Top Menu

Malinzi na Mwesigwa Mambo Magumu.....Warudishwa Tena Rumande

7/31/2017 11:42:00 pm
Kesi inayomkabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, Jamali Malinzi na wenzake imeendelea leo July 31, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusogezwa tena mbele hadi August 11, 2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika ambapo hata hivyo, Mawakili wa washtakiwa, James Bwana na Abraham Senguji hawakuwa na pingamizi na suala la upelelezi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi August 11, 2017.

TANZIA: Mmiliki wa Hoteli za Ngurdoto, Impala na Naura Springs za Arusha, Afariki dunia

7/31/2017 11:37:00 pm

Mfanyabiashara maarufu nchini anayemiliki hoteli za kifahari jijini Arusha, Maleu Mrema amefariki dunia  nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matababu.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Maleu ambaye anamiliki Hoteli za Impala, Naura, Ngurdoto zilizopo jijini Arusha, wamesema ndugu yao alifia Afrika Kusini na kwamba taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa leo.
 
Familia wamesema hadi sasa hawajapata taarifa rasmi kutoka hospitalini hapo kuelezea chanzo cha kifo cha mpendwa wao.
 
Mrema alipelekwa Afrika Kusini mwezi Juni mwaka huu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya kiafya.

The Impala Group of Hotels inajumuisha:
1) Impala hotel (Arusha)
2) Impala hotel (Moshi)
3) Ngurdoto Mountain Lodge (Arusha)
4) Naura Springs Hotel (Arusha)
5) Impala shuttle Services (Arusha)
6) The Classic Tours & Travels


7/31/2017 11:31:00 pm

Vikosi maalumu vya majeshi ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) vimepiga kambi kwenye eneo la mapango ya Amboni, Tanga kwa ajili ya mazoez ya kijeshi.

Katika mapango hayo, mwaka jana yalitokea mauaji yaliyofanywa na watu wasiojulikana na kuzua hofu kwa wakazi wa eneo hilo ambao mwishowe walihamishwa na Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari   jana, Mkuu wa mpango huo, Meja Jenerali Harrison Msebo, alisema vikosi hivyo vitakuwa vikifanya mazoezi katika eneo hilo kama sehemu ya kupambana na ugaidi na uharamia baharini.

Kwa mujibu wa Meja Jenerali Msebo, mazoezi hayo yajulikanayo kwa jina la EX Matumbawe, yanatarajia kuanza Agosti 2 hadi Septemba mosi mwaka huu.

“Mazoezi hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza  Tanzania baada ya vikosi vya majeshi ya nchi washirika kuanza kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kujihami dhidi ya matukio mbalimbali ya uhalifu tangu mwaka 2015.

“Pamoja na mambo mengine, lengo letu ni kuhakikisha vikosi vya majeshi katika nchi washirika vinajengewa uwezo wa kupanga na kutekeleza operesheni za vikosi maalumu  na kujifunza mbinu na weledi katika kupambana na matukio ya uvamizi yanayoweza kufanywa na maharamia na magaidi.

“Mazoezi hayo yanatokana na mbinu za kupigana vita pamoja na matishio ya ugaidi kubadilika mara kwa mara.

“Hivyo kupitia mazoezi hayo, tutaweza kuvitayarisha vikosi vyetu dhidi ya mapambano ya aina yoyote yanayoweza kutokea,” alisema Meja Jenerali Msebo.

Alizitaja nchi zenye majeshi yatakayoshiriki mazoezi hayo  kuwa ni Afrika Kusini, Botswana, Lesotho, Malawi, Zambia, Zimbabwe   na wenyeji Tanzania.

Naye  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, alisema mazoezi hayo yataimarisha uhusiano wa kijeshi baina ya nchi wanachama wa SADC na yatawasaidia wanajeshi hao kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi wao.

“Kwa hiyo napenda kuwaomba wananchi, kwamba watoe ushirikiano wakati wote wa mazoezi hayo ingawa pia nawaomba wananchi wasipende kuokota vitu ambavyo wana hofu navyo.

“Kama wananchi wakiona kitu wasichokielewa, basi watoe taarifa wahusika waje kuvitambua badala ya kuviokota kwa ajili ya matumizi yao,” alisema Shigela.

Wakati mazoezi hayo yakitarajia kuanza mwaka jana hali ilikuwa tete na ilizua taharuki jijini Tanga baada ya watu wasiojulikana, kuua idadi kadhaa ya watu katika eneo la mapango hayo.

Serikali ililazimika kupeleka vikosi vya Jeshi la Polisi na askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kukabiliana na wahalifu hao.

Wakati vikosi hivyo vya ulinzi na usalama vikifanya kazi, vilikuwa vikiendesha operesheni maalumu ya upekuzi ndani ya mapango hayo kwa lengo la kukabiliana na wahalifu hao.

Kutokana na hali ya usalama kuwa tete katika eneo hilo, baadhi ya watu walilazimika kuhama makazi yao kuokoa maisha yao

MAGARI 40 YANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI TABORA KUFUATIA MSAKO ULIOFANYWA NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) KANDA YA KATI, WA KUBAINI VYOMBO VYA MOTO VYENYE BIMA FEKI.

7/31/2017 06:15:00 pm

Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini  Kanda ya Kati Bi.Stella Rutaguza akizungumza na madereva pamoja na makondakta katika stendi kuu ya mabasi mkoani Tabora ,walipokwenda kugagua bima za vyombo vya moto kama ni halali ama feki.Picha na Vero Ignatus Blog
 
 Afisa Mwandamizi wa Bima Maneno Adam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima( TIRA)akikagua gari ili kuangalia kama bima inayotumika kama ni halali ama ni feki .Picha na Vero Ignatus Blog.
  Ukaguzi wa magari ukiendelea katika stendi kuu ya mabasi Mkoani Tabora kama inavyoonekana kwenye picha kutoka kushoto ni Meneja wa Kanda ya kati kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini bi.Stella Rutaguza akiwa na askari wa kikosi cha usalama barabarani Koplo Clement   .Picha na Vero Ignatus Blog.
Zoezi la ukaguzi likiendelea wakati huohuo madereva ,makondakta pamoja na abiria wakipata elimu namna ya kutambua Bima kama ni halali ama feki.Picha na Vero Ignatus Blog.

 
Wananchi ,madereva ,makondakta wa mabasi makubwa na madogo wakipewa elimu na namna ya kut5ambua bima feki kwa kutumia  simu ya mkononi au kwa njia ya mtandao mfumo wa TIRA MIS .Picha na Vero Ignatus Blog.
 

Na   Vero Ignatus, Tabora

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini (TIRA) imefanya zoezi la ukaguzi wa bima za vyombo vya moto katika manispaaa ya Tabora katika stendi kuu ya mabasi na kubaini magari mengi hayana bima na mengine yana bima tofauti na kile kilichoorodheshwa katika bima hizo.

Akizungumza juu ya zoezi hilo meneja ( TIRA) Kanda ya Kati Stella Rutaguza amesema kuwa katika wameweza kukagua magari zaidi ya 266 magari 27 yamebainika kuwa na bima za kughushi ,magari 13 hayakuwa na bima,magari mengine yanatumia bima za pikipiki,na baadhi ya magari madogo yanatumia bima za magari ya mizigo.

"Magari tuliyoyakagua na kuyakuta yana bima feki tumeyakamata na kuyapeleka kituoni ili kwamba watupe maelezo  kuwa hizo bima wamezipata wapi,"alisema

Amesema kwa ada za malipo ya bima kwa mujibu wa sheria kwa maana ya bima ndogo (Third party insurance) kwa jumla magari haya 40 ni shilingi Milioni  33,850,000/= ambapo magari hayo yaliyokamatwa ni mabasi ya abiria 65,Coster za abiria 26, Noa na magari madogo ya binafsi.

 Imebainika kuwa kuna wamiliki wa magari ambao walikuwa wamenunua bima kubwa (Comprehensive Insurance) ambapo kwa mabasi walikuwa wamelipia kuanzia shs.3,000,000/= na zaidi ambazo zimeingia kwenye mifuko ya matapeli wa bima.

"Tunataka hawa vishoka wa bima feki watafute kazi nyingine  halali za kufanya  kwani Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini haitawafumbia macho wadanyanyifu hawa

Bi Stella amesema kuwa kesi za matapeli wa bima zimekuwa zikikaa muda mrefu bila kupekekwa mahakamani na hata zikipelekwa zimekuwa zikichukua  pia muda mrefu pia.

'Tunaomba kesi za Bima ziwe zinashughulikiwa kwa haraka na mamlaka husika "alisisitiza bi Stella. 

Meneja huyo wa kanda ya kati Stella ametoa rai kwa mawakala wa bima na kusema kuwa yeyote atakayegunduliwa anauza bima feki atakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria na  atafutiwa leseni  maana amekiuka taratibu za kisheria .

" Hawa watu wengi wanaouza hizo feki bima siyo wakala wa bima ila ni matepeli tu wamtaani hivyo tukiwabaini tutawapeleka kwenye vyombo vya sheria hatuna utani wala mchezo katika hili".alisema.

 ********************************************************
Namna ya KUHAKIKI BIMA Kama ni  HALALI ama feki
 
Kwa njia ya simu ya mkononi  nenda kwenye uwanja wa ujumbe mfupi  andika neno STIKA weka namba ya stika tuma kwenda namba 15200
Kwa kupitia njia ya mtandaoni (internet)kwenda kwenye tovuti ya Tira mis  
htt/mis.tira.go.tz kisha ingiza namba za stika na bofya hakiki.

ALL STARS VETERAN KUFANYA BONANZA LA KUWAKUMBUKA WENZAO WALIOPOTEZA MAISHA SAME KILIMANJARO

7/31/2017 10:10:00 am
Kamati maalum ya Maveterani wa timu ya soka ya Arusha All Star ya Jjijini Arusha wakijadili mambo muhimu kwaajili ya kuwaenzi Veterans waliopata ajali  mwaka 1990.picha na Vero Ignatus Blog
Denis Zakaria Mkurugenzi wa benchi la ufundi katika kikosi cha All Star akitoa ufafanuzi kuhusu bonanza maalum kuhusu kuadhimisha siku ya Veteran waliopata ajali wilayani Same  mkoani Kilimanjaro.Picha na Vero Ignatus Blog
Pichani ni Azizi Nyoni Kocha wa All Stars Veteran akizungumza kuhusiana na bonanza hilo .Picha na Vero ignatus Blog.

 
Kamati ikiendelea na kikao wakijadili mambo muhimu kwaajili ya kuwaenzi Veterans waliopata ajali  mwaka 1990.picha na Vero Ignatus Blog

 Na.Vero Ignatus Arusha
 
Katika kuwa kumbuka wanasoka waliopoteza maisha katika ajali wilayani same mnamo mwaka 1990 timu ya soka ya veteran Arusha all stars wameandaa bonanza maalumu kwa ajili kuwaenzi baadhi ya wachezaji waliopoteza maisha katika ajali hiyo mkoa kilimanjaro.

Dennis zacharia shemtoi ni mkurugenzi wa dawati la ufindi katika kikosi cha waombolezaji wa timu ya Arusha all stars ya jijini arusha amesema kuwa kila ifikapo August nane huadhimisha siku hiyo kwa kuwa kumbuka wenzao waliopata ajali ya Gari mnamo mwaka 1990.

Amesema katika kuwaenzi veteran's Hao kamati ya uongozi wa Krabu ya arusha all stars pia wameandaa bonanza maalumu kwa ajili ya kushiriki katika michezo bonanza litakalo husisha mchezo wa kabumbu kwa maveteran mbalimbali. 

Kwa upande wake kocha anaekinoa kikosi Cha maveteran wa Arusha all stars Azizi Nyoni amesema kuelekea bonanza hilo mpaka Sasa kikosi chake kiko Sawa kwa ajili ya mapambano ambapo pia kocha Azizi akatumia fursa hiyo kutoa rai kwa wachezaji vijana kuwa na nidhamu na bidii katika mchezo wa  soka kwa ajili ya kujijengea nja ya kuitangaza Tanzania katika soka la kulipwa. 
Maveteran Hao wanataraji kuungana kwa pamoja kwa ajili ya kuwaombea dua wenzao walio Pata ajali na kupoteza maisha mkoani kilimanjaro ambapo Tarehe Sita mwezi wa nane watadhuru makaburi ya wenzao kabla ya kushuka dimbani siku ya Tarehe nane. 

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa bench la ufindi bwana Dennis Zacharia miongoni mwa walio poteza maisha katika ajali hiyo ni amani mwalimu, Judicate EStomihi, pamoja na Francis Lungu.
Mula Ametoa Mola ametwa Jina Lake litukuzwe. Amen.

 

 


 
 

Kampeni ya ‘MAGUFULI BAKI’ Kuanza Nchi Nzima Hivi Karibuni

7/31/2017 09:30:00 am
Kampeni ya ‘MAGUFULI BAKI’ iliyoanzishwa karibuni na mwanaharakati ambaye pia aliwahi kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Sengerema kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015, Laurence Mabawa, inatarajiwa kuanza karibuni.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana , Mabawa alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupigania rasilimali za wananchi wanyonge na masikini na kuunga mkono juhudi anazozifanya na hivyo kampeni hiyo inahamasisha yeye kubaki katika msimamo wake pasipo kusikiliza maneno ya watu.

“Napinga kwa nguvu zote, kama nilivyokwisha kufafanua toka mwanzo ,kampeni ya ‘Magufuli Baki’ ina lengo la kumtia moyo Rais Magufuli na kumwomba abaki katika msimamo wake wa kutetea maskini, wanyonge na kupigania rasilimali za taifa letu,

“Nirudie tena wito wangu kwamba nitazunguka nchi nzima kwa gharama zangu kupata fursa ya kuwasikiliza wananchi kupitia kampeni yangu inayojulikana kwa ‘Magufuli Baki’ kuhakikisha wananchi wanatoa maoni yao juu ya rais kuendeleza msimamo wake wa kiutendaji na sitavunjwa na propaganda za baadhi ya vikundi vinavyonikejeli mitandaoni pasipo kuthamini maendeleo anayoyafanya,” alisema.

Aidha alieleza kwamba toka aitangaze kampeni yake kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wanasiasa na wananchi ambao hutoa lugha za maudhi na kejeli kwa baadhi ya Watanzania wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 kifungu kidogo cha (1) na (2) kinatupa haki na fursa ya kutoa maoni na kueleza fikra zetu, hivyo amewaomba wanasiasa wasitumie kifungu hicho cha katiba kukivunja kwa kutoa maoni yenye kuudhi na kejeli, kwa hiyo, alisema, kitendo cha kushambuliana kwa maneno makali ni kosa kisheria.

Alisema kampeni aliyoianzisha itaweza kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao ambayo yatasambazwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kuanzia mwezi ujao.


JAFO AKEMEA TATIZO LA MIMBA KWA WANAFUNZI WILAYA YA UKEREWE.

7/30/2017 08:09:00 pm


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya sekondari wasichana ya Bukongo wilayani Ukerewe.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya kidato cha tano na sita   ya Pius Msekwa wilayani Ukerewe.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashuari ya wilaya ya Ukerewe wakati akihitimisha ziara yake wilayani humo.

Watumishi wa halmashauri ya Ukerewe wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo. 
.................................................................................

Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amekemea tatizo la wanafunzi wa sekondari kupata mimba wakiwa shuleni ambapo hadi sasa kuna wanafunzi 108 ambao wamebainika kuwa na ujauzito kwenye wilayani Ukerewe.

Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali wilayani humo.

Jafo amewataka viongozi wote wilayani humo kuungana kupambana na tatizo hilo bila ya kuoneana aibu. 

Naibu Waziri huyo amewataka wanafunzi kuzingatia masomo kwani elimu ndio msingi wa maisha kwa mwanadamu yeyote.

Amewakemea wanafunzi wakike wenye tabia ya kujihusisha kwenye mapenzi wakiwa na umri mdogo na kwamba jambo hilo linahatarisha mustakabali wa maisha.

Katika ziara hiyo,Jafo alifanya ukaguzi wa ujenzi wa mabweni, madarasa, maabara, na vyoo kwa shule ya sekondari Pius Msekwa na sekondari ya Bukongo ambapo serikali ilipelekwa fedha mwezi April mwaka huu zaidi ya sh. milioni 500 ili kuwezesha elimu ya kidato cha tano na sita wilayani humo. 


Naibu Waziri Jafo amemaliza ziara yake wilayani Ukerewe mkoani Mwanza na kuelekea wilaya na Tarime na Rorya mkoani Mara.

WAZIRI MKUU AZINDUA MELI MBILI ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI ITUNGI KYELA MKOANI MBEYA

7/30/2017 09:30:00 am
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa . Uzinduzi huo ulifanyika kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. Wapili kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye badari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chumba cha kulala cha mabaharia wa moja kati ya meli mbili alizozizindua kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na zimejengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha mitambo ya moja ya meli mbili alizozizindua katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017. Meli hizo zimenunuliwa na serikali na kujengwa na kampuni ya kizalendo ya Songoro Marine Transport Limited ili ziwahudumie wananchi katika ziwa Nyasa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika chumba cha nahodha wa moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali ili zihudumie wananchi katika ziwa Nyasa, baada ya kuzindua meli hizo kwenye bandari ya Kiwira wilayani Kyela Julai 29, 2017.Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Moja kati ya meli mbili zilizonunuliwa na serikali na kujengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ikiondoka kwenye gati la bandari Kiwira wialyani Kyela baada ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Julai 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.


*Ameonya zisitumike kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua meli mbili za mizigo za Mv Njombe na Mv Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye ziwa Nyasa na kuonya kwamba zisitumike kama eneo la kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo zilizogharimu sh. bilioni 11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo katika ziwa Nyasa.

Amesema ni jambo la faraja na la kujivunia kwa Serikali na wananchi kwa pamoja kushuhudia meli zilizotengenezwa na Mtanzania, zikiwa zimekamilika tayari kwa kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi, ambapo awali suala hilo lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni.

Waziri Mkuu amezindua meli hizo zilizojengwa na kampuni ya Kitanzania ya M/S Songoro Marine Transport leo (Jumamosi, Julai 29, 2017) katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.

Amesisitiza kwamba meli hizo zitumike katika kukuza uchumi wa wananchi kwa kusafirisha mizigo na biashara halali kati ya nchi za Tanzania na Malawi na zisitumike kama eneo la kuingiza wahamiaji haramu pamoja na dawa za kulevya nchini.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi na kuhakikisha meli hizo zifanya shughuli halali za kiuchumi ambazo zitawaletea tija wao na Taifa kwa ujumla na kamwe wasikubali zikatumika kama kichaka cha uhalifu.

“Changamoto ya usafiri wa mizigo katika ziwa Nyasa itakuwa historia kwani meli hizi zitarahisisha usafiri na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania nan chi za Malawi na Msumbiji, hivyo tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kutoa ahadi hii ambayo leo utekelezaji wake umekamilika.”

Awali,Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Karim Mataka alisema ujenzi wa meli hizo ulianza Juni 2015 zina uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo kwa kila moja.

Mhandisi huyo alisema mbali na kukamilika kwa mradi huo pia TPA imeingia mkataba na kampuni ya M/S Songoro Marine Transport Ltd kwa ajili ya ujenzi wa meli ya abiria yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 300 za mizigo. Mradi huo ambao upo katika hatua za mwisho kamilika utagharimu sh. bilioni 9.12.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 30

7/30/2017 09:23:00 am

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 30


Advertisement

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel