Top Menu

BAADA YA BAADHI YA WATU KUKAIDI AGIZO LA WAZIRI MKUU,MASHINE ZACHOMWA MOTO KARATU

12/30/2016 02:05:00 pm
 Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice
Picha na Vero Ignatus blog. Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice aliyevaa kitenge akiwa na baadhi ya wananchi wa wilaya ya karatu leo katika kito cha polisi mjini kati Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus blog.

 
 Baadhi ya wananchi kutoka wilaya ya karatu wakiwa nje ya kituo cha polisi mjini kati leo.Picha na Vero Ignatus Blog.


 
Vero Ignatus,Arusha

Sakata la viongozi wa Chadema na wananchi wa vijijini nne wilayani Karatu Mkoani Arusha kukamatwa na polisi kwa kosa la kuchoma  mashine ya kuvutia maji ni kufuatia haa za baadhi ya watu kukaidi amri ya Waziri Mkuu aliyetaka mashine hizo zote kuondolewa katika chanzo cha maji kilichokuwa na mgogoro wa muda mrefu.

Waziri Mkuu,Kassimu Majaliwa Mnamo desemba 5 mwaka huu,alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Karatu, Theresia  Mahongo kuhakikisha kabla ya saa 12 jioni nay eye kumaliza kikao na wananchi awe ameziondoa mashine hizo zilizowekwa katika chanzo cha maji.
Mbali ya hilo Waziri  Mkuu aliagiza chanzo hicho cha maji kutunzwa na mashine zote ziwe umbali wa mita 500 na mto utunzwe kwa mita 60 tofauti na hapo hatua kali zichukuliwe.

Kufuatia agizo hilo vifaa hivyo na vingine viliondolewa vyote kwa kusimamiwa na Mkuu wa wilaya Karatu mwenyewe na jeshi la polisi wilaya ya Karatu.

Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice akizunzgumza na waandishi wa habari leo amesema kuwa baada ya agizo hilo kutekelezwa walirudi katika vikao vya jumuiya ya uongozi wa vijiji saba vya kata mbili za Mang’ola na Qaedenti kwa ajili ya kufanya maazimio ya agizo la Waziri Mkuu.

Amesema vijiji vyote viliafiki agizo hilo na kuahidi kutunza chanzo hicho cha maji umbali wa wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho na mita 60 kutoka kwenye mto.

Patrice ameendelea kueleza kuwa maazimio hayo yalikubaliwa na viongozi na wananchi wa vijiji vyote kwani kiliagizwa na Waziri Mkuu ni msisitizo kwani katika vikao vya nyuma vya vijiji hivyo hayo yote yalikubaliwa katika vikao.

Alisema cha kushangaza baadhi ya viongozi na madiwani kukamatwa kwani ndio waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanatii amri ya Waziri Mkuu.

Diwani huyo alisema kuwa aliambiwa kuwa baadhi ya wananchi wamerudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha maji na kufikia hatua ya wananchi wengine kukasirishwa na kitendio hicho cha kudharau mamlaka za juu zilizoagiza.

‘’Baadhi ya watu waliokamatwa hawahusiki kabisa na uchomwaji wa mashine hizo kwani polisi imeamua kukamata hovyo hovyo ila mie ninachojuwa desemba 26 na 27 mwaka huu baadhi ya wananchi walialikwa kufanya usafi katika chanzo hicho na kwa kuw amaji yalikuwa yakipungua siku hadi siku’’alisema diwani huyo

Mkazi mwingine wa Kata ya Mang’ola aliyeomba kutotajwa jina lake alisema kuwa mgogoro huo ni wa muda mrefu sana kutoka mwaka 2007 na kijiji cha Qaedenti ndio chanzo mgogoro huo kwani wamekuwa waghumu kutii maagizo ya viongozi wa juu wa serikali pindi wanapotakiwa kukaa umbali wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho cha maji.

‘’wamekuwa wakileta vurugu kila mara kwa sababu ya madai kuwa chanzo hicho ni chao lakini sio kweli kwani chanzo hicho hutoa huduma ya maji kwa vijiji saba bila ya kuwa na ubaguzi wowote’’alisema mwananchi huyo

Alisema kuchomwa kwa mashine ni kutokana na wananchi kupatwa na hasira na jazba za baadhi ya wananchi kurudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha maji na kudharau agizo la Waziri Mkuu.

Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Karatu ,Willy Qambalo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ,Jubillet Manyenyo wameachiwa kwa dhamana na wametakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi Arusha januari 4 mwakani.

Wengine waliokamatwa na bado wanahojiwa na polisi Arusha ni pamoja na diwani wa kata ya Baray ,Thomas Darabe na diwani wa kata ya Mang’ola Lazaro Emmanuel .

Kamata kamata hiyo imewakumba wananchi wengine ambao ni pamoja na Godwin Mussa,Safari Awak,George Pius,Baridi John,Bartazar Lohay,Jafari Thiophil,Vicent Airo ,sebastian Mosses na Daniel Ninida.

Wengine waliokamatwa na polisi ambao ni ndugu ni pamoja na ndugu wawili ambao ni pamoja na Charles Lameck na Chrisopher Lameck .

Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa baada ya kuchukuliwa maelezo kwa watuhumiwa hao 15 majalada yanapelekwa katika ofisi ya Mwansheria wa serikali kwa ajili ya kufungua kesi.

   

Kilio cha mbunge Ridhiwani chasikika, RC Ndikilo atoa mwezi mmoja kwa wafugaji

12/30/2016 01:17:00 pm
unnamed-10
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini, mbunge wa Chalinze Mh RIDHIWANI KIKWETE ameiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro hiyo.

Mkutano huu unafuatia hali mbaya ya mapigano baina ya wakulima na watugaji kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari. Mapigano hayo ambayo yalianza siku nyingi, sasa yamefika pabaya baada ya matukio ya watu kuuawa, kuvunjwa viungo na hata wengine kukimbia makwao kwa sababu ya kile kilichoitwa kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji.

Kama ilivyoandikwa kwenye vitabu va dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge Ridhiwani kikapokewa vyema na Mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30, kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo, 

“Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa”…alisema Ndikilo
unnamed-9
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa maelekezo kwa wanakijiji baada ya kufika katika kijiji cha Kitonga kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza kabla ya mkuu wa mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo hajakaribishwa kuzungunza na Wananchi, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete alisema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi kinyume cha taratibu hivyo kutumia njia ya kijiji kama njia halali ya kupeleka mifugo yao mto Ruvu kuwanywesha maji.

 Vitendo hivyo vimepelekea wananchi wengi kupoteza mazao yao; jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga, hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo.

RC Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo. Mifugo imekuwa mingi sana katika eneo hili la kitonga na mkoa wa Pwani, Mkuu wa mkoa alisema.

 Kwa mujibu wa sensa iliyofanywa kwa kuwahoji wafugaji wenyewe, walidai kuwa wana Ng’ombe wapatao laki 5, lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho. “hata kama ukweli ndiyo huo, eneo la kufuga mkoa wa Pwani linauwezo wa kuchukua Ng’ombe laki 2 na Nusu. Hivyo kuna ziada ya mifugo laki 2 na nusu.

Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa Pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo. “Operesheni ya kuondoa mifugo katika Bonde la Ufa ndiyo iliyofungua mlango huo. Wafugaji walitengewa maeneo Lindi lakini wengi walishuka pwani kwa kuona maji na majani.”, alisema Mkuu wa Mkoa. Sasa muda umefika tusimamie taratibu tulizojiwekea.

unnamed-4
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid  Mwanga akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza

Akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima DC Ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo.

Katika Mkutano huo pia Mkuu wa Mkoa wa Pwani alitumia nafasi kuwaonya wote wanaojiona kuwa wako juu ya sheria na pia wale wanaojidai kuwa wao ndiyo mababa wa Kitonga kwa kuwa mbele ya sheria hakuna aliyejuu.

Alitoa tahadhari kuwa atashughulika wote na onyo kali kwa kiongozi wao Bwana Leki ambaye inasemekana yeye ndiyo anayewaita wenzake na kuwapa kiburi.

Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze mara baada ya kauli ya Mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa Chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoingia kinyemela.
unnamed-5
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo wakiwa kwenye mkutano huo.
unnamed-2
Wanakijiji cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza.
unnamed-10Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akisalimiana na watendaji mkoa wa Pwani baada ya mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza.

Mapya Yaibuka Sakata la Kijana Aliyefariki Baada ya Nyoka wake Kuuawa na Wananchi

12/29/2016 02:53:00 pm
Tukio  la kushangaza lililohusishwa na kifo cha Denis Komba (24) baada ya nyoka aliyekuwa naye kuuawa, limechukua sura mpya baada ya mambo kadhaa kuibuka.

Hayo ni pamoja na familia kudai mzoga wa nyoka na kwenda nao kuuzika nyumbani, jambo lililoendelea kuhusisha suala hilo na imani za kishirikina.

Imeelezwa kuwa familia ilielezwa na mganga wa kienyeji kuwa mwili uliohifadhiwa hospitali, si wa mtoto wao, jambo lililowafanya kuuchukua mzoga wa nyoka na kwenda kuuweka katika mfuko wa sarandusi (kiroba) na kuuzika.

Hata hivyo, mashuhuda walieleza kuwa, familia hiyo ilikikata kichwa cha nyoka na kukizika kivyake na kiwiliwili sehemu nyingine huku mwili wa Komba ambaye naye alizikwa jana, ukizikwa katika kaburi eneo lingine tofauti. Tukio hilo ni la juzi na lilimhusu Komba, mkazi wa Mateka, manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Nyumbani kwao ni kilometa tano kutoka katikati ya mji wa Songea. Kabla ya maziko, baadhi ya vijana waliokuwa wamebeba jeneza, walikuwa wakikimbia nalo mwendo wa mchakamchaka huku wakiimba “mkimbize mkimbize nyoka awahi asije kudhuru watu wengine”.

Katika maziko hayo, hakuna ndugu aliyeonekana kulia wala hakukuwa na ibada yoyote wakati jina la marehemu linadhihirisha kuwa ni wa imani ya Kikristo. 
Wakati hayo yakiendelea msibani, baadhi ya watu wake wa karibu walidai alikuwa na tabia ya kucheza na nyoka mara kwa mara.

Hata hivyo, baba mzazi alikana kumuona mwanawe na nyoka. Naye daktari aliyechunguza mwili, alisema kifo cha Komba kinatokana na kugongwa na nyoka mwenye sumu kali, lakini hakuna jeraha wala alama yoyote iliyoonekana katika mwili huo.

Habari zinaeleza kuwa juzi familia ilikwenda kuzungumza na watu wa Idara ya Maliasili, waliochukua mzoga wa nyoka kwa uchunguzi kama nyara ya serikali. Walikubaliana kuwa familia itakwenda kuufukia na ndipo Maliasili walimrudisha nyoka hadi eneo la tukio na familia kumchukua.

Ilielezwa kuwa hatua hiyo, inatokana na madai kuwa kuna mganga amehusisha mzoga wa nyoka huyo na mwili wa Komba.

Watu wa karibu wa familia hiyo, ambao hawakutaka kutaja majina yao wakiwemo mafundi seremala na majirani, walieleza kuwa familia wakiongozwa na baba mzazi Sevelin Komba, walirudi eneo la tukio baada ya kutoka kwa mganga wa kienyeji na kumchukua nyoka na kumpeleka nyumbani.

Habari zinaeleza kuwa familia baada ya tukio hilo, walikwenda kwa mtaalamu wa mambo ya asili (mganga wa kienyeji) ambaye hakufahamika mara moja na kuelezwa kwa nini wamekubali kumuacha mtoto wao akiteseka juani kwani mwili walioupeleka nyumbani kutoka hospitali si wa Denis (Komba).

Aidha familia baada ya kumchukua nyoka huyo eneo la tukio alikouawa, baada ya kufikishwa nyumbani alikatwa kichwa kwa makubaliano ya familia ya marehemu na kiwiliwili kuzikwa tofauti na kichwa katika mfuko wa sarandusi. Baba mzazi alikanusha suala hilo la kwenda kwa mganga.

Katika maziko hayo, hakukuwa na chakula wala matanga na watu wengi walijitokeza ili kushuhudia kitakachoendelea.

Amuua Rafiki Yake, Ala Ubongo wake na Sehemu Za Siri

12/29/2016 02:43:00 pm
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linamshikilia mchimba dhahabu, Shija Salum (38), mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumuua rafiki yake na kula ubongo wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba pamoja na mtuhumiwa huyo kula ubongo wa rafiki yake huyo aliyetambuliwa kwa jina moja la Shija, pia alitafuna sehemu zake za siri baada ya kuzikata.

Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, tukio hilo lilitokea Desemba 25, mwaka huu, usiku katika Kijiji cha Manyanya, Kata ya Makongorosi, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Alisema mtuhumiwa na marehemu walifika kijijini hapo wakitokea Shinyanga miezi mitatu iliyopita.

“Inasemekana wawili hao walikuwa ni marafiki kwani walifika wilayani Chunya, Kata ya Makongolosi kwenye machimbo ya dhahabu yanayomilikiwa na mfanyabiashara mmoja aitwaye Teddy Mwantega.

“Siku hiyo ya tukio, marehemu Shija, alikuwa amejilaza mahali na hapo ndipo alipofika rafiki yake huyo, akiwa na panga mkononi na kumkata kwa nguvu kichwani.

“Baada ya hapo, alimvua nguo na kuzikata sehemu zake za siri na kuzishika mkononi.

“Wakati akiwa na sehemu hizo za siri mkononi, alichukua ubongo wa marehemu na kuula, kisha akatafuna zile sehemu za siri.

“Kwahiyo, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” alisema Kamanda Kidavashari
 
 
Habari kwa mujibu wa 
Dunia Kiganjani Blog

BENKI YA KILIMO YAMUAGA DR. TONIA KANDIERO

12/29/2016 02:37:00 pm
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kushoto) akimpatia Zawadi ya Ramani ya Tanzania Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia).
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia aliyesimama) akizungumza wakati alipotembelea TADB. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga.
Afisa anayeshughulikia masuala ya kijinsia katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bibi Beatrice Mrema akitoa neno la Shukrani kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Wapili kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na maafisa waandamizi wa TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Katikati) akimkaribisha Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia). Kushoto ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia) akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipotembelea TADB. Anayemtazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru (Aliyesimama) akizungumza wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Aliyesimama) akizungumza wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Wapili kulia aliyesimama) akihimiza jambo wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.

JESHI LA POLISI ARUSHA:WATAKAOCHOMA MATAIRI,FAINI MILIONI NNE,MADEREVA WALEVI KUKAMATWA NA KUNYANG'ANYWA LESENI,WAZAZ I/WALEZI WATAKAOWAACHA WATOTO WAKAZURURA OVYO KUSHTAKIWA,WENYE VIBALI VYA KUFYATUA FATAKI KUTUMIA DAKIKA TATU TU

12/29/2016 02:10:00 pm
Image result for kamanda wa polisi charles mkumbo 
Na.Vero Ignatus,Arusha.


Jeshi la polisi mkoani Arusha limesema kuwa katika kusheherekea mwaka mpya ,kumekuwa na kasumba kwa baadhi ya watu kufanya matukio ya kuhatarisha usalama kwa kuchoma matairi,kupanga mawe barabarani,na hata kuwarushia mawe askari pindi wanapothibiti matukio hayo,haswa maeneo ya majengo,kwa mrombo,kwa mrefu huku wengine wakitumia mwanya huo kufanya uhalifu.


Kwa wale watakaochoma na watakaokamatwa wamechoma matairi barabarani,wakumbuke kwamba watashtakiwa kwa sheria za Tanroad, ambapo watatakiwa kulipa faini isiyopungua milioni nne


Lakini pia baadhi ya madereva huwa wanatumia vilevi kupita kiasi katika majumba ya starehe inapofika saa 00:00 usiku unapoanza mwaka mpya huwa wanashangilia kwa kuendesha vyombo vyao kwa mwendo kasi na kupiga honi mitaani huku wakiwa wamepakia watu kwa kuwaning’iniza milangoni kama njia ya kuonyesha furaha zao.


Uzowefu unaonyesha kwamba maeneo ya sakina mpaka kwa iddi baadhi ya madereva wanatuamia magari aina ya altezana Subaru huwa wanafanya maonyesho kwa kuendesha mwendo kasi vyombo hivyo huku vikitoa sauti kama risasi.


Kwa upande wa wamiliki wa bar wazingatie masharti ya leseni zao ambazo zinaonyesha muda halisi wa kufunga na wasiwe na tama ya kuendelea kupata pesa baada ya kuona wateja wengi katika biashara ,hali kadhalika wamiliki wa kumbi na maeneo mengine ya starehe wanatakiwa kuzingatia usalama katika maeneo yao hasa kwa kuweka wasimamizi na kutojaza watu kupita kiasi.


Aidha wazazi na walezi tunawakumbusha pamoja na kusheherekea mwaka mpya wa 2017 wasisahau majukumu yao ya kuwa makini na watoto kwa kutowaacha peke yao na hata kutoacha mtu yeyote katika majumba ili kuondokana na matukio yanayoweza kuepukika sambamba na kuangalia watoto wao katika maeneo ya round about hasa kijenge mnara wa mwenge,wasizagae barabarani


Jeshi la polisi linatoa onyo kwa baadhi ya watu watakaofanya makosa yaliyoorodheswa hapo juu ,tutawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wawe wahalifu ,wamiliki wa bar na kumbi nyingine za starehe pamoja na wazazi au walezi na madereva walevi ambao pia watapima na ikithibitika wamevuka viwango tutawafungia leseni.


Kwa upande wa waaliomba vibali vya kufyatua fataki ,watatakiwa watumie dakika tatu na wote kwa pamoja watatakiwa kufyatua saa 00:00 na pia hawataruhusiwa kufyatua katika makazi ya watu.


Tutahakikisha nyumba zote za ibada ,kumbi za starehe na maeneo mengine kutakuwa na ulinzi wa kutosha ambapo askari watakuwa katika doroa za miguu na doria za magari kila kona ya jiji la Arusha na wilaya zote za mkoa huu ,hivyo waumini wa dini mbalimbali wasiwe na hofu pindi watakapokuwa wanaendelea na ibada.


Kama ilivyo kwa nyakati zote tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana nasi katika kuwabaini na kuwafichua wahalifu na uhalifu ili kuimarisha amani na utulivu uliopo.


Mwisho tunatoa shukrani za dhati kwa vyombo vya habari radio,magazeti,blogs,televisheni,kwa  ushirikiano mkubwa mnaotoa kwa jeshi la polisi mkoa wa Arusha kwa kuwa mbele katika kufichua, kuelimisha,na kuhabarisha umma juu ya uhalifu.


Jeshi la polisi mkoa wa Arusha tunawatakia heri ya mwaka mpya wa 2017 wakazi wote wa Arusha .


       IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA

                         NAIBU KAMISHANA WA POLISI

                          (DCP)CHARLES MKUMBO

                                  TAREHE 29/12/2016

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

12/28/2016 02:07:00 pm
Na.Vero Ignatus ,Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha limeanza utekelezaji wa Agizo la Rais
John Pombe Magufuli la kuwatafutia wafanya biashara wadogo ‘machinga’
eneo salama kwa ajili ya kuendesha shughuli zao.

Katika utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli, sambamba na kuondoa
kero hiyo, uongozi wa Jiji la Arusha umenza hatua za awali za kujenga
jengo la kufanyia shughuli wafanyabiashara wadogo maarufu kama
‘Wamachinga complex.

Mradi huo unaolengwa kufanyika katika eneo lililopo mkabala na soko la
kilombero kiwannja Namba 69 chenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja,
lililorejeshwa hivi karibuni serikalini na waziri mkuu, Kasim Majaliwa
wakati wa ziara yake mkoani Arusha.

Akiliongelea suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,
Athumani Kihamia alisema eneo hilo lina uwezo wa kuhifadhi
wafanyabiashara wadogo zaidi ya 2000 pamoja na shughuli zao mara baada
ya mradi wa kujenga miundombinu utakapokamilika.

“Baada ya agizo la Rais na kero inayojitokeza tumeamua kufanya haraka
zaidi ambapo hadi jana tumeshaunda kamati inayofanya tathmini ya
ujenzi wa eneo hilo, na lengo ni kuakikisha tutawaondoa
wafanyabiashara kutoka kwenye maeneo hatarishi ambayo wengi ndio
wanayatumia kufanya shughuli zao, hii ni pamoja na kando za barabara
ya Maromboso, stendi kuu na ile ya Col. Middleton,” alisema Kihamia

“Pamoja na kuwa katika uongozi wa jiji ukiwaandalia maeneo mengine ya
kufanyia biashara zao, ni vizuri wafanyabiashara hawa waendeleze
shughuli kwa busara bila kuvunja sheria, hususan za barabarani au
kuvamia sehemu za maduka na biashara za watu wengine, ikiwemo kujali
usalama wao binafsi,maana sasa wamefunga hata badhi ya barabara,”
alisema Kihamia.

Mmoja wa wafanyabiashara wadogo anayeuza viatu, Hussein Issa, ameomba
kusiwepo na urasimu wakati wa ugawaji wa maeneo ya biashara
yaliyotengwa; “tatizo wala sio wingi wa wamachinga, bali ni kwamba
vingozi wakubwa huwa wanahodhi maeneo hayo ili baadae waje kuwauzia
watu wengine, sasa unakuta mtu anamiliki maeneo zaidi ya kumi peke
yake ili ayauze au awakodishie watu,” alisema.

Serikalini yatahadharisha wananchi Arusha na baa la njaa

12/28/2016 01:55:00 pm
Wito umetolewa kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kuchukua tahadharisha , kuanza kuchukua juu ya tishio la baa la njaa kwa kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha.

Tahadhari hiyo imetolewa na  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Gabriel Daqaro
alisema  uhaba wa mvua za vuli ulioikumba Arusha imefanya wakulima
kutopata mavuno mazuri na kuleta dalili tosha za wilaya zake kukumbwa
na njaa.

Kufuatia hilo aliwataka wananchi wa mkoa wa Arusha kupunguza matumizi
mabaya ya chakula walichonacho ikiwemo kusaza, na badala yake
wajiwekee akiba sambamba na wale wasio nacho wanunue wahifadhi.

"Kama mnavyoona upungufu wa mvua kwa msimu huu  ni dalili tosha za
uhaba wa chakula baadae ukizingatia wakulima wengi Arusha wanategemea
kilimo cha mvua  hivyo basi wajitahidi kila mtu kununua chakula mapema
hasa kipindi hiki ambacho bado hakijapanda bei maana hali itakuwa
mbaya zaidi,"alisema.

"Nasema hivyo kwa sababu kwa sasa chakula bado kiko sokoni kwa bei
nzuri, lakini kipindi cha ukame kukifikia mazao hayo yatakuwa ghali
sana hivyo kuwafanya wasiomudu gharama kuanza kulia kulia,"alisema

Mbali na hilo Daqaro aliwataka maafisa kilimo kutembelea wakulima
kuanza kutoa elimu juu ya mazao yanayostahimili ukame lakini pia ya
mda mfupi ili angalau wakulima waache kilimo cha mazoea badala yake
walime kuendana na mabadiliko ya hali ya hewa pia kwa ubunifu wa mazao
ya kulima

"Nasema hivyo kwa sababu nimegundua wakulima wengi wakiona mvua bila
kujua ni kidogo au ya kutosha wanalima mazao waliyozoea, badala ya
yanayostahimili hali ya hewa, lakini pia maafisa ugani wawaelimishe
wakulima wale walio karibu na miundombinu ya maji wajikite kwenye
kilimo cha umwagiliaji"

Kwa Wilaya ya Monduli inayojishughulisha zaidi na ufugaji, Mkuu wa
Wilaya hiyo, Idd Hassan Kimanta aliwataka wananchi wake kupanda nyasi
za kutosha kwa ajili ya malisho.

"Mvua za mwaka huu zimekuwa kidogo sana hivyo kutokana na wilaya yangu
kujishughulisha zaidi na ufugaji, niwatake tu watumie mvua hizi kidogo
kupanda nyasi kwa ajili ya malisho ingali ardhi ina unyevu nyavu hasa
sehemu za Selela, mto wa Mbu, Engaruka, na makuyuni ambapo manyunyu
bado inapita,"alisema.

"Lakini pia watumie  mifugo yao kibiashara badala ya ufahari kwa kuuza
kidogo wanunue chakula cha kuhifadhi tena msimu huu wa sikukuu ambao
mifugo ni bei juu, kuliko kusubiri hadi ikumbukwe na njaa na
kukondeana,"alisema.

Akizungumzia tahadhari hiyo, mmoja wa wakulima Kata ya Terrat Wilaya
ya Arusha, Sailevu Mollel  alisema  kilimo cha mwaka huu kimekuwa
kigumu, kutokana na serikali kutokuchukua tahadhari mapema ya
kutangaza mabadiliko hayo ya hali ya hewa juu ya uhaba wa mvua za
vuli, hivyo kupanda mazao yao ambayo yameishia kukauka na kuwa hasara
kwao.

"Tunasikia wako maafisa ugani kila eneo wanatakiwa kuja mapema kusema
jambo hili, lakini hatuwaoni hadi hasara itokee ndio serikali kuu waje
kusema wakati tumeshataabika, lakini pia pembejeo za kilimo wala
mashamba darasa hakuna vijijini ambako ndio sehemu zenye mashamba,
hivi tunaweza kweli kuepuka baa la njaa hasa sisi wakulima
tunaotegemea kilimo kwa asilimia 100,"alisema Sailevu

MWANAFUNZI AFA MAJI AKIOGELEA HOTEL YA MOUNT MERU ARUSHA

12/28/2016 01:37:00 pm
Mount Meru Hotel
Mwanafunzi  wa darasa la tano  shule ya msingi ya Sekei iliyopo
halmashauri ya Arusha DC wilayani Arumeru Criff Laiza (12), amekufa
maji wakati akiogelea kwenye  bwawa la maji yenye kina kirefu katika
hotel ya kitalii ya Mount Meru iliyoko jijini Arusha .


Tukio hilo limetokea Desemba 26 mwaka huu majira ya saa 12 jioni
wakati marehemu na watoto wengine wakiogelea katika hotel hiyo ikiwa
ni sehemu ya kusheherekea sikukuu ya X-mass .


Kaimu Meneja wa Hotel ya Mount Meru, Eric Mgenya akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi na atalitolea ufafanuzi
baada ya polisi kukamilisha upelelezi wa tukio hilo.


Alisema  baada ya kutokea uongozi wa hotel hiyo, walitumia gari aina
ya Noah lenye namba T.883 DJM pamoja na gari dogo lenye namba T.445
BSC aina ya Toyota Corrola walipakia mwili wa marehemu kwa lengo la
kuokoa uhai wake na walipofika katika hospital ya Aicc na mwili huo
kupimwa waliarifiwa kuwa tayari marehemu alishafariki kitambo.


Baadhi ya watoto  waliokuwa wakiogelea na marehemu  katika hotel hiyo
walisema, marehemu Laiza alihama ghafla kwenye bwawa la watoto na
kwenda kuogelea bwawa  linalotumiwa na watu wazima ambalo wakati huo
hapakuwa na mtu yoyote akiogelea, lakini ghafla hakuonekana tena hadi
alipo kutwa ameelea juu ya maji .


Kwa upande wake Babu wa mtoto huyo Emanuel Meage alisema tukio hilo
limeshtua sana, kwani  mjukuu wake aliaga kuwa anaenda kuogelea katika
hotel hiyo na wenzake hata hivyo alishangaa kupata taarifa za mjukuu
wake kufa maji.


Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wazazi  ambao hawakutaka kutaja
majina yao wameutupia lawama uongozi wa hotel ya hiyo kwa kushindwa
kuwa na usimamizi mzuri na ulinzi wa watoto hao, badala yake wamekuwa
wakijali kukusanya fedha ya kuogelea na kuwaacha watoto wafanye
wawezavyo kitendo ambacho sio sahihi wakidai kuwa eneo hilo ni hatari
na  sio salama kwa mazingira ya mtoto .


Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo alithibitisha tukio
hilo na kueleza kuwa polisi wapo katika hatua ya uchunguzi na
atalitolea ufafanuzi, mara baada ya uchunguzi kukamilika na hakuna mtu
yoyote hadi sasa anashikiliwa kutokana na tukio hilo.

Kijana afariki dunia baada ya Nyoka wake kupigwa hadi kufa

12/28/2016 01:27:00 pm
SeeBait

Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) afariki dunia baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.

Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.

Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.

Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.

Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.

Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.

Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.

Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.

Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel