Top Menu

Ujumbe wa Mugabe kwa Maseneta wa Marekani

7/31/2016 08:35:00 am
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewaambia maseneta wa Marekani
waliozuru taifa hilo kwamba watajutia kutofanya urafiki naye iwapo Donald
Trump atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa mwezi Novemba.

Maseneta hao Chris Coons na Adam Schiff waliambia gazeti la Politico nchini
Marekani kwamba walikuwa katika taifa hilo kuzungumzia kuhusu usafirishaji
wa wanyama mwitu na kwamba waliomba kukutana na rais huyo na
wakashangaa kwamba alikubali kuonana nao.

Maseneta hao wamesema kuwa Mugabe aliwataka kuelezea kwa nini Marekani
inaliwekea vikwazo taifa hilo ambapo walitoa sababu kadhaa.
Ni wakati huo ambapo bwana Mugabe aliwaambia: ''Wakati Trump
atakapokuwa rais mutatamani mungefanya urafiki nami''.
BBC

Mahafali ya KKKT Chuo Kikuu Muhimbili Yapigwa Marufuku Baada ya Wanafunzi Hao Kumwalika Lowassa Kuwa Mgeni Rasmi

7/31/2016 08:29:00 am
Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
umezuia mahafali ya wanafunzi waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT ) yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jana mchana chuoni hapo
jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikuwa
amealikwa na wanafunzi kama mgeni rasmi.

Mahafali hayo yalizuiwa jana saa 6 mchana ikiwa ni saa mbili kabla ya muda
kuanza
Tangazo lililobandikwa chuoni hapo na kushuhudiwa na wanahabari likiwa
linamnukuu Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Apollinary
Kamuhabwa liliwataka wanafunzi hao kutoweka mikusanyiko ya aina yoyote
chuoni hapo.

Profesa Kamuhabwa kupitia tangazo hilo aliwaonya wanafunzi hao kutojihusisha
na masuala ya siasa wawapo chuoni kama ilivyo kwa watumishi wa umma.
Jitihada za waandishi wa habari kuzungumza na uongozi wa chuo hicho ili
kupata ufafanuzi ziligonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa hawakualika
mkutano na waandishi wa habari.Mkurugenzi Bagamoyo afutwa kazi

7/31/2016 08:15:00 am
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Azimina Mbilinyi
ametumbuliwa na Rais John Magufuli baada ya kufanya kazi kwa siku 24 tangu
ateuliwe.

Azimina ambaye aliteuliwa Julai 7 mwaka huu uteuzi wake umetenguliwa na Dk
Magufuli kwa kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.
Kutenguliwa huko kulifanyika jana kwa mujibu wa barua iliyotolewa na Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Rais(Tamisemi), Musa Iyombe.

MAONYESHO YA 23 YA WAKULIMA NA WAFUGAJI 2016

7/31/2016 01:46:00 am
Baadhi ya Mabanda yakiwa yamekamilika tayari kwaajili ya maonyesho ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi siku ya jumatatu,katika viwanja vya nanenane njiro Mkoani Arusha.

Zana za kilimo Zikiwa tayari kabisa kwaajili ya maonyesho katika viwanja vya nanenane Njiro Jijini Arusha.
Mashine pamoja na trekta kwaajili yakilimo tayari vimeshawasilishwa viwanjani hapo tayari  kwa maomyesho yanayotarajiwa.kuanza tar 1/8/2016, katika viwanja vya nanenane njiro Jijini Arusha.

Maandaizi ya maonyesho 23 ya wakulima  wafugaji,na sikukuu za nanenane zimepamba moto huku kauli mbiu ya maonyesho hayo ikiwa ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ni nguzo ya maendeleo,Vijana shiriki kikamilifu hapa kazi tu.


Hayo yamesemwa na Katibu wa Taso Kanda ya Kaskazini ndugu Jeremia Solomon Sembosi ambapo wanatazamia maonyeshobya mwaka huu kuwa na washiriki wengi zaidi,huku Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda ndiye anayetazamiwa kufungua maonyesho hayo. 

Aidha manyesho hayo ya wakulima na wafugaji pamoja na sherehe za nanenane yanatarajiwa kuanza hapo kesho Siku ya jumatatu  2016 katika viwanja vya Taso nanenane Njiro Jijini Arusha .Wizara zote zatakiwa kuhamia Dodoma

7/29/2016 10:33:00 pm
Agizo la Rais Dk John Magufuli la kuzitaka wizara zote kuhamia Dodoma
limeanza kutekelezwa ambapo ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za
mitaa (TAMISEMI) imeandaa mipango maalum wa kuboresha mji wa Dodoma
ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu ya uhakika ya barabara nishati ya
umeme na maji ili kuweza kumudu ongezeko la watu wanaotarajiwa kuhamia
mkoani humo.

Akizungumzia mipango hiyo naibu waziri ofisi ya rais TAMISEMI Mhe Suleiman
Jafo amesema miongoni mwa mambo yatakayoanza kutekelezwa kwa haraka ni
pamoja na kuboresha miundombinu na kutenga maeneo tofauti ya ujenzi wa
ofisi za serikali ili kuepuka msongamano huku akiziagiza halmashauri zilizoko
pembezoni mwa mji wa Dodoma kutumia fursa ya makao makuu kujenga miji
ya kisasa ambayo itakuwa chanzo cha mapato ya uhakika kwa halmashauri
husika.

Katika hatua nyingine naibu waziri Jafo ametembelea wilaya ya Chemba ili
kuzungumza na watumishi na kujionea utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ambapo amebaini ubadhilifu mkubwa katika utekelezaji wa miradi mitano ya
maji uliofanywa na maofisa kutoka wilaya mama ya Kondoa na kuagiza
wahusika wake ambao tayari aliwasimamisha kazi kukamatwa mara moja na
kufikishwa mahakamani.

Awali akitoa taarifa ya ugonjwa wa ajabu uliosababisha vifo vya watu 13
ambao chanzo chake ilikuwa ni wilaya ya Chemba mkuu wa wilaya hiyo Husen
Mashimba amesema uchunguzi uliofanywa na mkemia mkuu wa serikali
umebaini kuwa ni ugonjwa wa sumukuvu ambao chanzo chake ni fangasi
anayeshabulia mazao yaliyohifadhiwa vibaya baada ya kuvunwa na mpaka hivi
sasa wapo wagonjwa watatu wakiendelea kutibiwa.
yMagufuli aonya

7/29/2016 06:30:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 29 Julai, 2016 ameanza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida,
Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo amezungumza
na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua
kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Akiwa Mkoani Singida, Rais Magufuli aliyeongozana na mkewe Mama Janeth
Magufuli amewasihi watanzania kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na
vitendo vya vurugu vinavyohamasishwa na baadhi ya wanasiasa huku akionya
kuwa serikali yake haitamvumilia mtu yeyote ambaye atathubutu kuchochea
vurugu ikiwemo maandamano kinyume cha sheria.

"Sitaki nchi hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia
kikamilifu bila huruma, na wasije wakanijaribu, mimi ni tofauti sana na kama
wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi sijaribiwi na wala
sitajaribiwa.

"Wananchi hawa wana shida, na siasa nzuri ni wananchi washibe, siasa nzuri ni
wananchi wetu wapate dawa" Amesema Rais Magufuli.
Kuhusu hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali yake ya awamu ya tano
tangu aingie madarakani Rais Magufuli ametaja baadhi ya hatua hizo kuwa ni
kufuta ada kwa shule za msingi na sekondari, kutoa mikopo kwa wanafunzi wa
vyuo vikuu zaidi ya laki moja na kuongeza fedha za miradi ya maendeleo katika
bajeti ya serikali kutoka asilimia 26 ya mwaka 2015/2016 hadi kufikia asilimia
40 katika bajeti ya mwaka huu 2016/2017.

Hatua nyingine ni kuondoa wafanyakazi hewa 12,500 katika orodha ya
waliokuwa wanalipwa mshahara na serikali, kudhibiti upotevu wa mapato
serikalini, kutenga shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Reli ya
kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard gauge na pia akazungumzia hatua
zilizochukuliwa dhidi ya wala rushwa na wanaojihusisha na ufisadi kwa kuunda
mahakama ya mafisadi huku akiapa kuwa katika kipindi chake hakuna fisadi
atakayeendelea kutamba.

Akiwa njiani Rais Magufuli amewasalimu wananchi wa Ikungi na baadaye
amefanya mkutano wa hadhara Singida Mjini ambako amesisitiza kuwa serikali
yake haiko tayari kumvumilia mtu yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ahadi
na Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Deni la biskuti lasababisha mauaji

7/29/2016 06:26:00 pm
Mtu mmoja na mkewe kutoka jamii ya Daliti inayobaguliwa tangu jadi nchini
India wameuawa, mmoja akiwa amekatwa kichwa na mwingine kunyongwa kwa
kushindwa kulipa deni la Rupee kumi na tano ambalo ni karibu senti ishirini na
mbili tu, BBC imeripoti.

Polisi kaskazini mwa taifa hilo wamethibitisha kisa hicho ambapo yasemekana
mfanyi biashara anayetokea jamii ya hadhi ya juu,aliwaua wanandoa hao kwa
kushindwa kulipa deni la biskuti walizokuwa wamewachukulia watoto wao.
Mfanyabiashara huyo amekamatwa.

Ubaguzi kwa misingi ya kijamii umeenea sana nchini India, huku watu wa jamii
ya Daliti waliokuwa wamebadikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa kwenye
daraja la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo 'caste'
ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki katika lindi
la umaskini .

Hata hivyo Visa vya ukatili wa kibaguzi dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la
Gujarat vimeongezeka mnamo siku za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la
maandamano kutoka watu wa jamii hiyo.

BBCWalimu 4 wamvua nguo na kumchangia viboko binti wa Kidato cha IV Mbeya huku Mwalimu Mwingine Akimtomasa Sehemu za Siri

7/29/2016 09:15:00 am

VITENDO vya ukatili wa kijinsia na dhuluma dhidi ya watoto wa kike vimekuwa
vikishamiri kila siku pamoja na kuwepo kwa taasisi za kutetea haki za
wanawake na kuanzishwa kwa madawati ya Kijinsia kwenye vituo vya polisi
nchini.

Msichana wa kidato cha Nne mwenye umri wa miaka 17,(jina tunalo)
anayesoma shule moja ya sekondari ya Kata mkoani Mbeya amekumbwa na
kadhia ya kuvuliwa nguo zake za ndani na kucharazwa bakora zisizo na idadi
na walimu wanne wa shule hiyo.

Tukio hilo ambalo limeripotiwa katika kituo kidogo cha Polisi Mbalizi wilaya ya
Mbeya kwenye jalada la uchunguzi namba MBI/IR/967/2016 na kuwekwa
kwenye taarifa yenye namba MBI/RB/2653/2016 linadaiwa kuwahusisha walimu
wanne akiwemo Mkuu wa shule hiyo pamoja na walimu watatu.

Akizungumza huku akiwa na maumivu makali katika Hospitali Teule ya Ifisi
ambako amelazwa akipatiwa matibabu, mwanafunzi huyo alisema kuwa aliitwa
na mwalimu wa nidhamu aliyemtaja kwa jina la Neema Mwaikenda aliyekuwa
pamoja na Mkuu wa shule hiyo aliyemtaja kwa jina la Mariamu Mwanisenga na
mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina la Adili.

Alisema walimu hao walianza kumuadhibu kwa viboko visivyo na idadi huku
akiwa amechojolewa nguo zake ambapo mwalimu wa kiume aliyemtaja kwa jina
la Adili akaanza kumshikashika sehemu zake za siri.

‘’Wakati naadhibiwa na walimu wote, huyu mwalimu wa kiume alianza
kunishika huku chini,na kunitaka niwataje wanaume zangu,nikawa nabana
miguu wakazidi kunishambulia kwa vibao na mateke na fimbo,’’ alisema
mwanafunzi huyo.

Alisema sababu zilizosababisha aadhibiwe ilikuwa ni utoro na kuwa siku moja
alipokuwa shuleni alioneshwa na walimu fimbo na kuelezwa kuwa fimbo hizo
zitamuishia mwilini ndipo akaogopa kufika shuleni kwa siku tatu.
Anafafanua kuwa siku aliyofika shuleni ndipo alipokutana na kadhia ya kupigwa
na walimu wanne hadi alipowaponyoka walimu hao na kukimbilia mitaani na
kujificha.

‘’Niliwaponyoka walimu nikakimbilia kwenye nyumba ya jirani na shule
nikajificha hadi jioni na baadaye kwenda nyumbani, kesho yake mama na dada
walinichukua na kunileta hospitali,’’ alisema.

Mwandishi wa habari hizi alifika shuleni anakosoma mwanafunzi huyo kwa nia
ya kukutana na uongozi wa shuleni hiyo ambapo Makamu Mkuu wa shule hiyo
aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwansanga alikataa kuelezea chochote.
‘’Mie sijui lolote kwanza mie sio msemaji wa shule, kwahiyo sijui lolote juu ya
taarifa mnazohitaji,’’ alijibu Makamu Mkuu wa shule na kuondoka zake.

Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Mkoa Charles Mwakalila alisema kuwa
adhabu aliyopewa mwanafunzi huyo ni kubwa kupitiliza kwa kuwa zipo taratibu
za adhabu kulingana na makosa na kuwa mwanafunzi anapaswa kupigwa
viboko vitatu na viboko visivyozidi sita au adhabu mbadala.
‘’Adhabu aliyopewa ni kubwa, tutafuatilia na waliokiuka taratibu watachukuliwa
hatua za kinidhamu,’ ’alisema Mwakalila.

Naye Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari alipoulizwa
juu ya tukio hili alidai kuwa halijafika ofisini kwake na kuwa kwa sasa yeye
yupo kikazi wilayani Chunya na mara atakapofika ofisini atafuatilia na kuchukua
hatua za kisheria kwa wahusika wa tukio hilo.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Mariamu Mtunguja ambaye alifika
Hospitalini alikolazwa mwanafunzi huyo alisema kuwa amemuangalia
mwanafunzi huyo na kuona namna ambavyo damu imevilia kwenye sehemu
zake za makalio na kwenye mapaja.

Mtunguja alisema kuwa kitendo kilichofanywa na walimu hao ni cha kinyama
ambacho hakipaswi kuvumiliwa na kuwa mara itakapobainika atahakikisha
walimu hao wanachukuliwa hatua za kinidhamu.

Muuguzi Mkuu Msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimati Sanga alisema kuwa
mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo Julai 21 saa 7:00 mchana ambapo
alipatiwa matibabu na kulazwa kutokana na majeraha na damu iliyovilia mwilini
sehemu za makalio na mapaja.

‘’Ameshambuliwa sehemu za mapaja, damu na masikio yake hasikii vyema
kutokana na kipigo, anaendelea na matitabu hapa hospitali,’’ alisema Sanga.

Muuguzi Mkuu msaidizi wa Hospitali Teule ya Ifisi Elimati Sanga akielezea
madhara aliyopata mwanafunzi anayedaiwa kupigwa na walimu wanne wa
shule ya Sekondari Malama."habari hii  Mkwinda Blog."


Aliyepiga picha mauaji ya Mwangosi afariki

7/29/2016 08:28:00 am
Tasnia ya habari imepata pigo baada ya mpiga picha wa gazeti la Tanzania
Daima aliyepiga picha za tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi, JOSEPH
SENGA,amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nchini India.

Senga amefariki siku ambayo muuaji wa Daudi Mwangosi amehukumiwa
kifungo cha miaka 15.

Ni yeye aliyepiga picha iliyochapishwa sana kwenye magazeti na mitandao ya
kijamii ikionyesha jinsi Mwangosi alivyouawa.

Licha ya kukabiliwa na mazingira magumu siku hiyo, Senga,anabaki kuwa
shujaa kwa kuhatarisha maisha yake.

Alisimama bila woga,akapiga picha akiwa katikati ya msitu wa askari polisi
wenye silaha,huku anga ikiwa imegubikwa na moshi wa mabomu ya machozi,
milio ya risasi ikisikika,na kuzitunza, zikasaidia kufichua mauaji ya Mwangosi.
Pengine bila yeye leo hii yawezekana kusingekuwa na kesi na mwisho hukumu
dhidi ya aliyemuua Mwangosi ingekuwa ndoto.

Senga amefariki nchini India alikopelekwa kwa ajili ya kupata matibabu ya
ugonjwa wa Moyo.
Mungu ailaze roho yake mahali pema, AMEN.

JPM ametengua uteuzi wa Dk Wanyancha Bodi ya Barabara

7/29/2016 08:23:00 am
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund
Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo Mjini Dodoma imeeleza kuwa
Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo tarehe 28 Julai, 2016.
Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo
Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.

Uteuzi wa Bw. Joseph Odo Haule umeanza leo tarehe 28 Julai, 2016.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Joseph Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa
Barabara (Road Fund).
Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi
zao.Mahakama ya wilaya ya Mpanda yamuachia huru Laurence Masha

7/28/2016 07:49:00 am
Mahakama ya Wilaya, Mpanda imemuachia huru Lawrence Kego Masha
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana Mwanza
pamoja na washtakiwa wengi ambao ni Viongozi wa Chadema Jimbo la
Nsimbo, Katavi katika makosa mawili ya Kula Njama Ili Kutenda Kosa na
Kuhutubia Wakimbizi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kosa lingine la
kuingia makazi ya Wakimbizi bila Kibali.

Mahakama imesema kwamba upande wa mwendesha mashtaka umeshindwa
kutoa ushahidi wowote unaonyesha kwamba washtakiwa hao walikutana na
kupanga njama kutenda kosa.
Pia hakuna ushahidi wowote kuonyesha kwamba washtakiwa walikamatwa
wakihutubia wakimbizi.

Ila Mahakama iliona kwamba washtakiwa hao wana kosa la kujibu kwa shtaka
la kuingia kwenye kambi/makazi ya wakimbizi bila kibali.
Mara baada ya uamuzi huo washtakiwa walitakiwa kutoa utetezi wao ambapo
washtakiwa Lawrence Masha na Stansalaus Kaswele walitoa utetezi
wakiongozwa na Wakili Albert Msando.

Leo Mahakama imetoa hukumu na kusema kwamba washtakiwa wote saba
hawana hatia kwa kukubaliana na hoja zote za Wakili wa Utetezi.Koffi afungwa jela

7/26/2016 11:35:00 pm
Mwanamuziki mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Koffi
Olomide amehukumiwa kifungo cha miezi 18 na Mahakama moja Kinshasa,
DRC.

Koffi alikamatwa mapema leo nyumbani kwake Kinshasa na kufikishwa
Mahakamani akituhumiwa kufanya shambulizi la mwili kwa mmoja wa
wanenguaji wake.

Ijumaa iliyopita akiwa kwenye uwanja wa ndage wa Jomo Kenyatta nchini
Kenya, Koffi alidaiwa kufanya shambulizi hilo.

Kipande cha video kilichosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku hiyo
kilimuonyesha Koffi akimpiga teke mnenguaji wake aliyekuwa anaonekana
kubishana na mnenguaji mwingine wa bendi hiyo ambaye anadaiwa kuwa na
uhusiano wa Kimapnzi na Koffi tangu mwaka 2012.

Tukio hilo lilimfanya Koffi atimuliwe nchini Kenya hivyo kushindwa kufanya
tamasha lililokuwa limepangwa kufanyika Jumamosi iliyopita.

Aidha nyumbani kwao DRC, watetezi wa haki za binadamu walianzisha kampeni
kuishinikiza Serikali imkamate Koffi kisha afikishwe Mahakamani kuadhibiwa
kutokana na tukio hilo la aibu alilofanya.

Ndipo leo alipokamatwa nyumbani kwake, akafikishwa Mahakamani, akakiri
kutenda kosa hilo na kuhukumiwa jela miezi 18 adhabu ambayo atalazimika
kutumikia mwaka mmoja jela.


Dkt Magufuli akutana na Makamu wa Rais wa AfDB

7/26/2016 06:44:00 pm

NASHUKURU MUNGU KWA KUUTUA MZIGO SALAMA HUKU NIKIIACHA NCHI IKIWA SALAMA TULII KABISA - DKT. JAKAYA KIKWETE

7/26/2016 07:25:00 am

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya
Kikwete akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha
Mapiduzi katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo
mstaafu wa CCM , iliyofanyika wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani .
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na Mke
wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ,mama Salma Kikwete, katika
hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo mstaafu wa
CCM ,iliyofanyika wilayani Bagamoyo ,wengine ni wabunge wa mkoa
huo wakimsalimia Mwenyekiti huyo mstaafu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM ).
wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi wakimsikiliza
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya
Kikwete katika hafla ya kumkaribisha nyumbani mwenyekiti huyo
mstaafu wa CCM ,iliyofanyika wilaya ya Bagamoyo .
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya
Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbili wa
mkoa wa Pwani . PWANI.
MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt .Jakaya
Kikwete amesema anashukuru Mungu Kwa kuutua mzigo salama
huku akiicha nchi ikiwa salama tulii kabisa.

Amesema kuwa safari yake ya urais ilianzia Bagamoyo akitokea
wilayani hapo ambapo baada ya hapo alikwenda Kibaha kutangaza
nia ya kugombea urasi nakudai kuwa amejisikia flaha kurudi tena
Bagamoyo akiwa salama .

Amesema wakati akielekea kutanga nia ya kugombea urais alikuwa
na mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambapo yeye alikuwa anaandika
na Ridhiwani anachapa kwenye Komputa .

Dkt.Kikwete ameyasema hayo leo wilayani Bagamoyo katika hafla ya
kumkaribisha Nyumbani baada ya kuitumikia nchi Kwa miaka mingi ,
ambapo iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani .

Alisema . anashukuru Kwa Mara nyingine kurudi mahala alipoazia na
kwamba amemaliza salama na ameacha nchi ikiwa salama na
imetulia tulii kama Maji kwenye mtungi. Akikumbuka mchakato wa
mwakajana wa kumpata Mgombea ulikuwa na mambo mengi lakini
mambo yalikwenda salama na hakuna lililokuwa limeharibika .

" Ilikuwa Kazi kubwa si ndogo lakini hatimaye wa kavuka na
wakaingia kwenye uchaguzi ambao ulikuwa na vurumayi " amesema
Dkt. Kikwete .Aidha amesema kuwa hata hivyo katika uchaguzi huo
kulikuwa hakuna mtu ambaye alipatwa na tukio la kumpiga mwezake
hali ambayo iliwashangaza hata nchi jirani .

Alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanya kazi kubwa
ya kusukuma maendeleo ya wananchi Kwa mikoa yote,wilaya zote
bila ubaguzi wowote ule huku akikiri kukabiliana na Changamoto ya
kunyoshewa vidole hususani pale alipojalibu kupeleka maendeleo
Wilayani Bagamoyo konakamba wananchi wa Bagamoyo walikuwa
hawana haki .

Aidha Dkt. Kikwete alisema kuna wakati alisimamisha fedha za ujenzi
wa barabara hiyo na kupeleka fedha hizo kujenga barabara ya Geita ,
Sengerema ,usagala ,na kulizuka na Maneno mengi dhidi yake na hadi
kufikia wabunge kulumbana.

Amesema hata hivyo anashukuru kwamba amemaliza salama na Kwa
Bahati nzuri amepatikana rais ambaye ana ari kubwa ya kuwaletea
maendelea watu huku akitaka watanzania kumuunga mkono .

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani leo
wamejitokeza Kwa wingi kumkaribisha nyumbani Mwenyekiti
Mstaafu wa Chama hicho Dkt .Jakaya Kikwete katika sherehe
zilizofanyika wilayani Bagamoyo . Wanachama hao ambao walitoka
katika wilaya zote za Mkoa wa Pwani wakiongozwa na Mwenyekiti
wa Chama hicho mkoa Masikuzi. pamoja na Katibu Joyce Masunga
walimuaga na kumkaribisha Kwa nyimbo mbalimbali.
Aliyemuua Mwangosi apatikana na hatia.

7/26/2016 07:13:00 am
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imemtia hatiani kwa kosa la kuua bila
kukusudia askari wa kikosi cha kuzuia ghasia, Picificus Simon anayetuhumiwa
kumuua mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi huko
Nyororo wilayani Mufindi.

Akisoma mwenendo wa kesi, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Dk Paul
Kihwelo amesema kuwa mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa kufuatia
ushahidi alioutoa kwa mlinzi wa amani.
Jaji Kihwelo amesema mbele ya mlinzi wa amani mtuhumiwa alikiri kosa hilo
akisema alitenda bila kudhamiria.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Adolf Maganga ameitaka mahakama hiyo
kumpa adhabu ya kifungo cha maisha wakati Wakili wa Utetezi, Rwezaula
Kaijage aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu ikiwa ni pamoja na
kumuachia huru kutokana na majukumu aliyonayo.
Hukumu ya kesi hiyo itatolewa Julai 27.

Waziri Mkuu Majaliwa adai atahamia Dodoma mwezi wa tisa

7/25/2016 09:33:00 pm
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametii lile agizo la viongozi wote kuhamia
mjini Dodoma huku akisema yeye atakuwa wa kwanza kuhamia huko.

Ameyasema hayo Jumatatu hii katika maadhimisho ya kuwakumbukua
mashujaa waliolipigania taifa yaliyofanyika mjini humo. Amewaambia wakazi
wa Dodoma kuwa mnamo mwezi wa tisa atakuwa tayari ameshahamia
huko.

“Nimemuita waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu na katibu mkuu,
nimewaambia wakamilishe nyumba yangu nahamia mwezi wa tisa haraka
sana pale juu mara moja,” alisema.
“Kwahiyo mimi nikitangulia mwezi wa tisa mawaziri wote wanifuate. Moja
tuhakikishe Dodoma ni kisiwa cha amani na pili watu wanakuja na
tunaamini mamaziri, mabalozi wanaotoka nje watakuja Dodoma, tunahitaji
huduma mbalimbali Dodoma, jipangeni sasa kuwekeza serikali hii ilivyosema
tunatoa fursa hizi ndio fursa.

 Ongezeni hoteli za kitalii, ongezeni nyumba za
kulala wageni, jengeni mahoteli makubwa, andaeni mazingira ya nyie kupata
tija kufuatia ujio wa mawaziri mbalimbali na wageni kutoka nchi mbalimbali,
huo ndo wito wangu,” alisisitiza.

Pia aliwashukuru wote walioudhuria maadhimisho hayo na kumshukuru Rais
John Pombe Magufuli kwa kumpa nafasi ya kuongea na wananchi wa
Dodoma na Watanzania kwa ujumla.

MASKINI Babu Seya Hali yake Kiafya Yawa Mbaya..Apelekwa Muhimbili..

7/25/2016 04:35:00 pm
Mwanamuziki nguli nchini anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza
Viking 'Babu Seya anadaiwa yu taaban ambapo amekimbizwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Mwandishi wetu alimshuhudia Babu Seya akiwa Muhimbili chini ya ulinzi wa
askari magereza watatu na wafungwa wengine watano katika Jengo la
Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) huku akiwa amedhoofu.

Haikuweza kujulikana mara moja ugonjwa uliosababisha Babu Seya
ahamishiwe Muhimbili kwa matibabu kwa sababu Jeshi la Magereza lina
hospitali yake na mwandishi alipoomba kwa mmoja wa askari magereza ili
aweze kumsalimia mwanamuziki huyo, hakupewa ruhusa.

Baadhi ya wananchi waliomshuhudia mwanamuziki huyo akiwa Muhimbili na
kuingizwa katika chumba cha daktari namba 112 walisema, anavyoonekana
ni dhahiri ni mgonjwa kwa sababu hakuwa mchangamfu kama ilivyo
kawaida yake.

“Nguza (Babu Seya) mara nyingi huwa mchangamfu lakini leo amekuwa
mnyonge, mwili umepungua na hata ngozi yake siyo ang’avu, bila shaka
anaumwa sana,” alisema mwananchi mmoja hospitalini hapo.

Hata hivyo, mara baada ya matibabu, Babu Seya aliingizwa katika gari la
magereza na kurudishwa Gereza la Ukonga kuendelea kutumikia kifungo
chake.

Dodosadodosa ya mwandishi hospitalini hapo ili kujua kinachomsumbua
Babu Seya, haikuambulia chochote kwani daktari mmoja alisema ni mwiko
kwao kutaja ugonjwa wa mgonjwa bila ridhaa yake na ni kinyume cha
maadili ya kidaktari.

“Umeniuliza anaumwa nini, kwanza mimi siye niliyemtibu lakini hata kama
ningejua ugonjwa wa Babu Seya, siwezi kukuambia ni unethical (kinyume
cha maadili). Lakini kweli ni mgonjwa na ndiyo maana ameletwa hapa
kutibiwa,” alisema daktari huyo aliyekuwa nje ya jengo moja akizungumza
na mwanamuziki huyo.

Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
Dar, Eddy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye Papii Kocha kwa
kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto wa Shule ya Msingi
Sinza-Mapambano, Dar na kuwafunga kifungo cha maisha jela huku rufaa
ya kesi yao ikiwekwa kiporo kwenye Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu iliyopo jijini Arusha.Diwani Akwepa Risasi sita akipambana na majambazi Moshi

7/25/2016 11:27:00 am
Diwani wa Kata ya Kiborlon (Chadema) katika Manispaa ya Moshi, Frank
Kagoma ameonyesha ujasiri wa hali ya juu alipopambana na majambazi
waliokuwa na silaha za moto.

Alinusurika kuuawa baada ya majambazi hao waliokuwa na bunduki na bastola
kumfyatulia risasi sita alipokuwa akiwafukuza ambazo hata hivyo,
hazikumpata.

Tukio hilo ambalo lilionekana kama sinema, lilitokea mwishoni mwa wiki baada
ya majambazi hao kuvamia duka la jumla la kuuza mitumba linalomilikiwa na
Menti Mbowe na kupora Sh10 milioni.

Katika tukio hilo lililotokea saa tano asubuhi eneo la Kiborlon, majambazi hao
walimjeruhi kichwani mfanyabiashara huyo anayemiliki pia mabasi ya Machame
Safaris.

Hali ya majeruhi huyo inaendelea vizuri. Akisimulia tukio hilo, diwani huyo
alisema siku hiyo akiwa maeneo ya Kiborlon, alipigiwa simu kuwa
mfanyabiashara huyo amevamiwa na majambazi ndipo alipoendesha gari lake
hadi eneo la tukio.

“Nilipofika pale wale majambazi watatu ndiyo walikuwa wanatoka kwenye duka.
Nikampelekea gari yule aliyekuwa ameshika bunduki. Kuona hivyo akafyatua
risasi hewani,” alisema Kagoma.

“Yule mwenye bunduki akaingia uchochoroni kuelekea Barabara ya Stendi ya
Kidia. Mwenzake aliyekuwa na bastola naye akawasha risasi nyingine hewani
kunitisha,” alisema.

Baada ya hali hiyo, diwani huyo alilazimika kujificha kwenye gari na majambazi
hao walidandia pikipiki na kuanza kukimbia kuelekea Barabara ya Msaranga,
naye akawafuata kuelekea huko.

“Wakati huo tayari vijana wangu wa bodaboda wakawa nao wamesikia hilo
tukio tukaanza kusaidiana kuwafukuza lakini mbele kidogo pale Msaranga wale
majambazi wakasimamisha pikipiki yao umbali wa mita 30 kutoka nilipokuwa
na mmoja wao mwenye bunduki alifyatua risasi mbili na mwenye bastola risasi
mbili kuelekea uelekeo wangu.

“Nililazimika kujificha kwenye kiti, wale majambazi wakajua wameniua.
Wakapanda tena pikipiki ili watoroke. Nikawasha tena gari huku vijana wangu
nao wakinisaidia tukaanza kuwafukuza,” alisema.

Kagoma alisema majambazi hao walipita maeneo ambayo gari haliwezi kupita
wakaelekea eneo la Mabogini Moshi Vijijini hadi lango la TPC na baadaye
wakaelekea Rundugai wilayani Hai.

“Kuna eneo vijana wangu wanasema kulikuwa na vumbi sana, ndipo
walipowapoteza na majambazi wakatoroka kupitia njia ya reli ili kukwepa polisi
waliokuwa wakiwasubiri mbele,” alisema na kuongeza: “Hatukuwa na silaha,
lakini tulijitahidi kupambana nao kwa ujasiri. Tatizo nafikiri tulikosea kidogo.

Ilitakiwa wakati tukifukuzana nao tuwape polisi uelekeo wa majambazi.”
Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa
Jeshi lake litatoa taarifa rasmi kwa wanahabari leo kuhusiana na msako
unaoendeshwa na jeshi hilo.

“Kuna mambo tumeyafanya tangu tukio hilo litokee lakini kesho (leo) saa sita
mchana tutatoa taarifa rasmi pamoja na mafanikio tuliyofikia hadi sasa.
Tunaendelea vizuri na upelelezi,” alisema.

Kamanda Mutafungwa, alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi
hilo ikiwamo kuwafichua wahalifu na mbinu wanazozitua akisema polisi
wamejipanga kukabili wimbi jipya la ujambazi.
vAskofu Gwajima amjibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemuita muongo

7/25/2016 11:18:00 am

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu katibu
mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo
akisema leseni yake ni ya kuendesha magari makubwa na siyo vibajaji na
maguta.
Akihubiri katika kanisa lake jana, Gwajima bila kutaja jina la Makamba, alisema:
“Siwezi kushughulika na vigari vidogovidogo nyie mnanifahamu, mimi nina
leseni ya kuendesha semi trailer …nadhani mmenielewa,” alisema huku waumini
wake wakimshangilia.
Juzi, Makamba aliwaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kuwa
Askofu Gwajima ni kiongozi wa dini lakini ni muongo na kuwa uongo wake
unawaudhi hata waumini wake ambao ni wanachama wa chama hicho.
Alisema Gwajima amekuwa akisema uongo kuwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete
hataki kuachia madaraka ya uenyekiti wa chama hicho, kitu ambacho Rais huyo
mstaafu alikanusha akisema ni yeye alikwenda kumshawishi Dk John Magufuli
kuchukua nafasi hiyo kabla ya muda wa uliopangwa kikatiba.
Katika mahubiri hayo, Gwajima pia alisema mafunzo aliyoyapata tangu akiwa
mdogo ni kuogopa kugombana na watu wa aina tatu, walevi, wazee na
wagonjwa.
“Baba yangu alinifundisha nisigombane na walevi, wazee na wagonjwa kwani
ukimpiga kidogo mtu wa aina hiyo anaweza kufa,” alisema Gwajima.
“Hata nyie waumini wangu nawaomba msigombane na watu wa aina hiyo
kwani mnaweza kupata matatizo,” alisema.
Kiongozi huyo aliongoza mamia ya waumini wake kumuombea Rais Magufuli
kwa kushinda uenyekiti wa CCM akisema kofia hizo mbili zimempa meno ya
kung’ata na zitamwongezea kasi ya kutatua matatizo ya wanyonge nchini.
Rais Magufuli juzi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata
kura zote 2,398 alizopigiwa na wajumbe wa mkutano huo.
Kutokana na ushindi huo, Gwajima alisema Magufuli amepewa meno ya
`kung’ata’ kila upande tofauti na alipokuwa na kofia moja ya urais.
Alisema kwa muda mfupi aliokaa madarakani, elimu ya msingi na sekondari
zimeanza kutolewa bure kitendo ambacho maskini na wanyonge wa nchi hii
wameanza kuuona mwanga.
Alisema ataendelea kumwombea Magufuli kwa sababu kazi anazozifanya
zinawanufaisha wanyonge na maskini ambao kwa muda mrefu walipuuzwa
katika nchi yao.
“Kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti ni zawadi kwetu Watanzania, tuendelee
kumwombea kila siku ili aendelee kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi,”
alisema.
Alisema nafasi hiyo mpya itamwezesha kupambana na rushwa tatizo ambalo
ameonyesha kuwa `atalivalia njuga’ hata ndani ya chama hicho.
Mbali na Rais Magufuli, Gwajima aliwaombea pia Makamu wa Rais, Waziri
Mkuu, mawaziri na Spika wa Bunge kwamba Mungu awalinde ili wamsaidie
Rais kutekeleza majukumu yake.
Kwa mwezi mzima, Askofu Gwajima amekuwa akitafutwa na Polisi baada ya
kusambaa kwa sauti inayosikika kama yake ikitaka Rais mstaafu Kikwete
afikishwe mahakamani kwa makosa yote yaliyofanyika katika utawala wake.
Katika mkanda huo, sauti hiyo inadai baadhi ya viongozi wa CCM wametuma
watu mikoani kupiga kampeni ya kutaka Magufuli asipewe uenyekiti ambao
umekuwa ukishikiliwa na Kikwete.
Baada ya sauti hiyo, Gwajima aliondoka nchini kwenda Japan lakini Polisi
waliendelea kumsaka hadi Julai 12 walipomkamata katika Uwanja wa Mwalimu
Julius Nyerere (JNIA), aliporejea. Alihojiwa na kuachiwa siku hiyohiyo
Rais wa Uturuki ahutubia Bunge

7/24/2016 10:18:00 pm
Rais wa UTURUKI, RECEP TAYYIP ERDOGAN amelihutubia bunge la nchi hiyo
kwa mara ya kwanza baada ya jaribio la kuipindua serikali yake kushindwa na
kulaumu baadhi ya watu wanaosema utawala wake ni wa kidikteta.

Rais ERDOGAN amesema serikali yake kupitia Wizara ya Mambo ya Nje,
itaonesha picha za video na mnato kote duniani zinazoonesha matukio ya
uvamizi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, ili kuonesha ushahidi wa
namna serikali yake isivyo na utawala wa kidikteta.

Zaidi ya watu Elfu hamsini wamewekwa kizuizini na wengine kufukuzwa kazi
baada ya jaribio hilo kushindwa


Magufuli achaguliwa kwa kishindo CCM

7/24/2016 12:13:00 am
Mkutano Mkuu wa chama cha Mapinduzi(CCM) umemchagua kuwa Mwenyekiti
wa chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk John Magufuli kwa kupata kura 2,398 sawa na asilimia 100.

Mkutano huo uliohudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi
wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali, pia ulihudhuriwa na wajumbe takribani
asilimia 99 ya wajumbe wote.

Rais Magufuli amewashukuru wajumbe wote wa mkutano huo kwa kumchagua
kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi.
Ameahidi kukisimamia chama cha Mapinduzi kwa weledi kama ilivyokuwa kwa
watangulizi wake.

Dk Magufuli amesema uzoefu wa zaidi ya miaka 40 aliyoupata ndani ya chama
hicho utaweza kumsaidia kuiongoza CCM kufikia malengo yake.
Dk Magufuli ameahidi kukomesha usaliti ndani ya chama hicho akiweka bayana
kuwa wote wanaokisaliti chama hicho hawana nafasi.

Ameahidi kukomesha rushwa ndani ya chama hicho kwani amesema ilifika
kipindi kupata uongozi ndani ya CCM ni lazima uwe na pesa.
Rais Magufuli ameahidi kusimamia rasilimali za chama hicho kwa weledi ili
chama kiweze kujitegemea.

Dk Magufuli amesisitiza azma ya Serikali yake kuhamia Dodoma ambapo
ametoa ahadi kuwa atahakikisha ndani ya kipindi cha utawala wake, Serikali
yote itahamia Dodoma.

Wakati huo huo Rais Magufuli, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi(CCM)
amesema licha ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdurahman Kinana
kuwasilisha barua ya kujiuzulu wadhifa wake kutokana na mabadiliko ya
uongozi, amemtaka kiongozi huyo kuendelea na wadhifa wake.

Aidha Mwenyekiti huyo wa CCM ameagiza Sekretarieti ya CCM iliyokuwa chini
ya Katibu Mkuu ndugu Kinana, iendelee na kazi yake hadi hapo itakapotolewa
taarifa nyingine.

Mapema kabla ya zoezi la kupiga kura kumchagua Rais Magufuli, Mwenyekiti
mstaafu wa CCM Dkt Jakaya Kikwete alimtaka Mwenyekiti huyo mpya
kushughulikia baadhi ya mapungufu yanayokitia hasara chama ikiwemo kuokoa
mali za chama.

Akitaja baadhi ya mali hizo, Jakaya Kikwete amesema kuna wanachama ambao
wamejimilikisha viwanja vya chama hicho bila utaratibu rasmi na kuwapa
tahadhari ya kuvirejesha katika chama haraka.

Amemtaka mwenyekiti mpya wa chama hicho kushughulikia suala la viwanja
ambavyo bado havijapewa hati ili viendelezwe na kugeuzwa kuwa vitega uchumi
na kuongeza wigo wa mapato ya chama.

Aidha Kikwete aliwakumbusha wakuu wa wilaya kuwa wanapaswa kutambua
mojawapo ya jukumu walilonalo ni kulinda maslahi ya chama katika ngazi ya
wilaya.

“Kuna wakuu wa wilaya wamesema eti wao ni wasomi na kwamba siasa
haiwahusu, lakini wajue kuwa wao ni wajumbe wa kamati za siasa za wilaya,
hivyo wajue kuwa wamewekwa kule kwa makusudi kama kiungo kati ya chama
na serikali”

Aidha, DK Kikwete ameivunia mafanikio aliyoyapata ndani ya uongozi wake wa
kipindi cha miaka 10 ikiwa ni pamoja na ongezeko la wanachama kutoka
wanachama 5,433,425 mwaka 2006 hadi kufikia wanachama 8,782,833 mwaka
huu.

Amesema kiwango hicho cha wanachama ni mtaji mkubwa katika uchaguzi, kwa
kuwa chama kinakuwa kinaingia katika uchaguzi kikiwa na kura zaidi ya milioni 8

Jambo lingine ni kufanikisha kujenga ukumbi mkubwa na wa kisasa wa chama
hicho ulioko Dodoma kwa ajili ya mikutano, na kumtaka mwenyekiti ajaye
aendelea kumalizia ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya chama hicho.

Mafanikio mengine aliyoyataja Kikwete ni kuhakikisha chama hicho kinaendelea
kushinda katika chaguzi mbalimbali ikiwemo zile za serikali za Mitaa ambapo
mwaka 2009 chama hicho kilishinda kwa zaidi ya asilimia 90 na mwaka 2014
kikishinda kwa asilimia 80.

Mbali na mafanikio hayo, Kikwete ametaja baadhi ya changamoto alizokutana
nazo ikiwa ni pamoja vikwazo viwili vikubwa kutoka kwa wananchama.
Vikwazo hivyo ni pamoja na wanachama kutohudhuria vikao na la pili
wanachama kutolipa ada.

Amesema wanachama wengi hawalipi ada zao na wengine wanasubiri hadi
wakati wa kampeni ili walipiwe na wagombea, huku akieleza kuwa endapo
wanachama wangekuwa wanalipa ada zao kwa uaminifu, basi chama hicho
kingeweza kukusanya hadi bilioni 10.5 na kuacha kuendesha chama kwa
kutegemea ruzuku ya serikali.

Amesema wakati mwingine chama kinategemea michango ya wafanyabiashara
ambao nao huchangia chama wakati wa kampeni pekee.
“Wakati wa uchaguzi wafanyabishara wanatuchangia sana, wanasema
wanataka CCM iendelee kubaki madarakani, lakini uchaguzi ukiisha hatuwaoni,
hata simu zetu hawapokei” Amesema Kikwete.

Kikwete pia ametumia fursa hiyo kuelezea sababu kubwa ya chama hicho
kulegalega kuwa ni kutokana na viongozi wa ngazi mbalimbali kutowafikia
wanachama wao kama ambavyo wapinzani wamekuwa wakifanya, na
kumshauri mwenyekiti mpya kuongeza msukumo ili viongozi wawe wanatoka
katika kueneza kazi nzuri zinazofanywa na chama hicho.

Mbali na hayo Kikwete ameendelea kukiri kuwa nusura chama kivujike mwaka
2015 kutokana na hali ya kisiasa ilivyokuwa lakini amefanikiwa kukivusha
salama.

“Katika historia ya CCM hakuna wakati ambao chama kilipata tishio la
kuanguka kama ilivyokuwa mwaka jana, lakini haikuwa hivyo, na badala yake
kimekuwa imara zaidi”

Amekanusha taarifa kuwa alikuwa anakataa kuachia nafasi hiyo na kusema
kuwa si kweli, bali Rais Magufuli ndiye aliyekuwa anakataa kupokea kazi hiyo,
na yeye kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi akiwemo Makamu Mwenyekiti
Bara Philip Mangula walifanya kazi ya kushawishi hadi Magufuli akakubali.

Amewashukuru wanachama wa chama hicho kwa kumpa ushirikiano kwa kipindi
chote cha miaka 10 na kutaka wanachama hao kuendelea kumpa ushirikiano
zaidi mwenyekiti mpya Dkt John Magufuli.

John Cheyo Mwenyekiti wa UDP na Augustino Mrema Mwenyekiti wa TLP ni
miongoni mwa viongozi wa vyama 12 waliohudhuria mkutano huo.
Aidha viongozi mbalimbali wa kisiasa wamepongeza uchaguzi huo wa CCM
uliomalizika kwa amani.

Mmoja wa viongozi hao ni Zitto Kabwe kiongozi wa ACT Wazalendo ambaye
amempongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa
Mwenyekiti wa CCM.

Zitto amesema uchaguzi huo wa CCM unapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa
vyama vyote vya siasa kuwa na utaratibu wa kuachia madaraka kila baada ya
miaka kadhaa.

Aidha amemtaka Rais Magufuli, Mwenyekiti mpya wa CCM kulegeza msimamo
wa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa kwani bila mikutano hiyo vyama vya
siasa kikiwemo chama chake, vitaathirika
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel