Top Menu

MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA KASKAZINI: ECHO YASISITIZA KISAMVU CHA CHAYA

Inline image 1
Na.Vero Ignatus.Arusha.

Maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini yanaendelea katika viwanja vya Themi Njiro Arusha  yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayao Zalisha kwa tija mazao ya Kilimo,Mifugo,na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ,Shirika lisilo la kiserikali la ECHO limeendelea kuhimiza jamii kupanda kwa wingi zao la chaya ili kutekeleza kauli mbiu ya mwaka huu inayosema.

 Akizungumza katika viwanja vya nane nane Bwana Shamba Charles Bonaventure kutoka (ECHO) amesema; “zao la kisamvu cha chaya lina kalshamu nyingi na lipo katika mboga za majani bora nne duniani.

 Amesema kuwa mmea huo una kwa wingi wa protini likufuatia Katuk, Kisamvu cha kawaida, mlonge na baadaye kisamvu cha chaya. Mboga nyingine bora duniani  ni pamoja na mnavu ambao ni namba nane, sukuma wiki(namba kumi na saba) na mchicha(namba kumi na tisa) kutokana na ubora ulio orodheshwa kwenye tafiti ambazo ECHO inazisoma na kuelimishia jamii”.
 Inline image 1Inline image 2
 Mmea wa Chaya kama unavyoonekana pichani
 
Baadhi ya faida za kisamvu chachaya ni pamoja na:

  • kinasaidia mfumo wa umeng’eaji (digestion) wa chakula,
  • kinaimarisha macho kuona,
  • unapunguza wingi wa mafuta mwilini (cholesterol),
  • kinapunguza uzito mkubwa,
  • kinapunguza kikohozi,
  • kinaongeza nguvu za mifupa ya mwili kwa kuwa na kiasi kikubwa cha kalsiamu,
  • kinaongeza damu,
  • kinaongeza uwezo wa kumbukumbu,
  • kinasaidia kwa wenye magonjwa ya kisukari
Akiongelea kuhusu ukuaji wa kisamvu cha chaya na mapishi yake ndugu Bonny amesema kuwa, “mara nyingi kisamvu chochote kinakuwa na sumu (cynide) kitaalamu inaitwa hydrocyanic acid-(HCN), hivyo kinahitaji kupikwa kwa muda mrefu. Kwa kisamvu cha kawaida, kisamvu kinashauriwa kupikwa kwa muda usiopungua dakika thelathini na tano (35) na kwa kismavu cha chaya muda usiopungua dakika ishirini(20). Hakikisha hakifunikwi wakati wa kupika kuwezesha hewa mvuke kuweza kutoka kwa urahisi ili sumu iliyopo kwenye chungu kinachopikia ipotee hewani”.

Kuhusu ukuaji na jinsi ya kusambaza kwa wakulima,Bonny amesema kuwa ukianza na miche miwili unaweza kutosha kugawa katika kijiji kizima baady ya miaka miwili kwani wao (ECHO) walianza na miche miwili mwaka 2013 na hadi sasa wameshagawa kwa wakulima zaidi ya vipingili elfu sita (6,000).

Ametoa wito kwa wadau na watu mbalimbali kuwahi na kutembelea banda la ECHO ili kupata mbegu za bure  zao hili pamoja na mazao mengine ambayo ECHO itayagawa katika kipindi hiki cha nane nane.

Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel