Top Menu

Mvua kubwa za masika Pemba zasababisha maporomoko ya ardhi na madaraja kukatika

4/30/2017 10:29:00 pm


 MITI mbali mbali ikiwa imeanguka katika moja ya sehemu ya Barabara ya Chake-Mkoani, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 MAGUNIA 518 ya Karafuu Kavu zikiwa hazikuharibika katika ghala la kuhifadhia karafuu la Shirika la ZSTC Mkoani, baada ya ghala hilo kuanguka sehemu ya Ukuta na gunia tisa kufukiwa na dongo zikiwa na karafuu kavu.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 SEHEMU ya Ghala la Kuhifadhia karafuu la ZSTC Mkoani, likiwa limebomoka baada ya kuangukiwa na mti uliokuwa katika mlima na kupelekea Gunia Tisa za Karafuu Kavu zenye thamani ya Zaidi ya Milioni 5 kufukiwa na dongo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 WATOTO wadogo wakisafisha kwa kutoa dongo nje katika Msikiti wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, baada ya sehemu kubwa ya msiki huo kuangukiwa na Udongo ulioporomoka na kuharibu Msikiti, kama unavyoonekana katika Picha.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 WATOTO wadogo wakisafisha kwa kutoa dongo nje katika Msikiti wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, baada ya sehemu kubwa ya msiki huo kuangukiwa na Udogo ulioporomoka na kuharibu Msikiti, kama unavyoonekana katika Picha.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 WANANCHI wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, wakitoa msaada kwa kuondosha Udongo, ili kutoa Vitu vilivyofukiwa na Fusi baada ya Nyumba ya Fadhil Amour Mohamed kuangukiwa na Udongo na kutokupata hata kitu Kimoja.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 MOJA ya nyumba wanazoishi wananchi katika shehia ya Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, ikiwa imeelemewa na Udongo uliokatika katika mlima, uliopelekea nyumba hiyo kuvunjika sehemu ya Ukuta huo, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 KIJIKO cha Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Pemba, kikiondosha dongo lililoporomoka katika milima na kuingia barabarani, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 ZAIDI ya Mita 150 katika barabara ya Mgagadu Kiwani eneo la Darajani, likiwa limeharibiwa Vibaya na Mvua zinazoendelea Kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiongoza na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, wakikagua sehemu ya barabara ya Mgagadu Kiwani Ilivyoharibika kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, 

 MATUMAINI ya wananchi kupata kilimo chao cha mpunga walichokilima kwa muda mrefu yameanza kupotea, kufuatia mashamba ya kilimo hicho kujaa maji mengi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 MIONGONI mwa Nymba 58 za wananchi wa shehia ya Mwambe Wilaya ya Mkoani, zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 MVUA zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba, zimeanza kuleta madhara kwa wananchi wanaoishi, Pichani baadhi ya vitu vya mmoja wa wananchi wa Shehia ya Wambaa vikiwa nje baada ya nyumba yake kujaa maji.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA


 VIONGOZI mbali mbali wa Serikali wakiongoza na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe;Mwanajuma Majid Abdalla, akiwangalia daraja la Pujini lililowatenganisha wananchi wa Pujini na Chake Chake baada ya sehemu ya barabara hiyo kukatika, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

 WANANCHI wa Kipapo Mgelema wako hatarini kukosa barabara ya kupita baada ya mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba, kuharibu barabara yao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)


RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA IBADA YA JUMAPILI MAKANISA MAWILI TOFAUTI MJINI MOSHI

4/30/2017 10:17:00 pm


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitakiana amani na mmoja wa mapadre katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi Mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Ekaristi Takatifu toka kwa Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiungana na waumini  katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

 Waumini wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliposalimia waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini katika ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiombewa na Askofu Isaac Aman katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini alikohudhuria ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na watawa katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya  ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na waumini katika Kanisa la Kuu la Katoliki Parokia ya Kristo Mfalme Moshi mjini baada ya  ibada ya Jumapili leo Aprili 30, 2017

 Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na waumini wengine wakimsikiliza Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo akitoa mahubiri wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikaribishwa na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akikaribishwa na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na waumini na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na waumini na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiombewa sala maalumu na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo kuongea na wananchi baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadick wakati wa kuhitimisha ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongozana na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Muhagama, Askofu Mstaafu Evarist Kweka wakipata picha ya pamoja  baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo na Askofu Mstaafu Evarist Kweka baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Askofu Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Frederick Shoo na Askofu Mstaafu Evarist Kweka na kiongozi mwingine baada ya  ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini katika Usharika wa Moshi Mjini leo  Aprili 30, 2017. PICHA NA IKULU

Taarifa Potofu Zinazomuhusisha Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dr Asha Rose Migiro

4/30/2017 10:53:00 am


Ubalozi wa Tanzania London umepokea Habari inayozagaa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa instagram ikiwa na nukuu ifuatayo:

''Binafsi bado sijaona umuhimu na mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zaidi ya vingozi kujikusanyia mali na utajiri mkubwa sambamba na kung'an'gania madaraka kwa nguvu. Mfano uchaguzi uliofanyika mwaka 2015 kwa yaliyotokea Zanzibar ni miongoni mwa Athari mbaya kabisa zinazotokona na Muungano,nadhani kila Mtanzania aliyaona"

Ukurasa huo wenyewe jina la UKUTA inaihusisha nukuu hiyo na jina la Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro. 

Ubalozi wa Tanzania London unapenda kutumia fursa hii, kuwajulisha Watanzania Waishio Uingereza na Watanzania kwa ujumla kuwa Balozi Migiro ahusiki na nukuu hiyo kama inavyosambazwa.Hivyo ni wazi kuwa wanayoisambaza wana malengo ya kulichafua jina la Balozi Migiro kwa sababu wanazozijua wao. 

Ubalozi wa Tanzania London unaendelea kutoa wito kwa Watanzania Waishio Uingereza kutumia muda wao na mitandao ya kijamii kutoa mawazo chanya yatakayo imarisha Muungano wa Taifa letu na mustakabali wa maendeleo ya Nchi yetu na Watanzania wa pande zote za Muungano. 

Ubalozi wa Tanzania London 
29 Aprili 2017.

MKUU WA MKOA WA PWANI MHANDISI NDIKIRI AISHUKURU TANESCO KWA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI.

4/30/2017 10:44:00 am


Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiri, (kulia), akipeana mikono na Kaimu Meenja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi. Leila Muhaji, wakati akipokea msada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya kituo cha Afya Mkoani mjini Kibaha Aprili 29, 2017.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro, ameishukuru TANESCO kwa msaada wake wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya Kituo cha Afya Mkoani Mjini Kibaha.

Mhandisi Ndikiro alisema, hatua hiyo yaTANESCO ni ushahidi tosha wa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma afya katika mazingira ya usafi.

"Niseme tu mlichokifanya ni kitu kizuri sana, na ningeshauri taasisi nyingine za umma na binafsi, kutoa sehemu ya faida wanayopata kutokana na shughuli zao na kurudisha kwa umma kwa njia ya kusaidia shughuli za kijamii kama hii ya usafi." Alisema.

Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi Leila Muhaji alisema, TANESCO kama mtoa huduma ya umeme kwa Wananchi na ikitambua kuwa wananchi ndio wateja wake wakubwa, pia imeona ni busara kusaidia serikali katika kuhakikisha mazingira yanayowazunguka kama vile kituo hiki cha afya yanakuwa safi." Alisema.

Bi. Leila pia alisema, TANESCO imetoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha umma kufanya usafi wa jumla kila mwisho wa wiki. "Tumeungana nanyi leo Jumamosi ambayo ni siku ya usafi, ili tufanye usafi pamoja kwenye kituo chetu hiki cha afya, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, napenda muwashukuru sana na mpokee msada wetu huu mdogo ambao nina hakika utasaidia kwa sehemu fulani katika kuweka mazingira ya hospitali yawe safi." alsiema

Awali Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikiro, aliwaongoza watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Pwani na wachache kutoka makao makuu katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwa kufyeka nyasi kuzunguka mazingira ya kituo hicho cha afya.

Mhandisi Ndikiro, akiwa na Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akitoa hotuba yake

Bi leila Muhaji, (katikati), akitoa hotuba yake, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro, na Meneja Rasilimali watu TANESCO mkoa wa Pwani, Bi.Nisile Mwakalinga

Wafanyakazi wa TANESCO mkoa wa Pwani

Mhandisi Ndikiro akimshukuru Bi.Nisile, huku Bi. Leila (wapili kushoto) na Bi Salama Juma, ambaye ni Afisa Uhusiano TANESCO

Wafanyakazi hawa wa TANESCO wakiwa wamebeba sehemu ya vifaa hivyo

Mhandisi Ndikiro, (kulia) na Bi. Leila Muhaji wakifyeka majani kwenye eneo la Kituo hicho cha Afya

Wafanyakazi wa TANESCO wakifagia mazingira kuzunguka kituo hicho 

Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akifafanua baadhio ya mambo kwa waandishi wa habari

Watumishi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha, wakifyeka nyasi

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO

Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO

Mhandisi Ndikiro akiwa amenyanyua baadhi ya vifaa alivyokabidhiwa

Watumishi wa kituo hicho cha afya wakikusanya sehemu ya vifaa hivyo

Mtumishi wa kituo cha Afya cha Mkoani mjini Kibaha, akwia amebeba sehemu ya vifaa hivyo

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel