Top Menu

NDEGE 5HSAL 206 YAPATA AJALI YAUA MMOJA MONDULI

Ndege yenye namba  5HSAL 206 ambayo inayomilikiwa na kampuni ya Safari Air Link kama inavyoonekana ilipoangukia katika hilo limetokea katika kijiji cha Engalaoni kilichopo katika mpaka wa wilaya za Monduli na Arumeru za mkoani hapa.

 
Na.Vero Ignatus, Arusha.
 
Mtu mmoja mkazi wa jijini Dar Es Salaam,  David Mbale(25),ambae ni Rubani amefariki dunia baada ya ndege ndogo aliyokuwa akiendesha kuanguka juu ya vilima vya Monduli.

Akizungumzia tukio hilo  Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji cha Engalaoni kilichopo katika mpaka wa wilaya za Monduli na Arumeru za mkoani hapa.

Amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi Agosti 9,ambapo marehemu alikuwa akiendesha ndege ndogo  yenye namba  5HSAL 206 ambayo inayomilikiwa na kampuni ya Safari Air Link.

Alisema kuwa ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria watano iliondoka katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha,majira ya saa 1;30 asubuhi ambayo ilikuwa ikielekea katika eneo la Kogatende,Serengeti kuwachukua watalii.

"Ndege hiyo alikuwepo rubani peke yake na alikuwa anasubiriwa Serengeti na watalii jambo ambalo lilifanya  taarifa zilianza kuenea saa 4 asubuhi kuwa ndege hiyo imeanguka katika vilima vya Monduli maarufu kama Monduli Hills,"alisema na kuongeza

"Mara baada ya taarifa hizo kutolewa saa 6;30 tulipozipata taarifa hizo tulijulisha kikosi cha zima moto na wenzetu wa uwanja wa ndege wa Arusha,na walipofika kwenye kilima hicho walikuta rubani ameshafariki dunia,mwili ulichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi,"

Amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo umeanza jana na kuwa watashirikisha wataalamu ambao wamebobea katika masuala hayo kutoka kwa wataalamu wanaoshughulikia masuala ya ndege wakishirikiana na maafisa wa jeshi hilo ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel