Top Menu

TBS: PIGA VITA BIDHAA HAFIFU

9/30/2016 07:08:00 pm
Na.Vero Ignatus  Arusha.

Imebainika kuwa nchi ya Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la uwo wa bidhaa duni na zenye viwango hafifu,ambapo tatizo hilo linanmadhara makubwa siyo tu kwa walaji au watumiaji wa bibdhaa au hudhuma hizo bali pia lina athari kubwa sana katika ukuaji wa uchumi wa nchi .
Mkuu wa Walaya ya Ngorongoro Rashid Taka ambaye amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha katika mkutano wa majadiliano kuhusu uboreshaji wa utekelezaji wa matakwa ya viwango uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha kimataifa (AICC) ukumbi wa Twiga.


 Ameyasema hayo mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka ambaye   alikuwa  amemuwakilisha mkuu wa mkoa wa ARusha Mrisho  Mashaka  Gambo.katika mkutano wa majadiliano kuhusu uboreshaji wa utekelezaji wa matakwa ya viwango uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha kimataifa (AICC) na kuwashirikisha wadau mbalimbali wanaohusika katika utekelezaji na usimamiaji wa maswala yahusuyo utekelezaji wa matakwa ya viwango waliohudhuria mkutano huo.

Amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa wadau wa maswala ya viwango kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuthibiti uzalishaji wa uwepo wa bidhaa duni nchini ,hivyo hatua ya kujadili na kukubaliana mikakati ya pamoja katika eneo hilo litaleta mazingira mazuri  ya kiutendaji yasiyo na muingiliano au mgongano wa kimaslahiikiwemo pia kulinda  mazingira hivyo kupata matumizi endelevu na kuiepusha jamii na athari za kiafya zitokanazo na utumiaji wa bidhaa duni zisizo na viwango.

"Jambo hili linahitaji ushirikishwaji mpana wa wadau katika upigaji vita upambanaji na uzalishaji wa bidhaa hafifu,hii ni vita yetu sote Watanzania wote kwa ujumla,inatakiwa hata mgeni anapokuja nchini mwetu atambue yakuwa sisi ni watu  wa Viwango" alisisitiza Rashid mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.

Akizungumza katika mkutano huo kaimu mkurugenzi wa Mamlaka  ya kupima viwango vya ubora nchini ( TBS  ) Dokta Egid Mabofu  amesema  kuwa lengo la kuwa na mkutano huu  ni pamoja na  kuwaleta wadau wa utekelezaji wa matakwa ya viwango hapa nchini ili kujadili mambo muhimu yanayohusiana na viwango, 

" kufanya muendelezo  wa meza ya majadiliano  mkutano  kama huu umeshafanyika katika mikoa mitatu ambayo   ni pamoja na  Dar-es salaam,Mtwara,Tanga na leo hii tupo Arusha kwa nia ileile  hatuhitaji tena Nchi yetu iwe na bidhaa duni ambazo mwisho wasiku hupelekea madhara na kuathiri afya zetu" alisisitiza  Mabofu.

Kwa upande wake  wa muwakilishi  wa Shirika la mazingira la Umoja wa
 wa Mataifa (UNEP) CLara  Makenya amesema kuwa hawakubaliani na bidhaa zisizokuwa na viwango ndiyo maana wao pamoja na Shirika  linalosimamia viwango nchini Tanzania wameonelea kuwa na mkutano wa pamoja na Taasisi zote zinazojihusisha na kusimamia na kuthibiti viwango ili kupata suluhu juu ya uzalishaji wa bidhaa zisizokuwa na viwango ambazo pia zinaharibu mazingira kwa ujumla.

Aidha mkutano huo wa siku moja umewashirikisha wadau kutoka Mamlaka za usimamiaji wa viwango,Wizara mbalimbali,Polisi,Taasisi za elimu na Utafiti,Watumiaji wa huduma na bidhaa,wazalishaji wa bidhaa,Taasisi ya Sekta Binafsi nchini,Shirikisho la wafanyabiashara na Taasisi ukuzaji biashara.

 
Meneja viwango (Tbs)  Mary  Meela ambaye pia ni mratibu mradi  akizungumza na wanahabari juu ya mradi huo ambao umefadhiliwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Shirika la viwango Tanzania (TBS).Picha na Vero Ignatus.

 
Muwakilishi wa Shirika la Mazingira Umoja wa Mataifa  Clara Makenya akifafanua jambo kwa wanahabari kuhusu uhafifu wa bidhaa ,mazingira .Picha na Vero Ignatus.
 
Baadhi ya wadau wa waliohudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu uboreshaji wa viwango wakifuatilia mazunguzo kwa makini.Picha na Vero Ignatus.
 
Wakwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka ,aliyepo katikati ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akifuatiwa na Mary Meela ambaye ni Meeja viwango (Tbs )na mratibu wa mradi huo.
 
Baadhi ya wadau wa mkutano wa majadiliano kuhusu uboreshaji wa utekelezaji wa matakwa ya viwango uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa (AICC) wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo wa siku moja.

TBS: PIGA VITA BIDHAA HAFIFU

9/30/2016 07:06:00 pm
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo katika mkutano wamajadiliano kuhusu uboreshwaji wa wa matakwa ya viwango uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha kimataifa( AICC) Katika ukumbi wa Twiga.Picha na Vero Ignatus.

Na. Vero Ignatus Arusha. 

Imebainika kuwa nchi  ya Tanzania inakabiliwa na tatiazo kuwa la kuwa na bidhaa duni na zenye viwango hafifi,ambapo tatizo hialpo lianamadhara makubwa  siyo kwa mlaji au watuamiaji bidhaa au huduma hizo bali pia lina athari kubwa sana katika ukuaji wa uchyumi wa nchi.
Ameyasema hayo mkuu wa wilaya ya Ngrorongoro Rashid Taka ,ambaye alikuwa anamuwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo katika mkutano wa siku moja wa majadiliano kuhusun uboreshwaji wa utekelezaji wa matakwa ya viwango uliofanyioika katika Kituo cha Mikutano cha kimataifa (AICC)na kuwashirikisha wadau mbalimbali katika utelkelezaji wa usimamiaji wa matakwa ya viwango waliohudhuria katika mkutano huo.

A mesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa wa wadau wa maswala la viwango klufanya kazi kwa ushirikiano ili kuthibiti uzalishaji wa uwepo wa bidhaa duni nchini,hivyo hatua ya kujadili na na kukubaliana miakakati ya pamoja katika eneo hilo litaleta mazingira mazuri ya kiutendaji yasiyokuwa namuingiliano aua mgongano wa kimaslahi  ikiwepo pia kulinda mazingira hivyo kupata matumizi endelevu na kuiepusha jamii na atahari za kiafya zitokanazo na utumiaji wa bidhaa duni zisizo na viwango.
.
"Jambo hili linahitaji ushirikishwaji mpana wa wadau katika upigaji vita upambanaji na uzalishaji wa bidhaa hafifi,hii ni vita yetu sote na watanzania wote kwa ujumla inatakiwa hata mgeni akija nchini mwetu atambue ya kuwa sisi ni watu wa viwango"alisisistiza Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.

Akizungumza na  katika mkutano huo kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya kusimamia na kupima viwango vya ubora nchini (TBS) Dokta Egid Maofu amesemakuwa lengo la kuwa lengo la kuwa na mkutanohuo hapa nchini kuwaleta wadau wa utekelezaji wa matakwa ya viwango hapa nchini ili kujadili mambo ya muhimu yanayohusiana na viwango.

"Kufanya muendeklezo wa meza ya majadiliaano mkutano kama huu umefanyika katika mikoa mitatu ambayo ni ambayo ni pamoja na Dar-es salaam,Mtwara,Tanga na hivi tupo Arusha ka nia ileile ya hatuhitaji tena nchi yetu iwe na bidhaa duni ambazo mwisho wasiku hupelekea madhara na kuathiri afya zetu" alisisitiza Mabofu.

Kwa upande wake muwakilishi wa shirika la Umoja wa mataifa la mzaingira Clara Makenya (UNEP)amesema akuwa hawakubalianai na bidhaa zisizokuwana viwango ndiyomaana wao kwakushirikiana na (TBS) wameonelea kuwa na mkutano wa pamoja taasisi,na wadau wote wanaojihusisha na kusimamaia na kithibiti viangoviwango ilikupatasuluhi juu ya uzalishaji wa bidhaa zisizokuwa na viwango ambazo pia zina athiri mazingira kwa ujumla.

Aidha mkutano huo wa siku moja umewashirikisha wadau kutoka Mamlaka za usimamiaji wa viwango,Wizara mbalimbali,polisi,Taasisi za elimu na utafiti,Watumiaji wa huduma na bidhaa,Taasisi ya sekta binafsi nchini,Shirikisho la wafanyabiashara na Taasisi za ukuzaji biashara. 
Meneja wa viwango( TBS) Mary Meela ambaye pia ni mratibu mradi akizungumza na wanahabari juu ya mradi huo ambao umefadhiliwa na Shirika la Mazingira la Umoja wa mataifa( UNEP)KWA KUSHIRIKIANA NA Mamlaka ya viwango Tanzania (TBS).Picha na Vero Ignatus.Muwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa( UNEP) Clara Makenya akifafanua jambo kwa wanahabari kuhusu uhafifu wa bidhaa na mazingira .Picha na Vero Ignatus.

Wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka,aliyepo katikati ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akifuatiwa na Meneja viwango (TBS) na Mratibu wa mradi huo Mary Meela wakibadilisha na mawazo .Picha na Vero Ignatus.
Baadhi ya wadau wa mkutano wa majadiliano kuhusu uboreshaji wa matakwa ya viwango uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha kimataifa (AICC) wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo wa siku moja. Picha na Vero Ignatus.Mapokezi ya Maalim Seif Buguruni yaota mbawa

9/30/2016 05:10:00 pm


Mapokezi makubwa yaliyopangwa kufanyika leo  jijini Dar es salaam ya kuwapokea Wajumbe wa Baraza Kuu la CUF na  Kamati ya Uongozi ya chama na Katibu Mkuu Maalim Seif yameota mbawa kufuatia kusitishwa  kwa hofu ya kutokuwepo usalama.

Mapema jana, ilitangazwa kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, wajumbe wa baraza kuu la CUF na kamati ya uongozi ya chama wangefanyiwa mapokezi makubwa katika ofisi hizo lakini yaliahirishwa ghafla baadaye usiku kwa kuhofia kuwapo vurugu.

Kiongozi wa wabunge wa CUF waliokuwa wameandaa mapokezi hayo, Riziki Shahari alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa wameahirisha mapokezi hayo baada ya kujiridhisha kuwa hali ya usalama siyo nzuri.

“Tunazo taarifa kuwa yapo makundi hatari ya watu yanayoishi ndani ya ofisi huku yakilindwa na vyombo vya dola tangu ofisi hiyo iporwe na aliyewahi kuwa mwanachama na kiongozi wa juu wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akishirikiana na watu wanaomuunga mkono.

 “Tunajipa muda wa kushauriana na viongozi wa juu wa chama chetu huku tukiwaomba wanachama wote walioko Dar, mikoani na Zanzibar wawe watulivu kwani chama kina viongozi makini na hawawezi kuwa tayari kuona maisha ya wanachana na viongozi yanahatarishwa kwa kuigeuza ofisi kuu kuwa uwanja wa mapambano,” alisema Shahari.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro alisema wabunge 41 kati ya 43 wa CUF walioandaa mapokezi hayo walikuwa wamekwishafika Dar es Salaam, lakini wamechunguza na kubaini kuwa yangeleta maafa.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF – Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema pamoja na hayo, chama hicho kimeshamalizana na Profesa Lipumba na kusisitiza kuwa si mwanachama tena.
 

Chadema Waahirisha Tena Maandamano ya Oparesheni UKUTA

9/30/2016 05:01:00 pm


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe ametangaza kuwa Operesheni UKUTA iliyokuwa ifanyike Oktoba Mosi haitofanyika tena.

Mbowe amesema hayo leo baada ya kimya cha muda mrefu tangu kuahirishwa kwa maandamano Septemba Mosi. Aidha, Mbowe amesema kuwa hawatataja tarehe ya kufanya maandamano ili kutompa adui nafasi ya kujipanga. Amesisitiza kuwa maandamano yapo, ila tarehe hawataweka hadharani.

Operesheni hii ilikuwa ifanyike Septemba Mosi mwaka huu lakini iliahirishwa ili kuwapa nafasi viongozi wa dini kuweza kukutana na kujadiliana na Rais Dkt Magufuli juu ya mustakabali wa hali ya kisiasa nchini kufuatia kuzuiwa kwa shughuli mbalimbali za kisiasa.
Hadi leo viongozi wa dini bado hawajakutana na Rais Magufuli licha ya wao kueleza kuwa Rais Magufuli hajakataa kukutana nao kama inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari

Simbachawene Wakaguzi wandani kuweni makini.

9/27/2016 05:45:00 pm

Waziri George  Simbachawene akizungumza na wakaguzi wa ndani katika mkutano unaoendelea kwa siku tatu katika kituo cha kimataifa cha mikutano (AICC)Katika ukumbi wa Simba.
Waziri George  Simbachawene akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) Aliyepo kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,aliyeko kushoto kwa waziri ni Mkuu wa wakaguzi wa ndani Mohamed Mtonga,akifuatiwa na aliye kulia kwake ambaye ni Rais wa wakaguzi wa ndani Richard Magongo akifuatiwa na makamu wa rais wa wakaguzi wa ndani Gabriel Mwero.
Waziri George  Simbachawene akiwasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) Aliyepo kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,aliyekokulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,aliyeko  kushoto kwa waziri ni Mkuu wa wakaguzi wa ndani Mohamed Mtonga,akifuatiwa na aliye kulia kwake ambaye ni Rais wa wakaguzi wa ndani Richard Magongo akifuatiwa na makamu wa rais wa wakaguzi wa ndani Gabriel Mwero.
Waziri Simbachawene  akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,aliyepo pembeni yake ni Mkuu wa wakaguzi wa ndani Mohamed Mtonga.
Rais wa wakaguzi wa ndani Richard Magongo akizungumza na wakaguzi katika mkutano wa siku tatu ulioanza leo katika kituo cha kimataifa cha mikutano( AICC) katika ukumbi wa Simba.


Waziri Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na wakaguzi wandani nchini Tanzania.
 .Na. Vero Ignatus Arusha.

Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tawala za serekali za mitaa na TAMISEMI George Simbachawene amewataka wakaguzi wa ndani katika  halimashauri hapa nchini kuhakiksha wanasimamia kwa umakini mapato ya halimashauri ili kuchochea chachu ya maendeleo.

Waziri Simbachaweni ameyasema hayo leo hii kituo cha kimataifa cha mikutano (AICC)katika  ukumbi wa Simba katika mkutano wa siku tatu ulioanza leo katika  wa mkutano wa 10  wa wakaguzi wa ndani  ambao uilofanyika jijini hapa ikiwa na lengo la wakaguzi hao wa ndani kuangalia njia muafaka za kukubiliana na changamoto wanazokubiliana nazo.

Amesema kuwa wakaguzi wa ndani katika halimashauri zetu ni watu muhimu sana katika kuangalia hali ya miradi inayoendeshwa na halmashauri kwa maana miradi mingi inafanywa na halmashauri zetu na hivyo kupelekea kuingiziwa pesa nyingi.

Aidha waziri huyo wa TAMISEMI amesema kuwa kwa sasa wameagiza katika halmashauri zote kuhakisha kuwa wakaguzi wa ndani wanakuwa na bajeti yao inayojitegemea tofauti na halmashauri ili kuweza kuboresha hali ya utendaji wao,


Aidha kwa upande wake Raisi wa chama cha wakaguzi wa ndani nchini Tanzania  (IIA)  Richard  Magongo amesema kuwa mkutano huo wa kumi utakwenda sambamba na kushereke miaka kumi tangu kuanzishwa kwa kwa taasisi ya ukaguzi wa ndani.

Amesema kuwa katika mkutano huo wa siku tatu mada mbali mbali zitajadiliwa ambazo kwa kiwango kikubwa kitawqeza kuwasaidia wakaguzi wa ndani katika kuboresha ufanisi wao wa kazi za ukaguzi.

Pamoja na hayo ametoa shukurani kwa Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kusikia kilio chao cha siku nyingi kwa kuweka ofisi
ya mkaguzi mkuu wa ndani Serekalini na amesema kuwa katika kuadhimisha miaka hii 10 ya taasisi ya wakaguzi tangia ianzishwe amewaomba wakaguzi waangalie kama kuna mahali kuna kasoro yeyote  wafanyie marekebisho .

Sambamba na hayo wakaguzi wa ndani  wamechangia shilingi milioni tano (5,000,000 )kwaajili ya waathirika  wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera huku Waziri Simbachawene nae akiwaunga mkono kwa kuchangia shilingi laki tano(500,000) taslimu

WATOTO 4000 HUZALIWA NA VICHWA VIKUBWA.

9/27/2016 03:00:00 pm

Kaimu mkurugenzi wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma akimuonyesha mkuu wa wilaya  ya Arusha
Gabriel Daqarro sehemu ambayo mtoto D0rcus John( miezi2 )amefanyiwa upasuaji wa kichwa.


 Mkuu wa wilaya ya Arusha akiwasili katika hospitali ya Mount Meru iliopo jijini Arusha tayari kwakwenda kuangalia watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa
 Mkuu wa wilaya ya Arusha akiwasili katika hospitali ya Mount Meru iliopo jijini Arusha tayari kwakwenda kuangalia watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa


  Kaimu mkurugenzi wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma akiwa anampa mkuu wa wilaya ya Arusha maelekezo ya picha inayoonyesha jinsi mtoto Praise Gudluck( miezi 9) alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro  akiwa katika picha ya pamoja na  Kaimu mkurugenzi wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma ,pamoja na( RMO)Fridah Mbokiti,na baadhi ya timu ya GSM Foundation.


Na Vero Ignatus , Arusha
Imebainika kuwa jumla ya watoto ya 4000 wanazaliwa kila mwaka na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi na kati ya hao ni watoto 500 tu ndio wanafikishwa hospitalini kwa ajili ya upasuaji huku wengine 3500 awajulikani wanapopelekwa.

Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma wakati akiongea na waandishi Wa Habari Mkoani hapa.
Alisema kuwa  wao kama taasisi ya moi walikaa chini na kuona kuna watoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya garama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho sivyo.
Alibainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 ambayo ni awamu ya kwanza na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.
"Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 atujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma.

Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji Wa kichwa Nasson Daniel 17 aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman 17aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada . 
"Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa mud a mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto ,tusisikilize dhihaka za watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa kinaendelea kupungua ,tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.
Naye mkuu Wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa wito kwa jamii hususa ni wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto anapona kabisa .
Alisema anapenda kuwashukuru madaktari hawa walioibua na kuangalia namna gani wanaweza kusaidia watoto  hawa pamoja na shirika la GSM foundation ambao ndio waliothamini Huduma hii ya upasuaji bure  ambapo alisema kwa upande wa Arusha jumla ya watoto 35 wameonwa huku watoto sita wakiwa wamekishwa fanyiwa upasuaji.

JUMLA YA WATOTO 4000 WANAZALIWA NA TATIZO LA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI KILA MWAKA HAPA NCHINI TANZANIA

9/26/2016 11:25:00 pm
Kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma akimuonyesha mkuu wa wilaya  ya Arusha
Gabriel Daqarro sehemu ambayo mtoto D0rcus John (miezi 2)amefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa .


 kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma akiwa anampa mkuu wa wilaya ya Arusha maelekezo ya picha inayoonyesha jinsi mtoto Praise Godluck (miezi 9 )alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji.

Mkuu wa wilaya ya Arusha akiwa kwenye picha ya pamoja na  Maimu mkurugenzi wa Moi RMO na wawakilishi kutoka kampuni ua GSM katika hospital ya Mount Meru .
Na.Vero Ignatus ..Arusha 

Jumla ya watoto 4000 wanazaliwa kila mwaka na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi na kati ya hao ni watoto 500 tu ndio wanafikishwa hospitalini kwa ajili ya upasuaji huku wengine 3500 awajulikani wanapopelekwa.

Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma wakati akiongea na waandishi Wa Habari Mkoani hapa.
Alisema kuwa  wao kama taasisi ya moi walikaachini na kuona kunawatoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya garama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho sivyo.
Alibainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 ambayo ni awamu ya kwanza na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.
"Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 atujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma
Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji Wa kichwa Nasson Daniel 17 aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman 17aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada .
"Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa mud a mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto ,tusisikilize dhihaka za watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa kinaendelea kupungua ,tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.
Naye mkuu Wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro ametoa wito kwa jamii hususa ni wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto anapona kabisa .

Mrisho Gambo, afanya mazungumzo na ujumbe kutoka nchini China

9/26/2016 08:35:00 pm
Na Vero Ignatus .Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka  nchini China , waliotaka kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo Mkoani Arusha,mzungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake hvi karibuni.

Amewahakikishia kuwapa ushirikiano,mazingira mazuri  na usalama kwa wawekezaji kutoka China watakaofika kuwekeza katika Mkoa wa Arusha, na watakapoitaji msaada wowote kutoka Serikalini basi watapatiwa kwa wakati.


“Kwa Mkoa wa Arusha mtapata ushirikiano wakutosha kutoka Serikali na mtakapoitaji msaada sehemu yoyote katika utendaji wenu wa kazi basi msisite kuwasiliana nasi na tutawasaidi”,alisema Gambo.


Aidha mjumbe kutoka ubalozi wa China kwa Tanzani bwana Gou Huodong,amemwakikishia Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuwa ataenda kuwahamasisha wachina wengine waliopo China kuja kuwekeza zaidi Mkoani Arusha hasa kwenye sekta ya Utalii ambayo ndio inayokuwa kwa kasi sana na inaongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa.


“Nitaenda  kuwahamasisha wenzangu huko China waje kwa wengi hapa Mkoani Arusha kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbalia hasa ya Utalii kwasababu sekta hii inakuwa kwa kasi sasa,”alisema Gou.


Pia Muheshimiwa Gambo aliwaelezea mpango wakufunga Kamera za barabarani(CCTV) kwa Mkoa wa Arusha ilikuimalisha zaidi ulinzi na Usalama hasa kwa wawekezaji na watalii wanaoingia katika Mkoa huu, na hivyo kuwaomba waangalie hiyo fursa kwa upande wao iliwaisaidie Serikali katika kuimalisha ulinzi wake maeneo mbalimbali ya Mkoa.


Ugeni huu kutoka ubalozi wa China hapa nchini ulikuwa na lengo kubwa lakuweza kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo katika Mkoa wa Arusha, kwakuwa wageni wengi kutoka China waliofika katika Mkoa wa Arusha walikutana na mazingira mazuri ya uwekezaji.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka  nchini China , waliotaka kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo Mkoani Arusha,mzungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake.Picha na Vero Ignatus.Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipeana mkono na mjumbe kutoka ubalozi wa China nchini Gou Huodong kama ishara ya ushirikiano baina ya China na Mkoa wa Arusha.Picha na Vero Ignatus.

Nyuki Mabingwa Qambalo CUP Karatu

9/26/2016 08:06:00 pm
Na.Vero Ignatus.. Karatu.
TIMU ya soka ya Nyuki ya Mang'ola wilayani Karatu mkoa wa Arusha , juzi imetwaa ubingwa wa Soka katika michuano ya Qambalo CUP iliyoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo,Willy Qambalo baada ya  timu ya mwendokasi magoli 2-1.
Katika michuano hiyo, ambayo ilishirikisha jumla ya timu 55 na wachezaji 1350 kutoka wilaya hiyo ya Karatu, Mabingwa walizawadiwa na Mbunge wa jimbo jimbo  hilo, fedha taslimu sh 400,000 na seri ya jezi.
Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa uwanja wa Karatu, Washindi wa pili walizawadiwa seti ya jezi,mpira na fedha taslimu sh 200,000 wakati mshindi wa tatu  Beach BOYA BOYS
Katika mchezo huo wa  fainali, Nyuki ndio walikuwa wa kwanza kupata gari dk ya 21 goli lilifungungwa na Said  Mustapha  na mwendekasi walisawazisha Dk ya 25 kupitia Nassoro Haji.

Wakicheza kwa kushambulia, nahodha wa timu ya Nyuki  Sadamu Juma alifunga goli la pili dakika ya 33 kwa shuti kali goli lililodumu hadi mwisho wa mchezo.
Katika michuano hiyo, timu 12 zilipewa zawadiu ya seti ya jezi na mipira baada ya kuingia robo fainali katika michezo iliyochezwa kwenye kata zao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi, Qambalo alipongeza washindi na kuahidi timu bingwa na mshindi wa pili watapata fursa ya kutembelea bungeni Dodoma.
Hata hivyo, alisema michuano hiyo ni utekelezaji wa ahadi zake, katika kuendeleza michezo katika wilaya hiyo ambapo michezo ilikuwa nyuma.
Mwenyekiti wa halmashauri Karatu, Jubilate Mnyenye aliahidi pia kuandaliwa kwa mashindano mengine makubwa ili kuendeleza michezo katika wilaya hiyo.

Katibu na Mbunge wa Karatu, Stivin Siay akikabidhi zawadi ya seti ya jezi kwa nahodha wa timu ya beach boys baada ya kushika nafasi ya tatu.
Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halamashauri ya Karatu Jubilate akikabidhi zawadi kwa washindi hao.

Nahodha wa timu ya Nyuki Sadam Juma akikabidhiwa kikombe na mbunge wa jimbo la Karatu, Willy Gambalo  baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya Qambalo CUF.


CHADEMA YALAANI DIWANI KUSWEKWA RUMANDE

9/26/2016 04:47:00 pm


Na. Vero Ignatus

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Wilaya ya Arumeru Mashariki kimelaani vikali kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexender Mnyiti kumuweka rumande Diwani wa Kata ya Embaseny Gadieli Mwanda  kwa saa 48 na kudai kuwa kitendo hicho ni matumizi mabaya ya madaraka.

MKUTANO WA WADAU WA WATALII WAFANYIKA ARUSHA

9/23/2016 08:39:00 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na Wadau wa Utalii katika kikao cha siku moja kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa( AICC)Katika ukumbi wa Mbayuwayu Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus.
Na Vero Ignatus Arusha.

Mkutano wa siku moja wa umefanyika Mkoanin Arusha huku wadau w utalii wakiiitaka serikali kuweza kuainisha kodi zote na  kuweka katika mfumo mmoja  ili kuweza kuepuka usumbufu unaojitokeza Mara kwamara pindi wageni wanapokuwa katika matembezi yao.

Wadau hao wamesema kuwa  kodi hizo waotozwa katika sehemu mbali hususa ni  katika mageti  ambayo  wanaingilia watalii mbugani kwani hivi sasa kumekuwepo na kodi nyingi ambazo zinaleta usumbufu kwa wageni ambapo wanasimamishwa kila mahali kwa mud a mrefu na kushindwa kufurahia utalii wanaoukuja kuufanya nchini hapa
Mwenyekiti wa TATO Wilbroad Chamulo akizungumza na wadau  utalii walipokutana na Mkuu wa mkoa kujifanyia  Tathimini,kuangalia fursa zilizopo katika utalii pamoja na Changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika Utalii.       Picha na Vero Ignatus.


Kwa upande wake  mwenyekiti Wa chama cha wasafirishaji Wa utalii (TATO) Wilbroad chambulo wakati akiongea katika kikao cha wadau wa utalii kilichoandaliwa na mkuu Wa mkoa Wa Arusha cha kujadili changamoto na tathimini zinazokabili sekta hiyo .

Aliongeza kuwa mgeni anapofika nchini anatakiwa kupokelewa kama mfalme sio kusumbuliwa kwa kuwekwa mda mrefu katika viwanja vyetu vya ndege kwani inawakatisha tamaa na kujutia kuja kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini.

"Unakuta mgeni anakuja akifika kiwanja cha ndege anakaa zaidi ya lisaa limoja na nusu kwenye foleni akisubiria visa kweli huu ni usumbufu ,tunatakiwa mgeni akija hapa tumpokee kwa tabasamu ikiwezekana tumtandikie zulia jekundu ili akienda kwao atangaze nchi yetu na utalii wetu kwa ujumla "alisema Chambulo. 

Pia ameitaka serekali  ifutilie na ishughulike na utozwaji Wa ada za kodi zinazotozwa na mageti ya wilaya ya Monduli pamoja na geti la wilaya ya Ngorongoro.

"Serekali na Wadau wote tunatakiwa kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha ulinzi na usalama Wa watalii na Mali zao unaimarishwa zaidi"alisema 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa mkutano huo ameuita ilikuwaleta pamoja kushiriki na kujadili namna gani watakuza utalii na kuboresha utalii katika mkoa Wa Arusha kwa ujumla na iwapo watashirikiana kwa pamoja itasaidia pia kukuza mapato na kuwa maradufu zaidi.

Amesema nivizuri Wadau Wa utalii wakashirikishwa kwa  mabadiliko yoyote ya ongezeko la kodi ili baadae kusiwepo na malalamiko ya kuegemea upande mmoja.

Ameongeza kuwa wao kama mkoa wanamkakati Wa kifunga CCTV katika maeneo mbalimbali ya mkoa ili kuzibiti uhalifu wanaofanyiwa watalii au wageni wanaotembelea mkoa wetu pamoja na vivutio vilivyopo Mkoani apo.
Mmiliki wa Leopard Safari Faisal Zuhery akichangia jambo katika mkutano huo wa siku moja wa wadau wa Utalii Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus.


Katika mkutano huo mambo mambali mbali yaliathimiwa ikiwemo kuitaka serekali na Wadau Wa utalii kuweka mikakati ya ulinzi na usalama pamoja na kuangalia jinsi ya kuzuia ujangili.
Baadhi ya wadau wa Utalii wakiwa katika kikao cha siku moja kilichoitishwa na mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo wakiwa wanasikiliza kwa makini mjadala ulivyokuwa   ukiendelea,ambapo mwisho wakikao walipeana maazimio ya kufanyia kazi ili watakapo kutana tena waweze kuleta mrejesho wa majukumu waliyopeana.     Picha na Vero Ignatus.MKUTANO WA WADAU WA UTALII KUFANYIKA ARUSHA KESHO

9/21/2016 01:50:00 pm

Na Vero Ignatus Arusha

 Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne  Maghembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa siku moja wa  wadau wa sekta ya Utalii mkoani Arusha unaotarajiwa kufanyika kesho.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.akisisistiza jambo wakati akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani)ofisini kwake Jijini Arusha, kuhusiana na mkutano wa Wadau wa Utalii utakaofanyika kesho.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake,amesema kuwa mkutano kama huo ulifanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2012 hivyo wameona ni vyema serikali kushirikiana na wadau wa utalii kukaa pamoja kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili  ili kuboresha sekta hiyo,ambayo asilimia 80% ya watalii wanaoingia nchini hufika mkoani hapa .

Amesema kuwa mkoa wa Arusha ni kitovu cha cha utalii na unachangia pato la mkoa kwa asilimia20% na kitaifa kwa asilimia 17%ambapo mwaka 2015 idadi ya watalii iliyoingia nchini ilikuwa 1,137,182 na kuingizia Taifa kiasi cha dola za kimarekani 1.9 milioni,katikaq idadi hiyo asilimia 80%watalii walitembelea mkoa  kwasababu ya vivutio vingi vilivyopo mkoani Arusha.

 
Pichani ni Katibu tawala wa Mkao wa Arusha Richard Kwitega akiwa na wadau wa sekta ya Utalii nyuma yake kama wanavyoonekana pichani wakifuatilia kwa makini wakati Mkuu wa mkoa akizungumza na wanahabari kuhusiana na mkutano wa wadau wa utalii utakaofanyika kesho.picha na Vero Ignatus
Amesema kwamba madhumuni ya mkutano huo ni kujadili hali ya maendeleo ya utalii ya mkoa ,fursa zilizopo,mafanikio ,changamoto na kuweka mikakati yakuboresha huduma mbalimbali za utalii ambapo wadau watapata fursa ya kubadilishana mawazo na kuadhimisha siku ya utalii duiaani amabayo huadhimishwa kila mwaka septemba 27.

“Maadhimisho haya ya utalii  mwaka huu yamebeba kauli mbiu UTALII KWA WOTE,Kwa kuzingatia hilo wadau mbalimbali wa sekta hiyo ya utalii zikiwemo TANAPA,NCAA,HAT,TTB,TATO,TTGA,TRA,TACTO Watawasilisjha mada ambazo zitalenga kuboresha utalii,pamoja na kuhakikisha elimu na fursa za Utalii zinaifikia jamiii “ alisisitiza Gambo.

Amesema kuwa wadau watakaoshiriki mkutano huo ni wahifadhi,Wakala wa waongozaji watalii,Wakala wa wausafirishaji watalii,watoa huduma za malazi,Bodi ya Utalii,na Viongozi watendaji wa serikali ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe.

Mkutano huo wa siku moja umefadhiliwa na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA)kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na Ofisi ya Kanda ya Utalii ndiyo waandaaji wa mkutano huo wa wadau mbalimbali wa Utalii Mkoani Arusha
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel