Top Menu

Timu ya Daladala yaibuka kidedea mbele ya timu ya Bodaboda


Na. Vero Ignatus, Arusha

Timu ya madereva wa dala dala imefanikiwa kuonyesha ubabe mbele madereva wenzao wa boda boda Mara baada ya kuwafunga kwa penati 3-2

Mchezo huo uliochezwa katika viwanja vya sheikh Amri Abeid Jijini Arusha yenye lengo la kupunguza ajali kwa kukuza ushirikiano baina ya madereva hao wawapo  baranarani ulihudhuriwa na wachezaji Jonas Mkude na Ibrahim Ajib sambamba na shiza Kichuya.

Katika mchezo huo dala dala walitangulia kufunga goli dakika ya 25 kupitia kwa mchezaji wake Juma Hassan lakini katika kipindi cha pili boda boda waligomea ushindi huo baada ya kusawazisha dakika ya 73 kupitia kwa  Abdul Mzambia na kufanya dakika 90 kumalizika

 Kupitia ushindi huo timu ya dala dala imefanikiwa kuzawadiwa kombe la ushindi pamoja na kitita cha shilingi laki sita huku boda boda wakipewa shilling laki nne.

Akizungumzia mashindano haya, mgeni rasmi Katibu Tawala Wilaya ya Arusha David Mwakiposa aliwataka madereva hao kuhakikisha wanatumia barabara kwa kujali watu wengine ili kupunguza ajali na kukomesha kabisa

Kwa upande wake mratibu Wa bonanza hilo, Ashura Mohamed alisema kuwa wameamua kushirikisha timu hizo baada ya kuona Wingi Wa ajali barabani lakini pia kukuza ushirikiano

Share this:

Post a Comment

 
Designed By Arusha Publicity | Developed By Gadiola Emanuel