Top Menu

WATANZANIA WAASWA KUTUMIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NDANI YA NCHINa.Vero Ignatus ,Arusha.

Wito umetolewa kwa Watanzania watumie bidhaa za ndani zaidi kuliko kuzipa kipaumbele bidhaa za nje ya nchi kwani wazalishaji wa ndani wanazalisha bidhaa zenye ubora zaidi.


Hayo yamesemwa na mzalishaji wa bidhaa zitokananzo na maziwa kutoka kwenye kampuni ya The Grand Demam iliyopo jijini Arusha Omari Cuba  ambapo wameiomba serikali wapunguze kodi kwa wasindikaji wa ndani kwani ni kubwa ukilinganisha na wale wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi.


Amesema kuwa changamoto kubwa waliyo nayo kama wazalishaji ni ushindani wa bei,bidhaa za ndani zinakuwa na bei ya juu zaidi kuliko bidhaa zinazotoka nje ya nchi,hivyo basi wameiomba serikali kuwatupia macho wajasiriyamali wa ndani zaidi.


Pia ametoa ushauri kwa wananchi wasitumie maziwa ambayo hayajafanyiwa usindikaji kwani hayana usalama yanakuwa na vyanzo vya magonjwa,au la yakiwa hayajasindikwa wahakikishe kuwa maziwa yanachemshwa kwa kiwango kinachotakiwa kwa matumizi ya kibinadamu.


“Ukiwa umekunywa maziwa ambayo hayajachemshwa unakunywa bacteria walio hai, unakuwa umepanda katika mwili wako maradhi ambayo yatakuja kuibuka hapo baadae”alisema Omar.


Sambamba na hayo wameiomba serikali ifanye matangazo lau mara mbili kwa mwezi kwa njia ya radio,Luninga na mitandao ya kijamii ili kufanya uhamasishaji kwa wananchi waweze kutumia maziwa pamoja na bidhaa zitokanazo na maziwa.

Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel