Top Menu

BASI LAGONGANA USO KWA USO NA LORI LA MIZIGO NA KUUA WATU 34, KUJERUHI 16

12/31/2017 04:05:00 pm


Habari kutoka Kenya zasema kuwa watu 34 wamefariki katika ajali nyingine mbaya ya barabani, iliyotokea leo  Jumapili asubuhi.

Watu 16 wamejeruhiwa wengi wao wakiwa katika hali mahututi, baada ya Basi moja la abiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo, katika maeneo ya barabara ya Sachangwan/ Salgaa, takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Nairobi.

Afisa mkuu wa idara ya polisi wa trafiki maeneo ya Bonde la Ufa, Zero Arome amesema ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa tisa alfajiri, kwenye barabara kuu ya kutoka Nakuru kuelekea Eldoret Magharibi mwa Kenya.

Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya limeandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Tweeter, kuhusiana na ajali hiyo ambapo mabaki ya magari hayo yaliyohusika kwenye ajali, yangali katika eneo la tukio, huku majeruhi wakipelekwa katika Hospitali za Nakuru Level Five na ile ya Molo Sub-County.

Mapema mwezi Disema zaidi ya watu 20 walifariki katika ajali maeneo hayo hayo.


Chanzo- BBC


MWILI WA MAREHEMU MAYAGE WAAGWA LEO NYUMBANI KWAKE MBWENI

12/28/2017 07:12:00 pm

Padre wa Kanisa Katoliki, John Kaniki akiongoza misa ya kuombea mwili wa marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wanafamilia wa marehemu, ndugu na jamaa wakiwa fuatilia ibada ya kuagwa kwa aliyekuwa mwandishi mkongwe Mayage S. Mayage nyumbani kwake Mbweni Kijijini leo.

 Neno la Mungu likisomwa 

Mbunge wa Mtama na Waziri wa zamani wa Habari, Nape Nauye na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole pamoja na ndugu na jamaa wakiwa kwenye ibada ya mazishi Marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye ibada ya kuagwa kwa mwili wa Marehemu Mayage S. Mayage aliyewahi kuwa mwandishi wa habari leo nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.

Na Said Mwishehe, Blogu  ya Jamii

TASNIA ya habari imeombwa kuendeleza mapenzi baina yao kama walivyoonyesha katika ugonjwa wa Mayage S. Mayage aliyefariki juzi. 

Hayo yamesemwa leo  mchana huu na Padre John kaniki wa Kanisa Katoliki katika ibada ya mazishi ya marehemu Mayage iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es  Salaam.

Padre Kaniki amesema maumivu aliyokua akipata kitandani Manage wakati anaumwa aliyatoa kwa ajili ya watu anaowapenda ikiwemo wanahabari wenzie.

Alisema msiba ni sehemu ya kutubia kwa wale wanaobaki hivyo ni vema wote kuwa wanyenyekevu kwa Mungu.

Amesema yeye binafsi alimfahamu Mayage  S. Mayage katika kipindi ambacho alikuwa anaunwa kwani alikuwa akimfanyia maombi na alichojifunza ni upendo na uvumilivu. 

“Alikuwa ni mtu mwenye upendo na huruma, ni vema tukaendeleza mema yake na kubwa zaidi ni kumuombea kwa  Mungu, “amesema Padre Kaniki. 

 Mayage S. Mayage wakati wa uhai wake amesoma katika vyuo mbalimbali vya ndani  na  nje na baada ya kuhitimu amefanya kazi katika maeneo mbalimbali.

Ilipofika mwaka 1995 ndipo alipojiunga na kampuni ya magazeti ya Habari Coparation ambayo sasa ni New Habari na baadae alikwenda gazeti la Raia Tanzania. 

Akizungumza katika maziko ya Mayage S. Mayage, Mhariri Mtendaji wa New Habari, Absolum Kibanda amemuelezea Mayage kama mwandishi aliyeacha alama ya ujasiri na uthubutu katika taaluma. 

Kibanda amesema mchango wa Mayage katika tasnia ya habari na hasa uchambuzi wa habari za siasa.

“Mimi na Mayage pamoja na wengine tuliojariwa pamoja Habari Coparation, anayeweza kumzungumzia vizuri Mayage ni mhariri na mwalimu wetu kitaalum.

MWILI WAWASILI NYUMBANI KWAKE

Mwili uliwasili saa saba na nusu ambapo maombi yalianza kama ratiba ilivyoeleza huku waombolezaji wakiendelea kuwasili.

Miongoni mwa wanahabari waliofika ni wahariri wa vyombo mbalimbali vya magazeti na luninga wakiongozwa na Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba.

Wengine ni wanasiasa ambapo waziri wa zamani wa Habari, Nape Nauye aliwasili akifuatiwa na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole. 

Marehemu ni miongoni mwa wanahabari waliozunguka katika vyumba vingi vya habari, hali hiyo imefanya kuwepo kwa wanahabari wengi msibani


TAMASHA LA TUKUZA UTALII TANZANIA LA ZINDULIWA ARUSHA

12/27/2017 07:15:00 pm
Na.Vero Ignatus Arusha.

Katibu mkuu baraza la Sanaa Tanzania  amewataka wazazi na walezi wa hapa nchini  kuwalea watoto na kuhakikisha kuwa wanaishi katika maadili ili kuzuia mmomonyoko wa maadili.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha la kwanza la Tanzania Tukuza Utalii Genesis 1,Godfrey Ngereza alisema kuwa tanzania imebarikiwa kwa tunu mbali mbali hivyo watanzania hawana budi kuzitunza na kuzilinda.

Aidha alisema kuwa wazazi hawana budi kuwafundisha watoto uzalendo na kuhakikisha kuwa tamaduni zilizopo haziishi.

"Waswahili walisema samaki mkunje Angali mbichi tukiwalea watoto vizuri ni ngumu kuona maadili yanamomonyoka kwa kuwa tutakuwa tumetengeneza watoto wema" Alisema Godfrey

Kwa upande wake Raisi wa Mtandao wa wasanii wa nyimbo za Injili Tanzania(TAGOANE)Dkt.Godwin Maimu Nnyaka alisema kuwa watoto yatima hawahitaji mavazi na chakula peke yake bali kujengewa msingi bora wa maisha yake.

Dkt.Nnyaka alisema wakati umefika wazazi kuwalea watoto katika misingi ya Imara na kuhakikisha wanakuwa wazalendo.

Aidha alisema kuwa kupitia tamasha hilo litasiadia kujenga vijana wenye hofu ya Mungu na kurejesha uzalendo na maadili kwa vijana.

Nao baadhi ya Washiriki akiwepo mmiliki wa kituo cha faraja Ophanage Faraja Maliaki aliishukuru TAGOANE na kuwataka wadau wengine kuungana na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kuwapa faraja kwa kuwa nao wanastahili kuheshimiwa kama watoto wengine.

Katibu mkuu mtendaji Baraza la sanaa nchini( Basata)Godfrey Mngereza akiwa anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha hilo.Picha zote kwa Idhini ya Vero Ignatus Blog
Rais wa Mtandao wa Wasanii wa wasanii wa Muziki wa Injili Tanzania na maandili nchini Tanzania (TAGOANE) Dkt.Godwin Maimu akiwa anazungumza katika ufunguzi wa Tamasha la Tukuza utalii Tanzania lililozinduliwa rasmi Jijini ArushaPicha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi katika mazinhira hatarishai na baadae wakachukuliwa na kupelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto yatima.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Rais wa Tagoane Dkt.Godwin Maimu akiwa anacheza pamoja na watoto katika Tamasha lililoandaliwa la Tukuza Utalii Tanzania lililoandaliwa na Tagoane.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Mgeni rasmi Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la sanaa nchini (BASATA) pamoja na Rais wa Tagoane nchini wakikata keki kama ishara ya Ufunguzi wa Tamasha la Kuza Utalii Tanzania .
Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Shamrashamra zikiendelea 
 Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Faraja wakiwa katika picha ya pamoja  wakiwa na mlezi Faraja Maliaki,wapo zaidi ya watoto 200 katika ukubi wa Club D Jijini Arusha.

Mgeni rasmi kutoka Baraza la sanaa la Taifa (Basata)Godrey Mngereza akifurahi pamoja na watoto yatima katika tamasha lililoandaliwa na Tagoane Jiiini Arusha.
Wakila chakula pamoja na watoto katika Tamasha 
Meza kuu Rais wa Tagoane,Katibu Mkuu mtendaji kutoka Baraza la Sanaa nchini (Basata)Katibu mkuu Tagoane,na wakurugenzi wa vituo vya kulelea watoto yatima Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Jijini Dar es salaam Gifted Wilson akiimba katika uzinduzi wa tamasha la Tukuza Utalii Tanzania Genesis 1 Jijini  Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Muimbaji wa nyimbo za Injili Miriam Makunja kutoka Arusha akiimba. Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Muimbaji Wolter Chilambo kutoka Jijini Dar es salaam akiwa anaimba katika Tamasha hilo.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog

Hellen Masai akutoka Arusha kiimba .Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Katibu mtendaji  wa Baraza la sanaa la Taifa akiwa anafurahia kwenye ufunguzi wa Tamasha la Tukuza Utalii Tanzania likilofanyika Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Katibu mkuu mtendaji wa Baraza la sanaa Nchini (Basata)wa kwanza kushoto akiwa pamoja na Rais wa Tagoane katika uzinduzi wa Tamasha la Tukuza Utalii Tanzania.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog
Watoto wakionyesha mavazi ya ubunifu chini ya Mwanamitindo mbunifu Diana Magesa kutoka Mwanza,Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog

Picha za watoto yatima waliohudhuria katika tamasha la Tukuza Utalii Genesis 1 lililofanyika Jijini Arusha.Picha kwa idhini ya Vero Ignatus Blog

MWANAHABARI MAYAGE S. MAYAGE KUZIKWA MBWENI, DAR

12/27/2017 08:25:00 am


Na Mwandishi Wetu.

Mwanahabari mwandamizi, Mayage Mayage, (56), amefariki dunia jana (Jumatatu) baada ya kuugua kwa muda.

Mayage amekutwa na umauti katika Hospitali ya Misheni ya Mbweni, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa muda wa wiki mbili.

Taarifa kutoka kwa mdogo wake Emmanuel Mayage, alisema kuwa madaktari waligundua kaka yake kuugua saratani na kifua kikuu (TB).

Emmanuel alisema kuwa Mayage atazikwa Alhamis Desemba 28, 2017 katika makaburi ya Mbweni, eneo linaloitwa Maputo.

Taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu Mbweni Kijijini, eneo la Maputo ambako ndugu na jamaa wanakutana.

“Mayage aligundulika kuwa na saratani mwaka mmoja uliopita na alianza matibabu katika hospitali mbalimbali nchini ikiwemo Ocean Road na Muhimbili.

Alisema hali yake iliimarika kwa muda, lakini ikabadilika wiki tatu zilizopita na kusababisha kulazwa katika hospitali ya Mbweni.

Emmanuel alisema kuwa akiwa hospitalini hapo, kaka yake aligundulika  pia kuwa na maradhi ya kifua kikuu na alianzishiwa tiba.

Mayage alianza kazi za uandishi wa habari mwaka 1995, akifanya kazi katika kampuni ya magazeti ya Habari Corporation; inayochapisha magazeti ya Mtanzania, RAI, Dimba, The African na Bingwa.

Baadaye Mayage aliondoka katika magazeti hayo na kuanza kazi ya uandishi wa habari wa kujitegemea, yeye akijiita “mwandishi huru.”

Akiwa mwandishi huru, Mayage alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali nchini, yakiwemo ya Raia Tanzania, MwanaHalisi na mpaka kufariki kwake alikuwa mwajiriwa wa gazeti la TAZAMA.

Salva Rweyemamu, aliyekuwa mhariri mtendaji wa magazeti ya Habari Corporation amemzungumzia Mayage na kueleza kuwa alikuwa mwandishi mzuri, mahiri, asiyeogopa na aliyefanya kazi yake kwa weledi, huku akiwa mchambuzi mzuri wa habari za siasa za nchi hii.

“Mayage hakushindwa kazi yoyote aliyotumwa, ukimwagiza lazima uwe na uhakika wa kuifanikisha, hakika tumepoteza mchapakazi,” alisema Salva kwa masikitiko


RPC Shanna: Atakaefunga Barabara Na Kuchoma Matairi Mkesha Wa Mwaka Mpya Kukiona

12/27/2017 08:09:00 am


Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna ,ametoa onyo kwa watu wenye tabia ya kufunga barabara kwa kuchoma matairi katika mkesha wa mwaka mpya na kupelekea usumbufu kwa watuamiaji wengine wa barabara kuacha kufanya kitendo hicho .

Amesema atakaejaribu kuchoma moto matairi kwenye mkesha huo,jeshi la polisi mkoani hapo litamchukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya kiusalama inavyoendelea hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu ya mwisho wa mwaka ,kamanda Shanna alisema wanazidi kuimarisha doria katika pande zote za mkoa huo.

Alisema kipindi cha sikukuu ya x-mas hali ilikuwa shwarii hivyo wanaendelea na misako ya miguu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na doria hizo zitakuwa mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha watu waishi kwa amani .

Akielezea kuhusiana na hali ya uhalifu katika kipindi cha Januari hadi disemba mwaka huu ndani ya mkoa huo ,kamanda Shanna alisema wamefanikiwa kupunguza idadi ya makosa kwa kiwango kikubwa.

Kamanda huyo alisema,matukio ya makosa ya uvunjaji yamepungua kutoka 771 kipindi kama hicho 2016 na kufikia 233 mwaka huu ikiwa ni tofauti ya matukio 538.

Makosa mengine ni yale ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambayo yamepungua kutoka 31 mwaka jana hadi nane kwa mwaka 2017  tofauti makosa 23.

“Unyang’anyi wa kutumia nguvu  yameripotiwa makosa 43 ,kipindi kilichopita ilikuwa 112 tofauti makosa 69,:;na mauaji makosa yaliyoripotiwa januari hadi disemba mwaka huu ni 34 ,mwaka uliopita ilikuwa 126  tofauti ni makosa 92.” alifafanua kamanda Shanna.

Aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo mara wanapotilia shaka kundi ama mtu ni mhalifu ,kwani kila mmoja ana wajibu wa kudhibiti vitendo vya uhalifu .

Kamanda Shanna ,alisema Pwani yenye utulivu,amani ,yenye kushikamana inawezekana endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake.

UBALOZI WA KUWAIT WAKABIDHI VIFAA VYA WALEMAVU NA MISAADA MBALIMBALI MKOANI TABORA

12/26/2017 11:05:00 pm


Kutoka kushoto, Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mh. Jasem Al-Najem, Naibu Waziri wa sera, Bunge, Kazi, vijana, ajira na walemavu Mh Stella Ikupa, na Mwenyekiti wa Dr Amon Mkoga Foundation. Ubalozi wa Kuwait umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora.

PICHA: Tundu Lissu akiwa amesimama kwa miguu kwa mara ya kwanza

12/26/2017 10:56:00 pm


Hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inaendelea kuimarika na ameanza rasmi kufanya mazoezi ya viungo katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu ya majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma mnamo Septemba 7, 2017.

Picha kutoka Hospitali ya Nairobi imemuonesha Lissu akifanya mazoezi ya kusimma kwa msaada wa madaktari wa hospitali hiyo. Lissu ameanza mazoezi madogo ya kuimarisha misuli ya miguuni ili aweze kutembea.

Akizungumza kutoka Hospitalini hapo, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanansheria Tanganyika (TLS), amesema “Wapendwa wote wiki iliyopita niliwataarifu kwamba  madaktari wangu wamesema nitasimama, nitatembea na nitarudi Tanzania.

“Leo Boxing Day nimeweza kusimama kwa mguu mmoja kwa msaada wa mababa cheza kama inavyoonekana, hatua inayofuata nitawajulisheni.

“Hatua inayofuata ni magongo kesho na nitawajulisheni hatua nyingine katika matibabu yangu accordingly, Wasalaam,”  Mhe. Tundu Lissu.

TANESCO YAFURAHISHWA NA HATUA ZA SERIKALI KULINDA VYANZO VYA MAJI YA KUFUA UMEME

12/26/2017 10:54:00 pm

INAELEZWA kuwa umeme wa maji, (Hydro power) ndio umeme wenye bei nafuu zaidi ukilinganisha na umeme unaotokana na vyanzo vingine.

Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa TANESCO anayeshughulikia uzalishaji (Power Generation), Mhandisi Abdallah Ikwasa, matumizi ya juu ya umeme nchini kwa sasa ni Megawati 1,060, kati ya hizo, TANESCO kwa kutumia mitambo yake, huzalisha Megawati zaidi ya 1,000, na kati ya hizo, Megawati 381 zinatokana na umeme unaozalishwa kutokana na maji, (Hydro powere) kutoka vituo vinne vya umeme wa maji vya Kidatu, Mtera, New Pangani Falls, Hale na Nyumba ya Mungu.

Hata hivyo katika siku za karibuni shughuli za kibinadamu zimekuwa zikiongezeka kwenye vyanzo vya maji yanayoelekea kwenye vituo vya kufua umeme, na hivyo kutishia shuhghuli za uzalishaji umeme kwenye vituo hivyo.

Mhandisi Ikwasa alitoa mfano Mto Pangani ambapo yapo maeno ambayo shughuli za kilimo zinaendelea karibu na mto, na madhara yatokanayo na shughuli hizo hupelekea kingo za mto kuwa dhaifu na wakati wa mvua maji yanachukua udongo na kuingiza kwenye mto na hivyo kina cha mto kinakuwa kifupi.

“Sasa kipindi ambacho mvua zinanyesha unatarajia maji mengi yatiririke kwenye mto lakini kwa sababu kina kimepungua mto hauwezi kubeba yale maji na badala yake maji yanasambaa na kusababisha mafuriko na mbaya zaidi hayafiki kwenye mabwawa kwa kiwango kinachohitajika.” Alisema Mhandisi Ikwasa.

Alisema TANESCO kama wadau wakubwa wa maji wamekuwa wakishirikiana na mamlaka zinazosimamia mabonde, ili kuelimisha watumiaji wengine wa  maji.“Tunataka kuhakikisha kwamba, kunakuwepo na matumizi endelevu ya maji, tunatambua wananchi wanahitaji maji kwa kilimo na sisi tunayahitaji kwa uzalishaji umeme kwa hivyo yakitumika vizuri yanaweza kufanya kazi zote.” Alisema.

Mhandisi Ikwasa aliipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazochukua kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa.“Makamu wa Rais aliunda kikosi kazi cha kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa na juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda.” Alisema.

Ili kuhakikisha wananchi wanajenga dhana ya umiliki wa miundombinu ya TANESCO, Shirika limekuwa likishirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia kutoa huduma za afya, elimu ya awali na usafiri katika maeneo yanayozunguka vituo vya kuzalisha umeme.

“Tunataka wananchi wafahamu kuwa pamoja na kwamba kazi yetu ni kuzalisha umeme, lakini tunataka tuwe sehemu ya maisha yao, kwa kusaidia mambo ya kijamii kama vile kutoa elimu bure ya awali, zahanati, na usafiri wa basi unaosaidia wananchi kusafiri kuelekea kwenye shughuli zao, tunadhani kwa ushirikiano huu, wananchi watakuwa wakwanza kulinda miundombinu yetu na pia kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwenye vyanzo vya maji.” Alisema Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji.

Ili kuhakikisha ujumbe huo pia unawafikia wananchi wote kupitia vyombo vya habari, wahariri wa vyombo vya habari walipata fursa ya kutembelea vituo vya kufua umeme wa maji vya Hale, New Pangani na Nyumba ya Mungu, vilivyoko mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, kituo cha Mtera kilichoko mkoani Iringa na Kidatu mkoani Morogoro ili hatimaye watoe elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya vyanzo vya mito ambayo maji yake ndio huelekea kwenye vituo vya kufua umeme. Meneja wa kituo cha kufua umeme wa maji cha Kidatu, Mhandisi Anthony Mbushi, (kushoto), akizungumza kuhusu jinsi mageti ya kuruhusu maji kwenye mabwawa kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme yanavyofanya kazi. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji umeme. Mhandsisi Abdallah Ikwasa. Wananchi wa Kidatu, wakisubiri usafiri wa basi la Shirika la Umeme TANESCO, kuwapeleka kwenye mnada ili kuuza mazao yao. Usafiri huo hutolewa bure na Shirika katika mpango wake wa Corporate Social Responsibility (CSR) ili kujenga uhusiano mwema.

Moja ya mashine za kufua umeme wa maji, (turbine), kituo cha Hale


 Wasimamizi wa kituo cha kudhibiti mfumo wa umeme cha Mtera.
 Bwawa la New Pangani Water Falls.


 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza jambo.


Mhandisi Mahenda S.Mahenda, Meneja vituo vya kufua umeme vya Pangani Hydro Systems, akifafanua jambo


 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel