Top Menu

POSSI: JAMII IWASHIRIKISHE WATU WENYE ULEMAVU KATIKA FURSA ZOTE ZA MAENDELEO

11/30/2016 07:51:00 am
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akizungumza na baadhi ya watu wenye ulemavu (hawapo pichani) na watendaji wa Serikali juu ya umuhimu wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli za maendelea wakati wa ziara yake Wilayani Peramiho mkoa wa Ruvuma Novemba, 2016.


Na.Mwandishi Wetu
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameiasa jamii kuwashirikisha watu wenye ulemavu katika shughuli zote za maendeleo ili kusaidia kuwainua na kuondokana na dhana ya utegemezi na kuwakwamua kiuchumi.
Dkt.Possi ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Wilaya za Mbinga, Songea Vijijini na Nyasa mkoani Ruvuma ambapo alitembelea Shule zenye kuhudumia watu wenye mahitaji maalum za Songea Boys, Luhira, Huruma na Kituo cha Kulelea wenye ulewavu cha Peramiho Disabled Persons Action (PEDIPA) na Kituo cha kulele wazee na wenye ukoma cha Nge Wilayani Nyasa.
Katika ziara hiyo Mhe.Possi alibaini changamoto nyingi za watu wenye ulemavu na kuishauri jamii namna pekee ya kutatua changamoto wanazokabiliana nazo ni jamii kuona umuhimu wa kuwashirikisha watu hao katika mipango yote ya maendeleo.
“Halmashauri ziandae mipango ya kuwawezesha watu wenye ulemavu kuweza kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato na hii itasaidia kuondokana na hali ya utegemezi na kuondoa mitazamo hasi juu ya watu wenye ulemavu kuwa hawawezi” .Alisema Mhe.Possi.
Waziri Possi alisisitiza kuwa ni lazima Halmashauri ziwe na ubunifu wa miradi ya maendeleo itakayo walenga watu wenye ulemavu, “Ni vyema sasa kuwe na jitihada za makusudi za kuunda miradi maalum kwa ajili ya kuwapa nafasi za ushiriki ili kujitafutia vipato na kuyakabili mazingira yao, ikumbukwe wakina mama waliachwa nyuma kwa muda mrefu ila baada ya kupaza sauti zao tunaona sasa wanasikika hivyo hivyo iwe kwa watu wenye ulemavu” Alisitiza Dkt.Possi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa Dkt.Osca Albano alisisitiza kuyapokea maelekezo yote ya Naibu Waziri Mhe.Possi kwa vitendo na kumhakikishia kuwa Wilaya yao itakuwa mstari wa mbele katika kulitekeleza hilo.
 “Sisi tunafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Halmashauri hivyo ni vyema tukalichukua hilo kuangalia namna tunavyoweza kuliweka katika mipango yetu yote ya maendeleo ili kuwasaidia na kufikia lengo la serikali,” alisema Dkt. Albano.
Nae Katibu Tawala Wilaya ya Songea Bw. Edmund Siame aliomba halmashauri zote ziwe zinatoa mrejesho mapema juu ya maagizo yanayotolewa na viongozi wa juu huku Mwalimu Elswida Charles anayehudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum akimweleza Dkt. Possi kuwa watu wenye ulemavu wanafarijika kutokana na jitihada anazofanya kuwainua watu wenye ulemavu.

Ajali ya Gari Yaua Watu 6

11/30/2016 06:48:00 am


Watu  sita wakiwamo mfungwa na wanafunzi wamekufa huku wengine wanane wakijeruhiwa, baadhi yao vibaya baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka mara nne katika Kijiji cha Kipande wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa katika barabara kuu ya Mpanda – Sumbawanga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema ajali hiyo ilitokea saa 8.10 jana mchana katika Kijiji cha Kipande.

Aliwataja waliokufa kuwa ni mfungwa wa Gereza la Kitete lililopo Nkasi, Gaudensi Nyambo (27), Gasper Malimi (18) na Kenzi Mwambige (18) wote wakiwa wanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Nkasi na Ofisa Mipango wa Wilaya ya Nkasi, Godfrey Mwanansao.

Alisema marehemu wawili hawajatambuliwa huku miili yote ikiwa imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Rukwa ya Mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga .

“Mfungwa Nyambo alikuwa akitumikia kifungo katika Gereza la Kitete wilayani Nkasi ambako alikuwa na kesi nyingine mahakamani alikufa wakati akitibiwa hospitalini hapa,” alieleza Kamanda Kyando.

Alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Hiace Nissan Vannette lenye namba za usajili T 966 DHP lililokuwa likiendeshwa na Lusanjo Mwaipopo aliyekimbia baada ya ajali hiyo.

Alisema gari hilo lilikuwa likitokea wilayani Nkasi kwenda mjini Sumbawanga ambapo liliacha njia na kupinduka mara nne kabla halijaanguka ndani ya gema.

Alisema chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika huku uchunguzi wa kipolisi ukiendelea. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa, Dk John Lawi alisema majeruhi tisa wamepokewa hospitalini hapo ambao mmoja ambaye ni mfungwa alikufa OPD.

Aliwataja majeruhi kuwa ni pamoja na askari Magereza wa Gereza la Kitete, Fortunatus Saanane (44) aliyelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) huku hali yake ikiwa tete. Wengine ni askari Magereza, Francis Elay (30) ambaye alitibiwa na kuruhusiwa.

Kwa mujibu wa Dk Lawi, majeruhi wengine ni Mbagala Hale, Mamadelwa Kafadhila, Mathias Mwandaliwa (28) na wengine ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja. Alisema hali za majeruhi hao ni mbaya.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA GEREZA LA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

11/29/2016 10:42:00 pm
  Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi  na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja ili aongee  na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Mmoja wa askari wa Kikosi Maalumu cha Magereza wakitoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akichukua maelezo kutoka kwa  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
  Baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Rais Dkt John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
  Askari wakiwa na shauku ya kutoa kero zao mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipoongea  na  maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016
 Mkuu wa gereza la Ukonga akieleza changamoto za kazi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli  alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo 
Novemba 29, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016

PICHA NA IKULU

ANNA MAKINDA ATAKA MABADILIKO YA SHERIA YA NDOA

11/29/2016 10:32:00 pm
Image result for ANNA MAKINDA PICHA
Spika mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, ameeleza kusikitishwa na kitendo cha serikali kushindwa kufanyia marekebisho baadhi ya vifungu vilivyopo katika sheria ya ndoa ya mwaka 71 licha ya mchakato kuanza muda mrefu hali inayosababisha vitendo vya ukatili kuendelea.

Makinda ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, kwenye kongamano la kwanza kitaifa kutetea na kusimamia haki za wanawake kwa kuwawezesha na kusimamia kiuchumi ambapo amesema baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye sheria ya ndoa inayotumika sasa vinakiuka na kukandamiza haki za wanawake hasa wale wasio na uelewa wa kisheria.
“Ningeomba serikali isaidie kufinance kucontribute kwasababu development partners kweli wanatusaidia watafika siku nyingine wataondoka. Tumemaliza si wanawapaga muda mradi wa miaka miwili mitatu subject to renew au basi kabisa, wanakuja viongozi wa nchi yanakuwa majitu wanasema hayo mambo out tutaweza kweli,” alisema.
“Sheria ya ndoa ya mwaka 71 inachelewa wapi? Tumeiimba wee toka mi nikiwa waziri mpaka leo kuna tatizo gani ile si iliandikwa na watu tu?,” alihoji.

KUTOKUZINGATIA VIGEZO KWAKWAMISHA RUFAA YA LEMA

11/29/2016 04:45:00 pm
Wananchi wa Arusha wakiwa mahakamani siku ya jana.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wafuasi wa chadema wakiwa wamevalia tshirt zilizoandikwa Justice 4 Lema mahakamani jana.Picha na Vero Ignatus Blog.
Watu wakiwa nje ya maakama jana .Picha na Vero Ignatus Blog
Watu wakiwa nje ya mahakama jana .Picha na Vero Ignatus Blog


Image result for mbunge lema
Na .Vero Ignatus Arusha.
Upande wa jamhuri waweka pingamizi juu ya rufaa  hiyo iliyokatwa ya kusikiliza pingamizi ya uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi juu ya kumnyima dhamana mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.

Akizungumza na waandishi wa habari ,Wakili mwandamizi  Mahakama kuu ya kanda ya Arusha ,Matenus Marando ,alisema wameweka pingamizi la rufaa hiyo kutokana na upande wa utetezi kushindwa kuzingatia vigezo vya ukatwaji wa rufaa hiyo 

Alisema kuwa vigezo hivyo  kwa  upande wa utetezi hawakuonesha nia ya kukata rufaa kwa kuandika notisi ya rufaa na badala yake walikata rufaa bila kufuata utaratibu huo .

Wakili Marando alisema kuwa  kulingana na kifungu cha sheria cha 361(1)(a) cha CPA kilimtaka mkataji rufaa kuonesha nia ya kukata rufaa kwa kuandika notisi ya rufaa  na si kukata hivyo waliitaka mahakama itupilie mbali rufaa hiyo 

""Tulikuja na pingamizi na tukawapatia upande wa pili baada ya hapo tulienda kwa jaji Fatuma Massengi ,tumekubaliana kuwa hilo pingamizi lisikilizwe kwanjia ya maandishi ,"alisema Marando  

"Hivyo tarehe 30 tutawasilisha pingamizi letu saa 2 asubuhi ,saa 6 mchana upande wa utetezi utajibu ,saa 10 upande wa serikali utajibu hoja lakini tarehe 2 uamuzi utatolewa na mahakama juu ya pingamizi letu ,"alisema Marando 

"Kama pingamizi letu likishindwa basi rufaa itasikilizwa na kama litashinda basi watatakiwa tena kukata rufaa kama sheria ilivyoangiza,


Upande wa wakili wa utetezi ,Peter Kibatala ,alisema kikubwa kitakachoenda kubishaniwa ni muda uliotumika kuleta hitaji ya kusudi la kukata rufaa  ambako itaenda kuangaliwa kama ilikuwa lipo ndani ya muda au nje ya muda.

UZINDUZI WA KISMATY ADVERT MEDIA COMPANY LTD WAFANA JIJINI ARUSHA

11/28/2016 02:38:00 pmMkurugenzi wa Kismarty Advert Media Company Ltd, Mary Kismarty Mollel akiwa anazungumza siku ya uzinduzi wa kampuni hiyo katika ukumbi wa ukumbi wa Asili Resort uliyopo jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Company Ltd ,akiwa anasalimiana na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo katika ukumbi wa Asili Resort iliyopo jijini Arusha

Wa kwanza kulia ni Meya wa jiji la Arusha Calist Lazaro ,akifuatia na aliyeko kulia kwake ni mkuirgenzi wa Kismarty Advert,akifaria na aliyeko kulia kwake ni Dotto Kimaro siku ya uzinduzi wakampuni hiyo.iliyofantika katika ukumbi wa Asili Resort iliyopo jijini Arusha.

Mchekeshaji Steve Nyerere nae hakubakia nyuma alikuwepo akifanya yake katika uzinduzi wa Kismarty Advert Media,.iliyofantika katika ukumbi wa Asili Resort iliyopo jijini Arusha.
Watatu kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro ,akifuatiwa na msaidizi meya Viola Lazaro ,aliyepo kushoto kwake ni diwani wa kata ya Themi Kinabo akifuatiwa na Diwani wa kata ya Ngarenaro Nathaniel Nanyaro katika uzinduzi wa Kismarty Advert  Media,iliyofantika katika ukumbi wa Asili Resort iliyopo jijini Arusha.
Mameneja wa Venus Hotel wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa wa Kismarty Advert Media Company ltd.
Mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Company Ltd, Mary Kismart akikata keki kwa kushirikiana na Meya wa Jiji la Arusha Calist Lazaro wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo ya matangazo.iliyofanyika katika ukumbi wa Asili Resort iliyopo jijini Arusha.

Keki ya ndafu nayo ilikuwepo katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kismarty Advert Media Company Ltd .


Mambo haya nayo hayakosekaniki katika hafla kama hii shampein ikifunguliwa hapa na  mmoja wa waandishi wa habari wa kituo cha TV jijini Arusha Millan Cable Hamza Kalemela ,pamoja na mwandishi wa habari kutoka gazeti la Mwananchi communication Zulfa Musa.iliyofantika katika ukumbi wa Asili Resort iliyopo jijini Arusha.Mambo yakiendelea kama uonavyo hapo pichani
Afisa uhusiano  wa Kismarty Advert Media  Company LTD,Gadiola Emmanuel akipongezana na Mkurugenzi wa Kismart Advert Media company ltd,iliyofantika katika ukumbi wa Asili Resort iliyopo jijini Arusha. Wakiwa wanapongezana katika uzinduzi wa Kismarty Advert Media Company ltd ,iliyofantika katika ukumbi wa Asili Resort iliyopo jijini Arusha.

Na Vero Ignatus Arusha.


Meya wa Jiji la Arusha amesema kuwa ni vyema kusapoti na kuyapa kipaumbele mambo mazuri yanayofanyawa na wazawa haswa kwa uthubutu wao wa kufanya mambo ya maendeleo .

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampuni ya matangazo inayojulikana kama Kismarty Advert Media company ltd , iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Asili Resort iliopo katika Jiji la Arusha na kuhudhuriwa na wamiliki wa makampuni mbalimbali hapa nchini.

Meya huyo amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutangaza biashara zao kwani bila kufanya hivyo hata kama bidhaa itakuwa na uzuri kiasi gani hakuna atakayefahamu thamani yake bila kuitangaza ndipo ifahamaike.

"Jengeni tabia ya kutangaza biashara zenu na bidhaa mnazokuwa nazo ndugu zangu biasahara ni matangazo msikae kimya,ukizingatia hii ni kampuni ya kitanzania,tuache kukuza vya watu tutukuze vya kwetu ndugu zangu "alisema meya.

"Mnapoona kampuni kama hii ya matangazo ndiyo fursa yenyewe hii ya kuitumia kuzitangaza biashara zenu,ukikaa kimya hakuna mtu anayeweza kuifahamu bidhaa yako au biashara yako hata kama unauza vitu vuzuri kiasi gani" alisema Meya.

Kwa pande wake mkurugenzi wa Kismarty Advert Media Company ltd ,bi Mary Mollel amesema kuwa kampuni hiyo inapokea matangazo ya aina mbalimbali na kwa bei ambayo mteja atakayoimudu .

Hivyo amewataka wafanyabiashara biashara mbalimbali kutokuwa waoga kutangaza biashara zao kwani ndiyo njia pekee itakayowasaidia biashara zao kufahamika zaidi na kupata wateja zaidi.

"Msiwe waoga kuthubu kutangaza biashara zenu hapa tunasaidiana wewe unaleta tangazo nakutangazia kwa bei nzuri na wakati huohuo unapata wateja kwa upande wako ,kwa maana nyingine tunawezeshana karibuni sana. " alisisitiza bi Mary.ABEDNEGO HANGO: TUMIENI VIPAWA MLIVYONAVYO ILI KUIJENGA TANZANIA YENYE AMANI NA UPENDO

11/26/2016 09:04:00 pm

Mkurugenzi wa na Muanzilishi wa  The worshiperz  Abednego Peter Hango.
Muanzilishi mwenza na wa The worshiperz  Grace Hango,ambapo ni muimbaji katika kundi hilo.
Kundi  The worshiperz wakiwa katika mojawapo ya huduma wanazozifanya.
Na.Vero Ignatus Arusha.
Wito umetolewa kwa watanzania watumie vipaji walivyonavyo ili kuijenga Tanzania yenye Amani na upendo bila kujali itikadi za dini wala vyama huku wakijuaya kwamba watu wote wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.

Hayo yamesemwa na muanzilishi na mkurugenzi wa The worshiperz  Abednego Peter Hango katika hafla  ya kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea iliyofanyika katika ukumbi wa New Safari Hotel jijini hapa .

Hango amesema kuwa wameamua kiufanya hafla hiyo kwani yapo mambo mengi ambayo Mungu amewatendea siyo tu kwa mwaka huu wa 2016 ila tangia kuanzishwa kw kundi hilo mwaka 2008 ,wakiwa na malengo ya kuwaleta vijana pamoja wenye shauku ya kumtumikia Mungu,ambapo hadi sasa waapo waimbaji 36 .

Amesema kuwa maono ya kundi hilo ni kuwafundisha na kuwaleavijana pamoja na waimbaji kwa ujumla ili wawe waabuduo halisi na wahudumu na siyo kuwa waimbaji pekee jambo ambalo wamefaulu .

Wakati huohuo  Kundi  The worshiperz  wameandaa tamasha kwakushirikiana na kundi la Gospel Kitaa linalofahamika kama Sifa za Yeriko litakalofanyika hivi karibuni katika Newlife City Church lililopo mkoani hapa tarehe 9.12.2016.

Tamasha hilo litawashirikisha waimbaji kutoka nchini Afrika ya kusini,akiwemo Mercy Manqele kutoka kundi la Joyouus Celebration,Spokazi Nzumalo kutoka kundi la Soweto Gospel Kwaya pamoja na Kgotso Makgalema kutoka kundi la Spirit of Praise.


Aidha ameainisha waimbaji wakataokuwepo kutoka jijini hapa ni pamoja na Pcasf,Cahogos,Machalii wa Yesu ,Voice of Joy,na Yusuph Nahashon

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SUKUHU HASSA ATEMBELEA KIWANDA CHA A TO Z MKOANI ARUSHA

11/26/2016 08:21:00 pmMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shah, na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo. Makamu wa Rais amefanya ziara kwenye kiwanda hicho ikiwa sehemu ya kutambua mchango wa wawekezaji wa ndani na changamoto wanazokutana nazo ili kupata majibu ya kurahisisha kufanikisha Tanzania mpya ya Viwanda. 
**************************************
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuviimarisha vyuo vya ufundi stadi nchini –VETA- ili viweze kutoa wahitimu bora ambao watakidhi katika soko la ajira hasa kwenye viwanda vilivyopo na vitajengwa nchini.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo mkoani Arusha katika ziara yake ambayo imeingia siku ya Pili ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani humo ili kujua changamoto zinazokabili viwanda hivyo na serikali kuzitafutia ufumbuzi.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imetenga fedha za kutosha zitakazotumika kuviimarisha vyuo vya Veta ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayosidia vijana kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.


Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha A to Z,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kulinda na kutetea haki za wafanyakazi kwa kutoa maslahi mazuri ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii.


Makamu wa Rais pia amesisitiza usawa katika ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje ya nchi walioajiriwa kwenye kiwanda hicho ili kuondoa tofauti za mishahara hali ambayo ijenga motisha kwa wafanyakazi.Kiwanda cha A to Z kilichopo eneo la Kisongo mkoani Arusha ambacho kinatengeneza vyandarua, nguo na mifuko mbalimbali ikiwemo ya saruji kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 7500 ambapo asilimia 80 ya wafanyakazi wote ni wanawake.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wawekezaji kote nchi walipe kodi za serikali mapema kodi ambazo zitatumika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembezwa Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shahkatika,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Kalpesh Shah akipata maelezo ya namna kiwanda cha A to Z kinavyofanya utafiti wa kupambana na wadudu wanaoharibu mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha utafiti cha Africa Technical Research Centre Dkt.Johson Ouma Odera. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA 21 WA WANANSHERIA WA AFRIKA YA MASHARIKI

11/25/2016 06:06:00 pm
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Naibu Spika, Dkt.Tulia Ackson baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua  Mkutano wa 21 wa Chama cha Wanansheria wa Afrika ya Mashariki Novemba 25, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Rais wa  Chama cha Wanansheria Afrika ya Mashariki, Wakili Nassor Hamis baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua  Mkutano wa 21 wa Chama cha Wanansheria wa Afrika ya Mashariki Novemba 25, 2016.  Wapili kushoto ni Naibu Spika, Dkt.Tulia Ackson, Watatu kushoto  Jaji Kiongozi, Frednand Wamabali,  wanne kushoto ni Mwanansheria Mkuu wa Serikali, George Masaju na kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria,Dkt Harrison Mwakyembe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt, Harrison Mwakyembe (kushoto) na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ​baada ya kuwasili kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam kufungua  Mkutano wa 21 wa Chama cha Wanansheria wa Afrika ya Mashariki Novemba 25, 2016.
 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Mwaka wa 21 wa Chama cha Wanasheria Afika ya Mashariki   kwenye ​ Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.  Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano   wa 21 wa mwaka wa Chama cha Wanansheria Afrika Mashariki wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipofungua mkutano huo  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016.
 aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Rais wa Chama cha Wanansheria Afrika  Mashariki Wakili Nassor Hamis Mohmmed (kushoto) na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia)  baada ya kufungua ​Mkutano wa Mwaka wa 21 wa Chama cha Wanasheria Afrika ya Mashariki  kwenye ​ Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kiwa katika picha na ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa 21 wa Wanansheria Afrika ya Mahariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.  Harrison Mwakyembe baada ya kufungua mkutano wa 21 wa Chama cha Wanasheria Afrika Mashariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016. 
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel