Top Menu

RC GAMBO:MAMBO GANI SERIKALI IYAPE KIPAUMBELE ILI KUONDOA CHANGAMOTO KWA JAMII?

1/31/2017 03:12:00 pm

Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akiingia ukumbini tayari kwa kuanza rasmi kwa kongamano na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Arusha.picha na Vero Ignatus Blog. 

Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa maendeleo katika komgamano hilo.Picha na Vero Ignatus Blog
 Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano cha kimataifa AICC Elishilia Kaaya akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo na yeye kama mwenyeji wa eneo hilo akiwakaribisha katika kituo hicho.Picha na Vero Ignatus Blog
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano ambalo aliwaahidi waandishi kuwa ataliiitisha kwaajili ya kujadili na kupata taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha pamoja na wadaumbalimbali.Picha na Vero Ignatus Blog
Mwenyekiti wa Arusha press club (APC) Akizungumza na katika kongamano hilo.Picha na Vero Ignatus Blog
Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizungumza katika kongamano hilo .Picha na Vero Ignatus Blog
Wa kwanza kushoto ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ,akiwa kwenye kongamano katika kituo uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.Picha na Vero Ignatus Blog
Wadau wa Utalii  kutoka TANAPA wakiwa katika kongamano la wadau wa habari mkoa wa Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.Picha na Vero Ignatus Blog
Wa kwanza kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Mussa Juma ,akifuatiwa na Omary Moyo wakiwa katika kongamano hilo.Picha na Vero Ignatus Blog
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano hilo.Picha na Vero Ignatus Blog
Mwandishi wa habari wa kituo cha luninga cha chanel ten Jamillah Omary akiwa na mkurugenzi mwenza wa Me Production ambaye pia ni mpiga picha wa kituo cha luninga cha ITV Anold Rweyemamu.Picha na Vero Ignatus Blog
Kutoka kulia ni  Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia,aliyeko kushoto kwake ni mwenyekiti wa ccm mkoa ndugu Laizer
Na.Vero Ignatus, Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mashaka Mrisho Gambo amefungua Kongamana kutoa taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha ambapo kongamano hilo limewashirikisha wadau wa habari katika kuangalia na kutafakari na kupitia pamoja na kuangalia mpango mkakati wa maendeleo katika mkoa.

Gambo amesema kuwa kongamano hilo lina lengo la kutoa mrejesho kwa Watanzania kupitia waandishi kwa kipindi cha miezi sita ,na kuangalia mambo gani serikali ikiyapa kipaumbele itaondoa changamoto mbalimbali katika jamii kwa ujumla.

Aidha amesema kuwa utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miezi sita hadi kufikia desemba 2016 umekuwa na mafanikio makubwa ,ambapo amesema kuwa hii ni kutokana na utamaduni wa kufanya na kutekeleza majukumu ya kazi kwa vitendo.

Amesema utekelezaji huo umechangia katika kuboreka kwa maeneo mbalimbali ya sekta muhimu katika kukuza uchumi katika mkoa hasa pato la mkoa na wananchi moja kwa moja.

“Katika kipindi hiki,miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na kupewa kipaumbele cha kutosha hivyo kwa namna moja kutekeleza mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini (MKUKUTA II)katika mkoa na taifa kwa ujumla”alisema Gambo.

 Amesema kuwa Mkoa umesimamia utekelezwaji wa shughuli za serikali na kushuhudia mafanikio katika sekta za kilimo,afya,maji,barabara,mofugo,maliasili na nyinginezo kama takwimu zilivyowasilishwa .

Amesema kuwa serikali imejipanga kuhangaika na wale wote ambao wanachochea migogoro kwa wananchi na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi hatutawafumbia macho.

Kwa upande wamafanikio utekelezaji wa mkoa kuanzia mwaka 2005 mkoa ulikuwa na shilingi 723,809 milioni kwa mwaka huo mkoa ulikuwa wa (9) katika kuchangia patao la Taifa,ambapo pato la mkazi lilikadiriwa kuwa shilingi 506,902 kwa mwaka sawa na shilingi 1,389 kwa siku.

 Kwa mwaka 2010 pato la mkoa wa Arusha lilikuwa shilingi 2,136,514milioni kwa kuchangia pato la taifa Arusha ilikuwa ya 7.mwaka huo pato la mkazi wa Arusha lilikuwa shilingi 1,283,361 kwa mwaka sawa na shilingi 3,516 kwa siku.

Hadi mwaka 2015 pato la mkoa linakadiriwa kuwa shilingi 4,271,447milioni.
 kwa takwimu hizo pato la mkazi wa Arusha lilikuwashilingi 2,322,031 milioni kwa mwaka ni sawa na shilingi 6,361 kwa siku.MKUU WA MKOA WA MBEYA MH. AMOS MAKALLA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI MKOANI MBEYA LEO.

1/30/2017 06:33:00 pm

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla  akizungumza na wafanyabiashara pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoani Mbeya.
 Mkuu wa mkoa amefanya kikao cha mazungumzo na wafanyabiashara mkoa wa Mbeya pamoja na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mbeya, wadau wa biashara na wakurugenzi juu ya kukuza na kupanuka kwa biashara mkoani wa Mbeya. Picha na Mr.Pengo Mmg
Mmoja wa wafanya biashara akichangia mada wakati wa mkutano na Mkuu wa mkoa wa Mbeya
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini Mh.William Ntinika katika kikao na wafanyabiashara

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla  akijib baadhi ya maswali ya wafanyabiashara walioudhuria mkutano huo.

Baadhi ya wafanyabiashara, wadau mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa jiji la Mbeya wakifuatilia mkutano wa mkuu wa mkoa wa Mbeya
Mkutano ukiendelea katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya leo                 
 
 

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA (UN) PIA AHUDHURIA MKUTANO WA AU MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

1/30/2017 06:22:00 pm
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Marais wa wa mataifa mbalimbali  katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Abba nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Malawi Peter Mutharika kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na Rais wa Malawi Peter Mutharika pamoja na viongozi wengine mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Kidemokrasia ya Sahrawi(SADR) Brahim Ghali katika Ofisi za  Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. 

PICHA NA IKULU

TAZAMA YATAKIWA KUBANA MATUMIZI ILI KUONGEZA UZALISHAJI

1/30/2017 06:15:00 pm

Kampuni ya Kusafirisha Mafuta Ghafi ya TAZAMA imetakiwa kutumia uchumi kushusha gharama za matumizi ili kumudu ushindani wa soko Nchini Zambia.

Wito huo umetolewa hivi karibuni kwa nyakati tofauti na Mawaziri wa Nishati wa Tanzania na Zambia, Profesa Sospeter Muhongo (Tanzania) na Mabumba David (Zambia) walipokuwa wakizungumza na wafanyakazi wa Vituo vya Kusukuma Mafuta (Pumping Stations) vilivyopo Mkoani Mbeya na Iringa wakati wa ziara ya kutembelea vituo hivyo.

Profesa Muhongo alisema dhamira ya Serikali za Tanzania na Zambia ni kuhakikisha Bomba pamoja na Mfumo mzima wa uendeshaji wa kampuni hiyo vinaboreka na kuweza kushusha bei ya mafuta ili kumudu ushindani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David (nyuma yake) wakikagua Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi (Pumping station) cha TAZAMA kilichopo Mkoani Mbeya.

 Alisema kampuni ya TAZAMA haiwezi kuendelea na utendaji wa kizamani huku ikitumia gharama kubwa kwenye uendeshaji na hivyo kusababisha kuuza mafuta yake kwa bei ya juu ikilinganishwa na wauzaji wengine kwenye soko.

Aliongeza kwamba zinahitajika jitihada za makusudi kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kwa lengo la kuweza kuingia kwenye ushindani wa soko.

Alisema teknolojia inayotumiwa na kampuni hiyo kwa ujumla wake imepitwa na wakati na ili kuongeza uzalishaji ni muhimu kuhakikisha teknolojia hiyo inaboreshwa sambamba na uboreshwaji wa utendaji wa wafanyakazi wake. “Hampaswi kuridhika na kiwango mnachosafirisha kwani ni kidogo sana ikilinganishwa na hapo awali; mkiendelea hivi mnaweza kujikuta mnasafirisha hata lita laki moja,” alisema.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akikagua moja ya mtambo wa Kusukuma Mafuta Ghafi wa TAZAMA Mkoani Iringa.

Kwa upande wake Waziri David alisema TAZAMA inapaswa kuelewa dhamira ya Serikali hizo mbili ili ifanye jitihada ya kufikia malengo hususan ikizingatiwa kwamba mahitaji ya mafuta nchini Zambia yameongezeka tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Alisisitiza kuwa ni lazima kukafanyika mabadiliko ya kiteknolojia na kiutendaji ili kufikia lengo na alitaja sababu mojawapo inayosababisha mafuta ya TAZAMA kuuzwa kwa bei ya juu kuliko wengine ni kwamba mafuta yanayosafirishwa ni machache wakati gharama ya usukumaji wa mafuta hayo inabaki kuwa kubwa.

“Mkisafirisha mafuta mengi ni lazima gharama zitapungua na hivyo mtaweza kuuza mafuta yenu kwa bei ndogo ikilinganishwa na wengine,” alisema.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na wafanyakazi wa Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi cha TAZAMA kilichopo Mkoani Iringa. Kulia kwake ni Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Zambia, Brigedia Jenerali Emelda Chola.

Aliwaasa wafanyakazi wa TAZAMA kuwa waelewa na kukubali kubadilika kwa faida yao binafsi na kwa faida ya nchi za Tanzania na Zambia kwa ujumla.

“Nyie mtakua sehemu ya mabadiliko na mabadiliko hayo ni kutoka kwenye Usafirishaji wa Tani 650,000 hadi kufikia Tani milioni 1.1 ambayo ndio uwezo wa Bomba,” alisema Waziri David. Alisema kuwa kwa tathmini iliyofanywa ya mahitaji ya mafuta Nchini Zambia ifikapo Mwaka 2030, itakuwa ni tani milioni 4 na kwa namna ambavyo kampuni hiyo ilivyo hivi sasa, haitoweza kukidhi soko hilo hivyo ni vyema ikajipanga kujiboresha.

Mawaziri hao wapo katika ziara ya kutembelea njia ya Bomba la Mafuta Ghafi la TAZAMA na Vituo vya Kusukuma Mafuta (Pumping stations) kwenye maeneo yote linapopita Bomba hilo.
Mfanyakazi wa TAZAMA katika Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi cha Iringa, Yerusalem Anthony akiuliza swali na kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresha kampuni husika mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia) na Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David (kulia).
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kutoka kulia waliosimama) na Waziri wa Nishati wa Zambia, Mabumba David (kushoto kwake) pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha Kusukuma Mafuta Ghafi cha TAZAMA cha Mkoani Iringa.
Moja ya Mtambo (Pampu) wa Kusukuma Mafuta Ghafi wa TAZAMA Mkoani Iringa. Pampu hizo zilifungwa Mwaka 1968

HUU NDIO MUONEKANO MPYA WA RAY C

1/30/2017 06:08:00 pm
Mashabiki wamjia juu Ray c.


 

BODI YA WAKURUGENZI DCB YALIPONGEZA TAWI LA MAGOMENI KWA KUFANYA VIZURI 2016

1/30/2017 06:02:00 pm
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


BENKI ya DCB wamewazawadia tuzo tawi la Magomeni inayojulikana kama Chairman's awards baada ya kufanya vyema kiutendaji na kuwapiku matawi mengine ya benki hiyo na kutakiwa kuendelea kudumisha ufanisi wa kazi.

Akizungumza kabla ya kutangaza kwa mshindi, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa alisema kuwa matawi ya benki hupimwa kwa kutekeleza viashiria mbalimbali ikiwemo ukuaji wa amana zitokanazo na akaunti za hundi na akiba kwa asilimia 15, utoaji wa mikopo kwa asilimia 15, faida kabla ya kodi, ufuatiliaji wa mikopo chechefu na asilimia ya mikopo chechefu.

Mkwawa alisema kuwa, ili mshindi aweze kutangazwa ni lazima tawi husika kufikisha alama 60 ambzo zitagawiwa katika kutekeleza viashiria 10 na shindano hili lilianza toka Oktoba 2011 na tawi la Tabata ndilo lilikuwa la kwanza kuanza kuchukua tuzo hiyo.

Mbali na hilo, benki hiyo iliweza kutoa zawadi kwa meneja wa mikopo kwa vikundi kiasi cha shillingi laki tano (500,000), wasimamizi 9 wa mikopo kutoka matawi yoye kila mmoja akizawadiwa shilingi laki tatu (300,000) na maafisa watano kila mmoja shilingi laki mbili (200,000) ikiwa na lengo la kuwapatia motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kusimamia vizuri uendeshaji wa mikopo hiyo.

Makamau Mwenyekiti wa bodi hiyo, Lucian Msambichaka amewapongeza tawi la Magomeni kwa jitihada kubwa walizozionyesha na kuwataka kuendelea kufanya vizuri zaidi na kuwasisitiza kuongeza ufanisi wa kibiashara kwa kuleta changamoto ya kushindanisha matawi hayo katika kila nyanja za huduma za kibenki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo kwa tawi la Magomeni baada ya kufanya vyema kiutendaji na kuwapiku matawi mengine ya benki hiyo na kutakiwa kuendelea kudumisha  ufanisi wa kazi.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichaka akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo kwa tawi  la Magomeni baada ya kufanya vyema kiutendaji na kuwapiku matawi mengine ya benki hiyo na kutakiwa kuendelea kudumisha  ufanisi wa kazi.
 Makamau Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichaka akikabudhi zawadi kwa  na maafisa watano kila mmoja shilingi laki mbili (200,000) ikiwa na lengo la kuwapatia motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kusimamia vizuri uendeshaji wa mikopo hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichakana (wa pili kutoka kulia)akitoa zawadi ya mfano wa hundi kwa maafisa tisa  kila mmoja shilingi laki tatu(300,000) ikiwa na lengo la kuwapatia motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi na kusimamia vizuri uendeshaji wa mikopo hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichakana (wa pili kutoka kulia) akimkabidhi  Meneja wa Mikopo ya vikundi Maria Kabeho mfano wa hundi wa shilingi laki tano (500,000) akishuhudiwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa pamoja na wajumbe wa bodi hiyo Maharage Chande na Stephen Mulisa.
 Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichakana akimkabidhi alyekuwa meneja mwandamizi wa tawi la Magomeni Gray Ndandika tuzo ya Chairman's awards baada ya kuibuka kidedea.
Wafanyakazi wa tawi la Magomeni wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichakana,  Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa pamoja nawajumbe wa bodi hiyo Maharage Chande na Stephen Mulisa.
  Washindi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichakana, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa pamoja na wajumbe wa bodi hiyo Maharage Chande na Stephen Mulisa.
 Wafanyakaiz wa Magomeni wakiwa wanashangilia ushindi baada ya kutangazwa.
Makamu Mwenyekiti wa bodi ya DCB Lucian Msambichakana (wa pili kutoka kushoto) akipiga makofi sambamba na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa pamoja na  wajumbe wa bodi hiyo Maharage Chande na Stephen Mulisa. Picha na Zainab Nyamka.
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel