi wasio waaminifu kushiriki vitendo vya ujangili
pia kuwashughulikia wawindaji haramu wanaojihusisha moja kwa moja kuua
wanyama kufanya udalali na kusafirisha wanyama hao.

Aidha, amesema kuwa katika kupambana na ujangili Serikali inaendelea
kufanya doria ili kuwashughulikia wawezeshaji ngazi ya nchi wanaonunua
nyara, kusambaza silaha, watakatishaji fedha , majangili nguli wa kimataifa
kwa kukitumia na kukiimarisha kitengo cha Intelijensia ili kiweze kutimiza
majukumu ya kiulinzi kwa ufanisi zaidi.

Pia amesema kuwa Wizara hiyo imeendendelea kuongeza idadi ya askari
wanyamapori 447 na maafisa 111 na kufanya idadi ya watumishi waliopo kwa
sasa kufikia 2,064 pamoja na kuanzisha kada nane za doria za ushirikiano
katika mifumo ya ikolojia ya Selous-Niassa-Mikumi, Ruaha- Ruangwa, Katavi
-Rukwa , Moyowosi -Kigosi, Tarangire- Manyara-Simanjiro na Ngorongoro –
Serengeti.


JUMLA YA WATUMISHI HEWA 132 WILAYANI ARUMERU WASHIKILIWA

5/24/2016 08:04:00 pmMkuu wa Wilaya Ya Arumeru Wilson Nkambaku.


NA       VERO IGNATUS ARUSHA.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Wilson Nkambaku,
ametangaza kubaini na kuwashikilia watumishi hewa 132 ambao
wamepatikana katika  Halmashauri ya Arusha na Meru zilizopo
kwenye Mkoa  huo.

Mkuu huyo wa wilaya, Nkambaku amesema bado wanaendelea kuwahoji huku
uchunguzi zaidi ukiendelea, na kwamba tayari akaunti zao
zimefungwa lengo likiwa ni kudhibiti kutoingiziwa tena fedha.

Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri
ya Arusha, Nkambaku amesema kati ya hao, 28 wanatoka katika
Halmashauri ya Arusha na waliobaki wanatoka Halmashauri ya Meru.

Amesema kufuatia hatua hiyo, tayari Wilaya imesharudisha zaidi ya Sh
milioni 70, baada ya watuhumiwa wote kujisalimisha na kurejesha
fedha hizo, na kwamba zaidi ya milioni 10 zimepatikana Halmashauri
ya Arusha na nyingine Halmashauri ya Meru.

Nkambuka ameongeza kuwa mara baada ya uchunguzi kukamilika
watuhumiwa wote watakaobainika watafikidhwa mahakamani kujibu
tuhuma zinazowakabili, ikiwa ni pamoja na uhujumu uchumi wa nchi.
Bunge Latolea Ufafanuzi Madai ya Kitwanga Kujibu Swali Bungeni Huku Akiwa Amelewa

5/24/2016 08:01:00 pm

Nape Nnauye Ashindwa Kuhutubia Kwenye Tamasha la Muziki Jijini Mwanza Kutokana na Zomeazomea Ya Wananchi Wanaotaka Bunge Lionyeshwe Live

5/24/2016 01:08:00 pm


Mzimu wa kuzuia shughuli za Bunge kuonyeshwa moja kwa moja na
vituo vya televisheni uliopachikwa jina la ‘Bunge Live’, umeendelea
kumwandama Waziri wa Habari, Nape Nnauye baada ya juzi kupokewa
kwa kelele kiasi cha kushindwa kuhutubia wapenzi wa muziki jijini
Mwanza.
Nape alitangaza uamuzi wa kusitisha kurusha moja kwa moja baadhi ya
shughuli za Bunge, akisema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)
linashindwa kumudu gharama, lakini wabunge, hasa kutoka vyama vya
upinzani wamepinga hatua hiyo wakisema inawanyima wananchi haki
yao ya kikatiba ya kupata habari kuhusu chombo chao cha kutunga
sheria.
Lakini Serikali imeshikilia msimamo wake, ikitoa sababu tofauti na
kwenda mbali zaidi kuzuia vituo binafsi vya televisheni kurusha
matangazo, huku TBC1 ikirusha kipindi cha maswali na majibu pekee
ikielezwa kuwa huo ni uamuzi uliopitishwa katika Bunge la 10.
Juzi, Nape aliyekuwa mgeni rasmi katika tamasha la Jembeka Festival
lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, alipokewa na kelele za
maneno “Bunge Live” wakati akikaribishwa kuhutubia mamia ya wapenzi
wa burudani waliohudhuria tamasha hilo, ambalo lilijumuisha wasanii
nyota kama Shaffer Chimere Smith a.k.a Ne-Yo kutoka Marekani na
Diamond Platnum.
Baada ya mkurugenzi wa kampuni ya Jembe ni Jembe, Sebastian Ndege
kumkaribisha waziri huyo kuzungumza na wananchi hao, Nape
alisimama lakini akapokewa kwa kelele.
“Bunge live, Bunge live, Bunge live,” walipiga kelele mashabiki
waliohudhuria tamasha hilo.
Kelele za “Bunge Live” zilisababisha Waziri Nape kushindwa kuhutubia na
kulazimika kuketi chini na Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula
alisimama kujaribu kuokoa jahazi, lakini naye akakumbana na kimbunga
cha sauti za wananchi walioamua kulitaja jina la mbunge wa zamani wa
jimbo hilo, Ezekia Wenje.
“Wenje, Wenje, Wenje,” wananchi hao waliimba kwa sauti wakati Mabula
akijaribu kuwatuliza ili Nape ahutubie.
Akizungumzia tukio hilo, Nape alisema wananchi waliompigia kelele za
“Bunge Live” walisukumwa na masuala ya kisiasa, ndiyo maana aliepuka
kuendelea kuzungumza ili kutochafua hali ya hewa uwanjani.
“Pale uwanjani tulikwenda kwa ajili ya burudani, sasa baada ya kuona
wananchi wanaanza kuleta masuala ya kisiasa nikaona ni busara kuacha
kuhutubia. kuepusha shari,” alisema Nape.
Pamoja na Nape, tamasha hilo pia lilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano), January Makamba, Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Mabula.
Ukiachilia mbali dosari hizo, tamasha hilo lilikonga nyoyo za wapenzi wa
sanaa ya muziki waliokesha uwanjani hapo hadi saa 11:00 alfajiri
wakiburudishwa na wasanii nguli.
Wasanii wengine waliopata nafasi ya kutumbuiza ni Juma Nature, Ney
wa Mitego, Ruby na Fid Q.
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel