Top Menu

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI AFARIKI DUNIA , CHAMWITA WAMLILIA

2/28/2017 02:20:00 am
Image may contain: 1 person, smiling, stripes
Muimbaji wa muziki wa Injili Atupyanie Paulo Metili enzi za Uhai wake
Baadhi ya Wachungaji  kutoka Dayosisi ya Kaskazini kati na kutoka mathehebu mengine ya Kikristo waliohudhuria kwenye msiba wa Mke wa mwenzao Mchungaji Paulo Metili.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mamia ya waombolezaji waliojitokeza kumuaga aliyekuwa Muimbaji wa njimbo za Injili Atupyanie Paulo Metili ambaye pia alikuwa mke wa mchungaji Paulo Metili wa kanisa la KKKT mjini kati  Dayosisi ya Kaskazini ,Alizaliwa tare 25/12/1976 aliyefariki tarehe 20/2/2017 na kuzikwa katika makaburi ya kanisa huko Elboru mkoani Arusha 25/2/2017.Picha na Vero Ignatus Blog


Gari lililoubeba mwili wa marehemu Atupyanie Paulo Metili ukiwasili katika viwanja vya kanisa la KKKT Usharika wa Elboru .Picha na Vero Ignatus Blog.
Jeneza lililobeba mwili wa Muimbaji wa nyimbo za Injili Atupyanie Paulo Metili(mama mchungaji Metili) likishushwa kutoka kwenye gari .Picha na Vero Ignatus Blog.
Jeneza likiwa tayari kanisani tayari kwa ndugu jamaa na marafiki kuuaga mwili.Picha na Vero Ignatus Blog.

 
Mume wa marehemu mchungaji Paulo Metili akiwa na watoto wake wawili aliyeko kushoto kwake na kulia kwake .Picha na Vero Ignatus Blog.
CHAMA cha waimbaji wa muziki wa Injili kanda ya kaskazini(CHAMUITA) wakiimba wimbo maalum katika msiba huo kumuaga muimbaji mwenzao. Picha na Vero Ignatus Blog.Mkuu wa jimbo Arusha Magharibi mchungaji Isac Kisiri akizungumza katika msiba huo.Picha na Vero Ignatus Blog
Msaidizi wa askofu Dayosisi ya Arusha Kati Gidion Kivuyo akitoa neno la faraja kwa waombolezaji.Picha na Vero Ignatus Blog

Aliyebeba msalaba ni mchungaji Paulo Metili ambaye ni Mume wa marehemu pamoja na watoto wake wakielekea makaburini tayari kwa kwenda kuuhifadhi mwili wa mpendwa wao.Picha na Vero Ignatus Blog
Aliyevaa joho jeusi ni Mchungaji Kiongozi Usharika wa Ilboru akiwa na Naibu katibu mkuu Dayosisi ya Kaskazini kati  Godson Abel ,aliyevaa joho jeupe.Picha na Vero Ignatus Blog.


Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali mapingamizi dhidi uya Lema

2/27/2017 11:28:00 pm


Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali mapingamizi (rufaa) ya Serikali dhidi ya maamuzi ya Mahakama Kuu kwa msingi kwamba hayana mashiko na kuiagiza Mahakama Kuu kuendelea na utaratibu wake wa kutoa haki ya dhamana mapema iwezekanavyo!
 
Kutoka kushoto (viongozi wa CHADEMA): Mwenyekiti Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa; Katibu Mkuu Vincent Mashinji, Mwenyekiti Taifa Freeman Mbowe na Katibu wa Mkoa wa Arusha Kalisti Lazaro.

RAIS MAGUFULI AMTEUA NUNDU KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TTCL,AMWAPISHA ANDENGENYE KUWA KAMISHNA JENERALI JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

2/27/2017 11:13:00 pm
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Bw. Omary Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Omary Rashid Nundu umeanza tarehe 24 Februari, 2017.

Bw. Omary Rashid Nundu anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Prof. Tolly Salvatory Augustine Mbwete.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Thobias Emir Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Kamishna Jenerali Thobias Emir Andengenye anachukua nafasi ya Kamishna Jenerali Pius M. Nyambacha ambaye amestaafu.

Pia, Mhe. Rais Magufuli amewaapisha Mabalozi wanne walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kama ifuatavyo;

Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Nairobi, Kenya ambako anachukua nafasi ya Mhe. John Haule ambaye amestaafu.

Mhe. Silima Kombo Haji ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Khartoum, Sudan ambako anakwenda kufungua Ubalozi.

Mhe. Abdallah Abas Kilima ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Muscat, Oman ambako anachukua nafasi ya Mhe. Ali Ahamed Saleh ambaye amestaafu.

Mhe. Matilda Swila Masuka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Seoul, Korea Kusini ambako anakwenda kufungua Ubalozi mpya

Aidha Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mabalozi wote wanne wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa ummakilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU


 

   

 

 

 

  

  

 

 


 

 

 

 

 

 

 


 

 

 


TAASISI YA SEKTA BINAFSI YAJIPANGA KUWAJENGEA UWEZO WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI

2/27/2017 08:45:00 pm


Na Jovina Bujulu MAELEZO Dar es Salaam

TAASISI ya sekta binafsi nchini (TPSF) imetoa wito kwa wahitimu na vijana waliopo vyuoni kuchangamkia fursa ya mpango maalum uliobuniwa baina yake na Serikali ambao umekusudia kuwajengea ujuzi kabla ya kuajiriwa ili waweze kufanya kazi kwa weledi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye wakati alipokuwa akichangia mada kuhusu wahitimu wa vyuo vikuu kushindwa kuonyesha ujuzi baada ya kuajiriwa.

“Upo upungufu mkubwa wa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wengi wanaomaliza vyuo vikuu nchini na imedhihirika kuwa wahitimu hao hushindwa kufanya kazi kwa weledi wanapokuwa wameajiriwa na sekta mbali mbali.

Alisema kuwa mpango huo maalum umeanzishwa kwa lengo la kuwatayarisha wahitimu wa vyuo kupata mafunzo ya muda mfupi ili kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo pindi wanapoajiriwa au kutaka kujiajiri.

Simbeye alisema Mpango huo pia umekusudia kuwapunguzia gharama waajiri, hasa wa sekta binafsi kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakitumia pesa nyingi kwa kuwapeleka waajiriwa wapya katika mafunzo ili waweze kumudu kazi zao.

Akifafanua zaidi alisema katika mpango huo waajiriwa wataweza kupata mafunzo mtambuka na gharama zote za mafunzo zinagharimiwa na Serikali.

“Chini ya mpango huu, wahitimu na vijana walioko vyuoni wanatakiwa kujiandikisha kwa hiari, na baada ya mafunzo inakuwa rahisi kwao kupata ajira kupitia katika sekta binafsi au makampuni” aliongeza Bwana Simbeye.

Aidha Bwana Simbeye alisema kuwa mpango huo pia utawawezesha wahitimu kutengeneza mazingira ya kuanzisha biashara nyingi na kupanua biashara zilizopo ili waweze kupata fursa nyingi za kuajiriwa na kujiajiri hasa katika wakati huu ambao nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda.

Akizungumzia mpango huo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana, na Walemavu), Anthony Mavunde alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa kila chuo kinajitengenezea mwongozo wake unaomwezesha kila mwanafunzi kupata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo.

Aidha aliongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu na unafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kutoa wito kwa sekta binafsi na waajiri kutoa maoni yao ili kuboresha mpango huo.

Halmashauri Nchini Zaagizwa Kuwasilisha Taarifa Kuhusu Maendeleo ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Nchini.

2/27/2017 08:40:00 pm
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika Halmashauri nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Kamati ya Uongozi ya MKURABITA na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
 Watendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miji Dkt. Mkuki Hante pamoja na Mkurugenzi wa Utawala kwa Serikali za Mitaa Bibi. Miriam Mmbaga wakifuatilia mjadala wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na MKURABITA kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akipokea taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akisoma taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati(hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala mara baada ya  mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya hiyo Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Na: Mpiga Picha Wetu.

 

KIGWANGALLA: KUTANGAZA MAJINA YA MASHOGA HADHARANI NI SAWA NA KUFUNGULIA JINI LILILOWEKWA KWENYE CHUPA"

2/27/2017 08:26:00 pm
Leo February 27 2017 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilikuwa na mpango kuwa na Mkutano na Waandishi wa habari ulioandaliwa kuwataja Watanzania wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kujiuza mitandaoni lakini baadae leo Mkutano huo uliahirishwa.

Baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameandika kupitia account yake ya twitter haya……
“Kwa orodha tuliyonayo, kutangaza majina ya mashoga hadharani, ni sawa na kufungulia jini lililowekwa kwenye chupa!”-Kigwangalla.
“Kwa sababu za kimkakati, na ili kuepuka kuharibu ushahidi, tutalishughulikia jambo hili kwa namna nyingine, tutawajulisha matokeo kila hatua”-Kigwangalla.

chanzo Millardayo

Mwanariadha afia getini Kili Marathon

2/27/2017 11:47:00 am
Mwanariadha, Charles Maroa kutoka nchini Kenya amefikwa na maut katikahospitali ya KCMC mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuanguka katika geti la viwanja vya Ushirika wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu Marathon za Kilimanjaro zilizofanyika jana Februari 26.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, RPC Raymond Mtafungwa alisema kuwa Mwanariadha huyo alikutwa na umauti huo jana majira ya saa tano asubuhi katika hospitali la KCMC mjini Moshi baada ya kuanguka.

"Tumepokea taarifa za kifo cha Mwanariadha huyo alietambulika kwa jina la Charles Maroa,ambaye ni raia wa Kenya (Mkurya), baada ya kukumbwa na hali hiyo alikimbizwa hospitali ya KCMC kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka ghafla katika geti kuu la kuingia katika viwanja vya Ushirika hapa mjini Moshi wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu Marathon za Kilimanjaro na tunaendelea na uchunguzi kujua nini kilitokea mpaka kuelekea kifo chake" alisema.

Mwili wa Mwanariadha huyo umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.

Rais Museveni awakaribisha Watanzania kuwekeza Uganda

2/27/2017 11:27:00 am
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni ametoa wito wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini Uganda.

Rais Museveni ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea viwanda vya Kampuni ya  Bakhresa vinavyozalisha Unga na Juisi  vya  Buguruni na Vingunguti jijini Dar es Salaam.

“Nawakaribisha  wafanyabiashara wa Kitanzania kuja nchini Uganda kuwekeza kwani kufanya hivyo kutasaidia kuzalisha bidhaa, upatikanaji wa soko pamoja na ajira,” alisema Rais Museveni.

Kauli hiyo ya Rais Museveni imetokana na mafanikio yanayotokana na Mwekezaji wa Kitanzania Said Salim Bakhresa aliyewekeza nchini Uganda ambapo anamiliki Kiwanda cha kusanga ngano nchini humo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa  Mahusiano wa Kampuni za Bakhresa Hussin Sufiani amesema kwamba Kampuni hiyo iko mbioni kuongeza uzalishaji wa unga wa ngano kutoka tani 1,100 hadi kufikia tani 2,000 kwa siku nchini Uganda.

Aidha, amesema kutokana na uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Uganda jumla ya Waganda 650 wamenufaika na ajira mbalimbali ambazo zinasaidia kuwapatia kipato.

Kwa upande wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage amesema kuwa Uganda na Tanzania zimeingia makubaliano  ya ushirikiano katika sekta mbalimbali  ikiwemo sekta ya viwanda.

Amesisitiza Watanzania wanaweza kwenda kuwekeza nchini Uganda kwa vile nchi hiyo wanalima tani milioni 4 za mahindi lakini wana uwezo wa kutumia tani milioni moja pekee, hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini humo.

“Tunawahamasisha wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania kuwekeza katika nchi zao ili kuzalisha , bidhaa na ajira za kutosha kwa wananchi,” alisema Waziri Mwijage.

Waziri Mwijage alitoa Wito kwa Watanzania kushiriki katika uchumi wa viwanda kwa kufanya uzalishaji wa bidhaa zinazotumika viwanda mfanio kwa kulima matunda au mbogamboga.

Rais Yoweri Museveni aliwasili nchini jana kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili ambapo akiwa nchini alifanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kutembelea Viwanda vya  Said Salim Bakhresa vya Tazara na Vingunguti.
Na Immaculate Makilika na Lilian  Lundo- MAELEZO

Makubwa haya!! Mtu mmoja atiwa mbaroni kwa kujaribu kujikata uume

2/27/2017 11:18:00 am
Jeshi la Polisi mkoani Singida, inamshikilia mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 60 kwa tuhuma za kujaribu kujiua baada ya kukata kwa panga  uume wake hadi kuutenganisha kabisa na mwili, kwa madai ya kuchoka kuhangaika na ugumu wa maisha unaomkabili.

Mwanaume  huyo Ntandu Mahumbi  mkulima na mkazi wa Kijiji cha Maghojoa wilaya ya Singida, anadaiwa kutenda kosa hilo juzi saa tano asubuhi, muda mfupi baada ya kurejea nyumbani akitoka kulima shambani.

Alisema mzee Mahumbi amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa chini ya ulinzi wa askari polisi,na pindi uchunguzi utakapokamilika, atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya kutaka kujiawa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida, ACP Debora Magilingimba alisema tukio hilo la kusikitisha, limetokea Februari 23 mwaka huu huko katika kijiji cha Maghojoa
.
Katika tukio la pili, Magiligimba alisema mkulima wa kijiji cha Mwanyonye kata ya Ikhanoda wilaya ya Singida, Salome Mwanga (55) amefariki dunia baada ya kupigwa kichwani kwa jiwe na mtoto wake Ally Ramadhani (30).

Alisema kuwa kifo  hicho kimechangiwa na mgogoro wa kugombea shamba.
Kamanda huyo alisema tukio hilo limetokea Februari, 21 mwaka huu saa nne asubuhi huko katika kijiji cha Mwanyonyi kata ya Ikhanoda.

Alisema siku ya tukio, mtuhumiwa Ally alikuwa analima katika shamba lililopo jirani na nyumbani kwao ambalo mama yake pia hulilima.

“Salome alimwendea Ally na kumtaka asiendelee kulima katika shamba hilo,na Ally aligoma na kumwangiza mama yake aondoke haraka hapo shambani.Salome hakuondoka kitendo kilichosababisha Ally aokote jiwe na kumpiga kichwani na kumsababishia kupata jereha na maumivu makali,” alisema Magiligimba.

Alisema Salome aliweza kukimbizwa katika kituo cha afya cha Ilongero kwa ajili ya kupatiwa matibabu.Hata hivyo ilipofika saa mbili usiku,alifariki dunia.
Alisema wanamshikilia Ally na pindi uchunguzi utakapokamilika,atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya mauaji.

Na Nathaniel Limu, Singida
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel