Top Menu

DC MKURANGA AZINDUA JUKWAA LA UWEZESHAJI WANAWAKE WA WILAYA HIYO

6/30/2017 11:05:00 pm

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga amewataka wanawake wa Wilaya hiyo kuachana na masuala ya utegemezi kwa wanaume na zaidi wajikite katika kujiendeleza kiuchumi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ikiwemo kuanzisha vikundi vya ujasiriamali  ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi..

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 57 MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 30, 2017

6/30/2017 11:01:00 pm


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe,Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Eng,Edwin Ngonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe.Cosato Chumi akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akiteta jambo na Mbunge wa Karagwe Mhe.Innocent Bashungwa katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Shally Raymond akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe.Dk Mary Mwanjelwa akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Mbunge wa Bububu Mhe.Mwantakaje Juma akiuliza swali katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017.
Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya Kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika nchini Marekani Kutoka kushoto Ndg.Rashid Kikwete,Kassi Juma Nkamia na Abdallah Rubeya wakiwa bungeni kujifunza shughuli balimbali za Bunge.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akimsikiliza Mbunge wa Vunjo Mhe.Eng.James Mbatia katika kikao cha hamsini na saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 30, 2017. Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma

UTAFITI UNAONYESHA KUWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 WILAYA YA MONDULI IMEATHIRIWA NA MMOMONYOKO WA ARDI,WANANCHI WASHAURIWA KULIMA KILIMO HIFADHI

6/30/2017 10:43:00 pm
Watafiti kutoka vyuo vikuu vitatu nchini Uingereza vya Plymounth,Exeter,na Schumacker wakiwa wanamsikiliza kwa makini mkalimani ambaye ni  ndugu Sitayo aliyevaa (miwani ) katika warsha ya Wadau wa Jali Ardhi iliyofanyika Chuo Cha Ualimu Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.
 
Wakwanza kushoto ni Profesa Patrick Ndakidemi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akiwa anafuatilia kwa karibu Profesa William Blake kutoka nchini Uingereza akipanda mti katika eneo la chuo cha Ualimu Monduli.Picha na Vero Ignatus BlogMtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akitoa elimu kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.

Mtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Issakwisa Ngondya aliyeshika karatasi mkononi akitoa elimu kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.

Profesa Willium Blake akifuatilia kwa makini kinachoendelea katika Warsha hiyo.Picha na Vero Iganatus Blog.

Zoezi la upandji Miti likiwa likiendelea kwa wageni kutoka vyuo vikuu vitatu nchini Uingereza vya Plymounth,Exeter,na Schumacker wakishirikiana na Dkt Kelvin Kimei (anayeandika )kutoka  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.
 Mtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Issakwisa Ngondya aliyeshika karatasi mkononi akitoa elimu kwa wadau wa Mradi wa Jali Ardhi waliohudhuria Warsha ya siku mbili wilayani Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.
 Profesa Patrick Ndakidemi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Arusha akiwa anatoa ufafanuzi wa jambo katika warsha ya Mradi wa Jali Ardhi kwa wadau waliohudhuria katika Chuo Cha Ualimu  Monduli.Picha na Vero Ignatus Blog.
 Profesa William Blake kutoka nchini Uingereza akitoa neno la shukrani baada ya kumalizika kwa warsha ya siku mbili iliyowakutanisha wadau wa Mradi wa Jali Ardhi aliyesimama kushoto kwake ni Charles Bonaventure kutoka Taasisi isiyo ya kiserikali ya ECHO.Picha na Vero Ignatus Blog. Na.Vero Ignatus .Monduli

Wananchi wa monduli wameaswa kulima kilimo cha uhifadhi ili kuhifadhi  mazingira na kuepusha kutokea kwa mmomonyoka wa ardhi katika maeneo yao  na kudhibiti makorongo yakiwa katika hatua za awali.


Hayo yamesemwa na  Issakwisa Ngondya mtafiti kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  Arusha ambapo amesema kuwa zaidi ya asilimia 50 katika wilaya ya Monduli imeathiriwa na mmomonyoko wa ardhi .


 Ameainisha vijiji vilivyoathirika zaidi ni pamoja na Emaerete,Lendikinya,Arkaria,Orchoropus ,Likamba,Oletushora pamoja na Nangungwa,amesema kutokana na uharibifu  huo wa ardhi  umesababisha rutuba kupotea katika ardhi na husababisha upatikanaji hafifu wa mazao kwa mkulima.

Amewataka wadau hao kuhifadhi uoto  kwa kuotesha mimea na miti ili kuzuia udongo usisombwe na maji au upepo kwani  ardhi iliyofunikwa ni madhubuti zaidi dhidi ya mmomonyoko wa udongo kuliko ardhi ambayo haijapandwa kitu amesisitiza  kupanda mazao ya kudumu na kupanda mazao yanayofunika ardhi.
Nae Profesa  William Blake  kutoka nchini Uingereza amesema kuwa amefurahishwa sana na matumaini makubwa waliyonayo wana Monduli kwaajili ya kurudisha ardhi liyokuwa imeharibika  kwa mafanikio makubwa kwani warsha hiyo ina umuhimu mkubwa kwa watu wote wa sasa na kwa vizazi vijavyo pia


Kwa upande wake Profesa Patrick Ndakidemi  amesema akiona mashamba yameharibika huwa anajisikia vibaya kwani bila ardhi hakuna maisha amewataka washiriki wote kuyatendea kazi yale yote waliyojifunza ambapo amewataka wadau hao kuwa mfano bora  katika maeneo yao.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya serikali  Afisa kilimo na ushirika na umwagiliaji Ridhiwani kombo kutoka halmashauri ya Monduli amewashukuru waliofanya utafiti na kurudisha majibu kwani wengine huwa wanafanya utafiti lakini hawarudishi majibu,amesema utafiti walioufanya utatumika katika maeneo mengine hapa nchini.
 
 Kwa upande wawashiriki akitoa neno la shukrani katika semina hiyo ya siku mbili Adiso Matayo kwa niaba yawengine amewashukuru wawezeshaji kwa kuwapatia elimu ambayo ni faida kwao na kwa kizazi kijacho amesema elimu waliyoipokea wataifanyia kazi.

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO YAANZA AINA MPYA YA UTALII

6/30/2017 08:32:00 pm
 Mkomazi National Park
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro nchini  imeanza aina mpya ya utalii inayolenga kuboresha utalii unaojali mazingira ili kuvutia zaidi watalii.

Mhifadhi Mkuu wa mamlaka hiyo Freddy Manongi amesema, aina hiyo mpya ya utalii inalenga kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea eneo hilo la utalii linalotambuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), lililoko kilomita 180 kutoka mji wa Arusha nchini Tanzania.

Amesema mamlaka hiyo imeshatambua maeneo ya utalii unaozingatia mazingira ikiwemo milima, maeneo ya kijiografia, na maeneo ya kale, ambayo yalianzishwa miaka 58 iliyopita.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA ,ASHUHUDIA MAGARI 103 YAKIWA NA SHEHENA YA MAHINDI NJIA PANDA YA HIMO.

6/30/2017 10:01:00 am

ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili mpakani mwa nchi jirani ya Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha Malori yanayosafirisha Nafaka kwenda nchi jirani ya Kenya.
Uchunguzi uliofanywa na Globu ya Jamii umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha Malori hayo ,mengine yakiwa na Matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika Magari Madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.
Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio  ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari  zilizopo katika  vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.
Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda kusiko julikana .
Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.
“Magari yetu yapo pale Sheli Maount Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi  Matandiboi wakapiga simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi ,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara Mariam.
Alisema alimuelewa Waziri Mkuu katika agizo lake kwamba magari yaliyopo mpakani ndio yashikiliwe  na si kama lilivyofanya jeshi la Polisi kukamata magari yaliyokuwa Njia Panda kuelekea Moshi na Arusha huku wakimuomba Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi  kwa wasaidizi wake juu ya agizo lake.
Mfanyabiashara Kanyota alisema amekuwa akifanya biashara ya kusafirisha mazao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi lakini anashangazwa na hatua ya kuzuiliwa kwa  Mahindi yake ambayo amekuwa akinunua na kuyauza katika viwanda vya kutengeneza unga kwa ajili ya Chakula.
“Tulikua tunaomba Mkuu wa mkoa ajue kwamba sisi ni wafanyabiashara tunaolipa kodi halali ya serikali atusaidie tufikishe mazao yetu sehemu yanapotakiwa kufika ,Mahindi yangu yanatoka Mbeya ,mkulima aiyeniletea mimi kama Dalali ametoka Tunduma.”alisema Kanyota.
Kauli ya Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro imepigiria msumari katika Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaifisha Mahindi pamoja na gari litakalokutwa kuanzia June 26 mwka huu likiwa limebeba na kusafirisha Mahindi kwenda nje  ya nchi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa alisema jana ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari kuwa magari 103 yaliyokamatwa Himo na Njia Panda yatahesabiwa kama sehemu ya uhujumu uchumi na kwamba yatataifishwa .
“Magari yaliyokamatwa kule Siha ,tayari tulikwisha amua kwamba yatapelekwa Nationa Milling(Ghala la chakula la taifa)  Arusha ,lakini haya ya Himo ,Waziri Mkuu Alisha agiza kwamba kuanzia tarehe 26 ,magari yote yatakayokamatwa ,Bidhaa pamoja na magari yenyewe yatahesabiwa kuwa ni sehemu ya uhujumu Uchumi ,kwa hiyo yatataifishwa.”alisema Mghwira.
Mghwira alisema baada ya mfululizo wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro juu swala zima la uuzaji na usafirishaji wa chakula nje ya nchi,kamati imefanyia kazi tamko la Waziri Mkuu kutaka kujiridhisha vya kutosha juu ya hali ya chakula iliyopo Kilimanjaro na mikoa ya jirani.
“Uogozi wa mkoa wa Kilimanjaro unapenda kuwatangazia wananchi wote,hususani Wafanyabiashara wa Sukari na Nafaka za Mpunga,Mchele ,Mahindi na Unga wa Mahindi ya kuwa ni marufuku kwa mfanyabiashara yoyote au mwananchi yoyote kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi bila kibali cha serikali”alisema Mkuu huyo wa Mkoa .
Alisema kukiuka agizo hilo ni kuhujumu uchumi wa nchi  kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 3 cha jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu Uchumi sura ya 200 ya sheria za Tanzania na pia ni kukiuka agizo la Waziri Mkuu,kupitia waraka wake alioutoa  Mei 30,2017,uliozuia utokaji  wa vyakula na sukari kwenda nchi jirani .
Alisema kwa kukiuka sheria hiyo kunaweza kusababisha upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini na kusababisha Mamlaka ya Mapato hapa nchini (TRA)  kukosa takwimu muhimu wa bidhaa zinazosafirishwa nje
“Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro imejiridhisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari  na nafaka hizo nyakati za usiku na hiki ndicho kinaleteleza kukosa takwimu muhimu kwa kupitia njia ambazo si rasmi kwa kushirikiana na baadhi ya askari polisi ambao sio waaminifu.
Wakati wa baraza la Idd lilifanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi,Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa alitangaza kupiga marufuku usafirishaji wa Mahindi kwenda nchi jirani na kwamba atakaye kiuka utaratibu huo atahukuliwa hatua kali za kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo Kamanda wa Polisi ,Hamis Issah na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba wakitembelea maeneo ambayo yameshikiliwa magari yaliyobeba shehena ya Mahindi .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizunbgumza na baadhi ya wafanyabaishara wa Mahindi ambao magari yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Wafanyabiashara ambao Mahindi yao yanashikiliwa katika eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipofika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitizama Malori yenye Shehena ya Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyuma ya vituo vya Mafuta .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiongozana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issa wakiodoka katika eneo hilo baada ya kuangalia malori yanayoshikiliwa yakiwa na shehena ya Mahindi.
Baadhi ya Magari yakiwa yameegeshwa katika maeneo tofauti tofauti yakiwa na shehena ya Mahindi.
 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel