Top Menu

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI BI. SARAH COOK AMTEMBELEA KAMISHNA JENERALI WA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA BW. ROGERS WILLIAM SIYANGA

3/31/2017 06:27:00 pm

.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cook Leo amemtembelea ofisini kwake Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya  Bw. Rodgers William Siyanga na kufanya mazungumzo ya  namna serikali za  Uingereza  na Tanzania zitakakavyoweza kushirikiana katika kudhibiti tatizo la dawa za kulevya . Katika ziara hiyo Balozi Cook aliambatana na maafisa kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania  Bw. Christopher Kiddle na Bw. Andrew Stephens.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cook (wapili kutoka kushoto) alipomtembelea  Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya  Bw. Rodgers William Siyanga (wa kwanza kulia) ofisini kwake leo asubui Jijini Dar es salaam. Balozi Cook aliambatana na maafisa kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Bw. Christopher Kiddle (wa kwanza kushoto) na Bw. Andrew Stephens (wa tatu kushoto), kutoka kulia (wapili) Makamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na  Kupambana na dawa za kulevya

FRIDAY, MARCH 31, 2017 WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AWASILI NCHINI NA KUPOKELEWA NA RAIS MHE.DKT. MAGUFULI

3/31/2017 06:25:00 pmRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.

Shamra shamra zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

SHULE ZATAKA PEDI KWA AJILI YA WANAFUNZI WA KIKE SHINYANGA,DC AOMBA MSAMAHA WA KODI

3/31/2017 06:22:00 pm


Pamoja na jitihada zinazofanyika kuhakikisha kuwa na vyumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri wanapokuwa katika hedhi lakini bado changamoto kubwa ni upatikanaji wa vitambaa wakati wa hedhi "pedi"kwa watoto wa kike hasa kwa watoto wasio na uwezo.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya waandishi wilayani Kishapu walipotembelea shule mbalimbali kuangalia hali ya upatikanaji wa vyumba kwa ajili ya kujisitiri watoto wa kike wanapokuwa katika hedhi na upatikanaji wa vitambaa ‘pad’ ili kuimarisha usafi wa mtoto wa kike anapokuwa shuleni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu wa wakuu wa shule za msingi na walimu walezi wa wanafunzi wa kike wilayani Kishapu walisema wamejitahidi kuwa na vyumba maalumu kwa ajili ya watoto wa kike kujistiri wanapokuwa kwenye hedhi lakini changamoto ni upatikanaji wa pad kwani watoto wengi hawana uwezo wa kununua pedi.

Walisema shule nyingi hazina uwezo wa kifedha kuweza kununua pedi na kuzigawa bure kwa wanafunzi hivyo kuwaomba wadau mbalimbali wa watoto kujitokeza kusaidia watoto wa kike kwani wazazi wengi wamekuwa wakidai hawana uwezo wa kununua vitambaa hivyo.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyenze iliyopo katika kata ya Mwadui Lohumbo,Yohana Saraton alisema changamoto waliyonayo sasa ni upatikanaji wa vitambaa ‘pad’ kwa ajili ya watoto wakiwa katika hedhi.

“Sisi tuna chumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri lakini pad hazipo tunaomba mashirika na wadau mbalimbali wajitokeze kufadhili ugawaji wa pad katika shule hiyo”,alisema Saraton.

Naye Mwalimu Mlezi wa wanafunzi wa kike katika shule hiyo Leanita Kalinjuna alisema ukosefu wa pad unawafanya baadhi ya wanafunzi wa kike kutohudhuria masomo wanapokuwa katika siku zao ‘hedhi’.

“Kutokana na kukosekana kwa vitambaa hivyo wanafunzi huwa wanatoa taarifa kama wapo hedhi na huwa tunawapa ruhusa,tunaomba kupatiwa vifaa hivyo maana sisi tuna chumba maalum na tuna vifaa vya kuhifadhia pad zilizotumika”,aliongeza mwalimu Kalinjuna.

Kwa upande wake Ofisa Elimu wa mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi alisema ni kweli kuna tatizo la upatikanaji wa vitambaa hivyo kwani bajeti inayotolewa na serikali haijitoshelezi kuhudumia wanafunzi wote wa kike katika shule kwa kuwanunulia pedi.

“Asilimia 10 ya fedha za huduma ya kwanza katika shule haitoshi kuhudumia wanafunzi wote kwani shule zetu zina wanafunzi wengi lakini tunaendelea kuangalia namna ya watoto hawa ili waweze kuhudhuria masomo yao ikiwemo kuwahamasisha walimu walezi wa wanafunzi hao kuwa karibu na watoto wa kike”,aliongeza Kahundi.

“Kuweka chumba maalum katika shule ni sera mpya tuliyoianzisha kupitia mradi wa “School Wash” ambao unatekelezwa kila halmashauri ya wilaya zote japokuwa siyo katika shule zote,pale tunajenga vyoo vipya tumeamua tuwe tunatenga chumba kwa ajili ya watoto wa kike ili kupunguza utoto shuleni”,alieleza Kahundi.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba alishauri vifaa kwa ajili ya watoto wa kike visamehewe kodi vinapoingizwa nchini kwa sababu vina gharama kubwa ukilinganisha kuwa watoto hao hawana ajira.

“Ukisema kwamba shule zitumie pesa za vifaa zinunue haviwezi,kila mtu aangalie kuwa ni jukumu lake kuwahudumia watoto wa kike ,jamii kama jamii ituone sisi wanawake kuwa tuna mahitaji mengine ambayo yanahitaji yaonwe kwa jicho la ziada”,aliongeza Talaba.

Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Vyoo vya wanafunzi (kushoto) na cha walimu (kulia) katika shule ya msingi Nyenze iliyopo katika kata ya Mwadui Lohumbo wilayani Kishapu

Choo cha wanafunzi katika shule ya msingi Nyenze ambacho kina chumba kimoja maalum kwa ajili ya wanafunzi wa kike kinachotumiwa na wanafunzi hao wanapokuwa katika hedhi

Chumba maalumu kwa ajili ya watoto wa kike/wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule ya msingi Nyenze.Pamoja na kuwepo kwa chumba hicho lakini hakuna kifaa chochote kwa ajili ya watoto wa kike wanapokuwa katika hedhi

Chumba maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa kike kikiwa hakina pedi yoyote.

Jukwaa la Wahariri Latoa Tathmini ya iki moja ya Kususia Habari Makonda

3/30/2017 09:26:00 pm


Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia. Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.

Aidha, Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu. Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.

Wakati huo huo, kituo cha Clouds kimepongezwa kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda.

Bodi pia imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.

Theophil Makunga,

Mwenyekiti TEF

Imetolewa Leo,

Machi 30, 2017

WAZIRI MAKAMBA ATOA MAAGIZO KWA MAMLAKA YA NGORONGORO

3/30/2017 08:20:00 amNa Lulu Mussa,Ngorongoro 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira nchini Mhe. January Makamba amesema kuwa ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili kudhibiti mimea inayohatarisha uoto wa asili katika Mamlaka ya Ngorongoro. 

Katika kutatua changamoto hii, Waziri Makamba ameagiza kuundwa kwa jopo la wataalamu kutoka Tume ya Sayansi na Tecknolojia, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Hifadhi za Taifa za Tanzania, Wizara ya Kilimo na Mifugo na Mamlaka ya Ngorongoro ndani ya miezi sita kufanyika kwa utafiti wa kina wa kisayansi wa kubaini mbinu mpya ya kupambana na mimea hiyo vamizi inayotawala mimea inayotumiwa na wanyama. 

Akizungumza katika kikao kilichojumisha Wahifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro na Wajumbe wa Baraza la wafugaji, Waziri Makamba amesikitishwa na kitendo cha Uongozi wa Mamlaka ya Ngorongoro kushindwa kuandaa mpango kabambe wa usimamizi wa hifadhi baada ya ule wa awali kuisha muda wake.  Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa Ngorongoro kuandaa mpango huo mapema na kuwa shirikishi. ” Mpango mtakoandaa hakikisheni kuwa unakuwa shirikishi kwa jamii inayozunguka na wadau na Taasisi muhimu likiwemo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo kujionea changamoto za kimazingira. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Baraza la wafugaji (hawapo pichani) katika Wilaya ya Ngorongoro. Wafugaji hao walimweleza Waziri kilio cha muda mrefu cha mradi wa Josho Wilayani hapo, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Ngorongoro na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kuleta ufumbuzi mapema. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo kujionea changamoto za kimazingira.

BALOZI WA KUWAIT NCHINI MHE. JASEM AL-NAJEM NCHINI ATEMBELEA MAKAO YA TAIFA YA WATOTO YATIMA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAAM

3/30/2017 08:13:00 am


Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza na watumishi,watoto yatima katika Makao ya Taifa ya Watoto yatima Kurasini katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali jijini Dar es Salaaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akitembezwa kwenye viunga vya Makao ya Taifa ya Watoto yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akipanda mti katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi bengu za mbogamboga, Afisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Beatrice Lawrance(kulia) leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishina Msaidizi wa Ustawi-wa Jamii,Siman Panga
Kamishina Msaidizi wa Ustawi-wa Jamii, Simon Panga akizungumza katika hafla ya kutembelea miradi mbalimbali katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaaam.

Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akiwakatika picha ya pamoja katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akitembezwa viunga vya Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
Afisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Beatrice Lawrance(kulia)akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.ambapo alishukuru Ubalozi wa Kuwait nchini kwa msaada wa miradi mbalimbali na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikagua mradi wa maji Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MAKAMU WA RAIS WA KLABU YA SIMBA, GEOFREY NYANGE KABURU AZINDUA TAWI LA SIMBA LA KICHWABUTA BUKOBA

3/30/2017 08:07:00 am

Makamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu jana amefungua Tawi la kwanza la  Simba mjini Bukoba na kuweza kuwaunganisha Wana Simba wa hapa Kagera. 

Pia katika Uzinduzi huo wa Tawi ambalo lipo Kashabo pia walikuwepo Wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha Jonas Gerald Mkude, Kichuya na Wengine. Piacha na Faustine Ruta, Bukoba

Pia wameweza kumshukuru ndugu Omary Makoye, Mratibu wa Tawi wa Klabu ya Simba kwa kuwatembelea wakiwa katika Mchakato wa kuunda Tawi hilo. 

Na pia wameshukuru kwa msaada aliowapa na ulikuwa ukihitajika kwa muda huo. Shukrani pia kwa Ndugu Sued Mkwambi kwa kukubali kuwa mlezi wao wa Tawi.

Makamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburuakiteta na Wanatawi na wanakagera waliokuwa eneo la Tawi hilo la Kichwabuta.


Mh. Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu(wa pili) kutoka kushoto akiwa na  Viongozi wa Tawi la Kichwabuta lililozinduliwa leo hii mjini Bukoba. Tawi hilo limepewa Jina la Kichwabuta kutokana na kuenzi kazi ya Mwananchama maarufu wa Klabu ya Simba MZEE HUSSEIN OMARY KICHWABUTA ambaye alishiriki kikamilifu kama mpenzi na Mwanachama wa Simba katika maendeleo ya Klabu hiyo ya Simba.

 Tawi hilo mpaka sasa lina Wanachama 160 waliojiandikisha na taratibu zinaendelea kuhakikisha wanapata kadi za uanachama kulingana na utaratibu wa Klabu.

 Tawi linaongozwa na Mwenyekiti Ndugu Priscus Isdory Massawe, Katibu ndg. Fauzu BinaMungu, Mhasibu Ndg. Dickson Ishengoma, Msemaji Ndg. Miraji Kichwabuta na Viongozi wengine ili kuhakikisha wanapata Wanachama wengi zaidi.

Wadau na Wapenzi wa Simba wakiwa tayari kwa Uzinduzi wa Tawi hilo.Wakifuatilia kwa karibu Uzinduzi wa TawiMakamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu akisaini kwenye Kitabu 

Vichwa vya magazeti ya leo.

3/30/2017 06:52:00 am


 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel