Top Menu

Dawa ya mpango wa uzazi kwa wanaume

10/31/2016 09:17:00 pm
Dawa inanuia kupunguza idadi ya manii
Dawa mpya ya mpango wa uzazi kwa wanaume

Dawa inayotolewa kwa njiya ya sindano imetajwa kama mafanikio makubwa ya njiya ya mpango wa uzazi miongoni mwa wanaume.Watafiti kutoka Marekani wamesema dawa hiyo imefikia asili mia 96 ya mafanikio baada ya kufanyiwa majaribio miongoni mwa wanaume 270. 

Kati ya wanaume hao ni wanne pekee walioweza kuwafanya wenzi zao kutunga mimba. Hata hivyo dawa hiyo imeripotiwa kuwa madhara mengi miongoni mwa wanaume ikiwemo vipele usoni na kuwa na usununu. Watafiti wamekua wakitafuta dawa ya kupanga uzazi ya wanaume kwa miaka 20. 

Wataalamu hao wamekua wakitafuta jinsi ya kupunguza idadi ya manii bila kusababisha madhara ya uzazi. Kimaumbile wanaume hutoa manii kila wakati na wanasayansi wamekua wakitaka kupunguza idadi kutoka milioni 15 hadi milioni moja.
Dawa inanuia kupunguza idadi ya manii  copyright Thinkstock 
Dawa mpya ya mpango wa uzazi kwa wanaume
Utafiti wa dawa hii ulilenga wanaume kati ya umri wa miaka 18 hadi 45, na walio na uhusiano na mwenzi mmoja wa kike. Walishiriki kwenye utafiti huo kwa mwaka mmoja. Walidungwa sindano hiyo na kupunguza idadi ya manii hadi milioni moja. Kisha hawakupokea dawa hiyo ili kubaini kasi ya kuongezeka kwa manii yao hadi milioni 15. 

Baadhi walisema iliwachukua mwaka mmoja kabla ya idadi kamili na inayotakikana kurudi. Baadhi ya madhara kama vile mfadhaiko, usununu, vipele usoni na maumivu ya misuli yalisababisha wanaume 20 kujitoa kwenye utafiti. Mtafiti mkuu wa dawa hii Dkt. Festin amesema wanaangazia njiya nyingine ya kuboresha dawa hiyo ikiwemo kuiotoa kama mafuta.

Rais wa Uganda arudi shambani

10/31/2016 09:09:00 pm
 
Rais wa Uganda arudi shambani
Rais wa Uganda arudi shambani
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amerudi shambani kwake ambapo atakuwa kwa kipindi cha juma moja akikuza kilimo mbali na kusimamia miradi ya serikali katika wilaya ya Lowero.
Rais wa Uganda na msafara wake akielekea shambani
Rais wa Uganda na msafara wake akielekea shambani
Msafara wa rais sasa utakuwa wa baiskeli kwa muda ambayo atatumia kuteka maji ili kunyunyizia mimea.
 
Rais wa Uganda
Rais wa Uganda
Kulingana na msemaji wa serikali,Museveni tayari amekuwa akiwaonyesha wakaazi jinsi ya kupanda migomba na kahawa kwa kutumia chupa za plastiki ili kunyunyizia maji.


chanzo Bbc

Kifo cha muuza samaki chazua maandamano Morocco

10/31/2016 08:59:00 pm
Maandamano baada ya muuza samaki kukanyagwa na lori hadi kufa nchini Morocco
Maelfu wa raia wa Morocco walifanya maandamano wikendi hii katika miji kadhaa baada ya muuza samaki mmoja kukanyagwa hadi kufa na lori la kubeba takataka alipokuwa akijaribu kuchukua samaki wake ambao alikuwa amepokonywa na maafisa wa polisi.

Kifo cha Maouhcine Fikri katika mji wa kaskazini wa Al-Houciema siku ya Ijumaa kilizua hasira kali miongoni mwa raia katika mitandao ya kijamii.
Kifo chake kinafananishwa na kile cha muuza matunda wa Tunisia mwaka 2010 ambacho kilisababisha maandamano makubwa.

Mfalme wa Morocco King Mohammed VI amewaagiza maafisa wake kutembelea familia ya Fikri.

Wizara ya maswala ya ndani pamoja na ile ya Haki zimeahidi kuanzisha uchunguzi

Halmashauri ya manispaa ya Ilala jijini DSM kesho inaanza rasmi Operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara kando ya barabara za mwendo kasi

10/31/2016 08:28:00 pm
SeeBait
Halmashauri ya manispaa ya Ilala jijini DSM kesho inaanza rasmi Operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara kando ya barabara za mwendo kasi kuanzia eneo la Gerezani Kariakoo hadi Fery Kivukoni kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria mbali ya kusababisha usumbufu na ajali kwa watembea kwa miguu.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema akizungumza na waandishi wa habari amesema zoezi hilo litaanza mapema asubuhi na kuwataka wafanyabiashara hao kwenda katika maeneo waliyopangiwa ikiwemo soko Mburahati, Kigogo Sambusa na maeneo rasmi yaliyoainishwa.

Katika eneo la kariakoo chanel ten imeshuhudia adha kubwa kwa wananchi wanaotembea kwa miguu ambapo wanalazimika kupita katikati ya barabara ya magari ya mwendo wa haraka huku magari hayo yakipita kwa kasi na kuhatarisha maisha yao kutokana na wafanyabiashara hao kupanga biashara zao katika njia za watu wanaotembea kwa miguu.

TAARIFA TOKA IKULU JUU KINACHOENDELEA ZIARA YA RAIS MAGUFULI NCHINI KENYA

10/31/2016 06:34:00 pm

Picha 25:RC SHINYANGA AFUNGUA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA KWA WATOA HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

10/31/2016 06:12:00 pm

  

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack
****
Hapa ni katika ukumbi wa mikutano katika Hotel ya Liga mjini Shinyanga ambapo leo Jumatatu Oktoba 31 yameanza kufanyika mafunzo ya lugha ya alama kwa watoa huduma katika sekta za afya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Chama Cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) mkoa wa Shinyanga.

Mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku saba yamefadhiriwa na shirika la The Foundation For Civil Society kupitia mradi wa mafunzo ya lugha ya alama za msingi sekta za afya.

Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack aliwataka watoa huduma katika sekta za afya mkoani Shinyanga wametakiwa kutumia muda mwingi kuwasikiliza watu wenye ulemavu wa kutosikia na kutoongea ili kuhakikisha kuwa watu hao wanapata huduma za afya kama wanavyopata watu wengine wasio na ulemavu.

Telack alisema watu wasiosikia na kuongea (viziwi) wamekuwa wakishindwa kupata huduma muhimu katika sekta za afya kutokana na vikwazo vya mawasiliano hivyo kuwataka watoa huduma waliopata mafunzo hayo kutumia muda wao mwingi kuwasaidia watu hao.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha 25 za matukio yaliyojiri leo Oktoba 31,2016

Wanachama wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoa wa Shinyanga ambacho sasa kina wanachama 544 tangu kilipoanzishwa mwaka 1990 kikiwa na wanachama sita pekee.

Mkalimani wakati wa mafunzo hayo ya lugha ya alama Prisca Mwakasendile akitoa maelezo kwa maneno na alama kwa wazungumzaji ukumbini ili kurahisisha mawasiliano na kuelewa mafunzo hayo,ambayo yamehudhuriwa na watoa huduma za afya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Viziwi Tanzania mkoa wa Shinyanga.

Watoa huduma za afya kutoka hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mratibu wa mradi wa mafunzo ya lugha ya alama za msingi sekta za afya,ambaye pia ni katibu CHAVITA mkoa wa Shinyanga Justine Shinday akizungumza wakati wa mafunzi hayo ambapo alisema viziwi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa wakalimani katika maeneo muhimu na nyeti kama vile hospitali,mahakamani,polisi na vyombo vya habari maeneo ambayo hufikiwa mara kwa mara katika shughuli za kila siku kwa jamii yote.

Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.

Katibu CHAVITA mkoa wa Shinyanga Justine Shinday aliiomba serikali kupitia halmashauri za wilaya kuteua viongozi walau wawili watakaofanya kazi na CHAVITA kwa muda wote kama waajiriwa hali itakayowezesha asasi kuongeza ufanisi na ubora wa kuhudumia wanachama wake.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Ntuli Kapologwe akizungumza ukumbini ambapo aliuomba uongozi wa CHAVITA kupitia shirika la The Foundation For The Civil Society kuendelea kutoa elimu kwa watumishi wengine katika vituo vya afya kwani wengi hawana elimu ya lugha ya alama.
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Ntuli Kapologwe alisema kupitia mafunzo hayo,watoa huduma katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga watapata watajifunza lugha ya alama hivyo kuwasaidia kuhudumia watu wenye ulemavu wa kutosikia kuongea wanaofika kupata huduma za afya hospitalini.

Watoa huduma za afya kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini

Kushoto ni Emmaculatha Mihangwa,ambaye ni mwanachama wa CHAVITA mkoa wa Shinyanga akisoma risala ambapo pamoja na mambo mengine alisema viziwi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto lukuki na kusababisha wakose huduma muhimu zinazoathiri maisha yao hivyo ni vyema watoa huduma katika sekta muhimu na nyeti kama sekta ya afya wakafundishwa namna ya kuwasiliana na viziwi.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alisema watu  wenye ulemavu wa kusiosikia na kuongea (viziwi) wamekuwa wakishindwa kupata huduma muhimu katika sekta za afya kutokana na vikwazo vya mawasiliano hivyo kuwataka watoa huduma waliopata mafunzo hayo kutumia muda wao mwingi kuwasaidia watu hao.Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack aliwataka wananchi kutoa taarifa za watoto waliozaliwa na ulemavu wa kutoongea na kusikia ili serikali iweze kuwasaidia kwa kuwapeleka katika shule maalum kwa ajili ya kuwapa haki ya elimu.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini.

Katibu CHAVITA mkoa wa Shinyanga Justine Shinday akitoa elimu ya lugha ya alama ambapo alisema mafunzo hayo yawasaidia watoa huduma katika sekta za afya kuwasiliana na watu wenye ulemavu wa kutosikia na kuongea.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea na mafunzo ya lugha ya alama
Katibu wa CHAVITA mkoa wa Shinyanga Justine Shinday akitoa elimu ya lugha ya alama

Mafunzo yanaendelea

Mafunzo yanaendelea ukumbini

Washiriki wakiwa ukumbini

Tunafuatilia kinachoendelea

Mafunzo yanaendelea

Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini

Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia somo ukumbini

Picha ya pamoja,washiriki wa mafunzo ya lugha ya alama na mkuu wa Shinyanga Zainab Telack


Picha ya pamoja.

BondiaThomas Mashali amefariki dunia

10/31/2016 01:23:00 pm
Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali amefariki dunia usiku wa kuamkia leo October 31 2016 maeneo ya Kimara DSM, Taarifa zinadai kuwa alishambuliwa na wananchi baada ya madai ya kuitiwa mwizi.
Taarifa kutoka kwa Promota wake, Siraji Kaike amesema watu aliokuwa anagombana nao walimwitia mwizi na wakawa wamemshambulia na baadaye wakawa wamemtupa na bodaboda waliokuwa wanamjua Thomas Mashali walimuokota na kumpeleka hospitali ambapo baadaye zilitolewa taarifa kuwa amefariki.

Rais Magufuli Aaalikwa na Rais Kenyatta kufanya ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya

10/31/2016 01:10:00 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 31 Oktoba, 2016 ataanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi.

Pamoja na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Nairobi

Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Barabara hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji hilo.

Rais Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
 
 

MABALOZI WA USALAMA BARABARANI ARUSHA WAMSHANGAZA KAMANDA MPINGA.

10/31/2016 09:26:00 am
 Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. PICHA NA GADIOLA EMANUEL
  Kamanda Mohamed Mpinga akipokea "Birthday Surprise Cake " kutoka kwa Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akikagua "Birthday Surprise Cake " aliyopewa na Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akipokea Chupa ya Shampeni kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bw. Bakari Msangi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akigonga Cheers na  Mabalozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga wakishiriki shampeni na Mabaozi katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Balozi Daniel Urioh akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Katibu wa RSA - Arusha Bw. Gadiola Emanuel akigonga Cheers na Kamanda Mohamed Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Katibu wa RSA - Arusha Bw. Gadiola Emanuel akigonga Cheers na Kamanda Mohamed Mpinga huku kulia akishuhudiwa na Mwenyekiti. Bi. Stella na Kushoto ni Balozi Wilbard Ngambeki katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.

 Balozi Mustafa Panju akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Balozi Wilbard Ngambeki akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Balozi Seria Tumainiel akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Balozi Vero Ignatus akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Balozi Vero Ignatus akigonga Cheers kwa furaha na Kamanda Mpinga huku mwenye kiti akishuhudia katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Kamanda Mohamed Mpinga akikata "Birthday Surprise Cake " huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
  Balozi Mustafa Panju akimlisha keki Kamanda Mpinga kwa niaba ya wazee waliopo katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
   Balozi Vero Ignatus akimlisha keki Kamanda Mpinga  kwa niaba ya wadada waliopo katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
   Kamanda Mpinga akimlisha Keki Mwenyekiti wa RSA -Arusha Bi. Stella Rutaguza katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani akimlisha keki Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Mlezi wa RSA-Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha ,SSP. Eng. Nuru K. Selemani wakipongezana na Kamanda Mpinga katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Kamanda Mohamed Mpinga akifurahia mlo wa usiku na Mabalozi  katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Kamanda Mohamed Mpinga akipata mlo wa usiku na Mabalozi  katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Kamanda Mohamed Mpinga akipata picha ya pamoja na Mabalozi  katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.
 Kamanda Mohamed Mpinga akipata picha ya pamoja na Mabalozi  katika hafla ya Siku ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016.Mabalozi  wakizungumza na kufurahi ujio wa Kamanda Mpinga Jijini Arusha na kututafuta Mabalozi katika hafla ya Sikukuu ya kuzaliwa kwake (Mpinga ) iliyoandaliwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani na Kufanyika katika ukumbi wa Milestone Park, Sakina Jijini Arusha, 30/10/2016. Picha Zote na Gadiola Emanuel.Na Vero Ignatus, RSA Arusha.
 Mabalozi wa usalama wa barabarani (Road Safety Ambassadors - Arusha) wamesherehekea sikukuu ya kuzaliwa ya Kamanda Mohammed  Mpinga jijini Arusha.
 
Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Milestone Park -Sakina ,
imeandaliwa na kamati ya (RSA -Arusha) chini ya mwenyekiti wa mkoa Bi. Stella
Rutaguza na kuhudhuriwa na wajumbe wa( RSA - Arusha)

"Kwakweli mmenistua jamani sikutegemea kama mmeniandalia jambo kubwa
kama hili ,nilijua nakuja kukutana tu na mabalozi ili kufahamiana na
kuongelea maswala yetu ya usalama barabarani "alisema Mpinga.
 
DCP Mpinga mbaye yupo kikazi jijini Arusha alikutana na mabalozi wa
usalama barabarani,kwa lengo la kuongelea na kujadili  maswala ya usalama
barabarani na mabalozi hao,ambao kazi yao kubwa ni kuelimisha
jamii,kukemea na kuripoti matukio yanayoathiri usalama barabarani,na
kushawishi mabadiliko ya tabia ,sheria na sera.
 
Amezungumzia changamoto iliyopo kwa sasa kwa utoaji wa risiti pale
dereva anapotakiwa kulipa faini kutokana na makosa yanayofanyika
barabarani,amesema kuwa mfumo huo wa kieletroniki tayari umeshaanza
kutumika jijini Dar-es-salaam na hivi karibuni mfumo huo utaanza
kutumika katika mikoa sita iliyopewa kipaumbela kabla ya mwaka huu
kumalizika.Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Arusha,Pwani,Morogoro,Mbeya,
Dodoma,
na Mwanza,na amewataka askari wa usalama barabarani kutumia lugha
njema kuwaelewesha madereva pale wanapohitaji kupewa risiti za(
EFD)ili waweze kutambua changamoto hiyo kwa sasa ambayo serikali
inalishughulikia.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Bushbuck safaris Bw. Mustafa Panju amemuomba
mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha SSP. Eng.Nuru
Suleimani ampe ruhusa ya kutoa mafunzo kwa askari wa usalama barabarani
Arusha kuhusu huduma kwa mteja.


"Nipo tayari kutoa ofa ya mafunzo kwa askari wetu wa kikosi cha usalama
barabarani ukinipatia nafasi ,na hii itasidia sana " Alisema Panju.


 Naye mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Bi.  Stella
Rutaguza amempongeza Kamanda Mpinga katika siku yake ya kuzaliwa na
kumtakia maisha marefu, yenye afya tele.


Bi. Stella ameongeza kuwa katika mkoa wa Arusha kutakuwa na oparasheni
Abiria paza sauti itakayofanyika kwa miezi mitatu lengo kuu likiwa ni
kumjengea uwezo na kumuhamasisha dereva na abiria kuchukua tahadhari
kuepuka ajali.
 
Amesema kampeni hii inalenga kumfanya abiria atambue haki na wajibu
wake ,akiwa kwenye basi APAZE SAUTI pale panapotokea uendeshaji
hatarishi barabarani,na pia kumfanya dereva abadili mtazamo wake na
kujenga utamaduni wa usalama barabarani,hii inamfanya dereva na abiria
kuwa sehemu ya suluhisho la ajali za barabarani.
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel