Top Menu

Wahandisi 347 wafutiwa usajili

8/31/2016 09:57:00 am

Dar-es-salaam

Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) imewafutia
usajili wahandisi 347 kwa makosa mbalimbali ya kimaadili
katika taaluma hiyo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Msajili wa ERB, Injinia Steven Mlote amesema jana kuwa baadhi
ya makosa hayo ni kusimamia kazi ambazo zilikuwa chini ya
kiwango.

Injinia Mlote amesema hayo wakati akitangaza siku ya wahandisi
ambayo itafanyika kesho, Septemba Mosi na Rais John Magufuli
atakuwa mgeni rasmi ambako atashuhudia wahandisi 200 wakila
kiapo cha utii.

“Watakula kiapo mbele ya Rais Magufuli ili kuhakikisha
wanawajibika vyema kwa kufuata maadili kwenye taaluma yao,”
amesema.


Waziri aeleza sababu za kununua ndege Bombadier

8/31/2016 09:41:00 am

Dar es Salaam.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iliamua kununua
ndege aina ya Bombadier Q400 kutoka Canada kutokana na
uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya
nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua
mafunzo ya wakufunzi ya marubani yanatolewa na Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Mabibo, Dar es Salaam.
“Serikali imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier
Q400 kutokana na hali halisi ya viwanja vya ndege nchini kuwa
vya changarawe na lami kwa baadhi,” alisema Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa aliyeonekana kujibu hoja za wabunge wa
Kamati ya Miundombinu walipokutana na Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) mjini
Dodoma hivi karibuni, alisema kuwa Serikali haikukurupuka
kufanya uamuzi wa kununua aina hiyo ya ndege kwani
ilizingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa
ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia ATCL.

Katika kikao hicho cha Kamati ya Bunge ya Miundombinu,
Mbunge wa Misungwi (CCM) na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani, Charles Kitwanga alipinga Serikali kununua ndege hizo
zinazotumia injini za pangaboi kwa fedha taslimu huku kukiwa
hakuna mipango thabiti ya kuifanya ATCL iwe bora.

“Ukiangalia mikakati ya kutanua hili shirika (ATCL) liende juu
hakuna, tunachozungumzia ni kununua ndege. Sasa ukishanunua
zije zifanye nini? Zife na zenyewe? Ziishe kama tulivyonunua
nyingine? Hivyo ndivyo tutakavyoendesha uchumi wetu, mimi
naambiwa Q400 ndiyo tutakuwa watu wa kwanza kuipokea,
halafu mnaifahamu hii kampuni? Si kubwa kama inavyotajwa, ni
mali ya mtu binafsi,” alisema.

Lakini Profesa Mbarawa alitetea uamuzi wa kununua ndege hizo
huku akiwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni
kuhudumia wananchi, hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu
ndege hizo kwa kuwa zimezingatia mambo mbalimbali likiwamo
suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.
Uwezo na ubora

Profesa Mbarawa alisema ndege hizo zina uwezo wa kutua katika
viwanja vingi vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ni vingi
nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja
vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.

Pia, zinatumia kiasi kidogo cha mafuta ikilinganishwa na aina
nyingine ambapo kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi
Mwanza zitakuwa zikitumia tani 1.7 za mafuta tofauti na aina
nyingine zinazotumia hadi tani 2.8 kwa safari moja.

Vilevile, alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa
ndege hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na
sifa akisema kampuni hiyo imefanya biashara na nchi nyingi
ikiwamo Ethiopia yenye ndege 19 aina ya Bombadier Q400
zilizotengezwa na kampuni hiyo.

Tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo
kwa asilimia 40 na zitaanza safari ya kutoka Canada Septemba
15 mwaka huu kupitia Uingereza na zinatarajiwa kuwasili nchini
Septemba 19.Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iliamua kununua
ndege aina ya Bombadier Q400 kutoka Canada kutokana na
uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya
nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua
mafunzo ya wakufunzi ya marubani yanatolewa na Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Mabibo, Dar es Salaam.

“Serikali imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier
Q400 kutokana na hali halisi ya viwanja vya ndege nchini kuwa
vya changarawe na lami kwa baadhi,” alisema Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa aliyeonekana kujibu hoja za wabunge wa
Kamati ya Miundombinu walipokutana na Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) mjini
Dodoma hivi karibuni, alisema kuwa Serikali haikukurupuka
kufanya uamuzi wa kununua aina hiyo ya ndege kwani
ilizingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri wa
ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia ATCL.

Katika kikao hicho cha Kamati ya Bunge ya Miundombinu,
Mbunge wa Misungwi (CCM) na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani, Charles Kitwanga alipinga Serikali kununua ndege hizo
zinazotumia injini za pangaboi kwa fedha taslimu huku kukiwa
hakuna mipango thabiti ya kuifanya ATCL iwe bora.

“Ukiangalia mikakati ya kutanua hili shirika (ATCL) liende juu
hakuna, tunachozungumzia ni kununua ndege. Sasa ukishanunua
zije zifanye nini? Zife na zenyewe? Ziishe kama tulivyonunua
nyingine? Hivyo ndivyo tutakavyoendesha uchumi wetu, mimi
naambiwa Q400 ndiyo tutakuwa watu wa kwanza kuipokea,
halafu mnaifahamu hii kampuni? Si kubwa kama inavyotajwa, ni
mali ya mtu binafsi,” alisema.

Lakini Profesa Mbarawa alitetea uamuzi wa kununua ndege hizo
huku akiwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni
kuhudumia wananchi, hivyo watu wasipotoshe ukweli kuhusu
ndege hizo kwa kuwa zimezingatia mambo mbalimbali likiwamo
suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.

Uwezo na ubora
Profesa Mbarawa alisema ndege hizo zina uwezo wa kutua katika
viwanja vingi vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ni vingi
nchini tofauti na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja
vyenye urefu zaidi ya kilomita mbili.

Pia, zinatumia kiasi kidogo cha mafuta ikilinganishwa na aina
nyingine ambapo kwa safari ya kutoka Dar es Salaam hadi
Mwanza zitakuwa zikitumia tani 1.7 za mafuta tofauti na aina
nyingine zinazotumia hadi tani 2.8 kwa safari moja.

Vilevile, alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa
ndege hizo zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na
sifa akisema kampuni hiyo imefanya biashara na nchi nyingi
ikiwamo Ethiopia yenye ndege 19 aina ya Bombadier Q400
zilizotengezwa na kampuni hiyo.

Tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo
kwa asilimia 40 na zitaanza safari ya kutoka Canada Septemba
15 mwaka huu kupitia Uingereza na zinatarajiwa kuwasili nchini
Septemba 19

Godbless Lema Apandishwa Mahakamani.......Aachiwa Kwa Dhamana

8/29/2016 11:05:00 pm
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amepandishwa mahakamani katika
kesi mbili tofauti.

Kesi ya kwanza namba 351/2016 anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa simu wa
uchochezi Mkuu wa mkoa Arusha, Mrisho Gambo wenye maneno kuwa “Karibu
tutakudhibiti kama mashoga walivyodhibitiwa Uarabuni”

Kesi ya pili namba 352/16 Lema anatuhumiwa kuhamasisha maandamano
Septemba Mosi kinyume cha sheria.

Hakimu amepinga hoja za wakili wa Serikali, Vincent Njau kuzuia dhamana
kwa sababu za kiinterejensia kwa usalama wake.

Lema amekana mashitaka yote, na ameachiwa kwa dhamana baada ya
kutimiza masharti ambapo kwa shitaka la kwanza alitakiwa kupata mdhamini
na shilingi 10, na shitaka la pili dhama ni shilingi milioni 15.Kesi hiyo itatajwa
tena Septemba

Hakimu anayesikiliza kesi ni Desderi Kamugisha wakati wakili wa serikali akiwa
ni Innocent Njau.

Baadaye vurugu ziliibuka mahakamani wakati polisi wanataka kumpeleka Lema
magereza kwa madai kuwa wadhamini wamechelewa, lakini mbunge huyo
alipinga hatua hiyo kwa maelezo muda wa mahakama saa 9.30 ulikuwa bado.
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwa amepakatiwa na mkewe baada ya kuachiwa kwa dhamana kwa kesi inayomkabili mahakama ya hakimu mkazi.Pichani akiwa hoi baada ya kushinda njaa kwa siku mbili akidai kufunga kwa kushinda na njaa  kwaajili ya kuombea taifa
.
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akiwa hospitalini baada ya kutoka mahakamani na kusomewa mashtaka nakutajiwa makosa yake  1.kwanza likiwa ni kitoa lugha ya matusi yakumtukana mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Ghambo, 2.kufanya uchochezi kwa njia ya sauti na kuchochea maandamano yasiyokuwa halali ya septemba mosi.

Moto wa mkaa wamuuwa mchimba kisima

8/29/2016 09:29:00 amVero Ignatus....Arusha

 Mchimbaji wa kisima aliyefahamika kwa majina ya Waziri Omary (25) mkazi wa Ngaramtoni amefariki dunia kisimani wakati akichimba kisimani

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amekiri kutokea kwa tukio hilo marehemu alikutwa amefariki kisimani baada ya kutumia moto wa mkaa

Alisema marehemu huyo aliwasha moto wa mkaa kulainisha mwamba ili aweze kupata maji

Pia alisema kisima hicho akichokuwa anachimba chenye urefu wa futi 60, alikutwa saa 5 juzi akiwa ameshapoteza maisha

"Kilichotokea ni kwamba huenda wakati amewasha jiko, Carbonmonoxide ilizidi huku hewa ya Oxygen ilikuwa ndogo kiafya lazima angedhurika , "alisema 
"Mwili wa marehemu haujakutwa na jera lolote, tunaendelea na uchunguzi kubaini zaidi , "alisema Kamanda.

Pia amewatahadharisha watu kuhakikisha watu nawapotumia majiko ya mkaa ndani kuhakikisha kuna hewa ya kutosha..
Watu wazuiwa kuingia kwenye ukumbi AICC

8/28/2016 06:25:00 pm

                                                               Vero Ignatus .......Arusha

Wakazi wa Jiji la.Arusha na vuiunga vyake pamoja na kutoka mikoa jirani wamefurika katika Tamasha linaloitwa LETS PRAISE SUMMIT, lililoandaliwa na Mchungaji Adamu Haji katika Kituo cha kimataifa cha Mikutano (AICC) katika ukumbi wa Simba.

Maelfu ya watu hao walianza kumiminika katika Kituo hicho cha Mikutano kuanzia saa tatu asubuhi ambapo hata kabla tamasha hilo halijaanza tayari Ukumbi wa Simba uliopo AICC ulikuwa umejaa na hivyo kusababisha maelfu ya watu waliofika kuzuiliwa nje kwa kuwa kulikuwa hakuna namna ya wao kuingia ukumbini kutokana na kufurika kwa watu.

Akielezea hali hiyo ya maelfu ya wahudhuriaji wa tamasha kushindwa kuingia ukumbini, Muandaaji wa tamasha hilo mchungaji Adamu Haji amesema kuwa hakutegemea kuwa watu wangelikuwa na muitikio mkubwa namna hiyo hivyo amesema kuwa atamuomba muimbaji huyo asiondoke mapema ili lirudiwe upya maana watu wwengi wanatamani kumuona.

Mchungaji Adamu Haji ambae ni mwaandaaji wa tamasha hilo.

Mchungaji huyo amesemakuwa wameamua kufanya tamasha hilo ndani ya ukumbi kwasababu ya kutii agizo la serikali na wao hawataki kupingana na serikali hivyo watajitahidi kulifanya tamasha hilo kwa mara ya pili ili watu wote waweze kufaidi .

Kwa upande wake Afisa Itifaki na uhusiano wa Aicc Rodney Thadeus amesema kuwa ukumbi huo unauwezo wa kuchukua watu 1350 hivyo usingeliweza kuhimili idadi kubwa ya watu ambao walitaka kuingia ukumbini hapo kwaajili ya tamasha hilo.Martha Uhwelo Muimbaji wa nyimbo.za.injili ambaye hakufanikiwa kuingia ukumbini.
Daniel Philipo  Muimbaji.wa Nyimbo za injili ambaye na yeye hakufanikiwa kuingia.ukumbini katika tamasha hilo.

Kwa upande  waimbaji ambao hawakufanikiwa kuingia ukumbini kwenye tamasha hilo wamesema kuwa waandaaji wa tamasha hilo hawajajipanga."Huwezi kumleta muimbaji mkubwa kutoka kundi.kubwa linalifahamika.duniani la Joyous Celebration kutoka Afrika ya Kusini ,kisha tamasha lifanyike ukumbini"

"Kila mtu amekuja hapa kwaajili ya kumunaona muimbaji Mkhululi Bhebhe,sasa ona tunaondoka hata ukumbini hatujaingia kwasababu ya ukumbi mdogo siku nyingine hawa waandaaji wakiandaa tamasha kama hili waliweke kwenye uwanja kila mtu afaidi alisisitiza mmoja wa aliyekuja kwaajili ya tamasha "
Muonekano wa ukumbi wa Simba ulivyofurika watu ndani ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) 
Muimbaji Daniel Safari akiwa anaimba katika Tamasha hilo katika ukumbi wa Simba ndani ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)
Watu wakiwa nje ya Geti kuu AICC ambao wameshinndwa kuingia ndani ya ukumbi.
Muonekanonwa watu mbalimbali kila mtu akijadili na mwenzake baada ya kuambiwa hawawezi kuingia ndani ya ukumbi kutokana na ukumbi huo kufurika hivyo wanalazimika kurudi majumbani mwao.
Kiongozi wa kundi la Worshipers Aberdnego Hango .

Sambamba na hayo kiongozi wa kundi la Worshipers Aberdnego Hango ambao ni wenyeji wa Muimbaji Mkhululi Bhebhe kutoka kundi la Joyous Celebration kutoka Afrika ya Kusini amesema kuwa tamasha hilo ni kubwa mno watu wamekuwa na muitikio mkubwa sana japo kuwa ukumbi umekuwa mdogo,amewataka wale ambao hawajafanikiwa kuingia ukumbini wasivunjike Moyo kwani season II inakuja hivi karibuni.

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMSIMAMISHA KAZI AFISA MAENDELEO YA JAMII WA JIJI KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

8/28/2016 01:08:00 pm
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani J. Kihamia
amempuzisha kutekeleza majukumu yake Afisa Maendeleo ya Jamii
wa Jiji Bi. Mwantumu Dosi kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza
majukumu yake hivyo kukiuka kanuni za Utumishi wa Umma za
mwaka 2003.

Mkurugenzi Kihamia ametoa taarifa hiyo Jana tarehe 27.08.2016
baada ya kukamilisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kufanya
tathmini ya miradi iliyopitiwa na Mwenge na kugundulika kwa
dosari zilizojitokeza katika moja ya mradi ambao uko chini ya
Idara hii.

Mradi huo ni kikundi cha vijana wanaojishughulisha na Uselemara
pamoja na Uchomeleaji kinachojulikana kama Mbeshere Umoja
Group kilichopo Kata ya Olorieni kiligundulika kuwa na
wananchama waliovuka umri wa miaka 35 ambao hawastahili
kunufaika na Mikopo ya Vijana kwa mujibu wa Sera.

Mwenge wa Uhuru katika Jiji la Arusha ulikimbizwa tarehe
24.08.2016 na Kikundi hicho kilikua ni miongoni mwa miradi
iliyokua inapitiwa na Mwenge wa Uhuru ambapo wanachama wake
hawakizi vigezo. Wanachama hao walikua wameandaliwa kupewa
Hundi ya tsh Milioni tano kama ishara ya kuunga mkono jitihada
zao zakuboresha maisha. Mkimbiza Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.
George Jackson Mbijima alisitisha zoezi hilo baada ya kugundua
dosari za umri kwa baadhi ya wanachama.

Kupumzishwa kutekeleza majukumu ya Mkuu wa Idara hii
kunafuatana na masharti ya kukabidhi Ofisi kwa Mratibu wa Tasaf
Bi. Tajiel Mahega ambaye kwa sasa atakua Kaimu Mkuu wa Idara
hii mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
27Agosti,2016

Waalimu Wacharuka Arusha

8/27/2016 09:09:00 pm


Vero Ignatus ..Arusha

 Chama cha walimu mkoa wa Arusha waitisha maandamano ya waalimu yasiyo na kikomo kupinga uonevu wa walimu wanaotuhumiwa na wanafunzi hewa jijini Arusha 

Andrew Nazu ambaye ni Kaimu mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Arusha amesema, chama kimetoa siku 10 kwa Mkurugenzi wa jiji kufuta barua zilizowavua madaraka walimu 23 na waratibu wa Elimu kata kumi 

Wamesema hawatakubali kukaa meza moja na Mkurugenzi wa jiji mpaka pale watapowasikiliza madai ya walimu wanaotuhumiwa kuhusika na wanafunzi hewa 

"Tumegundua zoezi hili la uhakiki wa wanafunzi hewa na upatikanaji wa wanafunzi hewa kwa jiji umekuwa wa kionevu na tunao ushaidi , "alisema Kaimu mwenyekiti 

" Adhabu imetolewa bila kuwashirikisha chama wa walimu ama kamati ya walimu na pia hata hao walimu hawajapewa muda wa kusikilizwa, "alisema Kaimu

"Mkurugenzi alipigiwa simu kuwa asiwavue madaraka walimu mpaka watakapowasikiliza lakini hakufanya hivyo ,alikaidi na kuwavua madaraka ,tunasema atengue barua hizo ,"alisema Kaimu

Kwa upande wake Kaimu Katibu Nurueli Kavishe, amesema maandamano haya yatakuwa ya namna yake lengo likiwa ni kuhakikisha wanatetea uonevu unaofanywa na baadhi ya watu kisa ikiwa ni migogoro baina ya watu na watu na wengine wakifanya uonevu huo kwa lengo la kuweka watu wao kwenye nafasi hivyo

"Sisi hatutaogopa kupigwa na polisi ,tunasema polisi waandae mabomu na risasi lazima tuandamane ,"alisema Nuruel

Upande wa Katibu wa chama cha walimu wilaya ya Arumeru Jocye Kizaji, amemtaja afisa elimu wa msingi wa jiji Hussen Mgewa kuwa moja wa maafisa waliokuwa mwiba kwa waalimu hasa akiwa ni mwenye kutoa lugha chafu kwa waalimu na kupelekea waalimu kudharaulika mitaani

"Huyu Afisa amekuwa mfano mbaya kwakutoa lugha chafu na yote tumeyarekodi maneno machafu aliyokuwa anawatolea walimu ,"alisema Jocye Kijazi

"Mimi nashanga kuna shule mwalimu hajapewa barua ya kushushwa madaraka ila mratibu kapewa na kisa ni mwanafunzi hewa moja,hapo haki iko wapi?alisema Jocye

Hata hivyo amewataka walimu wa halmashauri ya jiji ya arusha kuunga mkono maandamano hayo kutetea haki ya walimu walionewa

Waziri Nape Atengua Uteuzi wa Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA

8/27/2016 09:31:00 am

Paul Makonda aitwa Tume ya Haki za Binadamu Kujieleza.....Ni kwa kauli yake aliyotoa Agosti 25 Akiwataka Polisi Wawapige Watu Wakiwakuta Msituni

8/27/2016 08:11:00 am

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na
matamshi ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
yanayokiuka misingi ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati
wa kuaga miili ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti
26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao
makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume
ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi wa
haki za binadamu.
Aidha, Tume imeona kuwa maagizo aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi
la Polisi hayana msingi wa kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa
Mkoa.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na (i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a) vya
Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya Sheria
za Tanzania 2002, THBUB ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu au
taasisi yoyote kuhusiana na utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka ya
madaraka yake, ili kuchukua hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.
Imetolewa na:
(SIGNED)
Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Agosti 26, 2016


Update: Majambazi Kadhaa Yauawa Katika Mapigano na Jeshi la Polisi huko Mkuranga

8/26/2016 03:02:00 pm
Majambazi ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa kuuwawa katika mapigano
hayo kati yao na polisi huko Vikindu, wilaya ya Mkuranga leo.

Milio ya risasi na mabomu vilisikika kuanzia saa saba usiku katika eneo hilo
ambalo majambazi hayo walikuwa wamejificha.

Habari zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa Polisi wameweka kizuizi cha
barabara eneo la Kongowe, wilayani Mkuranga ambapo magari yote yanayotoka
na kuingia Dar yanapekuliwa.Godbless Lema Atiwa Mbaroni na Jeshi la Polisi

8/26/2016 11:55:00 am

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema(CHADEMA) amekamatwa na polisi
akiwa nyumbani kwake alfajiri ya leo. Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro
amethibitisha tukio hilo, lakini hakutaja sababu za kukamatwa kwa mbunge
huyo.

Jana Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata viongozi waandamizi wanne
wa Chadema mkoa wa Kigoma na jimbo la Kigoma mjini kwa kile kinachodaiwa
ni kujihusisha na vitendo vya uchochezi.

Waliokamatwa na kuwekwa mahabusu ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa
Kigoma, Ally Kisala, Katibu wa Baraza la vijana Chadema mkoa (Bavicha),
Omary Gindi, Katibu wa chama jimbo la Kigoma mjini, Frank Ruhasha na
Mwenyekiti wa mtaa wa sokoni katika Kata ya Katubuka, Moses Bilantanye.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna msaidizi wa Polisi (DCP)
Ferdinand Mtui alikiri viongozi hao wanne kushikiliwa kituoni hapo kwa muda
lakini walipata dhamana, hivyo kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti
kituoni hapo leo Ijumaa.

Mahabusu Ajinyonga Arusha

8/25/2016 10:03:00 pm
Mahabusu aliyekuwa akishikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Arusha
aliyetambulika kwa jina la Victoria Wenga (51) mkazi wa Lemara jijini Arusha
amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia jana kwa kutumia shuka lake bila
kuacha ujumbe wowote.

Marehemu alikamatwa Agosti 21 mwaka huu majira ya Alfajiri kwa tuhuma za
kuchoma moto nyumba yake na maduka yake mawili kutokana na ugomvi wa
kifamilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kutokea kwa tukio
hilo katika Kituo cha Kikuu cha Polisi saa 6:20 usiku jana wakati wenzake
wakiwa wamelala.

“Polisi wa zamu alisikia kelele kutoka kwenye chumba cha mahabusu wa kike
ambapo polisi walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu huyo, lakini
ilishindikanika,” alisema Kamanda Mkumbo.

Mahabusu huyo, ambaye ni mkazi wa Lemara jijini Arusha, alijinyonga kwa
kutumia shuka lake alilokuwa anatumia kujifunikia wakati yuko mahabusi.
Mtuhumiwa huyo, alijinyonga kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka
yake.

“Jana ilikuwa afikishwe mahakamani kujibu kosa lililokuwa linamkabili,” alisema
Kamanda Mkumbo na kuwahakikishia kuwa hali ya usalama kituoni hapo na
tukio hilo, havihusiani na sababu zozote za kiusalama.

Marehemu Victoria anadaiwa kuwa na ugomvi wa kifamilia na mume wake
aliyetambulika kwa jina la Edward Wenga akimtuhumu kuzaa nje ya ndoa
kinyume na utaratibu.

Imeelezwa kuwa hicho ndo chanzo cha marehemu kufikia hatua ya kuteketeza
mali walizochuma na mume wake ambazo ni maduka mawili na nyumba ya
kuishi.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhia mahiti Hospitali
ya Mount Meru.

Diwani wa Chadema afikishwa Mahakamani

8/25/2016 08:40:00 pm
Vero  Ignatus Arusha
Diwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Kata ya Sombetini,Ally Bananga(40),amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kuhamasisha uchochezi

Akisomewa shauri hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi Augustino Rwezire, mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Arusha, diwani huyo anakabiliwa na shitaka la kuhamasisha wananchi kufanya maandamanao yasiyo halali, Septemba mosi mwaka

Diwani huyo alifikishwa mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mfawidhi,Agustino Rwizile,ambapo Wakili wa Serikali Charles Kagirwa,alidai kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo  Agosti 13 mwaka huu,wilayani Karatu mkoa wa Arusha.

Pia alisema kuwa siku ya tukio Bananga akiwahutubia wananchi katika mkutano wa wazi uliofanyika eneo la Hosteli ya Karatu, aliwahamasisha wananchi hao washiriki katika kusanyiko lisilo halali ya tarehe 1 septemba

Wakili huyo aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo kutokana na upelelezi wake kutokukamilika na kudai kuwa dhamana iko wazi kwa mshitakiwa.

Mawakili wa utetezi John Mallya Wakili James Lyatuu, wameiomba mahakama hiyo kumpa Bananga masharti nafuu ya dhamana kwani ni diwani na anaweza kujidhamini mwenyewe 
Hakimu Rwizile alikubaliana na ombi hilo na kumtaka Diwani huyo kujidhamini mwenyewe kwa dhamana ya shilingi milioni 5 na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 22 mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena.
Nae, Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema amesema maandamano ya Septemba Mosi yapo palepale na wamejianda kupambana na polisi

Diwani huyo alitiwa kizuizini kwa siku tatu huku nyumbani kwakwe kukutwa na fulana moja iliyoandikwa UKUTACWT Arusha yahofia uhakiki wanafunzi hewa

8/25/2016 10:40:00 am

Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba,


ARUSHA.

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Arusha,
kimetaka uhakiki wa wanafunzi hewa jijini hapa kuanza upya
kwa madai ya uwapo wa uamuzi wa chuki dhidi ya wakuu wa
shule.

Ameyasema hayo ofisini kwake  Makamu Mwenyekiti wa CWT
Mkoa wa Arusha, Andrew Ngazu ,ya kwamba chama hicho kinamtaka
mkurugenzi wa jiji kurudia uhakiki wa wanafunzi kwa sababu uamuzi
uliotolewa ulikuwa wa binafsi na haukufuata utaratibu
maalumu.

“Tunamuunga mkono Rais Johh Magufuli kuhakiki shule zenye
wanafunzi hewa, ila tunapinga kwa nguvu zote uhakiki
uliofanyika Arusha,” alisema Ngazu na kuongeza: “Tunaamini
umefanywa na maofisa wa elimu kwa chuki dhidi ya walimu
wa shule, hali iliyosababisha kuonewa kwa baadhi ya walimu
huku shule zenye wanafunzi hewa zikiachwa.”

Makamu Katibu wa CWT, Nurueli Kavishe alisema mpaka sasa wana ushahidi
unaojitosheleza kuwa mwajiri wao ambaye ni mkurugezi wa
jiji hakutumia takwimu zilizopo.

Katibu wa CWT Wilaya ya Arumeru, Joyce Kizaji aliwataka
wakurugenzi kuacha kuwatisha walimu kuhusu Mwenge kwani
siyo lazima.Waliofariki Italia waongezeka, manusura watafutwa

8/25/2016 09:50:00 am

Idadi ya watu waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi katikati mwa Italia
mapema Jumatano imefika 247 huku manusura wakiendelea kutafutwa.
Maafisa wa uokoaji wanaendelea na juhudi za kutafuta manusura na miili
kwenye vifusi.
Tetemeko hilo la nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter liliharibu vibaya miji ya
Amatrice, Accumoli na Pescara del Tronto ambapo watu wengi walifariki.
Maafisa wa uokoaji waliendelea na juhudi za kuwatafuta manusura usiku, lakini
wakati mmoja walitatizwa na mitetemeko mingine iliyotokea na kutikisa
majumba yaliyosalia yakiwa bado wima.
Eneo lililokumbwa na tetemeko hilo ni milimani katika majimbo ya Umbria, Lazio
na Marche.
Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa karibu na Norcia, kilomita 170 kaskazini
magharibi mwa mji mkuu Roma.
Mahema yamewekwa kuwasaidia watu walioachwa bila makao.

Waasi nchini Colombia wasaini mkataba wa amani

8/25/2016 09:45:00 am
Serikali ya Colombia na kundi la waasi la Farc wamesaini mkataba wa amani
kusitisha mgogoro uliopo zaidi ya miongo mitano.

Pande zote mbili zimekubaliana kusaidia jamii, kuwapa haki zao waathirika wa
mgogoro huo na kuleta amani.

Tamko la pamoja limesomwa katika sherehe zilizofanyika mji mkuu wa Cuba
huko Havana,ambapo makubaliano hayo ya amani yalianzishwa karibu mika 4
iliyopita.

Mgogoro huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya laki mbili na kuaawacha
zaidi ya milioni bila ya makazi huko colombia.

Muda wa makubaliano wa mkataba huo bado unahitajika kuwekwa na
wananchi wa Colombia kupitia kura ya pamoja itakayofanyika mwezi oktoba.
Kingunge awashauri viongozi wastaafu

8/25/2016 08:53:00 am
Mwanasiasa mkongwe nchini KINGUNGE NGOMBALE MWIRU amewashauri
marais na Mawaziri wakuu wastaafu nchini kuingilia kati mvutano kati ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA na serikali wa kutaka
kufanya mandamano na mikutano nchi nzima bila kibali cha kufanya hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini DSM KINGUNGE
amesema viongozi hao wana nafasi kubwa ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo.
Tayari viongozi mbalimbali wa dini na serikali wameshauri kuwepo kwa
maridhiano kati ya serikali na CHADEMA.

Hapo jana Msajili wa Vyama vya siasa nchini jaji FRANCIS MUTUNGI
alitangaza kuwepo kwa kikao tarehe 26 mwezi huu na kisha Baraza la Vyama
vya Siasa nchini tarehe 29 na 30 mwezi huu kwa lengo la kujadili hali ya kisiasa
nchini
CHADEMA imepanga kufanya mikutano na maandamano nchi nzima Septemba
Mosi mwaka huu.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani MBEYA limewahakikishia wananchi
wa mkoa huo amani na utulivu katika kipindi cha kuelekea maandamano
yaliyoandaliwa na vyama vya siasa Septemba Mosi mwaka huu.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya BUTUSYO MWAMBELO,
ametoa kauli hiyo baada ya kuhitimisha mazoezi ya kawaida ya Jeshi hilo
ambayo yamefanyika kuzunguka viunga mbalimbali vya Miji ya Mbeya na
Mbalizi.

Rais Magufuli apokea taarifa ya Ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Uganda hadi bandari ya Tanga.

8/25/2016 08:49:00 am
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javiero Rielo
amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kuwa maandalizi ya kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka
Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania yanaendelea vizuri
na kwamba kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa
mafanikio.

Bw. Javiero Rielo amesema hayo jana tarehe 24 Agosti, 2016 Ikulu Jijini Dar es
Salaam alipokutana na Rais Magufuli kwa lengo la kumpa taarifa juu ya
maendeleo ya maandalizi ya kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta.

Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo
litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya
Tanga nchini Tanzania na unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500
na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.

Gharama za mradi wa ujenzi wa bomba hilo zinatarajiwa kuwa takribani Dola
za Kimarekani Bilioni 4 na Kampuni ya Total inasema fedha hizo zipo tayari.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli amesema anaamini
kuwa mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania, Uganda,
Kampuni ya Total na nchi jirani.

Amebainisha kuwa pamoja na kwamba Tanzania ipo katika mazingira mazuri ya
kutekeleza mradi huo, Serikali yake itatoa ushirikiano mkubwa ili kufanikisha
mradi huo.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka kwa
mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao ni Mhe. Ian Myles – Balozi wa Canada hapa
nchini, Mhe. Prasittiporn Wetprasit – Balozi wa Thailand hapa nchini mwenye
makazi yake Mjini Nairobi nchini Kenya na Mhe. Harald Gunther – Balozi wa
Austria hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi nchini Kenya.

Pamoja na kuwasilisha hati zao za utambulisho Mabalozi hao wameelezea
kufurahishwa na mahusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zao na
Tanzania na wameahidi kufanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania ili
wananchi wa pande zote wanufaike na matokeo ya ushirikiano huo hususani
katika uwekezaji na biashara.

Kwa upande wake Rais Magufuli amewahakikishia Mabalozi hao kuwa Serikali
yake itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo na
ametoa wito kwa Mabalozi hao kuzishawishi zaidi nchi zao na wawekezaji
katika nchi hizo kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa viwanda, uongezaji
thamani ya madini, kuendeleza kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji,
uzalishaji wa nishati na biashara mbalimbali.

Pia Rais Magufuli ametoa wito kwa Mabalozi wa Thailand na Austria kuanzisha
ofisi za Ubalozi hapa nchini ili kurahisisha na kuharakisha shughuli za kibalozi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
24 Agosti, 2016

Jeshi La Polisi Lahusisha Mauaji ya Polisi Wanne na Sakata la Oparesheni UKUTA.........Lapiga Marufuku Mikutano yote ya Ndani ya Vyama vya Siasa

8/24/2016 08:42:00 pm
KUFUATIA mauaji ya askari wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa
watu wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari
hao kwa kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka
wahusika wote kujisalimisha.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limehusisha tukio hilo na Umoja wa Kupinga
Udikteta Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa
ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao
wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi
nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa habari
Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na
polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.

Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia amepiga marufuku mikutano ya
ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa
watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.
Amesema Jeshi hilo limebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika
kuchochea wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya
mapambano na jeshi la polisi

"Kwasababu hiyo basi,kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu
kuvunja sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi
nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani" amesema.

Aidha CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati
wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524
PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali
Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa Mbande.

"Katika tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa
kupora silaha mbili aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya
benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na
kusudio moja tu la kuwashambiulia askari polisi, " alisema.

Alisema katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu
waliandika mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi
na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari
polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa
na polisi Septemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari
wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.
Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio yote ya
uvunjifu wa amani nchini.UCHELEWESHAJI WA KESI ZA WATOTO WAKWAMISHA HAKI ZA WATOTO

8/24/2016 10:32:00 am
 
Vero Ignatus Arusha

Ucheleweshaji wa kesi za watoto walioko katika mahabusu za watoto umetajwa kuwa chanzo cha kukwamisha haki za watoto na kuwasababisha mlundikano katika mahabusu hizo hivyo kukosa haki ya elimu na malezi ya familia.


Baadhi ya watoto Bertha Jukaeli na Rose Wiliam waliopata msaada wa kisheria kutoka shirika lisilokua la kiserikali la Valonteer Tanzania Abroad ,wamesema kuwa licha ya kupata mawakili waliowasaidia bado kuna idadi ya watoto wanaokosa mawakili hivyo kushinda kujiwakilisha vyema mahakamani na kukosa haki zao.

Wameiomba serikali na Mashirika binafsi na Mawakili wa kujitegemea kuhakikisha kuwa watoto wanapata mawakili ili waweze kupata haki zao na kurejea katika jamii ili kujenga jamii bora na yenye ustawi mzuri.

Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Arusha Musa amesema kuwa miundombinu iliyoko katika mahabusu za watoto si rafiki kwa maana ya kukosekana kwa madarasa hivyo watoto wanapokaa muda mrefu wanapoteza haki zao za elimu ,pia ameiomba serikali ifanye maboresho katika mahabusu hizo.......

Kwa upande wake Mmmoja wa Wageni wanaojitolea kutoka nchini Ufaransa Ezis John anasema kuwa kuna uwazi mkubwa kutoka kwenye sheria na uhalisia wajamii bado haki za binadamu ni changamoto hususan kinamama na watoto pia wanaume wanapaswa kuhusishwa.

ASKARI POLISI WATATU WAUWAWA JANA USIKU HUKO MBAGALA MMBANDE JIJINI DAR ES SALAAM

8/24/2016 07:10:00 am
Taarifa iliyotufikia jana usiku inaeleza kuwa, kuna tukio la kuuwawa
kwa Askari Polisi, lililotokea huko Mbagala jijini Dar.

Inadaiwa kuwa askari hao walikuwa wakibadilishana lindo katika
Benki ya CRDB tawi la Mbagala Mmbande na mara wakaibuka watu
wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi na kuanza kuwashambulia kwa
risasi na baada ya shambulizi wanadaiwa kuondoka na pikipiki
wakielekea maeneo ya Mvuti.
ASKARI WALIOFARIKI ni
E5761 CPL YAHAYA
F4660 CPL HATIBU NA
G9544 PC TTITO.

Inasemekana kuwa tukio hilo limetokea mnamo saa 1: 30 ni katika
tukio la UVAMIZI WA BANK CRDB MBANDE na inadaiwa kuwa
wahalifu hao waliondoka na silaha moja aina ya SMG.

Tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. Mmoja
aliyefariki alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine
alikuwa dereva.

Inadaiwa kuwa majambazi hayo hayakuingia ndani ya benki.
Gari la Polisi (Leyland Ashok) limeharibiwa kwa risasi.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon
Sirro amethibitisha na kusema: "Ni kweli kumetokea tukio la uvamizi
hapa mbagala lakini kwa taarifa kamili ntazitoa leo kwakuwa
bado alikuwa eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi".


Noa iliyokua imebeba magazeti yaua 5 Makanya.

8/23/2016 11:47:00 pm
Moshi.

 Watu watano wamefariki duni kati yao wanne wamekufa
papo hapo baada ya gari aina ya Toyota Noah lililokuwa
limebeba magazeti kugongana uso kwa uso na lori aina ya
Scania.

Ajali hiyo imetokea leo saa 10:45 alfajiri katika eneo la
Alkachenje katika kijiji cha Makanya wilayani Same baada ya
gari hilo lililobeba magazeti ya kampuni ya New Habari
kugongana na lori hilo.

Gari hilo aina ya Toyota Noah ilikuwa ikitokea Jijini Dar Es
Salaam kuelekea Moshi na Arusha wakati lori hilo aina ya Scania
ilikuwa ikitokea Arusha kwenda Dar.

Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemary Staki ameliambia gazeti hili
leo kuwa, abiria wanne walikufa papo hapo na mmoja akafia
hospitali ya wilaya ya Same wakati madaktari wakijitahidi
kuokoa maisha yake.Diwani mbaroni kwa uchochezi.

8/23/2016 11:37:00 pm
Masaa machache baada ya Kamanda mkuu wa polisi Charles Mkumbo kutangaza kuwepo kwa kikundi kinachotaka kufanya vurugu mkoani hapo ,polisi wamemshikilia diwani wa chadema kata ya Sombetini Ally Bananga kwa tuhuma za kufanya uchochezi

Diwani huyo alishikiliwa juzi na polisi baada ya video zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazomuonesha akihamasisha maandamano ya UKUTA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo, amekiri kukamatwa kwa Diwani huyo na kusema  kuwa diwani huyo anatuhumiwa kwa kosa la kufanya uchochezi hivyo atapandishwa kizimbani baada ya uchunguzi kukamilika 

Pia alisema Polisi walienda kufanya uchunguzi nyumbani kwa diwani huyo na hana taarifa kilichopatikana ila upelelezi bado unaendelea kufanyika na utakapomalizika watapeleka jalada la kesi kwa mwanasheria wa serikali 

 Upande wa wawakili anayesimamia kesi hiyo ya Mwanasheria na Diwani , James Lyatu ameliambia amesema kuwa mpaka sasa diwani huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwaajili ya mahojino hivyo wanasubiri muda wowote kwenda mahakamani 

Pia alisema baada ya polisi kwenda nyumbani kwa diwani huyo wameweza kuchukua Fulana ya diwani huyo iliyokuwa imeandikwa "UKUTA "

"Diwani yuko salama nimemuona ,tunasubiri upelelezi utakapokamilika wamfikishe mahakamani,"alisema James

Licha ya kuwepo kwa taarifa za kutafutwa kwa Mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha ,Amani Golungwa na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,mwenyekiti huyo nae amesema amesikia taarifa hizo japo yeye hazijui ukweli wake 

Pia alisema kukamatwa kwa kiongozi huyo haiwezi kurudisha nyuma mipango yao ya kufanya maandamano kupinga udikteta wa rais Magufuli hivyo kama chama wako mbele kuendelea na mipango yao 

Alisema serikali ijiandae kwa matukio ya mfululizo kuendea mosi septemba na kwamba hawataacha walichodhamiria mpaka pale serikali itakapokuwa tayari kusikiliza madai yao 

"UKUTA si tu kwa viongozi hata wananchi wanapenda mabadiliko na wanaunga mkono maandamano hayo ,hivyo hta wakikamata viongozi wote ,bado UKUTA iko paleplae ,"alisema Amani 

Pia alisema kwa kanda ya kaskazini wamejianda vyema kuendea siku hiyo ya septemba 1 hivyo hawana hofu na lolote.

VIFAHAMU VYAKULA VINAVYOONGEZA AFYA YA AKILI.

8/23/2016 04:41:00 pm

Hivi ni baadhi ya vyakula vya kuongeza afya ya Akili.


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Afya ni hali ya kuwa na uzima kimwili,kiakili na kijamii (kimahusiano na kiuchumi) .Afya ya akili ni pale mtu anapoweza kufahamu uwezo wake na kustahimili mfadhaiko (stress) unaotokana na dhiki au matatizo ya kawaida ya kimaisha.

Afya ya akili inamuwezesha mtu kufanya kazi yenye kuleta mafanikio na kuchangia masuala tofauti katika jamii yake.

Lishe duni ni moja kati ya mambo yanayoathiri Afya ya akili na kusababisha udumavu wa akili.

Udumavu wa akili huchangia kuzorota kwa elimu kwa watoto hali inayoathiri uwezo wa kufundishika wanapokua darasani hivyo ufaulu wa mitihani kuwa duni .

Tanzania asilimia 42% ya watoto na vijana wanakabiliwa na tatizo la udumavu wa akili idadi ambayo ni kubwa hivyo kuhitaji juhudi za familia,jamii,taifa na serikali kuboresha lishe na kufanya uhamasishaji na utoaji elimu juu ya umuhimu wa lishe.

Viko baadhi ya vyakula vinavyosaidia kukua kwa akili ya ubongo ama afya ya akili ambavyo vitakusaidia .

 Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu,Ulaji wa samaki wenye minofu kama Samoni (salmon) na dagaa.Utaweza kupata faida hiyo kwasababu samaki hawa wana mafuta aina ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

Pilipili huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kikubwa cha Vitamini C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo,pilipili inaaminika kuwa na kiwango kikubwa cha Vitamin hiyo kuliko hata machungwa .

 Mbegu za maboga zina kiwango kikubwa cha Zinc ambayo husaidia kuongeza kumbukumbu (Memory) .

Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga mojawapo ni kuzikaanga na kuzila kama karanga ukila kiasi cha kiganja kimoja cha mkono inakua vizuri kwa afya.

Nyanya ni muhimu sana kwasababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na virutubisho aina ya Lycopene chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea.

Hivyo ulaji wa mara kwa mara wa nyanya unaweza kukupa kinga ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya akili .

Brokoli ni mboga ya majani aina Fulani kama maua ya maboga yana faida sana kubwa kwenye ubongo ,ina vitamin K na C na inatoa kinga ya mwili .

Vitamini K inahusika moja kwa moja kwenye utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na ubongo.

Karanga za aina zote za vitamin E ambazo huzia tatizo la upotevu wa kumbukumbu zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

Mayai ya Kuku yana Virutubisho aina ya Choline ,kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo ,hivyo kula mayai ya kienyeji utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini.

Ferdinandshayo@gmail.com
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel