Top Menu

VETA&AIRTEL: WAMEANZA KUTOA MAFUNZO KWA NJIA YA SIMU.

6/30/2016 09:15:00 pm
Bi Hawa Bayumi Meneja Huduma za Jamii kutoka Airtel Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Veta Kilichopo Kipawa Jijini Dar es salaam,Mhandisi Lucius Lutenganya.
Mkuu wa Chuo cha VETA kilichopo Oljoro Jijini Arusha,Ndugu Banga Deusdedit Mrefu.
Meneja masoko wa Kanda Airtel Brightone Majwala 
Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Msadizi Utawala Arusha akisalimiana na Mkuu wa chuo cha VETA,Mhandisi Lucius Lutenganya  walipokutana Jijini Arusha  kwenye kutoa Elimu kuhusiana na Mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu uliowezeshwa kwa ushirikiano wa Airtel na VETA.
Kutoka kushoto Meneja Masoko wa Kanda Brightone Majwala ,akiwa na Meneja Huduma za Jamii Bi Hawa Bayumi wakiwa wanatoa elimu kwa wananchi wa Arusha kuhusiana na VSOMO,yaani mfumo wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu.
Mratibu wa Mradi wa VSOMO Tanzania ndugu Gosbert Kakiziba kutoka VETA Kipawa Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Chuo cha VETA Oljoro Arusha akitoa elimu ya VSOMO pamoja na kujibu maswali mbalimbali aliyoulizwa.na baadhi ya wananchi na madereva Bodaboda maeneo ya Mountmeru Jijini Arusha
Mratibu mradi wa VSOMO Tanzania ndugu Gozbert Kakiziba kutoka Veta Kipawa Jijini Dar es salaam akiwa.anawaelekeza baadhi ya vijana namna ya kujiunga na Vsomo kupitia simu zao za mkononi yaani smartphone ya android
Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Utawala Arusha ndugu Mushashu Analet ,Mkuu wa Chuo VETA Kipawa  Mhandisi Lucius Lutenganya ,akifuatiwa na Mkuu wa chuo cha VETA kilichopo Oljoro Arusha ndugu Banga Deusdedit Mrefu pamoja na Mratibu Mradi wa Vsomo Tanzania Ndugu Gosbert Kakiziba .
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Arusha wakifuatilia kwa makini elimu inayotolewa kuhusiana na mfumo wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu yaani VSOMO yaliyokuwa ikiendelea kutolewa.
Wakazi wa Arusha wakifuatilia na kusoma vipeperushi vya Vsomo walivyopewa maeneo ya Mountmeru Jijini Arusha kuhusu mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu.
Mkuu wa chuo cha VETA Kipwa Jijini Dar  es salaam,Mhandisi Lucius Lutenganya akimsaidia kijana huyo pichani kuelewa maana ya VSOMO Jjini Arusha.


ARUSHA
Chuo cha Ufundi Veta kwa kushirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Airtel wamezindua mfumo wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu ujulikanao kama VSOMO ambapo mwanafunzi anasoma kwa kutumia simu yake ya mkononi ya smartphone ya android.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mkuu wa chuo cha VETA kilichopo Kipawa jijini Dar es salaam Mhandisi Lucius Lutenganya amesema kuwa VSOMO ni mfumo wa mafunzo ya Ufundi stadi kwa njia ya simu uliowezeshwa kwa ushirikiano wa Airtel na VETA.

Lucius amesema kuwa mfumo huo utamsaidia mwanafunzi kusoma mahali popote atakapo kuwepo kwa muda mfupi akiwa na simu ya smartphone,kisha atapatiwa mtihani wakufanya akifaulu vizuri anapatiwa cheti cha ufaulu kutoka VETA.

Kwa upande wake Meneja Huduma za Jamii bi Hawa Bayumi amesema kuwa namna ya kujiunga na VSOMO ni kwa kutumia smartphone ya android,unapakua App ya VSOMO kupitia google play store na unajisajili bure.

Bi Hawa ameainisha kuwa gharama za kujiunga na VSOMO kwa kila kozi  ni Tsh.120,000/= na mwanafunzi atalipia kupitia airtel money kwa kupiga *150*60# anakuwa tayari ameshalipa na anaanza masomo yake bila usumbufu wowote.

Naye Mratibu Mradi wa VSOMO ndugu Gosbert Kakiziba amesema kuwa hadi sasa kozi walizoanza nazo ni pamoja na Ufundi pikipiki( bodaboda) Ufundi wa umeme wa majumbani,Ufundi wa simu za mikononi,Ufundi wa Alluminium ,Utaalamu wa masuala ya urembo pamoja na ufundi wa kuchomelea vyuma.

Gosbert amesema kuwa baada ya mwanafunzi kusoma kwa njia ya simu kisha kupewa mtihani,wao VETA wanamchukua mwanafunzi huyu ili kujiridhisha  na kukaa nae chuoni kwa wiki mbili akipatiwa mafunzo kwa njia ya vitendo baada ya hapo muhitimu huyu atakabidhiwa cheti na mamlaka ya ufundi stadi nchini VETA.

Naye Meneja Masoko wa Kanda kutoka Airtel ndugu Brightone Majwala amesema kuwa hadi sasa tayari wameshafikia mikoa mitano ya Tanzania, kuhusiana na mfumo huu wa mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu na wanatarajia ifikapo desemba mwaka huu watakuwa wameshafikia mikoa ishirini hapa mchini.

Brightone amesema ili uweze kupata mafunzo ya ufundi kwa njia ya simu ya mkononi itampasa mwanafunzi awe line ya airtel vinginevyo ataikosa fursa hiyo.


Ibuprofen inaweza kupunguza makali ya Ebola

6/30/2016 06:12:00 pm

Dawa ya maumivu Ibuprofen na dawa ya kutibu saratani Toremifene zinaweza
kukata makali ya virusi vya ugonjwa wa Ebola ,watafiti wamesema.

Wanasayansi walitumia Kifaa cha Diamond Light Source kuvifanya uchanganuzi
virusi vya ebola kwa kina.

Walibaini kwamba dawa hizo mbili zinaweza kushirikiana kukabiliana na Ebola
wakati virusi hivyo vinapojiandaa kuambukiza seli za mwili wa bindamu.

Hatahivyo ,watafiti hao wameonya kwamba huo ni mwanzo na kwamba dawa
zaidi zilizo na uwezo mkubwa zinafaa kutafutwa.

Synchrotron hiyo huchochea kasi ya elektroni hadi kuzalisha mwanga mkali
sana.

Hii inaweza kutumika kwa kuchambua mradi wa kutengeza vitu wa atomiki
katika mpango mkubwa zaidi kuliko darubini za kawaida.

Lengo la utafiti huo ni protini kwenye uso wa virusi vya Ebola ambayo
inaviruhusu kuambukiza seli.

''Hili ndio lengo kuu katika uso wa virusi hivyo,hili ndio huwajibika kujiweka
katika seli ,ni protini muhimu kuelewa'',alisema mtafiti Prof Dave Stuart, kutoka
Chuo Kikuu cha Oxford.Mlipuko wa bomu wawaua watu 18 Somalia

6/30/2016 05:57:00 pm

Habari kutoka Somalia zinasema kuwa watu 18 wameuawa baada ya bomu
kulipuka na kuharibu kabisa basi walimokuwa wakisafiria katika mji mkuu wa
Somalia, Mogadishu.

Bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara lililipua gari lililokuwa limewabeba
abiria. Wote waliouawa walikuwa raia.

Mashambulizi hayo yalitokea katika mji wa karibu wa Lafole.
Inadhaniwa kuwa washambuliaji hao walikuwa wakilenga gari la wanajeshi
lililokuwa karibu.
Mara kwa mara wapiganaji wa Al Shaabab hulenga wanajeshi wa Serikali.

Habari hii ni kwa mujibu wa BBC.
Kesi ya Uchochezi: Tundu Lissu apandishwa kizimbani, apata dhamana....Kesi yaahirishwa hadi Agosti 2

6/30/2016 05:10:00 pm
Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo
kudharaulisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.

Lissu alisomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar
es Salaam leo Juni 30, 2016.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bernad Kongola
akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Nassoro Katuga na Salum
Mohammed.

Kongola alidai kuwa Juni 28,2016 eneo la Mahakama ya Kisutu Ilala Dar es
Salaam mshtakiwa alitamka maneno ya dhihaka kwa nia ya kushawishi na
kudharaurisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.

Alinukuu maneno ya Lissu kwamba"Mamlaka ya Serikali mbovu ya kidikteta
uchwara inahitaji kupingwa na kila mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikteta
uchwara lazima apingwe kila sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa
kijinga nchi inaingia ndani ya giza nene"
Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

Upande wa jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na uliomba tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali.
Upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili 11 akiwemo Michael Ngalo,
Peter Kibatala na wenzao uliomba dhamana kwa mshtakiwa kwa kuwa ni
mbunge atakuwa mwaminifu hataacha kufika mahakamani.

Hakimu Yongolo alisema mshtakiwa atakua nje kwa dhamana kwa kuwa na
wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya sh milioni 2.
Tundu Lissu alitimiza masharti na kuachiwa kwa dhama, atasomewa maelezo
ya awali Agosti 2,2016.


Wabunge watatu wa CHADEMA wasimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge

6/30/2016 04:59:00 pm
Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasi na Maendeleo
(CHADEMA), Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria na vikao 10 vya
Bunge kuanzi leo kufuatia kitendo cha kuonyesha kidole cha kati bungeni.

Joseph Mbilinyi alitenda kosa hilo alipokuwa akitoka nje ya ukumbi wa Bunge
baada ya kile alichoeleza kuwa kuna mbunge wa CCM aliyemtusi mama yake.
Hata hivyo alipohojiwa kama anamfahamu mbunge huyo, Mbilinyi alisema kuwa
hamfahamu.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson baada
ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Bunge kueleza kuwa kamati hiyo
ilijiridhisha kuwa kitendo kilichofanywa na mbunge huyo kuwa ni kosa.

Aidha wabunge wangine waliosimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge ni
pamoja na Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, James Ole Millya Mbunge wa
Simanjiro kwa makosa yanayofanana ya kusema uongo bungeni. Wabunge
hawa wamesimamishwa kuhudhuria vikao vitano kuanzi leo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahirisha mkutano wa
tatu wa Bunge lililokuwa na lengo la kujadili na kupitisha bajeti ya serikali ya
mwaka wa fedha 2016 2017. Kufuatia kuahirishwa huko, kuanzia kesho Julai
Mosi, serikali itaanza kutekeleza miradi na mpango mingine iliyoanishwa katika
bajeti hiyo.

Yanga yachapwa nyumbani 28-06-2016

6/28/2016 11:00:00 pm
Ikicheza kwenye dimba lake la nyumbani mbele ya mashabiki zaidi ya elfu
arobaini waliofurika kwenye dimba la Taifa, wawakilishi wa Tanzania katika
michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Yanga wamechapwa bao 1-0 na
TP Mazembe.

Yanga imepoteza mchezo wake wa pili mfululizo katika kundi A linaloongozwa
na TP Mazembe iliyofikisha pointi sita.
Yanga ilichapwa bao 1-0 na Mo Bejaia ya Algeria katika mchezo wake wa
kwanza uliopigwa nchini Algeria.

Licha ya kupoteza mchezo wa leo, Yanga imezidi kuimarika kwani iliweza
kuwadhibiti vijana Moise Katumbi kipindi chote cha kwanza.
Kipindi cha pili TP Mazembe ilirejea kwa nguvu, huku Thomas Ulimwengu
akiisumbua sana ngome ya Yanga.

Uzoefu wa mabingwa hao mara tano wa Afrika ndio uliofanya klabu hiyo itoke
na ushindi kwenye dimba la Taifa.

Licha ya uwanja kuonekana kufurika mashabiki wa Yanga waliokuwa wamevalia
mavazi ya timu hiyo, kulikuwa na idadi kubwa ya washabiki wanaodhaniwa
kuwa wa Simba ambao walikuwa wakishangilia klabu ya TP Mazembe tangu
mwanzo wa mpambano huo.

Yanga itacheza mchezo wake dhidi ya Medeama ya Ghana July 15, italazimika
kushinda mchezo huo kuweka hai matumaini yake madogo ya kutinga nusu
fainali.
Y

Polisi yanasa Bunduki zilizokuwa zikitoroshwa Tabora

6/28/2016 10:55:00 pm
Polisi Mkoani Tabora imekamata bunduki nne zilizokuwa zinatoroshwa ikiwa ni
siku kadhaa baada ya Mkuu wa mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri, kutoa wiki
moja kwa ajili ya wanaomiliki silaha mkoani humo kuzisalimisha kwa hiyari.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,
Kamishna Msaidizi wa Polisi Khamis Selemani Issa, amesema silaha hizo
zilikuwa zinatoroshwa kutoka wilaya ya Kaliua kwenda maeneo mengine baada
ya amri ya mkuu wa mkoa.

Kamanda Issa amesema kuwa kati ya waliokamatwa ni pamoja na mtoto wa
miaka 16 hiyo jeshi la polisi linachunguza kwa kina juu ya umri halisi ya
mtuhumiwa huyo aweze kufunguliwa mashtaka kutokana na umri wake.

Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora ameendelea kuwasihi wananchi
wanaomiliki silaha kinyume cha sheria Mkoani humo kuendelea kuzisalimisha
kwa hiari na kusisitiza endapo mtu atakutwa katika opresheni ya kuzisaka
silaha hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Lissu afikishwa Mahakamani

6/28/2016 10:49:00 pm


Mwanasheria wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu
ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani ameseme kuwa,
vitendo vinavyofanywa na serikali ya awamu ya tano ni vya hovyo.

Lissu ameyasema hayo muda mfupi baada ya kumaliza kusikiliza shauri lake
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam
Kwenye shitaka hilo, Lissu pamoja na washitakiwa wengine watatu wanadaiwa
kufanya makosa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchochezi kupitia gazeti la
Mawio la tarehe 14 Januari 2016.

Kwenye gazeti hilo lililoandikwa kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’
Lissu alinukuliwa kama mchangiaji wa gazeti hilo ambapo tayari limefutwa na
serikali.

Nje ya mahakamani hiyo Lissu amesema “nchi yetu imeingia katika giza nene,
mambo yanayofanywa na Serikali hayakubaliki.

“Kila msema kweli wa nchi hii, huu ni wakati wa kujitokeza na kusema hii ni
nchi ya vyama vingi, hii ni nchi inayotambua haki za binadamu kwenye Katiba
yake.

“Hatuwezi tukakubali nchi iongozwe kwa kauli za mdomo za mtu mmoja hata
kama amechaguliwa kuwa rais.”
Akizungumzia kesi iliyofunguliwa na kuhusishwa kwake Lissu amesema, kesi
iliyofunguliwa na serikali dhidi yake na wahariri wa gazeti la Mawio ya
uchochezi, ni ushahidi tosha kuwa nchi imeingia kwenye giza nene la
udekikteta.

Amesema, hata sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ipo wazi kwamba, kuikosoa
serikali sio uchochezi.

“Mashtaka haya yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezo, sio ya uchochezi hata
kidogo. Nilichosema, niliulizwa na waandishi … nilisema uchaguzi wa marudio
Zanzibar unaweza kuviingiza visiwani hivyo kwenye machafuko na umwagaji
damu… ni kauli ya raia anayefahamu na hapendezwi na mwenendo wa serikali”
amesema Lissu.

Amesema kuwa, hata sheria ya magazeti inasema kuwa kitendo chochote
chenye lengo la kueleza ubovu wa serikali au mamlaka yake sio kosa.
“Nilichosema mimi kuwa serikali hii na matendo yake ni ya hovyo… hali hii
inahitaji kupingwa na kila mwananchi,” amesema.

“Kama wanafikiria watatutisha kwa kutuleta mahakamani, tutamkabili
mahakamani na tutamkabili nje.
“Ni wakati wa wazalendo kusema kuwa, Tanzania ni nchi ya vyama vingi na ina
Katiba na sheria.

"Katiba yetu inatambua haki za binaadamu na moja haki za binaadamu ni
kueleza ujinga wa watawala wanapofanya ujinga,” amesema.


Tunaitafakari Uingereza bado:Marekani

6/28/2016 07:12:00 am

Kufuatia kura ya maoni ya Uingereza kujitoa ndani ya Jumuiya ya Ulaya
waziri wa mambo ya kigeni wa Marekari John Kerry amesema Marekani
inaangalia mfumo wa ushirikiano na Uingereza kiuchumi.

Msimamo huo wa Marekani dhidi ya Uingereza,ni kufuatia kura ya maoni ijumaa
wiki iliyopita, kujitoa katika jumuiya ya Ulaya. John Kerry ameyasema hayo
katika mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond

Hata hivyo waziri Hammond alitaka kujua kama Rais Obama anamtazamo
tofauti na kauli yake ya awali,kuhusiana na Uingereza ambapo awali alisema
Uingereza itarudi mstari wa nyuma kibiashara iwapo itapiga kura kujitoa.Lakini
Waziri Kerry akalitolea ufafanuzi hilo.

John Kerry anasema kilicho salia kwa Marekani ni kusubiri na kuona matokeo
ya mazungumzo hayo na kuamua ni kwa mfumo gani uendeshaji wa mahusiano
ya kibiashara utakuwa iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo.

Akizungumzia kauli ya Rais Obama alisema Uingereza imekuwa na ushirikiano
imara na Marekani kwa miaka mingi,na kuwa rais atafanya kila linalowezekana
kusaidia kwa namna yoyote kuimarika kwa umoja uliopo na Uingereza na pia
kusaidia jumuiya ya Ulaya kwa maslahi ya usalama wa dunia na ustawi wa
dunia kwa ujumla.

Habari hii ni kwa mujibu wa BBC.
Ajali ya EgyptAir kisanduku kuchunguzwa

6/28/2016 07:02:00 am

Wataalam wa masuala ya anga wamefanikiwa kurekebisha kifaa kinachotunza
kumbukumbu ya mwenendo wa ndege cha EgyptAir iliyoanguka mwezi uliopita
na kuua watu 66 waliokuwamo ndani yake.

Hatua hiyo inawapa nafasi wachunguzi hao kuweza kuzitafakari na kuzifuatialia
taarifa zitakazobainisha ni kwanini ndege hiyo ilianguka mashariki mwa bahari
ya Mediterranian. 

Taarifa rasmi kuhusiana na uchunguzi huo zinasema kuwa
kazi ya kusikiliza na kuzifuatilia sauti hizo itafanyika ndani ya saa chache
zijazo. Kisanduku hicho cha mawasiliano kimefikishwa mjini Paris Ufaransa jana
jumatatu kutoka Cairo Misri ambapo kimepelekwa huko ili kuondoa tabaka za
chumvi zilizokizunguka chombo hicho. 

Hata hivyo kinatarajiwa kurejeshwa katika maabara za mjini Cairo kwa uchunguzi zaidi baada ya marekebisho yotekukamilika ,mapema wanasheria nchini Ufaransa walifungua kesi ya mauaji
dhidi ya ajali hiyo kwa madai kuwa ilitokana na hujuma. Wanasema hakuna
uthibitisho wowote kuwa ajali hiyo ilitokana na ugaidi

Habari hii ni kwa mujibu wa BBC.Jeshi la Polisi laua vinara wa mauaji Tanga, Mwanza

6/27/2016 08:18:00 pm

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam leo limeeleza kumuua Salum
Saidi Muhangwa (30) kwa madai ya kuwa miongoni mwa waliofanya mauaji
kwenye msikiti huo.
Akizungumza na wanahabari Simon Siro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam amesema, mtu huyo ameuawa leo asubuhi wakati akijaribu
kuwakimbia polisi kupitia dirishani.
“Baada ya kufanya mauaji kule Mwanza na kikundi chake walikimbilia huku Dar
es Salaam, taarifa za raia wema zimetuonesha jambazi huyo alikua anaishi
Buguruni,” amesema.
Mauaji hayo yalifanyika tarehe 19 Mei mwaka huu katika msikiti huo uliopo
kwenye Kata ya Mkolani wilayani Nyamagana ambapo watu watatu, waumini
wa msikiti huo waliuawa wakati mwingine mmoja akijeruhiwa.
Kamanda Sirro amesema, mtu huo baada ya kugundua kuwa askari
wamezunguka jengo alilikuwemo, alijaribu kujihami kwa kuwarushia askari bomu
la mkono ambapo askari walifanikiwa kumpiga risasi ya mguu hatimaye kufariki
wakati akipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
“Tunashukuru askari hawakufanywa lolote katika tukio hilo na tunashukuru kwa
sababu wapo makini,”amesema Kamanda Sirro.
Hata hivyo amesema, mtu huyo amefanya matukio mengi pale Mwanza
yakiwemo kufanya unyang’anyi katika vituo vya M-Pesa, Tigo Pesa, uchinjaji
watu msikitini pamoja na maduka makubwa.
“Kuna timu yake imebaki hapa Dar es Salaam lakini tuwahakikishie wana Dar es
Salaam kwamba, tutawakamata na haki itatendeka lakini wakikaa vibaya
wasilaumu serikali.
“Kwa sababu silaha wanazozitumia hawajanunua madukani, wanakaa nazo
visivyokua halali wabadilike wawe raia wema itawasaidia lakini kwa staili hii
niwaambie wataacha familia zao kwa sababu ukamataji wa mtu mwenye silaha
sisi ndio tunajua namna ya kukamata,”amesema.
Katika tukio jingine, Jeshi hilo limefanikiwa kumuua jambazi sugu aliyefahamika
kwa jina la Mohamed Abdallah akiwa na bastora aina ya nolinko, risasi 19 na
bomu la kutupa kwa mkono.
“Baada ya kufanya mauaji Tanga na kikundi chake walikimbilia hapa Dar es
Salaam, naye akachomoka na kuanza kupambana na polisi, na askari wetu
waliweza kumjeruhi vibaya sana naye wakati akipelekwa hospitali alifariki
dunia.
Kamanda Siro amesema mtu huyo ni kiongozi mkubwa aliyebaki katika kundi la
majambazi mkoani Tanga na amehusika katika mauaji ya watu wanane pamoja
na ujambazi uliofanyika katika kituo cha mafuta mjini humo.
“Wananchi na hasa raia wema waendelee kutupa taarifa kwa watu
wanaowatilia mashaka,” amesemaMpango wa chakula Muhimbili wasitishwa

6/25/2016 10:58:00 pm


Ule mpango wa kuwauzia chakula kwa Sh6,000 kwa siku wagonjwa
wanaolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili umesitishwa kwa muda.

Mpango huo umesitishwa leo na Waziri Afya, Ummy Mwalimu akisema inabidi
Serikali ijiridhishe jinsi mpango huo utakavyotekelezwa.

Amesema wizara imebaini kwamba wananchi hawakushirikishwa vyema, hivyo
ameagiza uongozi wa hospitali hiyo kuanza kutoa elimu kwa wananchi ili
waelewe mpango huo.

“Ni mpango mzuri tumeukubali kama wizara, lakini tunaona kuna mambo
ambayo tunapaswa kujiridhisha kwanza, kama wagonjwa ambao wanatibiwa
kwa bima ya afya huku MNH wakihitaji kulipwa fedha taslimu kwa huduma hiyo" amesema

Janga la Watumishi hewa Mwanza

6/25/2016 10:50:00 pm
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema watumishi hewa 367 kati
ya 1057 wamebainika kutafuna zaidi ya Sh. bilioni 2 mkoani humo.

Ulipaji wa mishahara watumishi hewa unadaiwa kufanywa na baadhi ya wakuu
wa idara na wakuu wa vitengo wasiokuwa waaminifu huku wengine
wakituhumiwa kupokea fedha zilizokuwa zikitolewa.

Mkuu wa mkoa John Mongella ameyasema hayo mbele ya Susan Mlawi, Naibu
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma wakati wa
maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma.

Mongella amesema, kumekuwepo na baadhi ya wakuu wa idara na wakuu wa
vitengo mkoani humo wasiokuwa waaminifu ambao wamesababisha kuendelea
kuwepo kwa watumishi hewa, kitendo ambacho alidai hakitafumbiwa macho.

Amesema kuwa, katika uhakiki wa watumishi hewa katika mkoa huo, ulioanza
Aprili 18 na kumalizika Juni 3 mwaka huu, umefanikiwa kuwapata watumishi
hao hewa huku wengine wakiendelea kulipwa mishahara.

“Kuna watumishi wa 13 katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Halmashauri
ya Kwimba ambao wamekopa mikopo benki na wakati hawapo katika utumishi
wa umma na wanaofanya hayo ni wakuu wa idara.

“Pia kuna watumishi 72 ambao wamelipwa mapunjo ya mishahara katika
halmashari ya Wilaya ya Magu kupitia akaunti zao za benki na vilevile
wakalipwa tena kupitia dirishani (Double payment) na kila mmoja alikuwa
analipwa zaidi ya milioni tatu,” amesema Mongela.

Mongela amesema, kutona na kuwepo kwa watumishi hao, ofisi yake inakusudia
kuwafuta watumishi wote wasiojulikana kwa waajiri, kuwafuta kwenye malipo
watumishi waliofariki, walioacha kazi waliofukuzwa kazi na waliostaafu.

Wengine watakaofutwa ni waliogombea nafasi tofauti ikiwemo ubunge,
kuwachukulia hatua maofisa wa halmashauri waliohusika kuanzisha na
kuidhinisha mikopo kwa watumishi waliotoka katika utumishi wa umma.

Hatua nyingine zitakazochukuliwa ni kuhakikisha watumishi waliolipwa mapunjo
ya fedha za mishahara zaidi ya stahili zao zinarejeshwa, kuwachunguza na
kubaini maafisa na wasimamizi wa watumishi waliosababisha upotevu wa
fedha kupitia malipo ya mshahara wa watumishi hewa.

Hata hivyo Mongella amesema, Februari mwaka huu watumishi hewa waliolipwa
mshahara katika sekretarieti ya mkoa na halmashauri walikuwa 28,068,
halmashauri 27, 416 na katika sekretarieti ya mkoa walikuwa 652 huku
watumishi wa halmashauri waliohakikiwa ni 26, 359 ambao hawakufika
kuhakikiwa ni 1,057.

Na kwamba licha ya kutolewa kwa tangazo la kuwaita watumishi wote, waliopo
masomoni, likizo na waliohama vituo vyao vya kazi lakini wengine hawakuweza
kutekeleza agizo hilo jambo ambalo linaonesha wazi ni watumishi hewa.Msanii Afande sele ameweza kuweka wazi na kusema kwa sasa nawanawake kama sita hivi anawapima.

6/25/2016 11:01:00 am

Msanii Afande Sele amesema kuwa ana wanawake kama sita hivi ambao wanaangalia watoto wake, huku akiangalia kati ya watu hao alionao yupi anastahili kuwa malkia.

Afande Sele alisema hayo kupitia mishe mishe media na kusema kwa sasa yeye kusema atafunga ndoa itakuwa ni uongo mkubwa kwani watu alionao anaona bado wanapimana maana wao wanampima yeye na yeye anawapima wao na kuona yupi anastahili kuingia ndani kama mke.

"Niwe mkweli tu hilo wazo la kuvuta jiko sina, namshukuru Mungu nimepata watoto wawili naweza kwenda nao vizuri na kuwalea, kusema nifunge ndoa leo au kesho utakuwa uongo sababu ndoa si kusema mwanamke kuchukua nyanya tu gengeni,lazima nipate mwanamke amabaye atakuwa na vigezo vya kuwa na mimi atajua nini maisha ambayo mimi nayahitaji, atanielewa tabia zangu za nje na ndani hivyo sidhani kama ni rahisi kupata mke kwa kipindi hiki ila najivunia kuwa na marafiki ambao wanasaidia kulea watoto wangu, wanawapenda watoto zangu hicho nashukuru" alisema Afande Sele.
.
"Nipo kwenye kupima nawapima na wao wananipima mimi, mimi na marafiki wa hivyo wakati ukifika nikiona yupo anafaa kuwa na mimi nitakuwa naye lakini niwe mkweli, siko mwenyewe au kusema natumia sabuni hapana mimi na warembo kama kawaida, wananisaidia kukaa na watoto wangu, wanaheshima. Maana mimi ni kama mfalme hata mfalme Suleman alikuwa wa wake zaidi ya mia tatu kwenye nyumba yake, hata mimi wapo kadhaa ila hawazidi sita" aliongeza Afande Sele.

WATANZANIA TUACHE UWOGA KILIMO CHA NYUMBA YA KIJANI KINALIPA.

6/25/2016 10:51:00 am
o
Mkurugenzi wa Wigo Farming Production Godson Moshi akionyesha akionyesha mche wa Hoho ukiwa  katika hatua za awali za kutoa matunda,ambapo unaonekana ukiwa tayari na matunda sita ambapo kila mche unauwezo wa kutoa matunda kwa kila wiki.

Aina ya nyanya iitwayo Cherry tomato ambayo wengi wamezowea kuiita (nyanya pori ) ikiwa imezaa vizuri tayari pia imeanzwa kuvunwa ,mche wake unarefuka hadi urefu wa mita 10.Mbegu yake kwa kitaalam inafahamika kama FORTESA ambapo tawi moja linatoa nyanya 18-35.
Aina ya pilipili hoho ambayo pilipili za rangi ,inaanza kuwa Kijani,inaendelea kubadilika na kuwa Zambarao, baadae inakuwa Nyekundu ambapo mbegu zake zinafahamika kitaalam kama PASARELLA,Pilipili hizi ni nzuri sana kwa juice ,kupika inavirutubisho vya kutosha kwaajili ya mwili wa binaadamu.
Ndugu Godson Moshi akionyesha hoho.ya njano.inavyoonekana ikiwa  imeshabadilika rangi kutoka kijani kuwa ya Njano ,ikiww tayari kwa kuvunwa kupelekwa sokoni.
Cherry tomato ikiwa inaonekana jinsi linavyozaa kwa wingi ambapo tawi moja linauwezo wa kuzaa nyanya kuanzia 18-35 huku mche mmoja unauwezo wa kutoa kilo 20-30 za nyanya.
Pilipili hoho ikiwa katika muonekano tayari imeshaanza kubadilika rangi,kama inavyoonekana,Itaendelea kubadilika yote hadi kuwa na rangi moja ya Njano.


Hoho nyekundu zikiwa zimevunwa tayari kwa kwenda sokoni hizi zinabadilika kutoka Kijani na kubadilika rangi kuingia nyekundu.
Pilipili hoho za rangi inavyobadilika kutoka rangi ya Kijani ,Zambarau na kuingia rangi nyekundu kama inavyoonekana kwenye picha.
Mkurugenzi wa Wigo Farming Production akionyesha nyanya mshumaa,ambapo aina hii ya nyanya inalimwa kutokana na mahitaji ya soko kwani watu wengi wanazipenda kutokana siyo chachu na zina ladha nzuri kwenye chakula, pia ndiyo nyanya iliyopo kwenye soko kwa sasa.Mche wa nyanya hii unarefuka hadi kufikia mita 10,kwa wiki unaweza kuvuna kilo 1-1.5.
Ndugu Salum Sefu akiwa anavuna hoho ambazo zimekishawiva tayari ,kuzivuna lazima uwe na utaalamu ili usiharibu tawi na ili ziweze kuendelea kuzaa vizuri pia hizi nazo zinarefuka hadi urefu wa mita 10.
Ndugu Salum Sefu akiwa tayari ameshavuna hoho,anaziandaa kwa kupelekwa sokoni.Wito umetolewa kwa serikali iwasaidie wakulima kuondokana na kilimo cha wazi,watumie kilimo cha (Green house)nyumba ya kijani ili waweze kujikwamua kutoka kwenye kilimo cha umaskini ambacho wanatumia gharama kubwa na nguvu nyingi .

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mkuu wa Wigo Farming Production iliyopo jijini Arusha, ya kwamba mkulima anapotumia kilimo cha Nyumba ya Kijani( green house)inamsaidia mkulima kuuza mazao yake kwa usahihi na kwa uhakika maana atakuwa ametumia kilimo ambacho kinatumia mbolea za asili zisizokuwa na kemikali.

Amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo ni upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa (Green House)gharama zake na vifaa ni ghali, upatikanaji wa mbolea za asili kama vile mkojo wa Sungura ambao inawalazimu kuuagiza kutoka Nchi jirani ya Kenya, Mkojo wa ng'ombe ,kwani kilimo hiki hakitumii mbolea za kawaida.

Aidha ameongeza kuwa kama wakulima watasaidiwa nakupewa elimu ya kutosha kuhusu kilimo cha Nyumba ya Kijani, kitamuingizia mkulima faida mara  kwa mara kwani kwa sasa soko ni kubwa lakini bidhaa zinazohitajika ni watu wachache tu ndiyo wanalima.

"Kwa mkulima anayelima kilimo hichi cha  (Green house)gharama zake ataziona pale awali wakati anaandaa nyumba ya kijani,lakini baada ya muda mfupi sana mkulima huyu ataanza kuona faida na gharama zake zote zitarudi bila usumbufu wowote,hata kama umechukua mkopo utaulipa kwa wakati maana kilimo hichi kinalipa,pia masoko ya kuuza mazao yapo haswa nchi za Uarabuni na Ulaya pamoj na.kwenye mahoteli makubwa ya Kitalii, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu tuingie tuanze kulima ,tuondoe woga"Alisema Godson Moshi.

 

Alex Msama Amwangukia Mwakyembe Kumuomba Radhi Baada ya Gazeti ya DIRA Analolimiliki Kuchapisha Habari Zenye Utata

6/23/2016 09:05:00 pm
MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,
Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la
Dira ya Mtanzania analolimiliki

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema
amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa
Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.

Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya
Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.
Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na
kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri
Mwakyembe.

Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe
ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.
“Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa
habari, ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri
Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti
hilo,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi
mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake
kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi
wa habari na weledi.

Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya
hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za
kinidhamu zitafuata.

“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini
atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae
pembeni kwanza,” alisisitiza Msama.

Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni 27, kwa
ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari
mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo iliyochapishwa na
Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga
kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.bbnzjsisjsnbbn
KIJANA EPUKA MADAWA YAKULEVYA MICHEZO NI AFYA.

6/23/2016 08:36:00 am


Wapenzi na washabiki wa mpira wakifuatilia kwa waribu mchezo unaoendelea katika uwanja wa shule ya msingi Ngarenaro Jijini Arusha dhidi ya Timu ya Esso Star vs Timu ya Town Center.


Baadhi ya wadau mbalimbali wa soka wakifuatilia mchezo unaoendelea iatika kiwanja cha shule ya msingi Ngarenaro ,hii ikiwa ni siku ya ugunguzi rasmi.

Matata Bakari mchezaji aliyeipatia timu ya Timu ya Town Center bao la kwanza ndani ya dk ya 38 dhidi ya Esso Star.


Oscar Raphael mchezaji na aliyeipatia timu ya Town Center bao la pili dk 80 ambapo timu ya Town centre iliifunga Timu ya Esso Star mabao 2 kwa bila.
Timu zote mbili siku ya uzinduzi wa ligi ya vijana iitwayo Sakina Youth Cup katika muonekano wakiwa kiwanjani wakiendelea na mchezo.
Wapenzi na washabiki wa soka wakifuatilia mchezo.siku ya uzinduzi wa ligi ya vijana iitwayo Neema Youth Club uliokuwa ukiendelea katika kiwanja cha shule ya msingi Ngarenaro hivi karibuni.


Ikiwa zimebakia siku chache kuingia kwenye maadhimisho ya siku ya kupiga vita nakupambana na madawa yakulevya ,Jijini Arusha wamefanya uzinduzi wa Ligi ya Vijana iitwayo Neema Youth Club ikiwa nakauli mbiu "Kijana Epukana na Madawa ya kulevya."

 Muandaaji wa mashindano hapo ambapo pia ni mlezi wa timu hizo bi Neema Mollel amesema kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kuwaondosha vijana mitaani,kuepukana na madawa ya kulevya pamoja na mambo ambayo yapo kinyume na maadili katika jamii kwa ujumla.

Aidha bi Neema.amesema kuwa mashindano hayo ni ya awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza walianza na timu 10,lakini sasa vijana wamehamasika tayari simeongezeka timu nyingine 6 na kufanya idadi iongezeke nakufikia idadi ya timu 16 hadi sasa.

Amesema kuwa timu zile za awali tayari zimeshapata uzowefu wa kutosha jambo ambalo.linawafanya vijana kuwa bize katika mazowezi,mwitikio wao ni mkubwa, huku ukisingatia michezo ni afya, ni ajira ,pia inamfanya kijana kujiongeza kiakili, kuongeza marafiki bila kusahau michezo huongeza furaha nakuondoa msongo wa mawazo kwa vijana.

Bi Neema Mollel amesema kuwa wameanza na robo fainali baadae nusu fainali hatimaye watakuja kwenye fainali yenyewe ambapo atapatikana mshindi ,ambapo fainali inatazamiwa kuchezwa ndani ya  julai hivyo amewahasa wazazi na jamii.kwa ujumla kujitokeza kwa wingi.kuja kuwaona vijana wao yale wanayoyafanya ili kuwapa nguvu zaidi.

Maadhimisho ya siku ya kupiga vita madawa ya kulevya duniani huadhimishwa kila mwaka duniani kote june 26.


Bi Neema Mollel ambaye ni muandaaji wa mashindano hayo pia ni mlezi wa timu zote16,vilevile ni diwani kata ya Sakina kupitia (CCM)

MWIJAGE:TBS IFIKAPO JULAI MOSI WAWE WAMEMALIZA BIDHAA ZOTE BANDIA .

6/23/2016 08:00:00 am
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage.

Waziri wa Viwanda  Biashara na uwekezaji Charles Mwijage amelitaka shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na shirika la ushindani wa haki kuhakisha ifikapo July moja  wanamaliza bidhaa zote bandia na  zilizo chini ya  viwango na wasipo fanya hivyo ajira zao zitafutwa mara na bidhaa hizo kuteketezwa.

Tamko hilo amelitoa waziri Charles Mwijage lwakati alipokuwa anatembelea kujionea bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kusibitishwa ubora wake katika siku ya viwango afrika ambapo kwa upande wa kampuni ya cement ya Dangote ,Afisa mkuu masoko Joel Laizer amemhakishi a waziri ubora wa cement zinazozalishwa na kampuni hiyo.

Wakati huo huo kampuni ya Azania pamoja na Azam kwa kupitia kwa maofisa wao akiwemo Maofisa masoko  afisa mkuu wa masoko wa AZANIA  Naifa Abubakari pamoja Ibrahimu Masome wa AZAM  wamemuhakikishia waziri wa viwanda biashara na uwekezaji kuwa wao wamejipanga vizuri kuhakisha wanatoa bidhaa zinazokidhi viwango  bora na zenye ushindani na masoko kote duniani

Aidha kwa upande wao kampuni ya kuzalisha Bodi za magari ya kitalii pamoja na vyuma vya kujengea Maghala ya viwanda afisa biashara Mohan Krishan amemwambia waziri kuwa wao kama kampuni ya HANSPAUL  wataakikisha wanatengeneza bidhaa bora zenye bei nafuu.


Msanii Young Dee amewaomba Watanzania msamaha kwa kuonesha vitendo vya utovu wa Nidhamu

6/22/2016 04:12:00 pm


Rapa kiwango Bongo, Young Dar es salaam Young Dee, amewaomba Watanzania msamaha kwa kuonesha vitendo vya utovu wa Nidhamu vilivyompelekea kuingia katika matumizi ya Madawa ya Kulevya hivi karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mapema leo jijini Dar es Salaam, msanii huyo amedai kuwa hataki kumlaumu yeyote katika mazingira ya vitendo vibaya alivyokuwa ameloeya kwa muda, bali ameamua kubadilika hivyo kuwataka wapenzi na mashabiki zake kumuunga mkono. “Sitaki kumlaumu yeyote katika hili, najilaumu mimi kujihusisha na makundi na marafiki wabaya, nlianza kutumia Pombe, sigara mpaka Madawa, hivyo nawaomba radhi Watanzania, jamii na wote niliowakwaza kwa tabia zangu, nimebadilika na kitakacho fuatia kwa sasa ni kazi nzuri kutoka kwangu” Alisema.

Katika hatua nyingine Young Dee aliweka wazi kwamba ametumia Madawa ya kulevya kwa kipindi cha mwaka mmoja na Miezi minne

Vifungu vya sheria vyawakwamisha CHADEMA Mwanza

6/22/2016 05:44:00 am

Kesi ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuiomba mahakama
kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali.

Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni
Jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali
ya usalama nchini si salama.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo,
aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
(AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya
vyama vya siasa.

Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya
oparesheni iliopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la
kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata
katiba ya nchi.

Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua
kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, akiiomba
kutengua zuio hilo la polisi.

Mohammed Gwae, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, leo
amepitia ombi lililopelekwa mahakamani hapo na upande wa mlalamikaji
anayewakilishwa na mawakili John Mallya na Gasper Mwanalelya na kutoa
uamzi.

Jaji Gwae akitoa uamuzi wa ombi la walalamikaji amedai kuwa, amefikia hatua
hiyo baada ya walalamikaji kukosea kifungu cha kupeleka shauri hilo kortini
kitendo kilichosababisha kulitupilia mbali.

Amesema kuwa, walalamikaji baada ya kupeleka ombi hilo kortini, upande wa
wajibu maombi unaoongozwa na mawakili, Seth Mkemwa na Robert Kidando
waliweka pingamizi wakiomba mahakama kutokusikiliza ombi hilo.

Jaji Gwae amesema kuwa, walalamikaji katika ombi lao walikosea kutumia
kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu cha sheria ya mwaka 2014 badala ya
kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili ambacho kilitakiwa kutumiwa.

“Waleta maombi wametumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu badala ya
kutumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili kilichotakiwa kuwepo katika
kuleta ombi na kama kifungu hiki hakijatumika hapo na ombi halipaswi
kupokelewa,” amesema Jaji Gwae.

Hata hivyo Jaji Gwae amesema, licha ya kuwekewa pingamizi na wajibu
maombi, walalamikaji wamesema kanuni na kifungu hicho ndivyo vilitakiwa
kuwepo na hivyo vinavyopaswa kuwekwa sio sahihi.

Amesema kuwa, katika shauri la namna hiyo, kanuni na vifungu vilivyotakiwa
kuwepo ni kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili na kanuni ya tano na kifungu
kidogo cha sheria ya mwaka 2014 na kwamba wao waliviweka katika maelezo
(Statements) badala ya (chember samers).

Mallya, mwanasheria wa mpeleka maombi amesema kuwa, baada ya kukosea
kanuni na vifungu hivyo, watapeleka kwa mara nyingine ombi na kulifanyia
marekebisho kama Jaji Mohamed Gwae alivyoelekeza.

*Habari kwa hisani ya mtandao wa Jamii Forums*

y
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel