Top Menu

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA )KANDA YA KATI YAELIMISHA WANANCHI JUU YA UMUHIMU WA BIMA YA KILIMO NA MIFUGO

Meneja wa TIRA kanda ya Kati bi Stella Rutaguza akitoa ufafanuzi kwa mkuu wa mkoa wa Singida (aliyevaa vitenge) Dkt.Rehema nchimbi, pamoja na mkuu wa mkoa wa Dodoama Mhe.Jordan Rugimbana.Picha na Vero Ignatus Blog.
 
Mkuu wa mkoa wa Singida (aliyevaa vitenge) Dkt.Rehema nchimbi, akiwa anazungumza na  bi Stella Rutaguza  kushoto kwake ni mkoa wa Dodoama Mhe.Jordan Rugimbana,wa kwanza kutoka kulia ni Afisa wa bima kutoka TIRA Maneno Adam.Picha na Vero Ignatus Blog.

 Na.Vero Ignatus Dodoma

 Mamlaka ya Usimamizi wa Bima kanda ya kati (TIRA) Imewaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa wakulima na wafugaji kuhusiana na  Bima ya kilimo na mifugo.

Akiongea katika maonesho ya nanenane Kanda ya Kati Dodoma, Meneja wa Kanda ya Kati Bibi Stella Rutaguza amesema kuwa Mkulima au mfugaji anapokuwa na bima kwa ajili ya mazao katika shamba lake au mifugo yake itamuwezesha kupata fidia ya bima kwa kiwango cha hasara anayoipata na hivyo kuepuka hasara ambayo angeipata kiuchumi kama asingekuwa na bima. 

"Unapopata hasara badala ya kulia kilio kisichokuwa na mfariji badala yake ukiwa na bima utalia huku ukiwa na faraja kuwa mfariji wako bima yupo na atakufariji kwa kukupatia fidia ya hasara uliyopata, alimalizia Bibi Stella Rutaguza."

Sambamba na hayo (TIRA) imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi pamoja na wamiliki wa  vyombo vya moto namna ya kuhakiki na kutambua bima ya vyombo hivyo kama ni halali ili kuepuka kuuziwa bima mbazo ni feki

Mkurugenzi wa masoko kutoka TIRA bi.Adelaida Muganyizi akizungumza na mteja katika maonyesho ya nanenane mkoa wa Lindi

Wa kwanza kulia ni meneja  (TIRA)Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza akizu ngumza na mteja aliyetembelea katika banda hilo katika maonyesho ya nanenane viwanja vya Themi  Njiro Mkoani Arusha

Meneja wa TIRA Kanda ya Kati Bi Stellah Rutaguza akihojiwa na mwandishi wa habari katika maonyesho ya nanenane Dodoma
Afisa wa bima kutoka Tira Maneno Adam wa pili kushoto akitoa elimu ya bima kwa ndugu Dickson Pangamawe (aliyevaa tshirt nyeupe) pamoja na ndugu Emmanuel Fungo( aliyesimama) wakiwa pamoja na Meneja wa Kanda ya kati B.Stella Rutaguza.Picha na Vero Ignatus Blog
 Zao la zabibu ambalo pia ni zao kuu mkoani dodoma lipo kwenye shamba darasa katika maonyesho ya nanenane mkoani Dodoma.Picha na Vero Ignatus blog. 


Mbegu ya Mtama aina ya HAKIKA ,Nafasi  75 Cm x30CM Kiasi katika eneo  7-8 KG/ha,muda wa kukomaa siku 100-105 ,Mavuno Tani 2.5-3 kwa Hekta.Picha na Vero Ignatus Blog

Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel