Top Menu

VIFAHAMU VYAKULA VINAVYOONGEZA AFYA YA AKILI.


Hivi ni baadhi ya vyakula vya kuongeza afya ya Akili.


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Afya ni hali ya kuwa na uzima kimwili,kiakili na kijamii (kimahusiano na kiuchumi) .Afya ya akili ni pale mtu anapoweza kufahamu uwezo wake na kustahimili mfadhaiko (stress) unaotokana na dhiki au matatizo ya kawaida ya kimaisha.

Afya ya akili inamuwezesha mtu kufanya kazi yenye kuleta mafanikio na kuchangia masuala tofauti katika jamii yake.

Lishe duni ni moja kati ya mambo yanayoathiri Afya ya akili na kusababisha udumavu wa akili.

Udumavu wa akili huchangia kuzorota kwa elimu kwa watoto hali inayoathiri uwezo wa kufundishika wanapokua darasani hivyo ufaulu wa mitihani kuwa duni .

Tanzania asilimia 42% ya watoto na vijana wanakabiliwa na tatizo la udumavu wa akili idadi ambayo ni kubwa hivyo kuhitaji juhudi za familia,jamii,taifa na serikali kuboresha lishe na kufanya uhamasishaji na utoaji elimu juu ya umuhimu wa lishe.

Viko baadhi ya vyakula vinavyosaidia kukua kwa akili ya ubongo ama afya ya akili ambavyo vitakusaidia .

 Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu,Ulaji wa samaki wenye minofu kama Samoni (salmon) na dagaa.Utaweza kupata faida hiyo kwasababu samaki hawa wana mafuta aina ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.

Pilipili huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kikubwa cha Vitamini C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo,pilipili inaaminika kuwa na kiwango kikubwa cha Vitamin hiyo kuliko hata machungwa .

 Mbegu za maboga zina kiwango kikubwa cha Zinc ambayo husaidia kuongeza kumbukumbu (Memory) .

Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga mojawapo ni kuzikaanga na kuzila kama karanga ukila kiasi cha kiganja kimoja cha mkono inakua vizuri kwa afya.

Nyanya ni muhimu sana kwasababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na virutubisho aina ya Lycopene chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea.

Hivyo ulaji wa mara kwa mara wa nyanya unaweza kukupa kinga ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya akili .

Brokoli ni mboga ya majani aina Fulani kama maua ya maboga yana faida sana kubwa kwenye ubongo ,ina vitamin K na C na inatoa kinga ya mwili .

Vitamini K inahusika moja kwa moja kwenye utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na ubongo.

Karanga za aina zote za vitamin E ambazo huzia tatizo la upotevu wa kumbukumbu zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

Mayai ya Kuku yana Virutubisho aina ya Choline ,kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo ,hivyo kula mayai ya kienyeji utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini.

Ferdinandshayo@gmail.com
Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel