Top Menu

MAMLAKA YA MAWASILIANO NCHINI TCRA IMETOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA MAWASILIANO HUDUMA NAMNA YA KUHAMA MTANDAO MWINGINE WA SIMU BILA KUBADILI NAMBA YA SIMU YA KIGANJANI

 Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira alipotembelea katika banda la Mamlaka ya mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini katika maonyesho ya nanenane yalitofanyika katika viwanja vya Themi Njiro Mkoani Arusha,wa pili kushoto ni Meneja wa TCRA Kanda ya kaskazini Injinia Annette Matindi ,wakwanza kulia ni Injinia Jan Kaaya ,aliyepo katikati ni Afisa Oswad Octavian kutoka TCRA kanda ya kaskazini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiweka saini katika kitabu cha wageri  alipotembelea katika banda la Mamlaka ya mawasiliano nchini Kanda ya kaskazini katika maonyesho ya nanenane yalitofanyika katika viwanja vya Themi Njiro Mkoani Arusha.  
  

Injinia Jan Kaaya akiwa anamfanfanulia jambo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira kama inavyoonekana pichani katika maonyesho ya nanenane mkoani Arusha
 
Pichani Meneja wa TCRA kanda ya kaskazini Injinia Annette Matindi akiwa na wafanyakazi wengine wa TCRA wakitoa elimu kama wanavyoonekana pichani.Picha na Vero Ignatus Blog.

Injinia  Jan Kaaya akiwa anafurahia jambo mara baada ya kumuhudumia mteja katika maonyesho ya nanenane (haonekani pichani)yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog
 Afisa Oswad Octavian kutoka TCRA kanda ya kaskazini akitoa elimu kwa mteja alipotembelea katika banda lao katika maonyesho ya nanenane mkoani Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.Mhandisi masafa kutoka TCRA Julius  Felix alitoa elimu kwa wateja aliotembelea banda la Mamlaka hiyo katika maonyesho ya nanenane katika viwanja vya Themi Njiro Mkoani Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma mpya ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya kiganjani (MNP-Mobile Number Portabilitty service) ambapo namba ya kitambulisho itakuwa namba mtumiaji 

Huduma hii ilianza tarehe mosi machi 2017 na inapatikana nchi nzima kwenye maduka ya kutolea huduma kwa wateja wa mitandao ya makampuni yote ya simu za kiganjani
Huduma hiyo ya kuhama mtandao mwingine bila ya kubadili namba yako na mtumiaji anabakia na namba kumchagua mtoa huduma bora zaidi ,atapokea ujumbe mfupi wa maneno bila kujali ni mtandao upi umehamia, itamuepushia usumbufu wa kununua laini mpya mara kwa mara

Namna ya kuhama mtandao bila kubadili namba ya simu kiganjani,ili kuingia kwenye mfumo huu simu ya mtumiaji lazima iwe inatumika yaani haijafungiwa au kusimamishwa kwa muda.

MASHARTI YA KUHAMA

Ili uweze kutumia huduma hii ,inabidi kuzingatia masharti yafuatayo:
a)Hutaweza kuhama na namba ambayo imefungwa ama kusimamishwa huduma
b)Hutaweza kuhama na salio lililopo itabidi utumie salio kabla ya kuhama la sivyo salio lako litatunzwa kwenye akaunti maalumu ya mtoa huduma wako wa zamani na utalazimika kufuata taratibu za kudai ili urudishiwe.
C)Huwezi kuhama kama unamkopo wa aina yeyote ile(muda wa maongezi au pesa mtandao )kutoka kwa mtoa huduma wako hapa nchini.
D)Huwezi kuhama kama namba yako inahusishwa na uhalifu na imefungiwa
Tcra: Iwapo unatumia huduma kwa utaratibu wa malipo baada ya huduma yaani post-paid:zingatia mashrti yaliyotajwa hapo juu ya wateja wa pre-paid na masharti mengine yafuatayo;
a)Itabidi ulipe madeni yote kabla ya kuhama
b)Itabidi ukamilishe mashrti ya msingi ya mkataba na mtoa huduma wako 
wa sasa na kutimiza masharti ya malipo kila mwezi kwa mujibu wa mkataba kabla ya kuhama
C)Utaendelea kupokea ankra za matumizi hadi namba itakapokamilishwa kwa mtoa huduma mpya .

Utapokea ankra ya mwisho hadi siku 60 baada ya kuhamisha namba yako kisha unapewa mpaka siku 30 za kulipa ankra hizo vinginevyo utakuwa katika hatari ya uhamaji  wako  utasitishwa au namba yako kufungiwa,

UTARATIBU WA KUHAMA
1.Tembelea vituo vya mauzo au kwa wakala anayetambuliwa wa mtoa   huduma unakokataka kuhamia na umueleze mhudumu kwamba ungelipenda kuhama na namba yako.
2.Mhudumu atakutaka ujaze fomu maalum ya maombi
3.Sehemu ya fomu ya maombi ya kuhama ni tamko rasmi kwamba unakubali kuwa unawajibika kuwa madeni yote ambayo yanatokana na huduma ulizokuwa unapata kutoka kwa mtoa huduma wako wa awali 
4.unatakiwa kutoa vifuatavyo:

a)Kitambulisho chenye picha yako kinaweza kuwa kitambulisho cha Taifa Kadi ya mpiga kura  leseni ya udereva au pasipoti au kitambulisho chochote rasmi kinachotambulika
b)Simu ya kiganjani inayofanyakazi yenye namba unayotaki kubaki nayo

5.Iwapo una salio katika akaunti ya pesa mtandao unashauriwa kutoa pesa kabla ya kuhama ili kuepusha usumbufu baada ya kuhama mtandao mwingine.
6.Utatakiwa kutuma meseji yenye neno HAMA" kwenda namba 15080 ambaoyo ni namba maalum ya kuhama.msaada utatolewa iwapo utahitjikq ili kufanikisha hili.
7.Utapokea meseji kukujulisha kwamba maombi yako yamepokelewa
8.Iwapo namba yako haikuzuiliwa au kusimamishwa kwa muda kutokana 
na kutokukamilisha malipo ya madeni ya mtoa huduma wako wa awali maombi yako yatashughulikiwa na utakulishwa kwa meseji kuhusu maendeleo ya mchakato huu
9.Mtoa huduma wako mpya wa huduma za simu ya kupiga na kupokea na ujumbe mfupi zitaendelea kama kawaida
10.Ili kupokea mihamala ya fedha mtandao wakati wa kuhama ,huduma za kifedha zitasitishwa kwa muda mpaka namba itakapokamilishwa kwa mtoa huduma mpya ambapo utatumia huduma zake za fedha mtandao kama utajiunga na huduma zipo.
11.Katika kipindi chq kuhama huduma za kupiga na kupokea na ujumbe zitaendelea kama kawaida
12.Katika hali ya kawaida uhamaji utakamilika haraka  mara nyingi siku hiyohiyo au iwapo utachelewa sana,ndani ya siku mbili za kazi baada ya kukamilisha utaratibu wa maombi.wakati huo namba yako utakuwa umeshahamishwa kwa mtoa huduma wako mpya na laini
13.Ikifikia hapo weka laini mpya uliyopewa na mtoa huduma wako mpya kwenye simu yako ,iwapo huna uhakiki wa nn cha kufanya unaweza kwenda kwa mtoa huduma au wakala au kuwapigia simu na wataweza kuusaidia.
14.Mchakato umekamiliaka

Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel