Top Menu

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA UKUTA UNAOZUNGUKA ENEO LA MGODI WA TANZANITE MIRERANI LEO

Askari wa usalama barabarani akiuelekeza njia msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akikagua ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite eneo la Mirerani mkoani Manyara kabla ya kuuzindua ukuta huo wenye uerefu wa kilomita 24.5 leo Aprili 6, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa rasmi ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite eneo la Mirerani mkoani Manyara wakati wa sherehe za  kuuzindua ukuta huo wenye uerefu wa kilomita 24.5 leo Aprili 6, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akionedha hati aliyopokea kutoka kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa rasmi ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite eneo la Mirerani mkoani Manyara wakati wa sherehe za  kuuzindua ukuta huo wenye uerefu wa kilomita 24.5 leo Aprili 6, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidia kumweka kitini Mzee Jumanne Ngoma, mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, wakati wa uzinduzi  rasmi   wa ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite eneo la Mirerani mkoani Manyara wakati wa sherehe za  kuuzindua ukuta huo wenye uerefu wa kilomita 24.5 leo Aprili 6, 2018. Pamoja na kutambua kazi yake ya kutukuka Rais Magufuli amemzawadia Mzee Ngoma shilingi milioni 100. Kushoto ni binti wa Mzee Ngoma, Asha Ngoma.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikabidhi gari la wagonjwa kwa ajili ya wakaazi wa Simanjiro  wakati wa uzinduzi  rasmi   wa ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite eneo la Mirerani mkoani Manyara wakati wa sherehe za  kuuzindua ukuta huo wenye uerefu wa kilomita 24.5 leo Aprili 6, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakimsikiliza Mzee Jumanne Ngoma, mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, alipokuwa akimshukuru kwa kutambua kazi yake na hatimaye kumzawadia shilingi milioni 100 wakati wa uzinduzi  rasmi   wa ukuta uliojengwa kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite eneo la Mirerani mkoani Manyara wakati wa sherehe za  kuuzindua ukuta huo wenye uerefu wa kilomita 24.5 leo Aprili 6, 2018. Kushoto ni binti wa Mzee Ngoma, Asha Ngoma

  Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya shukrani Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo baada ya jeshi hilo kukamilishi mbele ya wakati ujenzi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi kitambulisho cha Taifa mmoja wa wamiliki wa migodi ya Tanzanitehati ya shukrani Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Jenerali Venance Mabe ili kuwawezesha kupata ruksa ya kuingia na kufanya kazi ndani ya eneo lililozungukwa na ukuta  eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018 .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli akifunua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa  ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli na viongozi wengine wakipata maelezo ya madini ya Tanzanite yanavyochakatwa wakati wa uzinduzi rasmi wa  ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la migodi ya madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli katika picha na mvumbuzi wa madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma  wakati wa uzinduzi rasmi wa  ukuta wenye urefu wa kilomita 24.5 kuzunguka eneo la mgodi wa madini ya Tanzanite huko Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara kwenye sherehe za kuzindua ukuta huo leo Aprili 6, 2018. Picha na IKULU

Na.Vero Ignatus Mirerani -Manyara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amezindua ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite  Mirerani Mkoani Manyara    wenye urefu wa kilometa 24.5  uliogharimu bilioni 5.65

Rais Magufuli amewataka viongozi wa Kitaifa pamoja na viongozi wengine wenye dhamana kuwatambua watu ambao wanafanya tafiti na kuvumbua vitu mambilmbali vyenye maslahi kwa Taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo mara baada ya kumtamhulisha Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite mzee Jumanne Ngoma ambae alivumbua madini hayo mwaka 1967.

Kwa upande wake waziri wa Nishati na madini Anjela Kairuki amesema kuwa kodi  zilizolizokuwa zinapatikana kabla ya kuthibiti utoroshwaji wa madini 2015 milioni 166,mwaka 2016 milioni 171 baada ya kuhibiti utoroshwaji wa madini ndani ya mitatu 2017 wamepata mrahaba wa shilingi milioni 714 .

"Hivi sasa madini yote yakitoka migodini yanathaminishwa na kulipiwa kodi  zote za serikali  na ndipo wachimbaji wenyewe wanaweza kulipana mapato yao" alisema Kairuki.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Mwinyi amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa ukuta huo kumejenga historia mpya  itakayosaidia kulinda rasilimali zote za madini ,maslahi mapana na endelevu ya Tanzania.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo  Mkuu wa majeshi Generali Venance Salvatory Mabeho amesema kuwa ujenzi wa ukuta ulianza rasmi novemba 2017 hadi kufikia Februari 2018 ukuta ulikuwa umekamilika .

"Mheshimiwa Rais wewe ulitupa miezi 6 lakini sisi Jeshi tumeikamilisha ndani ya miezi 3,tumetekeleza kwa uadilifu na uamnifu ujenzi huu.,tunatoa shukran za dhati kwa taasisi za uhandisi Tanzania kwa ushirikiano  wao"alisema Mabeho.

Amesema kuwa katika utekelezaji wa malengo haya ya ujenzi wa ukuta zipo changamoto mbalimbali zilizojitokeza ambazo ni pamoja na ugumu wa ujenzi kwenye maeneo ya miamba,uwepo wa njia nyingi za maji,

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Martin Busungu amesema  Jeshi la JKT lipo tayari kutekeleza maaagizo yoyote yakatayotolewa kwa mustakabali  wa Taifa,
 amesema vikosi 20 vya JKT vimejenga ukuta huo.

Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel