Top Menu

TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA YATOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA KUPELEKA VYAKULA KUPIMWA KUHAKUKI VIASILI VYA MIONZI


Wakwanza kushoto ni Afisa uhusiano kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Peter Ngamilo akiwa anatoa elimu kwa wateja waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini Njiro mkoani Arusha .Picha na Vero Ignatus Blog.

 
 Agrey kitosi  mwandisi wa mionzi kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki mkoani Arusha akitoa elimu kwa wateja waliotembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini.Picha na Vero Ignatus Blog.


 Mwanasayansi wa mionziDenis mwalongo  akizungumza na mgeni aliyetembelea banda hilo katika maonyesho ya nanenane mkoani Arusha


 
Umati wa wananchi waliofurika katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini kama wanavyoonekana pichani .Picha na Vero Ignatus Blog.

Na.Vero Ignatus. Arusha

Wito umetolewa kwa  kwa waanyabiashara ,Wakulima na wafugaji  waendelee kutoa  ushirikiano wa kuhakikisha kwamba wanatoa sampuli zao za vyakula /bidhaa kwenye Tume ya nguvu za Atomiki Tanzania kwaaajili ya uhakiki wa viasilia vya mionzi  ili kuweza kuwalinda watanzania na madhara yatokanayo na mionzi

Hayo yamesemwa na Afisa mahusiano mwandamizi kutoka tume ya nguvu za Atomiki Tanzania Peter Ngamilo mkoani Arusha ambapo amesema kuwa  Tume hiyo inajihusisha na udhibiti wa vyanzo vya mionzi kuhamasisha matumizi salama teknolojia ya nyuklia
Amesema kuwa lengo la kushiriki maonyesho ya nanenane
Kutoa elimu kwa wafanyabiashara wanaosafirisha bidhaa za vyakula nje ya nchi au kuingiza bidhaa za mazao ya kilimo ndani ya nchi kwani kazi yao kubwa ni kuangalia vimelea vyote vya mionzi kwenye chakula.

Ngamilo amesema kuwa mwitikio wa wakulima na wafugaji ni mkubwa mara baadaya kupata elimu wengine walikuwa wagumu kuleta sampuli za vyakula ili vipimwe mara baada ya kupata elimu wameleta sampuli za vyakula ili vikapimwe
"Miaka ya nyuma tulikuwa tunapata taabu sana pale unapomuelewesha mkulima au mfugaji kuhusiana na kuleta sampuli za vyakula kwenye Tume ili vikapimwe ila tunashukuru baada ya kupata elimu wakulima wenyewe wamekuwa wakileta sampuli ili zikzpimwe"alisema
Wamita kupata elimu juu ya upimaji wa sampuli tofauti na miaka mingine

Kwa upande wake Mwanasayansi wa mionzi Denisi Mwalongo amesema kuwa jukumu kubwa la tume ni kulinda wananchi dhidhi ya madara yanayoweza kusababishwa na mionzi huku akiainisha aina kuu mbili za mionzi ambayo ni Miaonzi ayonishi na Mionzi isiyoayonisha .

"Mionzi isiyoayonisha ni mionzi ambayo inaweza kuleta madhara kwa binadamu mfano xray gamareys,
Isiyoayonisha ni kama mionzi ya simu radio"Alisema.

Nchi zaidi 152 duaniani wanachama wa tume za nguvu za atomiki duniani 
Hadi sasa hawajaweza kubaini nguvu za mionzi katika vyakula vinavyoingia kutokana na ushirikiano walionao katika utendaji kwani vyakula vikitoka nje vinapimwa vikiingia vinapimwa pia mionzi iliyopo ni ya kawaida haijavuka hadi kuonekana ni hatari kwa mwanadamu
"Mionzi inaweza kusababisha ukemia au kansa
Ukitumia muda mrefu sana kuongea na simu kwa muda mrefu,kukaa kwenye kompyuta muda mrefu,kuhifadhi simu katika maeneo hatarishi katika baadhi ya sehemu za mwili kwasababu miili yetu ni tishu inazalisha mionzi kwa haraka sana"
.    
Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel